Nilivyonasa kwenye mtego wa simu za mkopo

Nilivyonasa kwenye mtego wa simu za mkopo

Nimefanya kazi kampuni anzilishi ya hii mikopo Tz. Kwa Samsung najua hapo utakua umekopa watu simu.

Mfano ungenunua simu kwenye kampuni niliyofanyia kazi riba ingekua ndogo kulinganisha na watu simu, riba ya watu simu ni kubwa kwakua ukipoteza simu ukaripoti unagewa nyingine.

Ushauri wangu kwa mtu anayetaka kuchukua simu ya mkopo. Jua muda wa malipo, jua bei halisi ya kifaa, jua riba, jua kama kuna benefits zozote kwa upande wako
Vipi ukishindwa kulipa ukasema urudishe simu yao?
 
Vipi ukishindwa kulipa ukasema urudishe simu yao?
Nitakujibu kwa kampuni niliyofanyia kazi sijajua kwa Watu Simu mtu akishindwa na kurudisha inakuaje.

Inabidi kuzingatia kama mteja amelipa angalau robo tatu ya deni, yaani malipo yamerudisha bei ya simu bila mkopo, kisha mteja anagewa punguzo ambalo atatakiwa kulipa mara moja na simu itafunguliwa.

Kuna return policy ambayo inataka urudishe simu dukani na muuza duka akurudushie kianzio chako. Isipokua hii ngumu kwakua muuza duka anaweza kurudishiwa simu ikiwa kwenye hali mbaya na atashindwa kuiuza au hata ikiwa nje ya box tu akashindwa kuiuza
 
Baada ya simu yangu ya tecno kuharibika sikuona haja ya kupoteza hela kuipeleka kwa fundi kwa sababu nilikuwa nimeitumia kwa miaka mitatu hivyo nikaona ni bora tu nikatafute simu nyingine mpya ya kutumia. Tarehe 2/2 nikaamua kwenda town kununua simu ila niliplan safari hii ninunue Samsung maana sikuwahi kuitumia kabla. Nilipofika town nikaenda kwenye duka moja la simu nikaulizia bei ya Samsung nikaambiwa 680,000 ila hela yangu ikawa haitoshi ndipo jamaa ambaye ni muuzaji akanishawishi kama vp kuna Samsung pia za mkopo hivyo kama sitojali naweza tu kuchukua halafu niwe nalipa kidogokidogo. Basi mi sikujali kwa sababu aliniambia kianzio cha mkopo ni 80,000 halafu hiyo iliyobakia nitakuwa nailipa mdogo mdogo hadi mda wa mkopo wangu utakapoisha. Akanipa Samsung Ao5 nikalipa kianzio halafu akanipa namba ya kampuni ambayo nitakuwa nalipia hela iliyobakia, kama ni kwa wiki, siku au mwezi. Kwa siku2260 au kwa wiki 15821. Sasa kitu ambacho mimi sikukigundua wala kuuliza ni kiasi cha riba kwenye hizi simu za mkopo kwa sababu wiki mbili baadae jamaangu mmoja nae alienda kununua simu kama hii ya kwangu lakini yeye haikuwa ya mkopo alilipa cash. Sasa kitu kilichonishtua ni bei jamaangu aliyonunulia, yeye aliuziwa 240’000 na mimi niliambiwa ni 411’000 nilipe kidogokidogo kwa miezi 6. Kilichonishtua ni bei halisi ya simu kwa cash na mkopo. Yaani 240’000 cash na mkopo 411’000 ikiwa ni ongezeko la 170’000 yaani riba ya mkopo ni robo tatu ya bei ya simu. Duh kweli vitu vya mkopo kwangu basi nilinasa kwenye mtego na sitorudia tena hakika huu ni wizi na utapeli wa waziwazi.
Yaani mpaka 2nd Feb ulikua hujawahi kumiliki samsung na umetumia tecno miaka mitatu? Who Are You??? Mbona umenichanganya saana. Najuta kusoma uzi wako. (na sijafanikiwa kuumaliza)
 
Tumieni hizi APK kwenye pc zenu mtoe hizo security plug
Cha kwanza download file la simu unalotaka kutoa security plug
Pitia hapa


Hatua ya pili ingia hapa chukua hii ikikushinda lipia unlock tool au tafuta iliyo cracked
Mkuu acha kufundisha watu wizi, hawakushikiwa mtutu kukopa
 
Yaani mpaka 2nd Feb ulikua hujawahi kumiliki samsung na umetumia tecno miaka mitatu? Who Are You??? Mbona umenichanganya saana. Najuta kusoma uzi wako. (na sijafanikiwa kuumaliza)
Smart ziko nyingi boss, kuna watu wametumia smu kwa miaka zaidi ya 20 na hawajawahi kutumia Samsung
 
Nilireport wakaniambia nitafute Los Report na nikafanya hivyo.
Wakaniambia niendelee kulipia watanipa simu nyingine, nikasema mtanipa lini? Wakasema wewe lipa lipa tukiona una mwenendo mzuri tutakuwa simu nyingine.
Nikasema tuandikiane halafu mniambie ni lini hasa mtanipa simu nyingine. Hapo ndio tulishindwa kuelewana. Nikaamua kupotezea tu.
So kumbe hata Mimi mwenye simu ya mkopo naweza itupa kisha nikawaambia imeibiwa? Nataka niachane na simu hii ya mkopo ninunue simu yangu hata ya laki na 20 maana hii naona niliingia chaka
 
Yaani mpaka 2nd Feb ulikua hujawahi kumiliki samsung na umetumia tecno miaka mitatu? Who Are You??? Mbona umenichanganya saana. Najuta kusoma uzi wako. (na sijafanikiwa kuumaliza)
Sawa mkuu tuachie wenye uzi wetu tuendelee kujifunza.
 
Yaani mpaka 2nd Feb ulikua hujawahi kumiliki samsung na umetumia tecno miaka mitatu? Who Are You??? Mbona umenichanganya saana. Najuta kusoma uzi wako. (na sijafanikiwa kuumaliza)
Watu mnajua kujimwambafai balaa

Tecno atumie yeye maudhi upate wewe, simu akope yeye maumivu upate wewe, uzi aandike yeye kero upate wewe
 
240 yenyewe amepigwa.hyo simu
Ukinunua añzia pc 3 bei 186,000
Pc 1 200,000
Kila siku tunatangaza biashara huku tatizo mna dharau
Hata mimi kuna mdau wangu aliniuzia kwa bei ya laki 2, akaniambia ameniuzia kwa bei ya jumla .ila kwa kawaida anaiuza 25000 mwisho 23000.
Nashangaa mtu anaikopa kwa 480000.
Aisee haya maisha kila mtu na mipango yake.
Ila wafanyabiashara wengi hapa bongo ni kama matapeli ndio maana sasahivi wanawalalamikia sana wachina kwamba wanauza bidhaa kwa bei ya chini
 
Binafsi ninakauli mbiu kwa mahitaji yangu asilimia 95.... if I can't buy it in cash I can't afford it.

Naheshimu mawazo ya wanaonunua hivi vitu kwa mkopo.

Simu siwezi nunua kwa mkopo.
Gari siwezi kununua kwa mkopo.
Furniture siwezi nunua kwa mkopo.

Kama nahitaji kununua gari nitasubiri mtu afulie aniuzie gari. Siwezi kwenda bank nikachukua mkopo wa kununua gari, simu, furniture, kujenga nyumba n.k

Zaidi ya asilimia 70 ya mamilionea duniani wanaendesha second hand cars.
Asilimia 70 ya mamilionea, hii umeifanyia research mwenyewe
 
Back
Top Bottom