Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Msemakweli, nadhani kuna ujumbe unaufunika kwa sababu fulani au kwa makusudio fulani. Kitu kunachosisitizwa hapa ni hicho ulichokitaja kuwa kujenga mfumo imara nimchakato endelevu, lakini tunachosisitiza wengine hapa ni siyo tu ni mchakato endelevu bali ili mfumo ufanikiwe na uende haraka ni lazima uwe SHIRKISHI.
Kwa sasa hivi imeonekana wazi kuwa kasi ya kuimarisha mfumo haipo na kama ikitokea umesonga mbele, husonga hatua sita na kurudi nyuma hatua kumi. Na hii inasababishwa na ukweli kuwa hatuna katiba ya nchi bali Itikadi ya chama iliyobatizwa na kuitwa Katiba ya Nchi na mfumo hali kadhalika siyo wa Taifa ni wa Chama!
Umeongelea hoja muhimu sana

1. Tunachotaka ni mfumo utakaojiendesha kwavile umeshirikisha wananchi na unaendeshwa na wananchi.

Uliopo sasa unaendeshwa na mtu au watu wachache.
Hatuwezi kuwa na vyombo vyote vya dola chini ya mtu mmoja tukafanikiwa

PCCB,DPP, DCI, IGP,TRA, n.k vina wajibika eneo moja.
Checks and balances ipo wapi?

2. Tunataka mfumo unaongalia mambo yote si majipu tu.

Tutafanya kosa walilofanya Wazanzibar linalowagharimu

Wznz badala ya kuangalia mfumo mzima walip idurusu katiba yao mwaka 2010, wao walilenga 'kutumbua jipu la Tanganyika'

Ondoa mafuta katika mambo ya muungano. Anzisha taasisi zisizo na maana bali majina tu, weka bendera na wimbo wa Taifa n.k.

Hawakuangalia katiba yao inasema nini kuhusu tume ya uchaguzi.
Kwamba, ule uwezo wa kutohojiwa mahakamani ulikuwa na maana?

Wakati ulipofika CCM hawana hoja za kwanini CUF wasiende mahakamani , CUF wanasisitiza ni mbinu za kunyang'anywa ushindi, katiba haielezi lolote

Hawakuangalia, ikitokea hakuna chama chenye wabunge asilimia 10 nini kitatokea
Kinachoendelea ni serikali ambayo kikatiba haipo lakini kikatiba haisemwi ni 'haramu'

Hawakuangalia serikali ya SUK inaundwa kwa msingi gani ikitokea isivyotarajiwa
Waliangalia CUF na CCM wanagawana vipi madarka.

Leo tunaona CCM wanajipa majina ya upinzani kwa uhalali na uharamu hapo hapo

Mifano hii inaonyesha kutokuwa na misingi imara ni tatizo mbele ya safari.

Ndio maana tunasema hatua za kutumbua majipu hazina shida, lakini lazima kwanza zitanguliwe na misingi ili kujenga mfumo imara na si mtu, show ya mtu mmoja
 
Mzee M.M.

Mzee M.M.Mwanakijiji,mm nakuheshimu sana lakini ujue kila mtu kupewa meno kutaleta mgongano katika kushughulikia mambo kiutawala na kuleta misunderstanding baina ya GVT machineries zake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
You are right, I concur with your argument. Auditor apaswi kuwa sehemu ya utendaji. objectivity itatoka wapi? Amuoni hatari ya kuingizwa kwenye chain ya makosa!
 
john-magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa baadhi yetu tuliokataa kuvingirisha mikono yetu kuunga mkono mabadiliko yaliyobinafsishwa kwa mtu mmoja tulijikuta hatuna budi kumuunga mkono Magufuli tukiamini anawakilisha mabadiliko ya kweli. Binafsi niliamini kabisa kuwa Taifa lilikuwa linamhitaji kiongozi kama Magufuli kuweza kulinasua mahali lilipo kuliko kiongozi yule mwingine toka upinzani. Niliamini kabisa kuwa Magufuli akishika madaraka atakuwa na kazi kubwa ya kulirejesha Taifa katika misingi yake ambayo inaonekana ilikuwa imepotea.

Hatua zake mbalimbali za mwanzo kushughulika na kubana matumizi, kupambana na ufisadi na kuondoa watendaji mizigo a.k.a majipu kulinifanya niamini kabisa kuwa Magufuli kazi aliyonayo akiendelea na kasi hiyo basi ndani ya miezi sita tu atakuwa ameleta heshima katika utumishi wa umma, kurejesha heshima kwa Watanzania na fahari ya taifa letu kurudishwa. Niliamini kabisa kuwa Magufuli atafanya kazi hii bila woga, huruma, husuda, wivu, au kusita sita. Kwamba, hatomwangalia yeyote, popote na kwa lolote. Ndani ya miezi sita hivi na kabla ya ujio wa bajeti ya kwanza ya serikali yake basi Magufuli atakuwa ameshaweka alama za namna gani taifa linataka kwenda na kila kiongozi atakuwa amepata ujumbe.

Nilifanya makosa.

Nilifanya makosa kwa sababu nilidhani hii ni kazi rahisi kwa Rais. Nilidhani ni kazi ya kutimua huyu, kuondoa yule na kumleta yule mwingine. Nilidhani ni kazi ambayo akimaliza teuzi mbalimbali basi atakuwa ameipanga serikali yake kwa ajili ya kuchapa kazi.

Sasa najua kuwa uamuzi wake wa kushughulika na watu kwanza kabla ya mfumo ni jambo muhimu sana. Ulikuwa ni uamuzi sahihi na unajitahi kutetewa. Watu ndio hutengeneza mfumo; ni watu ndio ambao hukaa chini na kufanya maamuzi mbalimbali yenye kuathiri (kwa uzuri au ubaya) uwepo na utendaji wa mfumo wa utawala. Ukiwa na watu wabovu, wabinafsi na wenye mwelekeo wa ufisadi basi mfumo utakuwa mbovu, wa kibinafsi na wenye uelekeo wa kifisadi kwa sababu moja kubwa; wale wenye kuiwamba ngoma ngozi huivutia kwao! Mfumo wetu wa utawala wa kifisadi ulitengenezwa na watawala wenye mwelekeo wa kifisadi. Matobo (siyo matundu) kwenye sheria zetu vilitengenezwa na watu ambao walijua wakiziba na wao watakuwa wamejizibia.

Magufuli asingeweza kutengeneza mfumo mwingine kwa kutumia watu wale wale walioutengeneza mfumo huu wa sasa na hasa kama watu hao ni wanufaika wa mfumo huu. Ingelikuwa ni sawa sawa na kumtaka Rais awalazimishe watu wakate matawi ambayo wamekalia huku wakijua kwa kufanya hivyo wataangukia mtoni kwenye mamba wengi. Hakukuwa na jinsi nab ado hakuna jinsi ni lazima kuwaondoa hawa na kuwashughulikia ili kuleta watu wenye fikra zinazoakisi mwelekeo wa serikali yake.

Ni kwa sababu hiyo, kumbe kazi ile ya miezi sita kwa kweli haiwezekani. Ni kazi ambayo inapaswa kuwa endelevu na yenye matokeo bora. Tayari tumeanza kuona dalili za yaliyomo ndani ya ripot ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) na tayari inatisha kama ilivyotisha mwaka 2006 na miaka iliyofuatia.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukijulishwa juu ya uchafu wa watendaji wetu na taasisi zetu na mara karibu hizo zote tumekuwa tukionesha kushtushwa na kusikitishwa tukiamini kuwa labda mwaka unaofuatia mambo yatakua tofauti. CAG aliyepita alikuwa anarudia baadhi ya hoja mwaka baada ya mwaka na wakati mwingine kuhusiana na taasisi au watu wale wale. Na safari hii tusije kushangaa kuwa hata CAG wa sasa anaweza kujikuta amegusa maeneo yale yale; matumizi mabaya ya sheria ya manunuzi ya umma, fedha kutumiwa bila maelezo, kutopatikana kwa vitabu vya masuala ya fedha wakati wa ukaguzi, na upotevu wa fedha za umma kwa namna ambayo inadokeza tu kuwa zimeliwa.

Magufuli basi ana kazi kubwa; kushughulikia viongozi wabadhirifu, wazembe, wezi, na wenye kutumia madaraka yao vibaya na wakati huo huo kupanga na kusimamia serikali yake huku akiuunda upya mfumo uliojaribiwa na kuharibiwa.

Kwa mwendo alioanza nao hakuna shaka yoyote jambo moja lilikuwa sahihi kwa upande wangu; kuunga mkono mabadiliko haya. Wapo wanadhani hali ni ngumu sasa na kuwa serikali inabana naamini bado hatujaona hasa ugumu kwani hadi hivi sasa bado serikali inahangaika na madudu ya nyuma na yanatisha. Kusahihisha uchumi (correcting an economy) ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) haiwezekani kuwa ni jambo moja.

Ni kwa sababu hiyo naamini:

1. Kuanza kazi kwa mahakama za kushughulikia ufisadi na uhujumu uchumi kunahitajika mara moja

2. Sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema zaidi ili CAG awe na madaraka ya kutoa agizo la kusimamishwa kazi na hata kufikishwa mahakamani kwa mtendaji yeyote wa umma ambaye uchunguzi wake (CAG) unaonesha kuwa kuna uvunjaji wa sheria. Ikiwezekana ofisi ya CAG iwe na Waendesha mashtaka wake kama ilivyo kwa TAKUKURU. Haipaswi madudu yam waka mzima yanasubiri mwaka mwingine kujulikana. CAG anapofanya ukaguzi na kukuta madudu na ushahidi wa kisayansi upo (forensic evidence) basi hatua zichukuliwe mara moja. Siyo awe na uwezo wa kupeleka mashtaka lakini kwa kupendekeza kwa DPP au hata yeye mwenyewe washutumiwa watiwe mbaroni, mali zao zinazohusiwa kupatikana kwa njia haramu kukamatwa ili zije kufilisiwa wakikutwa na hatia.

3. Sheria ya Usalama wa Taifa inahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka – hili ni jambo ambalo limekuwa katika mada zangu kwa karibu miaka kumi sasa. TISS bado ni dhaifu sana na udhaifu wake umechangia sana kutamalaki kwa utamaduni wa kifisadi. Natumaini Magufuli hatochukua muda mrefu kuifumua hii taasisi kwani ndio moyo wa taifa. Ikilegea taifa liko mashakani.

Kuna na mengine mengi ambayo naamini Magufuli atayafanya kwani tayari ameshaanza kuyafanya na kuwa endapo atafanikiwa tutakapofika mwisho wa mwaka huu kama taifa tutashusha pumzi kidogo kwani angalau tutakuwa katika mazingira ya kusema “kweli hakika huyu alikuwa anahitajika”.

Ni wazi pia kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema “hapana” na waleta “vikwazo”. Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu. La maana ni kukaza mwenzo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikani, na nidhamu ili hatimaye Ujenzi Mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni Zama Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu.

Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.
ndo uwache dhana ya kudhani life needs practice than theories
 
Kuirekebisha nchi hii sio kazi ya lelemama. Kwa haya matatizo yaliyopo JPM ana kazi kubwa sana. Kila upande kuna uozo
[emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji12] [emoji12] hata yy ana mauozo yake.........
 
Ni wazi pia kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema “hapana” na waleta “vikwazo”. Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu. La maana ni kukaza mwenzo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikani, na nidhamu ili hatimaye Ujenzi Mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni Zama Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu.

Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, asante kwa kuliona hili, ila katika hao watu uliowataja watakuwepo, pia tutakuwepo akina sisi ambao tutasifu kwenye kila muzuri atakayofanya, ila pia tutakosoa katika kila makosa atakayoyafanya kwa lengo la kumsaidia asiendelee kujikwaa mwishowe akaanguka!, watu watakaomsaidia zaidi ni wale watakaomkosoa na sio nyinyi mnaomsifu tuu as if Magufuli ni malaika fulani.

Nyerere alipoamua Tanzania tutajenga Ujamaa na Kujitegemea, alisema atatuchukua miaka 30!. Kuna watu walimkosoa akina Edwin Mtei, akina Prof. Rweyemamu na wengine waliotimkia nje. Baada tuu ya miaka 20, akakiri kuwa tulifanya makosa, na kukiri kuwa kufanya kosa sii kosa kosa kurudia kosa, hivyo na sisi kama wote tutaishia kusifu tuu haya anayoyafanya Magufuli ili hali mengine ni madudu, tutakuwa tunafanya kosa, hivyo sisi wengine ni ma kiritiki, tutakiritisaizi constirakitivilii, kwa kusema where he does wrong na kushauri the right way!.

Miongoni mwa mazuri ya Magufuli kwa taifa hili ni pamoja na hulka yake ya udikiteta, Tanzania tulipofika, tulihitaji mtu wa sample ya Magufuli, na Mungu kasikio kilio chetu, tumepatiwa. Hapa tumesifu.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simp

Na kutokana na ukomo wa kutawala ni miaka 10 tuu, tumeshauri 2020 tusipoteze muda na fedha kufanya uchaguzi wa rais, Magufuli aendelee tuu kwa miaka 10, ila pia miaka 10 pekee haitoshi kusafisha uchafu wote na madudu yote ya miaka 50, hivyo tunashauri angalau ashike vipindi 2 vya miaka kumi kumi!.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais

Ila sisi wengine hatusifu tuu, pia tunatoa na maangalizo.
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria! .
JF Modes, Magufuli ni Rais Wetu, Asiabudiwe, Asiogopwe, Bali Aheshimiwe!.
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki Haki za Binaadamu?!..
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyo
te

NB. Mwanakijiji karibu nyumbani katika majukumu yako mapya, kama bado hujajulishwa rasmi, soon utajulishwa, unless ukatae mwenyewe, lakini nakushauri, ukijulishwa kubali tuu, hata unaanzia chini, ni kipindi kifupi tuu cha mpito, baadae utapanda juu!.

Jumapili Njema.

Pasco
 
Uimara wa nchi ni katiba sio mtu...Ipo siku mtamkana huyu magufuli mnaeimba sifa zake.mawaziri wake Kitwanga,January wamesaatumbukia kwenye kashfa.tuone atafanya nini..
 
Uimara wa nchi ni katiba sio mtu...Ipo siku mtamkana huyu magufuli mnaeimba sifa zake.mawaziri wake Kitwanga,January wamesaatumbukia kwenye kashfa.tuone atafanya nini..
Ya Tomaso hayo,time will tell tuwe wavumilivu kwani Magu ni mashine mpya ndani ya mfumo wa kizamani na kwa kuwa yeye ni dereva na fundi at the sametime basi utaona injini ya gari ni efficient in performance na lastly gari itakwenda inavyotakiwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
Bado ni mapema sana mm nitaanza kumtathimini akishakuwa mwenyekiti wa chama sababu Kule nasikia chama kwanza taifa baadae
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, asante kwa kuliona hili, ila katika hao watu uliowataja watakuwepo, pia tutakuwepo akina sisi ambao tutasifu kwenye kila muzuri atakayofanya, ila pia tutakosoa katika kila makosa atakayoyafanya kwa lengo la kumsaidia asiendelee kujikwaa mwishowe akaanguka!, watu watakaomsaidia zaidi ni wale watakaomkosoa na sio nyinyi mnaomsifu tuu as if Magufuli ni malaika fulani.

Nyerere alipoamua Tanzania tutajenga Ujamaa na Kujitegemea, alisema atatuchukua miaka 30!. Kuna watu walimkosoa akina Edwin Mtei, akina Prof. Rweyemamu na wengine waliotimkia nje. Baada tuu ya miaka 20, akakiri kuwa tulifanya makosa, na kukiri kuwa kufanya kosa sii kosa kosa kurudia kosa, hivyo na sisi kama wote tutaishia kusifu tuu haya anayoyafanya Magufuli ili hali mengine ni madudu, tutakuwa tunafanya kosa, hivyo sisi wengine ni ma kiritiki, tutakiritisaizi constirakitivilii, kwa kusema where he does wrong na kushauri the right way!.

Miongoni mwa mazuri ya Magufuli kwa taifa hili ni pamoja na hulka yake ya udikiteta, Tanzania tulipofika, tulihitaji mtu wa sample ya Magufuli, na Mungu kasikio kilio chetu, tumepatiwa. Hapa tumesifu.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simp

Na kutokana na ukomo wa kutawala ni miaka 10 tuu, tumeshauri 2020 tusipoteze muda na fedha kufanya uchaguzi wa rais, Magufuli aendelee tuu kwa miaka 10, ila pia miaka 10 pekee haitoshi kusafisha uchafu wote na madudu yote ya miaka 50, hivyo tunashauri angalau ashike vipindi 2 vya miaka kumi kumi!.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais

Ila sisi wengine hatusifu tuu, pia tunatoa na maangalizo.
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria! .
JF Modes, Magufuli ni Rais Wetu, Asiabudiwe, Asiogopwe, Bali Aheshimiwe!.
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki Haki za Binaadamu?!..
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote

NB. Mwanakijiji karibu nyumbani katika majukumu yako mapya, kama bado hujajulishwa rasmi, soon utajulishwa, unless ukatae mwenyewe, lakini nakushauri, ukijulishwa kubali tuu, hata unaanzia chini, ni kipindi kifupi tuu cha mpito, baadae utapanda juu!.

Jumapili Njema.

Pasco
Kama Magu dikteta basi ni aina ya udikteta mzuri kwa maslahi ya nchi bana maana system ilikuwa dysfunction kabisa kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa nchi na mipaka yake achilia mbali dhuluma na manyanyaso ndiyo maana watz wengi walikuwa wanamwelewa Dr.Slaa kwenye majukwaa ya siasa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
 
Bado ni mapema sana mm nitaanza kumtathimini akishakuwa mwenyekiti wa chama sababu Kule nasikia chama kwanza taifa baadae
Chipaka rafiki yangu lazima mtu aibebe chama kwa mahali ilipofikia otherwise itaishiwa na pumzi mapema aliyasema haya comrade Kingunge Ngombali Mwiru siyo mzee wa kumbeza aisee!!!!.
 
Mkuu, uko sahihi , mifumo huundwa na watu sio mifumo huunda watu,(kwanza kinachoitwa mifumo ni nadharia tu) kwa hiyo aina ya watu waliopo kwenye mfumo au wanaounda mfumo ndio hutoa muelekeo wa mfumo wenyewe
Gooooood!!! Una akili sana wewe big up
 
Huwa nasema na nitarudia kusema kila siku kwamba Magufuli ni genius, watu wengi hawaamini lkn muda utaongea, mimi nilimkubali Magufuli jinsi tu alivyoweza kupenya CCM na kuibuka kuwa Mgombea wa CCM, ni mtu genius tu ndiyo anaweza kupenya kwenye mto uliojaa mamba wengi namna ile na kuibuka mshindi!
Watu kama Lowasa walijiandaa kwa zaidi miaka 20, walijenga mitandao ya watu wenye ushawishi mkubwa wa fedha na karibia kila kitu lkn hawakupita, na sababu kubwa ni kwamba watu kama Lowasa wana fedha na watu wenye fedha lkn siyo Inteligent men na ndiyo maana wanashindwa kama Lowasa angekuwa intelligent man huu uraisi ulikuwa wake kabisa!

Ikumbukwe kwambaMagufuli hakuwa na kundi, fedha wala watu wazito na wenye ushawishi kwenye Chama hivyo alitegemea Akili yake tu na ndiyo maana hata siku anaaongea na majaji alilisema hilo kwamba mtu kama yeye from now where akaweza kupenya na mwishowe kuapishwa kuwa Raisi wa JMTZ siyo jambo dogo!
Tangia hapo nikajua kwamba Magufuli siyo mtu wa kawaida, najua baadhi wanamdharau na kumdhihaki lkn siku zinavyozidi kwenda idadi yao inazidi kupungua, watu waliokuwa wanamkebehi na kumdhihaki Magufuli hapa JF mwanzoni walikuwa wengi sana leo hii wengi wao wamepotea!

Mambo aliyoyafanya Magufuli kwa nchi hii chini ya miezi 6 hata nchi za Wazungu tunazozifia viongozi wao hawawezi kufanya reforms kubwa namna hii, fikiria kupunguza utegemezi wa bajeti chini ya mwaka 1 ktk 40% mpaka 3% hii siyo kazi ndogo, uwezo tu wa kuteua watu makini kama Waziri Mpango kuwa waziri wa fedha inahitaji akili!

Hivyo kama alivyosema Kikwete hata mimi nalala usingizi kabisa tena nakoroma kwa maana najua TanZania yetu iko salama na tutavuka kama alivyosema Raisi Magufuli!
Na baada ya miaka mitatu tuu... Tz chini ya huyu JEMBE bajeti yetu tutakuwa tunajitegemea sisi wenyewe kama sijakosea
 
Inaonekana JPM alikuwa anautamani sana urais, na ainaonekana alikuwa anaumia moyoni kimya kimya! kuona mambo yalivyokuwa yanaenda ndivyo sivyo
 
Umeongelea hoja muhimu sana

1. Tunachotaka ni mfumo utakaojiendesha kwavile umeshirikisha wananchi na unaendeshwa na wananchi.

Uliopo sasa unaendeshwa na mtu au watu wachache.
Hatuwezi kuwa na vyombo vyote vya dola chini ya mtu mmoja tukafanikiwa

PCCB,DPP, DCI, IGP,TRA, n.k vina wajibika eneo moja.
Checks and balances ipo wapi?

2. Tunataka mfumo unaongalia mambo yote si majipu tu.

Tutafanya kosa walilofanya Wazanzibar linalowagharimu

Wznz badala ya kuangalia mfumo mzima walip idurusu katiba yao mwaka 2010, wao walilenga 'kutumbua jipu la Tanganyika'

Ondoa mafuta katika mambo ya muungano. Anzisha taasisi zisizo na maana bali majina tu, weka bendera na wimbo wa Taifa n.k.

Hawakuangalia katiba yao inasema nini kuhusu tume ya uchaguzi.
Kwamba, ule uwezo wa kutohojiwa mahakamani ulikuwa na maana?

Wakati ulipofika CCM hawana hoja za kwanini CUF wasiende mahakamani , CUF wanasisitiza ni mbinu za kunyang'anywa ushindi, katiba haielezi lolote

Hawakuangalia, ikitokea hakuna chama chenye wabunge asilimia 10 nini kitatokea
Kinachoendelea ni serikali ambayo kikatiba haipo lakini kikatiba haisemwi ni 'haramu'

Hawakuangalia serikali ya SUK inaundwa kwa msingi gani ikitokea isivyotarajiwa
Waliangalia CUF na CCM wanagawana vipi madarka.

Leo tunaona CCM wanajipa majina ya upinzani kwa uhalali na uharamu hapo hapo

Mifano hii inaonyesha kutokuwa na misingi imara ni tatizo mbele ya safari.

Ndio maana tunasema hatua za kutumbua majipu hazina shida, lakini lazima kwanza zitanguliwe na misingi ili kujenga mfumo imara na si mtu, show ya mtu mmoja

mkuu unaweza kutoa mfano hai wa misingi na mfumo, ambao unahisi au kuamini kuwa ni bora zaidi kuliko afanyacho magufuli

toa mfano mkuu
 
Ujue kitu kinacho nishangaza kwa baadhi ya watu wanaposema "magufuli ana kazi ngumu" hivi kazi ya kulijenga taifa ni rais peke yake! Kinacho takiwa kufanya ni kumshauri pale unapoona kuna mapungufu. Kama alivyo shauri mkuu mwanakijiji kuhusu usalama wa taifa kufanyia marekebisho ili uwende na wakati. Tunajua rais Ana vijana wake humu watamfikishia ujumbe ushauri wako. Tanzania itajengwa na sisi wenyewe kwa roho za kizalendo.
 
NB. Mwanakijiji karibu nyumbani katika majukumu yako mapya, kama bado hujajulishwa rasmi, soon utajulishwa, unless ukatae mwenyewe, lakini nakushauri, ukijulishwa kubali tuu, hata unaanzia chini, ni kipindi kifupi tuu cha mpito, baadae utapanda juu!.

Jumapili Njema.

Pasco
Pasco, hivi hii bado tu ama tayari ila imetolewa kimya kimya!
 
Napingana na maoni yako. Nyumba imara huanzia kweye msingi. Nyumba yetu imechakaa, Ina nyufa, na unatikisika. Anachofanya magu ni kuondoa baadhi ya bâti ailizooza sana, kupaka rangi kuta zenye nyufa na kuwaita wanakijiji waje kupiga picha na kushangilia.
Hivi magufuri ana ubavu Wa kuvunja mitandao ya kiharifu inayoongozwa na viongozi Wakuu Wa chama chake Kama ujangiri , mdawa ya kulevya nk. Tusidanganyane, mfumo ndio msingi kwanza mengine yatafuata. Tuache kushangilia maigizo.
Mkuu Gulwa ni kweli nyumba imara huanzia kwenye msingi na ili kurekebisha uozo uliopo juu mtu atahitaji kubomoa tokea chini ndipo arekebishe nyumba nzima kwa ujumla,lakini kazi ya ubomoaji msingi huenda isiwe rahisi kutokana na namna msingi huo ulivyosimamishwa ni imara kiasi gani,ikiwa ni imara itachukua muda na utashi mwingi ili kuubomoa

Ndo kinachotokea kwa mh rais wetu JPM msingi wa mfumo mbovu wa nchi yetu umejengwa kwa nyenzo imara na zenye nguvu hivyo basi kipindi cha miezi sita tu hakitoshi kuibomoa misingi hiyo na kujenga mfumo mpya juu ya msingi mpya

Hivyo basi wakati mwingine muda ndo jibu zuri zaidi hebu tuupeni muda utupe majibu.
 
Back
Top Bottom