Wakuu Habarini za Siku ya Leo? Natumaini mu wazima wa Afya. Na wale wagonjwa nawaombea uponaji wa mapema ili waendelee na majukumu yao ya kila siku.
Niende kwenye hoja.
Mimi sikuwa mdau wa kukopa kopa simu ila, baada ya kuwa na kazi kadhaa zinazotumia charge ya simu kwa kasi na kumaliza charge ndani ya masaa 12, nikajaribu kutafuta power bank nikaona nyingi ni fake, nikaamua kudondokea kwenye Samsung A 07 ya mkopo.
Sasa kitu kinachonishtua kwenye hii Samsung a07, ni kwamba, kila baada ya dakika kadhaa, ishara/notification ya kuonesha kuwa camera inatumika inaonekana kwenye screen kisha ina dissappear. Sasa wasiwasi wangu ni je, ina maana kila baada ya dakika kadhaa hawa wakopeshaji wanapiga picha za mahali simu ilipo? Na kama ni hivyo, je huko sio kuingilia faragha ya mtumiaji/mteja kinyume kabisa na sheria za nchi yetu?
Naomba kuwasilisha.