Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Kwa hiyo kesho na mimi nikiingia Ikulu ,nikauchukua mgodi wa Tanzanite basi ni sawa kwa sababu ni makosa niliyoyafanya nikiwa madarakani ?
Sidhani kama swali ni "sawa" au la. Ni kwamba huwezi kumshtaki Rais mahakamani akiwa madarakani; lakini unaweza kumuondoa Rais akiwa madarakani na hata kumshtaki kwa mambo mengine baada ya hapo kwa njia ya impeachment. Lakini ana kinga ya kutoshtakiwa akiwa madarakani. Hata na wewe ukiingia madarakani utakuwa nayo. Lakini haina maana hawezi kushughulikiwa; process ya Kibunge ndio njia pekee iliyobakia ya kumuondoa Rais ambaye anaonekana amevunja sheria akiwa madarakani.
 
Mfumo ni nini? Tuanzie hapo kwanza kwa maana isije kuwa tunanukuu tu mambo bila ya kuelewa hasa maana yake ni nini!
Hawa jamaa nimewauliza sana ili swali, huwa hawajibu ila utawaelewa ktk maelezo yao kuwa mfumo ni sisiemu tu. Ukiitoa sisiemu yaani serikali ya sisiemu basi umetoa mfumo, huko kwenye mashirika ya umma, serikali kuu mpaka chini kwao sio mfumo. Kwao mfumo ni serikali TENA ya sisiemu tu, hivyo wanaposema kubadilisha mfumo huwa wanamaanisha sisiemu kama serikali itoke iingie chadema.
 
Mwanakijiji unaheshima sana kuwa na uandishi mzuri, paragraph ya kwanza tu ilinionyesha kuwa umekaa kimajungu.., itaniwia vigumu sana kuelewa maana ya bandiko lako kwa kilichopo kwenye utangulizi wa bandiko hili.

Je waliokuwa wanaunga mkono mabadiliko nje ya chama cha mapinduzi hawakuwa na maana ya kufanya hivyo? Waiamini hii CCM kwa muda gani? Waendelee na majungu kama haya kwa miaka mingapi? Waendelee kuchukia watu kwa majina yao kwa muda gani?

Nadhani tunapaswa kuangalia mambo kwa mtizamo mpana zaidi, haya majungu na maumivu binafsi msiyaegeshe kwa watu wengine, je Dr Slaa angetufaa kama huyu Magufuli? hili hatulijui lakini wengine tungekuwa tuko huko tusikokujua.

Kwangu mimi sihitaji kuambiwa yanaoendelea kuhusu Magufuli kwa jinsi ulivyozungumzia hapa.
 
Hii makala ndefu nashindwa kuisoma yote. Kama unadhani TISS wanapaswa kuongezewa nguvu labda uongee na Ulimboka kwanza,au yule hurulaini wa DW,nimemsahau jina lake.
 
Sidhani kama swali ni "sawa" au la. Ni kwamba huwezi kumshtaki Rais mahakamani akiwa madarakani; lakini unaweza kumuondoa Rais akiwa madarakani na hata kumshtaki kwa mambo mengine baada ya hapo kwa njia ya impeachment. Lakini ana kinga ya kutoshtakiwa akiwa madarakani. Hata na wewe ukiingia madarakani utakuwa nayo. Lakini haina maana hawezi kushughulikiwa; process ya Kibunge ndio njia pekee iliyobakia ya kumuondoa Rais ambaye anaonekana amevunja sheria akiwa madarakani.
Mzee kama umesoma hapo hakuna sehemu nimesema raisi ashitakiwe akiwa madarakani ,
Nilisema kwa hiyo kesho nikiwa raisi nikauchukua mgodi wa Tanzanite ,sitoshitakiwa kwa sababu ni makosa niliyo yafanya nikiwa madarakani ,"Niliyo yafanya nikiwa ni wakati uliopita "hivyo haikua na maana ni raisi aliyepo madarakani

Sasa mbona nilipokuuliza Magufuli atafanyaje ikiwa anatakiwa kumpeleka rais aliyestaafu mahakamani ,ukanijibu hana la kufanya kwa makosa yaliyofanyika akiwa madarakani ??

Hapo juu unasema anaweza kushitakiwa kwa mambo mengine , sasa kipi ni kipi hapa ?
 
john-magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa baadhi yetu tuliokataa kuvingirisha mikono yetu kuunga mkono mabadiliko yaliyobinafsishwa kwa mtu mmoja tulijikuta hatuna budi kumuunga mkono Magufuli tukiamini anawakilisha mabadiliko ya kweli. Binafsi niliamini kabisa kuwa Taifa lilikuwa linamhitaji kiongozi kama Magufuli kuweza kulinasua mahali lilipo kuliko kiongozi yule mwingine toka upinzani. Niliamini kabisa kuwa Magufuli akishika madaraka atakuwa na kazi kubwa ya kulirejesha Taifa katika misingi yake ambayo inaonekana ilikuwa imepotea.

Hatua zake mbalimbali za mwanzo kushughulika na kubana matumizi, kupambana na ufisadi na kuondoa watendaji mizigo a.k.a majipu kulinifanya niamini kabisa kuwa Magufuli kazi aliyonayo akiendelea na kasi hiyo basi ndani ya miezi sita tu atakuwa ameleta heshima katika utumishi wa umma, kurejesha heshima kwa Watanzania na fahari ya taifa letu kurudishwa. Niliamini kabisa kuwa Magufuli atafanya kazi hii bila woga, huruma, husuda, wivu, au kusita sita. Kwamba, hatomwangalia yeyote, popote na kwa lolote. Ndani ya miezi sita hivi na kabla ya ujio wa bajeti ya kwanza ya serikali yake basi Magufuli atakuwa ameshaweka alama za namna gani taifa linataka kwenda na kila kiongozi atakuwa amepata ujumbe.

Nilifanya makosa.

Nilifanya makosa kwa sababu nilidhani hii ni kazi rahisi kwa Rais. Nilidhani ni kazi ya kutimua huyu, kuondoa yule na kumleta yule mwingine. Nilidhani ni kazi ambayo akimaliza teuzi mbalimbali basi atakuwa ameipanga serikali yake kwa ajili ya kuchapa kazi.

Sasa najua kuwa uamuzi wake wa kushughulika na watu kwanza kabla ya mfumo ni jambo muhimu sana. Ulikuwa ni uamuzi sahihi na unajitahi kutetewa. Watu ndio hutengeneza mfumo; ni watu ndio ambao hukaa chini na kufanya maamuzi mbalimbali yenye kuathiri (kwa uzuri au ubaya) uwepo na utendaji wa mfumo wa utawala. Ukiwa na watu wabovu, wabinafsi na wenye mwelekeo wa ufisadi basi mfumo utakuwa mbovu, wa kibinafsi na wenye uelekeo wa kifisadi kwa sababu moja kubwa; wale wenye kuiwamba ngoma ngozi huivutia kwao! Mfumo wetu wa utawala wa kifisadi ulitengenezwa na watawala wenye mwelekeo wa kifisadi. Matobo (siyo matundu) kwenye sheria zetu vilitengenezwa na watu ambao walijua wakiziba na wao watakuwa wamejizibia.

Magufuli asingeweza kutengeneza mfumo mwingine kwa kutumia watu wale wale walioutengeneza mfumo huu wa sasa na hasa kama watu hao ni wanufaika wa mfumo huu. Ingelikuwa ni sawa sawa na kumtaka Rais awalazimishe watu wakate matawi ambayo wamekalia huku wakijua kwa kufanya hivyo wataangukia mtoni kwenye mamba wengi. Hakukuwa na jinsi nab ado hakuna jinsi ni lazima kuwaondoa hawa na kuwashughulikia ili kuleta watu wenye fikra zinazoakisi mwelekeo wa serikali yake.

Ni kwa sababu hiyo, kumbe kazi ile ya miezi sita kwa kweli haiwezekani. Ni kazi ambayo inapaswa kuwa endelevu na yenye matokeo bora. Tayari tumeanza kuona dalili za yaliyomo ndani ya ripot ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) na tayari inatisha kama ilivyotisha mwaka 2006 na miaka iliyofuatia.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukijulishwa juu ya uchafu wa watendaji wetu na taasisi zetu na mara karibu hizo zote tumekuwa tukionesha kushtushwa na kusikitishwa tukiamini kuwa labda mwaka unaofuatia mambo yatakua tofauti. CAG aliyepita alikuwa anarudia baadhi ya hoja mwaka baada ya mwaka na wakati mwingine kuhusiana na taasisi au watu wale wale. Na safari hii tusije kushangaa kuwa hata CAG wa sasa anaweza kujikuta amegusa maeneo yale yale; matumizi mabaya ya sheria ya manunuzi ya umma, fedha kutumiwa bila maelezo, kutopatikana kwa vitabu vya masuala ya fedha wakati wa ukaguzi, na upotevu wa fedha za umma kwa namna ambayo inadokeza tu kuwa zimeliwa.

Magufuli basi ana kazi kubwa; kushughulikia viongozi wabadhirifu, wazembe, wezi, na wenye kutumia madaraka yao vibaya na wakati huo huo kupanga na kusimamia serikali yake huku akiuunda upya mfumo uliojaribiwa na kuharibiwa.

Kwa mwendo alioanza nao hakuna shaka yoyote jambo moja lilikuwa sahihi kwa upande wangu; kuunga mkono mabadiliko haya. Wapo wanadhani hali ni ngumu sasa na kuwa serikali inabana naamini bado hatujaona hasa ugumu kwani hadi hivi sasa bado serikali inahangaika na madudu ya nyuma na yanatisha. Kusahihisha uchumi (correcting an economy) ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) haiwezekani kuwa ni jambo moja.

Ni kwa sababu hiyo naamini:

1. Kuanza kazi kwa mahakama za kushughulikia ufisadi na uhujumu uchumi kunahitajika mara moja

2. Sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema zaidi ili CAG awe na madaraka ya kutoa agizo la kusimamishwa kazi na hata kufikishwa mahakamani kwa mtendaji yeyote wa umma ambaye uchunguzi wake (CAG) unaonesha kuwa kuna uvunjaji wa sheria. Ikiwezekana ofisi ya CAG iwe na Waendesha mashtaka wake kama ilivyo kwa TAKUKURU. Haipaswi madudu yam waka mzima yanasubiri mwaka mwingine kujulikana. CAG anapofanya ukaguzi na kukuta madudu na ushahidi wa kisayansi upo (forensic evidence) basi hatua zichukuliwe mara moja. Siyo awe na uwezo wa kupeleka mashtaka lakini kwa kupendekeza kwa DPP au hata yeye mwenyewe washutumiwa watiwe mbaroni, mali zao zinazohusiwa kupatikana kwa njia haramu kukamatwa ili zije kufilisiwa wakikutwa na hatia.

3. Sheria ya Usalama wa Taifa inahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka – hili ni jambo ambalo limekuwa katika mada zangu kwa karibu miaka kumi sasa. TISS bado ni dhaifu sana na udhaifu wake umechangia sana kutamalaki kwa utamaduni wa kifisadi. Natumaini Magufuli hatochukua muda mrefu kuifumua hii taasisi kwani ndio moyo wa taifa. Ikilegea taifa liko mashakani.

Kuna na mengine mengi ambayo naamini Magufuli atayafanya kwani tayari ameshaanza kuyafanya na kuwa endapo atafanikiwa tutakapofika mwisho wa mwaka huu kama taifa tutashusha pumzi kidogo kwani angalau tutakuwa katika mazingira ya kusema “kweli hakika huyu alikuwa anahitajika”.

Ni wazi pia kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema “hapana” na waleta “vikwazo”. Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu. La maana ni kukaza mwenzo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikani, na nidhamu ili hatimaye Ujenzi Mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni Zama Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu.

Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.

Mwanakijiji umekua msahaulifu sana na siasa za nchi hii, nakumbuka miaka kumi nyuma kila mtanzania aliiona Tanzania ya maishabora kwa wote iko mbeleyake ,hata sisi tuliokua wapinzani wa ccm tuliona mara hii kweli nchi itabadilika
Na pale JK alivyojaribu kubadilisha mawaziri kila baada ya muda ili kukabiliana na changamoto ambazo tulidhani zilimfanya Rais asifikie malengo ya maisha bora tulipata tamaa zaidi.

Lakini hatimayake nikuongezeka umasikini mitaani na kupanda uchumi ndani ya vitabu sio kwa wanachi wakawaida.

Nakusudia kusema Tanzania haitabadilika kama mfumo haujabadilika.
CCM bado ni kikwazo kwa Tanzania

Kila kiongozi anaekuja watu hupatatamaa kwa zile hadaa za miaka ya mwanzo.
Rudisha kumbukumbu tena miaka ishirini ya iliopita (Mkapa) utanielewa pengine.

Maneno haya yaweke kumbukumbu ili uje unisute baada ya muda wa magufuli kuisha.

Na natanguliza tena maneno 2025 ataibuliwa malaika mwengine kutoka ccm tutalisha maneno haya haya.

Kwakutumia vitendo ya miaka ya mwanzo vya Rais mtarajiwa.

Watanzania wenzangu mbona tunadanganywa kila siku na watu hawa hawa na sisi wengi tuliokosa elimu tunaburuza ila chakusikitisha na wasomi wetu pia huburuzwa tena wao ndio wanajifunga minyororo wenyewe,inakua afadhali ya sisi tusio na elimu !

Watanzania tunamatatizo gani?
 
Kila mtu anasisitiza mfumo mfumo kwa maana ya(SYSTEM) kwa lugha ya malikia naomba mchokoza mada atoe ufafanuzi,ukisema mfumo mbovu serikalini,una maana gani?? Na ulitaka au kushauri uweje na mfumo ni nini? Tafadhari
 
Hawa jamaa nimewauliza sana ili swali, huwa hawajibu ila utawaelewa ktk maelezo yao kuwa mfumo ni sisiemu tu. Ukiitoa sisiemu yaani serikali ya sisiemu basi umetoa mfumo, huko kwenye mashirika ya umma, serikali kuu mpaka chini kwao sio mfumo. Kwao mfumo ni serikali TENA ya sisiemu tu, hivyo wanaposema kubadilisha mfumo huwa wanamaanisha sisiemu kama serikali itoke iingie chadema.
Ni somo refu ila naomba nikujibu kama ifuatavyo...matatizo ya nchi hii yanaanzia kwenye mfumo wa utawala. Kinadharia toka mwaka 1992 Tanzania ni nchi ya mfumo wa vyama vingi lakini kiuhalisia bado nchi inaendeshwa kama vile tuko kwenye mfumo wa chama kimoja. CCM chama tawala kwa makusudi kiliamua kulinda maslahi ya viongozi wake na kutanguliza mbele maslahi ya chama badala ya taifa. Kwa msingi huo chama kilipoteza dira na matatizo yaliyojitokeza na kukiandama chama hicho moja kwa moja yakawa ya taifa.

Ni kweli tunao muundo (structure) wa vyama vingi lakini muundo peke yake hautoshelezi kuleta taswira ya mfumo (system) mpaka iongezewe dhana na vigezo na mamlaka. Hivyo mfumo tulio nao unahitaji marekebisho ya msingi kikatiba ili uweze kukidhi matakwa halisi ya demokrasia ya vyama vingi. Haya ni mapungufu makubwa na mpaka hapo watawala wetu watakapokiri ukweli huo na kuufanyia kazi mfumo wetu wa utawala utabakia kiini macho. Mfumo wetu una mapungufu makubwa unaotoa mwanya kwa utawala usiojali sheria.

Je nini athari ya mfumo kama huu? Taifa kupiga kambi kwenye bonde la kashfa baada ya kashfa halafu majipu kuanza kuigiza kutumbua majipu. Angalia huko visiwani...eti Shein naye anatumbua majipu akisahau ni yeye alikuwa Raisi kipindi kilichopita, ni usanii, usanii, usanii.

Nimejaribu sana kufupisha maelezo kwa sababu tu sitaki kuwachosha wasomaji.

NB: Tukumbuke pia kabla ya 1992, CCM ilikuwa haikaguliwi na ilikuwa inachota tu toka hazina kila wakihitaji hela. Baada ya vyama vyama vingi kuanzishwa CCM iliamua kupora mali zote zilizokuwa zimechangiwa na wananchi na kuzigeuza za kwake kama majumba. viwanja, makampuni, shule n.k. na mpaka leo wanazimiliki kiharamu.
 
Mwanakijiji umekua msahaulifu sana na siasa za nchi hii, nakumbuka miaka kumi nyuma kila mtanzania aliiona Tanzania ya maishabora kwa wote iko mbeleyake ,hata sisi tuliokua wapinzani wa ccm tuliona mara hii kweli nchi itabadilika

Una uhakika kweli kila Mtanzania aliona Tanzania ya maisha bora kwa wote iko mbele? Lakini hakuna ubaya kuwa mtu wa matumaini (optimist) kuliko mtu wa kuhofia mabaya wakati wote (pessimist).
 
Siku hizi tatizo limekuwa mfumo.... Nakumbuka hapo nyuma tuliambiwa tatizo ni mafisadi.. Sasa mafisadi wanashughulikiwa tunaambiwa hao sio tatizo tatizo ni mfumo... Sasa sielewi unaanzaje kuondoa ufisadi bila kuwashughulikiwa mafisadi.

Yani chadema toka wamchukue lowassa na wezi wengine awataki kabisa kusikia mafisadi wanashughulikiwa wanataka ubadilishwe mfumo eti ndio tatizo.
 
Hawa jamaa nimewauliza sana ili swali, huwa hawajibu ila utawaelewa ktk maelezo yao kuwa mfumo ni sisiemu tu. Ukiitoa sisiemu yaani serikali ya sisiemu basi umetoa mfumo, huko kwenye mashirika ya umma, serikali kuu mpaka chini kwao sio mfumo. Kwao mfumo ni serikali TENA ya sisiemu tu, hivyo wanaposema kubadilisha mfumo huwa wanamaanisha sisiemu kama serikali itoke iingie chadema.
Mkuu sijui ni jamaa wapi unaoongelea hata hivyo naomba nichangie hoja zako

1. Kuhusu mfumo ni nini, hili swali anauliza Barbarosa kila wakati. tuliwahi kuandika maelezo tukitaraji angeelewa. Kila mara anarudia, hivyo tunakaa kimya hatuna uwezo mwingine wa kumsaidia. Tunafahamu pia ni njia anayotumia kuhamisha mjadala

2. Kuna vitu viwili katika maoni yako.
Moja, kuna mfumo wa chama kimoja, miaka 50 umetufikisha katika 'utamaduni' wa ufisadi Kwamba, ni wakati tuangalie mfumo mzima kwanza

Pili, kuna CCM unaowasema. Mfumo ni kitu na humilikiwa na watu.
Kwa miaka 50 CCM ndio watawala wakitumikia mfumo huo.

Licha ya kelele za wananchi, bado wanaamini ni mzuri tu kwavile unawafaidisha binafsi

3. Kwavile CCM ndio kikwazo katika kufumua mfumo huu waliouasisi , kuna uhusiano wa moja kwa moja, wa mfumo, CCM na matokeo yake kama ufisadi.

Mfano,Rais anatumbua majipu, wanaopaswa kumsaidia wanachukua rusha, i.e Wabunge wa CCM. Hii inaeleza wanavyoujua mfumo na kuutumia bila woga kwasababu ndio 'wamiliki'. Wanajua wao na serikali lazima watii mfumo unaonedeshwa na CCM

Wala rushwa wanatetewa na Spika badala ya kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Spika anawabadilisha kamati ili kupooza habari ionekane ni jambo dogo.
Anajua jinsi ya kutumia mfumo uliopo kulinda wala rushwa kama wabunge-CCM

4. Hiki mnachosikia kutumbua majipu kwa vijana wadogo ni kitu cha kipekee sana.

Kwa watu waliokula chumvi kiasi na hapa niwaalike Mzee Mwanakijiji Mag3 JokaKuu Jasusi Andrew Nyerere kwa uchache wa kuwataja wanakumbuka tumbua majipu ifuatayo

a) Wahujumu uchumi na walanguzi wakati wa Sokoine hadi vipindi vya mikingamo
B)Usipo wajika utakumbwa na fagio la chuma wakati wa Mwinyi

Kwasababu hatukuwa na mfumo endelevu kazi yote ikawa bure tumerudi kwa kasi , ari mpya na nguvu mpya katika ufisadi kuliko wakati mwingine toka uhuru

Tunachosema ni kuwa, kama CAG, TISS wanatakiwa kuangaliwa kimfumo, isiishie hapo
Lazima tujiulize DPP, DCI, IGP, Bunge, BoT, Hazina, serikali n.k zipo katika nzuri?

Tunakumbuka mtifuano wa PCCB ya Hosea na DPP.
Tujiulize, tatizo ni hawa watu peke yao? Je walikwama wapi?

Iweje Magufuli anapata habari za wakati wa JK leo hii?

Kwa jicho pana, hakuna kilichokuwa hakijulikani. Mfumo wetu ndio iliokwamisha

DPP hana uwezo hadi Rais aseme, DCI hana uwezo mbele ya Rais, IGP anawajibika kwa Rais, BoT inaendeshwa kisiasa- Kagoda. DCI hana uhuru wa kutekeleza majukumu

Orodha ni ndefu sana. Haiwezekani CAG na TISS tu. Mfumo ni kitu 'intertwining'

Badala ya kuangalia tulipojikwa, tupo bize kuangalia tumeangukia wapi

Baada ya miaka 5 anakuja mpasua matambazi, miaka 5 anakuja mpaka GV vipele, miaka 5 anakuja mwondoa fungus!

No hatufiki kwa style hii
 
Mkuu sijui ni jamaa wapi unaoongelea hata hivyo naomba nichangie hoja zako

1. Kuhusu mfumo ni nini, hili swali anauliza Barbarosa kila wakati. tuliwahi kuandika maelezo tukitaraji angeelewa. Kila mara anarudia, hivyo tunakaa kimya hatuna uwezo mwingine wa kumsaidia. Tunafahamu pia ni njia anayotumia kuhamisha mjadala

2. Kuna vitu viwili katika maoni yako.
Moja, kuna mfumo ambao upo wa chama kimoja, na miaka 50 umetufikisha katika 'utamaduni' wa ufisadi Kwamba, ni wakati tuangalie mfumo mzima kwanza

Pili, kuna CCM unaowasema. Mfumo ni kitu na humilikiwa na watu.
Kwa miaka 50 CCM ndio watawala wakitumikia mfumo huo.
Licha ya kelele za wananchi, bado wanaamini ni mzuri tu kwavile unawafaidisha binafsi

3. Kwavile CCM ndio kikwazo katika kufumua mfumo huu waliouasisi , kuna uhusiano wa moja kwa moja, wa mfumo, CCM na matokeo yake kama ufisadi.

Mfano,Rais anatumbua majipu, wanaopaswa kumsaidia wanachukua rusha, i.e Wabunge wa CCM. Hii inaeleza wanavyoujua mfumo na kuutumia bila woga kwasababu tu ndio 'wamiliki' wa mfumo. Wanajua wao na serikali lazima watii mfumo unaonedesha na CCM

Wala rushwa wanatetewa na Spika badala ya kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sharia.

Spika anawabadilisha kamati ili kupooza habari ionekane ni jambo dogo.

Anajua kutumia mfumo uliopo kulinda wala rushwa kama wabunge-CCM

4. Hiki mnachosikia kutumbua majipu kwa vijana wadogo ni kitu cha kipekee sana.

Kwa watu waliokula chuimvi kiasi na hapa niwaalike Mzee Mwanakijiji Mag3 JokaKuu Jasusi Andrew Nyerere kwa uchache wa kuwataja wanakumbuka Tumbua majipu ifuatayo

a) Wahujumu uchumi na walanguzi wakati wa Sokoine hadi vipindi vya mikingamo
B)Usipo wajika utakumbwa na fagio la chuma wakati wa Mwinyi

Kwasababu hatukuwa na mfumo endelevu kazi yote ikaisha tumerudi kwa kasi , ari mpya na nguvu mpya katika ufisadi kuliko wakati mwingine toka uhuru

Tunachosema ni kuwa, kama CAG, TISS wanatakiwa kuangaliwa kimfumo, isiishie hapo

Lazima tujiulize DPP, DCI, IGP, Bunge, BoT, Hazina, serikali n.k zipo katika nzuri?

Tunakumbuka mtifuano wa PCCB ya Hosea na DPP.
Tujiulize, tatizo ni hawa watu peke yao? Je walikwama wapi?

Iweje Magufuli anapata habari za wakati wa JK leo hii?

Kwa jicho pana, hakuna kilichokuwa hakijulikani. Mfumo wetu ndio iliokwamisha kila j

DPP hana uwezo hadi Rais aseme, DCI hana uwezo mbele ya Rais, IGP anawajibika kwa Rais, BoT inaendeshwa kisiasa-ya Kagoda. DCI hana uhuru wa kutekeleza majukumu

Orodha ni ndefu sana. Haiwezekani CAG na TISS tu. Mfumo ni kitu 'intertwining'

Badala ya kuangalia tulipojikwa, tupo bize kuangalia tumeangukia wapi

Baada ya miaka 5 anakuja mpasua matambazi, miaka 5 anakuja mwingine kupaka GV vipele, miaka 5 mingine anakuja mwingine kuondoa fungus! No hatufiki
Mkuu, Hivi haya maelezo marefu uliyoeleza unadhani kwa dhati umeeleza maana ya mfumo?

Hivi kwa haya maelezo marefu unadhani mtu asiyefahamu maana ya mfumo ataweza kuelewa?

Kwangu mimi ulichokifanya ni kukosoa tu utendaji wa taasisi mbali mbali ndani ya serikali na vyama vyetu vya kisiasa.

Hujaeleza mfumo ni nini na unapatikana kwa namna gani.

Nani anayeleta huo mfumo, nani anayeujenga, kuusimamia na kuulinda? Siku ngapi zinachukuchua huo mfumo kupatikana?

Huu mfumo uliopo(kama upo) nani aliuleta na aliutoa wapi? Alikoutoa kwa sasa wana hatua gani?

Tueleze ni mfumo gani ambao hauna matatizo/mapungufu katika dunia hii na kama yapo, kwa nini yapo na kwa nini yasiwepo.

Halafu unaposema tumejikuta tuko pale pale kama taifa unakuwa unatumia vigezo gani kinachotambulika kubainisha hilo kwa sababu kuwa pale pale ina maana maisha yaliyokuwepo wakati wa Edward Sokoine ndiyo yaliyopo kwa sasa. Je, Tanzania ya sasa ni ile ile iliyokuwa wakati wa Edward Sokoine?
 
Kama umesoma hoja yangu 1, nimesema sitazungumzia mfumo, nimeuzungumzia sana kwa mifano n.k. siyo leo wala jana miaka mingi iliyopita na sana katika mwaka huu.

Kama watu hawajui mfumo, wapi wanashangiliaje bila kujua wanashangilia nini?

Kuhusu Tanzania ya Sokoine na ya sasa, ya Sokoine haikuwa hii

Kwa miaka 10 iliyopita rushwa si utamaduni tena, bali maisha yetu ya kawaida

Genge lililotufikisha hapa neno laini linaitwa majipu lipo pale pale
Tofauti ni kuwa utumbuaji unachugua ni jipu gani dhaifu

Hutasikia jipu la IPTL,DOWANS, STANBIC,ESCROW n.k. kwasababu ni ya na watu wa mfumo. Nani atamfunga paka kengele? Paka walioleta mkate mezani. Thubutuuu!

Pili, genge ni lile lile kwa maana kuwa Rais anatumbua majipu, Wabunge wanatuhumiwa kwa kuchukua rushwa.

Spika aliyepaswa kusaidia kazi anawabadilisha kamati 'mabadiliko ya kawaida''

Ingalikuwa daktari au mhasibu tungesikia ametumbuliwa hapo hapo.

Katika mazingira ya kawaida wabunge walipaswa kuwekwa pembeni hadi keshi ziishe! Hilo halitokei, ni watu wa mfumo ule ule wa watu wale wale waliotufikisha hapa

Fikiria, Rais anapambana na majipu, wabunge wapo katika tuhuma nzito za RUSHWA! nini kimebadilika hapo? Tusemeni ukweli tu jamani.

Bila kubadili mfumo ambao wengi hamuujui ingawa mnapinga hatufiki popote
 
Kama umesoma hoja yangu 1, nimesema sitazungumzia mfumo, nimeuzungumzia sana kwa mifano n.k. siyo leo wala jana miaka mingi iliyopita na sana katika mwaka huu.

Kama watu hawajui mfumo, wapi wanashangiliaje bila kujua wanashangilia nini?

Kuhusu Tanzania ya Sokoine na ya sasa, ya Sokoine haikuwa hii

Kwa miaka 10 iliyopita rushwa si utamaduni tena, bali maisha yetu ya kawaida

Genge lililotufikisha hapa neno laini linaitwa majipu lipo pale pale
Tofauti ni kuwa utumbuaji unachugua ni jipu gani dhaifu

Hutasikia jipu la IPTL,DOWANS, STANBIC,ESCROW n.k. kwasababu ni ya na watu wa mfumo. Nani atamfunga paka kengele? Paka walioleta mkate mezani. Thubutuuu!

Pili, genge ni lile lile kwa maana kuwa Rais anatumabua majipu , Wabunge bila aibu wanatuhumiwa kwa kuchukua rushwa.

Spika aliyepaswa kusaidia kazi anawabadilisha kamati 'mabadiliko ya kawaida''

Ingalikuwa daktari au mhasibu tungesikia ametumbuliwa hapo hapo.

Katika mazingira ya kawaida wabunge walipaswa kuwekwa pembeni hadi keshi ziishe! Hilo halitokei, ni watu wa mfumo ule ule wa watu wale wale waliotufikisha hapa

Fikiria, Rais anapambana na majipu, wabunge wapo katika tuhuma nzito za RUSHWA! nini kimebadilika hapo? Tusemeni ukweli tu jamani.

Bila kubadili mfumo ambao wengi hamuujui ingawa mnapinga hatufiki popote
Kwanza nianze kwa kukuambia, usidhani tunapokuuliza maana ya mfumo tunakuwa hatufahamu. Kama huo ndio mtazamo wako utakuwa unajipotosha kifikra. Hata mwalimu huwa anauliza maswali kwa wanafunzi wake na kwa kufanya hivyo haina maana kuwa hafahamu majibu ya maswali anayouliza.

Pili, kusema kuwa kwa sasa huwezi kueleza maana ya mfumo kwa kuwa umeeleza sana katika mada mbali mbali za nyuma ni njia tu ya kukimbia swali kwa sababu kama hicho ni kigezo chako, mbona huachi kukosoa kosoa kila mara kuhusu masuala yanayohusu kile unakiita mfumo kwa kigezo hicho hicho kuwa umekosoa kosoa sana huko nyuma au kwenye mada nyingi.

Hata kwenye hii comment yako umeendeleza tu yale yale ya kukosoa kosoa utendaji wa serikali bila kuelezea mbadala yake.

Unanikumbua haiba ya wanaharakati ambao wao kazi yao ni kufikiri kinadharia badala ya uhalisia.

Unachokifanya ni kuainisha mlolongo wa nadharia ambazo hazina nafasi katika dunia halisi na kwa maana hiyo sishangai unapoleta excuses kuhusu maswali yangu kwa sababu yanahusu hali halisi.

Ninaendelea kusubiri majibu ya maswali yangu ambayo yako kwenye bandiko namba 127.
 
john-magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa baadhi yetu tuliokataa kuvingirisha mikono yetu kuunga mkono mabadiliko yaliyobinafsishwa kwa mtu mmoja tulijikuta hatuna budi kumuunga mkono Magufuli tukiamini anawakilisha mabadiliko ya kweli. Binafsi niliamini kabisa kuwa Taifa lilikuwa linamhitaji kiongozi kama Magufuli kuweza kulinasua mahali lilipo kuliko kiongozi yule mwingine toka upinzani. Niliamini kabisa kuwa Magufuli akishika madaraka atakuwa na kazi kubwa ya kulirejesha Taifa katika misingi yake ambayo inaonekana ilikuwa imepotea.

Hatua zake mbalimbali za mwanzo kushughulika na kubana matumizi, kupambana na ufisadi na kuondoa watendaji mizigo a.k.a majipu kulinifanya niamini kabisa kuwa Magufuli kazi aliyonayo akiendelea na kasi hiyo basi ndani ya miezi sita tu atakuwa ameleta heshima katika utumishi wa umma, kurejesha heshima kwa Watanzania na fahari ya taifa letu kurudishwa. Niliamini kabisa kuwa Magufuli atafanya kazi hii bila woga, huruma, husuda, wivu, au kusita sita. Kwamba, hatomwangalia yeyote, popote na kwa lolote. Ndani ya miezi sita hivi na kabla ya ujio wa bajeti ya kwanza ya serikali yake basi Magufuli atakuwa ameshaweka alama za namna gani taifa linataka kwenda na kila kiongozi atakuwa amepata ujumbe.

Nilifanya makosa.

Nilifanya makosa kwa sababu nilidhani hii ni kazi rahisi kwa Rais. Nilidhani ni kazi ya kutimua huyu, kuondoa yule na kumleta yule mwingine. Nilidhani ni kazi ambayo akimaliza teuzi mbalimbali basi atakuwa ameipanga serikali yake kwa ajili ya kuchapa kazi.

Sasa najua kuwa uamuzi wake wa kushughulika na watu kwanza kabla ya mfumo ni jambo muhimu sana. Ulikuwa ni uamuzi sahihi na unajitahi kutetewa. Watu ndio hutengeneza mfumo; ni watu ndio ambao hukaa chini na kufanya maamuzi mbalimbali yenye kuathiri (kwa uzuri au ubaya) uwepo na utendaji wa mfumo wa utawala. Ukiwa na watu wabovu, wabinafsi na wenye mwelekeo wa ufisadi basi mfumo utakuwa mbovu, wa kibinafsi na wenye uelekeo wa kifisadi kwa sababu moja kubwa; wale wenye kuiwamba ngoma ngozi huivutia kwao! Mfumo wetu wa utawala wa kifisadi ulitengenezwa na watawala wenye mwelekeo wa kifisadi. Matobo (siyo matundu) kwenye sheria zetu vilitengenezwa na watu ambao walijua wakiziba na wao watakuwa wamejizibia.

Magufuli asingeweza kutengeneza mfumo mwingine kwa kutumia watu wale wale walioutengeneza mfumo huu wa sasa na hasa kama watu hao ni wanufaika wa mfumo huu. Ingelikuwa ni sawa sawa na kumtaka Rais awalazimishe watu wakate matawi ambayo wamekalia huku wakijua kwa kufanya hivyo wataangukia mtoni kwenye mamba wengi. Hakukuwa na jinsi nab ado hakuna jinsi ni lazima kuwaondoa hawa na kuwashughulikia ili kuleta watu wenye fikra zinazoakisi mwelekeo wa serikali yake.

Ni kwa sababu hiyo, kumbe kazi ile ya miezi sita kwa kweli haiwezekani. Ni kazi ambayo inapaswa kuwa endelevu na yenye matokeo bora. Tayari tumeanza kuona dalili za yaliyomo ndani ya ripot ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) na tayari inatisha kama ilivyotisha mwaka 2006 na miaka iliyofuatia.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukijulishwa juu ya uchafu wa watendaji wetu na taasisi zetu na mara karibu hizo zote tumekuwa tukionesha kushtushwa na kusikitishwa tukiamini kuwa labda mwaka unaofuatia mambo yatakua tofauti. CAG aliyepita alikuwa anarudia baadhi ya hoja mwaka baada ya mwaka na wakati mwingine kuhusiana na taasisi au watu wale wale. Na safari hii tusije kushangaa kuwa hata CAG wa sasa anaweza kujikuta amegusa maeneo yale yale; matumizi mabaya ya sheria ya manunuzi ya umma, fedha kutumiwa bila maelezo, kutopatikana kwa vitabu vya masuala ya fedha wakati wa ukaguzi, na upotevu wa fedha za umma kwa namna ambayo inadokeza tu kuwa zimeliwa.

Magufuli basi ana kazi kubwa; kushughulikia viongozi wabadhirifu, wazembe, wezi, na wenye kutumia madaraka yao vibaya na wakati huo huo kupanga na kusimamia serikali yake huku akiuunda upya mfumo uliojaribiwa na kuharibiwa.

Kwa mwendo alioanza nao hakuna shaka yoyote jambo moja lilikuwa sahihi kwa upande wangu; kuunga mkono mabadiliko haya. Wapo wanadhani hali ni ngumu sasa na kuwa serikali inabana naamini bado hatujaona hasa ugumu kwani hadi hivi sasa bado serikali inahangaika na madudu ya nyuma na yanatisha. Kusahihisha uchumi (correcting an economy) ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) haiwezekani kuwa ni jambo moja.

Ni kwa sababu hiyo naamini:

1. Kuanza kazi kwa mahakama za kushughulikia ufisadi na uhujumu uchumi kunahitajika mara moja

2. Sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema zaidi ili CAG awe na madaraka ya kutoa agizo la kusimamishwa kazi na hata kufikishwa mahakamani kwa mtendaji yeyote wa umma ambaye uchunguzi wake (CAG) unaonesha kuwa kuna uvunjaji wa sheria. Ikiwezekana ofisi ya CAG iwe na Waendesha mashtaka wake kama ilivyo kwa TAKUKURU. Haipaswi madudu yam waka mzima yanasubiri mwaka mwingine kujulikana. CAG anapofanya ukaguzi na kukuta madudu na ushahidi wa kisayansi upo (forensic evidence) basi hatua zichukuliwe mara moja. Siyo awe na uwezo wa kupeleka mashtaka lakini kwa kupendekeza kwa DPP au hata yeye mwenyewe washutumiwa watiwe mbaroni, mali zao zinazohusiwa kupatikana kwa njia haramu kukamatwa ili zije kufilisiwa wakikutwa na hatia.

3. Sheria ya Usalama wa Taifa inahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka – hili ni jambo ambalo limekuwa katika mada zangu kwa karibu miaka kumi sasa. TISS bado ni dhaifu sana na udhaifu wake umechangia sana kutamalaki kwa utamaduni wa kifisadi. Natumaini Magufuli hatochukua muda mrefu kuifumua hii taasisi kwani ndio moyo wa taifa. Ikilegea taifa liko mashakani.

Kuna na mengine mengi ambayo naamini Magufuli atayafanya kwani tayari ameshaanza kuyafanya na kuwa endapo atafanikiwa tutakapofika mwisho wa mwaka huu kama taifa tutashusha pumzi kidogo kwani angalau tutakuwa katika mazingira ya kusema “kweli hakika huyu alikuwa anahitajika”.

Ni wazi pia kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema “hapana” na waleta “vikwazo”. Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu. La maana ni kukaza mwenzo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikani, na nidhamu ili hatimaye Ujenzi Mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni Zama Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu.

Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.
Mzee M.M.

Ni wazi pia kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema “hapana” na waleta “vikwazo”. Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu. La maana ni kukaza mwenzo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikani, na nidhamu ili hatimaye Ujenzi Mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni Zamoa Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu.

Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.
Mzee M.M.Mwanakijiji,mm nakuheshimu sana lakini ujue kila mtu kupewa meno kutaleta mgongano katika kushughulikia mambo kiutawala na kuleta misunderstanding baina ya GVT machineries zake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
 
Ni kama vile umeanza kumpigia kampeni Ndugu Magufuli kwa term ya pili ya miaka mitano. Kwamba umeanza kutuaminisha kuwa miaka mitano haitamtosha kwa kuwa kazi ya "kushughulikia viongozi wabadhirifu, wazembe, wezi na wenye kutumia madaraka yao vibaya" ni kubwa na itachukua muda mrefu. Sasa unasema miezi sita haitoshi. Nachukulia haya ni maandalizi ya kutuambia hapo baadaye kuwa miaka mitano haitoshi, tumpe mingine mitano. Tutakukumbusha.
 
mi sijaona cha maana ambacho magufuli amekifanya kwani kila mtawala akiingia huwa anaweka watu anao wazania watakao fanya kutokana na matakwa yake au malengo ya chama.tatizo ni kuwa wanao tolewa post zao kwenye kipindi cha magufuli wanatuhuma za ubadilifu tofauti na uongozi uliopita ambapo watawala walikuwa wanabadilisha watu lakini hawana tuhuma za ubadhilifu.
mkuu hizo tuhuma za ubadhilifu amewabambikia Magufuli au amewakuta nazo?, kama kawakuta nazo wame zitoa wapi?. Uwepo wa tuhuma hizo kwa watu hao ni sehemu ya msingi ktk maada jadiliwa!.
 
Kwanza nianze kwa kukuambia, usidhani tunapokuuliza maana ya mfumo tunakuwa hatufahamu. Kama huo ndio mtazamo wako utakuwa unajipotosha kifikra. Hata mwalimu huwa anauliza maswali kwa wanafunzi wake na kwa kufanya hivyo haina maana kuwa hafahamu majibu ya maswali anayouliza.

Pili, kusema kuwa kwa sasa huwezi kueleza maana ya mfumo kwa kuwa umeeleza sana katika mada mbali mbali za nyuma ni njia tu ya kukimbia swali kwa sababu kama hicho ni kigezo chako, mbona huachi kukosoa kosoa kila mara kuhusu masuala yanayohusu kile unakiita mfumo kwa kigezo hicho hicho kuwa umekosoa kosoa sana huko nyuma au kwenye mada nyingi.

Hata kwenye hii comment yako umeendeleza tu yale yale ya kukosoa kosoa utendaji wa serikali bila kuelezea mbadala yake.

Unanikumbua haiba ya wanaharakati ambao wao kazi yao ni kufikiri kinadharia badala ya uhalisia.

Unachokifanya ni kuainisha mlolongo wa nadharia ambazo hazina nafasi katika dunia halisi na kwa maana hiyo sishangai unapoleta excuses kuhusu maswali yangu kwa sababu yanahusu hali halisi.

Ninaendelea kusubiri majibu ya maswali yangu ambayo yako kwenye bandiko namba 127.
Kwa mgeni unaweza kuona hatuna mbadala.Kwa wazoefu wanajua tunasema nini

Miaka michache iliyopita tulikemea safari za Rais.
Tulisema tunazo resources za kutosha hatuhitaji kuhemea vibaba.

Akina Mh Magu wakasema ziara za Rais zina manufaa, hivi karibuni baada ya MCC wanasema tuanze kujitegemea!!!

Tuliwahi kusema bandari yetu ina operate chini ya kiwango na kwamba tuna bandari ambazo tukizutumia vyema tutanufaika.

Walioshindwa kutuelewa walisema nadharia tu, leo akina Magufuli wanafanya tulichokizungumza miaka 5 iliyopita

Tunasema hivi, lazima kwanza ufumue mfumo mzima, uweke structure itakayohakikisha kila mmoja ana wajibika, ana maadili na uzalendo. Huo ni mbadala wa majipu.

Hilo haliwezekani kwasababu wakati tunazungumzia katiba mpya, Magu alikuwa upande wa mfumo. Kutumbua majipu ni njia ya mkato,haina suluhisho la kudumu

Huwezi kutumbua majipu ukiwa huna taratibu endelevu za kuzuia isitokee tena na ikitokea wahusika wanawajibishwa. Huo ndio mbadala si kuhangaika na issue moja moja

Magufuli alipokwenda Muhimbili akamfukuza mkurugenzi, walisema jipu limetumbuliwa.
Tuliokuwa na mawazo tofauti tulisema haiwezekani tatizo liwe mkurugenzi pekee.

Je hazina walifanya kazi yao? Je wizara ya afya walifanya kazi yao?

Miezi miwili Magu karudi muhimbili na kukuta akina mama wakilala na maji ya chooni.
Tatizo si mashine za MRI au maji, ni kwanini hayo yanatokea?

Tukamwambia aangalie mfumo mzima kwanini akiondoka mambo yanarudi kama zamani.

Nimekupa mifano michache kati ya mingi kukuonyesha kuwa sisi wengine hatuimbi tuu !

Nimalizie, tulimwambia suala la ZNZ litatugharimu sote, wakati huo tukaonekana wana harakati. Je, hali ipoje sasa? Si kweli yametokea?

Wenye uchungu na wazalendo tunashangilia jema na tunakosoa ubovu, hatushangilii tuu
 
Back
Top Bottom