Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

john-magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa baadhi yetu tuliokataa kuvingirisha mikono yetu kuunga mkono mabadiliko yaliyobinafsishwa kwa mtu mmoja tulijikuta hatuna budi kumuunga mkono Magufuli tukiamini anawakilisha mabadiliko ya kweli. Binafsi niliamini kabisa kuwa Taifa lilikuwa linamhitaji kiongozi kama Magufuli kuweza kulinasua mahali lilipo kuliko kiongozi yule mwingine toka upinzani. Niliamini kabisa kuwa Magufuli akishika madaraka atakuwa na kazi kubwa ya kulirejesha Taifa katika misingi yake ambayo inaonekana ilikuwa imepotea.

Hatua zake mbalimbali za mwanzo kushughulika na kubana matumizi, kupambana na ufisadi na kuondoa watendaji mizigo a.k.a majipu kulinifanya niamini kabisa kuwa Magufuli kazi aliyonayo akiendelea na kasi hiyo basi ndani ya miezi sita tu atakuwa ameleta heshima katika utumishi wa umma, kurejesha heshima kwa Watanzania na fahari ya taifa letu kurudishwa. Niliamini kabisa kuwa Magufuli atafanya kazi hii bila woga, huruma, husuda, wivu, au kusita sita. Kwamba, hatomwangalia yeyote, popote na kwa lolote. Ndani ya miezi sita hivi na kabla ya ujio wa bajeti ya kwanza ya serikali yake basi Magufuli atakuwa ameshaweka alama za namna gani taifa linataka kwenda na kila kiongozi atakuwa amepata ujumbe.

Nilifanya makosa.

Nilifanya makosa kwa sababu nilidhani hii ni kazi rahisi kwa Rais. Nilidhani ni kazi ya kutimua huyu, kuondoa yule na kumleta yule mwingine. Nilidhani ni kazi ambayo akimaliza teuzi mbalimbali basi atakuwa ameipanga serikali yake kwa ajili ya kuchapa kazi.

Sasa najua kuwa uamuzi wake wa kushughulika na watu kwanza kabla ya mfumo ni jambo muhimu sana. Ulikuwa ni uamuzi sahihi na unajitahi kutetewa. Watu ndio hutengeneza mfumo; ni watu ndio ambao hukaa chini na kufanya maamuzi mbalimbali yenye kuathiri (kwa uzuri au ubaya) uwepo na utendaji wa mfumo wa utawala. Ukiwa na watu wabovu, wabinafsi na wenye mwelekeo wa ufisadi basi mfumo utakuwa mbovu, wa kibinafsi na wenye uelekeo wa kifisadi kwa sababu moja kubwa; wale wenye kuiwamba ngoma ngozi huivutia kwao! Mfumo wetu wa utawala wa kifisadi ulitengenezwa na watawala wenye mwelekeo wa kifisadi. Matobo (siyo matundu) kwenye sheria zetu vilitengenezwa na watu ambao walijua wakiziba na wao watakuwa wamejizibia.

Magufuli asingeweza kutengeneza mfumo mwingine kwa kutumia watu wale wale walioutengeneza mfumo huu wa sasa na hasa kama watu hao ni wanufaika wa mfumo huu. Ingelikuwa ni sawa sawa na kumtaka Rais awalazimishe watu wakate matawi ambayo wamekalia huku wakijua kwa kufanya hivyo wataangukia mtoni kwenye mamba wengi. Hakukuwa na jinsi nab ado hakuna jinsi ni lazima kuwaondoa hawa na kuwashughulikia ili kuleta watu wenye fikra zinazoakisi mwelekeo wa serikali yake.

Ni kwa sababu hiyo, kumbe kazi ile ya miezi sita kwa kweli haiwezekani. Ni kazi ambayo inapaswa kuwa endelevu na yenye matokeo bora. Tayari tumeanza kuona dalili za yaliyomo ndani ya ripot ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) na tayari inatisha kama ilivyotisha mwaka 2006 na miaka iliyofuatia.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukijulishwa juu ya uchafu wa watendaji wetu na taasisi zetu na mara karibu hizo zote tumekuwa tukionesha kushtushwa na kusikitishwa tukiamini kuwa labda mwaka unaofuatia mambo yatakua tofauti. CAG aliyepita alikuwa anarudia baadhi ya hoja mwaka baada ya mwaka na wakati mwingine kuhusiana na taasisi au watu wale wale. Na safari hii tusije kushangaa kuwa hata CAG wa sasa anaweza kujikuta amegusa maeneo yale yale; matumizi mabaya ya sheria ya manunuzi ya umma, fedha kutumiwa bila maelezo, kutopatikana kwa vitabu vya masuala ya fedha wakati wa ukaguzi, na upotevu wa fedha za umma kwa namna ambayo inadokeza tu kuwa zimeliwa.

Magufuli basi ana kazi kubwa; kushughulikia viongozi wabadhirifu, wazembe, wezi, na wenye kutumia madaraka yao vibaya na wakati huo huo kupanga na kusimamia serikali yake huku akiuunda upya mfumo uliojaribiwa na kuharibiwa.

Kwa mwendo alioanza nao hakuna shaka yoyote jambo moja lilikuwa sahihi kwa upande wangu; kuunga mkono mabadiliko haya. Wapo wanadhani hali ni ngumu sasa na kuwa serikali inabana naamini bado hatujaona hasa ugumu kwani hadi hivi sasa bado serikali inahangaika na madudu ya nyuma na yanatisha. Kusahihisha uchumi (correcting an economy) ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) haiwezekani kuwa ni jambo moja.

Ni kwa sababu hiyo naamini:

1. Kuanza kazi kwa mahakama za kushughulikia ufisadi na uhujumu uchumi kunahitajika mara moja

2. Sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema zaidi ili CAG awe na madaraka ya kutoa agizo la kusimamishwa kazi na hata kufikishwa mahakamani kwa mtendaji yeyote wa umma ambaye uchunguzi wake (CAG) unaonesha kuwa kuna uvunjaji wa sheria. Ikiwezekana ofisi ya CAG iwe na Waendesha mashtaka wake kama ilivyo kwa TAKUKURU. Haipaswi madudu yam waka mzima yanasubiri mwaka mwingine kujulikana. CAG anapofanya ukaguzi na kukuta madudu na ushahidi wa kisayansi upo (forensic evidence) basi hatua zichukuliwe mara moja. Siyo awe na uwezo wa kupeleka mashtaka lakini kwa kupendekeza kwa DPP au hata yeye mwenyewe washutumiwa watiwe mbaroni, mali zao zinazohusiwa kupatikana kwa njia haramu kukamatwa ili zije kufilisiwa wakikutwa na hatia.

3. Sheria ya Usalama wa Taifa inahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka – hili ni jambo ambalo limekuwa katika mada zangu kwa karibu miaka kumi sasa. TISS bado ni dhaifu sana na udhaifu wake umechangia sana kutamalaki kwa utamaduni wa kifisadi. Natumaini Magufuli hatochukua muda mrefu kuifumua hii taasisi kwani ndio moyo wa taifa. Ikilegea taifa liko mashakani.

Kuna na mengine mengi ambayo naamini Magufuli atayafanya kwani tayari ameshaanza kuyafanya na kuwa endapo atafanikiwa tutakapofika mwisho wa mwaka huu kama taifa tutashusha pumzi kidogo kwani angalau tutakuwa katika mazingira ya kusema “kweli hakika huyu alikuwa anahitajika”.

Ni wazi pia kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema “hapana” na waleta “vikwazo”. Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu. La maana ni kukaza mwenzo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikani, na nidhamu ili hatimaye Ujenzi Mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni Zama Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu.

Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.
Kijana boghohe a.k.a mwanakiji, kweli jiemanini wewe ulikuwa unataka nchi iendelee, haukuwa mpinzani pasipo hoja, ila ulikuwa mpinzani kwa kuwa uliokuwa unaona mwenendo wa nchi hii hauko pouwa hasa kutoka kwa wanaccm.
Kwa andiko hili kijana nakuunga mkono, umeliandika kizalendo na kiusomi zaidi... Yaani ningekuwa na uwezo basi ningemwambia Magufuli akusikilize unachokisea.
Hapa hauko Chdm wala hauko ccm ila uko kitaifa zaidi. Na hii ndio vijana tunatakiwa tuwe. Sio kukosoa kila kinachofanywa eti kwa kuwa ni serikali ya CCM ndio inafanya.
Naamini mambo yamebadilika, maana nimemsikia hata MBOWE anasifia bajeti ya serika kwa kusema kwa mwafa ya kwanza ndio tumeona bajeti ya maendeleo imepanda na kufikia 40%.
Na leo wewe kijana ninayekufaham kuanzia darasani hadi kiitikadi unaleta post ya akili namna hii, naamini vijana wengine tubadilike, tukosoe pale tunapoina pana kosa na kupongeza pale inapofamywa cha maana na pia tushauri pale tunapoona ikiwa hivi itafaa.....
Big up kaka...

Kijana boghohe a.k.a mwanakiji, kweli ni eamini wewe ulikuwa unataka nchi iendelee, haukuwa mpinzani pasipo hoja, ila ulikuwa mpinzani kwa kuwa ulikuwa unaona mwenendo wa nchi hii hauko pouwa hasa kutoka kwa wanaccm.
Kwa andiko hili kijana nakuunga mkono, umeliandika kizalendo na kiusomi zaidi... Yaani ningekuwa na uwezo basi ningemwambia Magufuli akusikilize unachokisema.
Hapa hauko Chdm wala hauko ccm ila uko kitaifa zaidi. Na hii ndio vijana tunatakiwa tuwe. Sio kukosoa kila kinachofanywa eti kwa kuwa ni serikali ya CCM ndio inafanya.
Naamini mambo yamebadilika, maana nimemsikia hata MBOWE anasifia bajeti ya serika kwa kusema kwa mwafa ya kwanza ndio tumeona bajeti ya maendeleo imepanda na kufikia 40%.
Na leo wewe kijana ninayekufaham kuanzia darasani hadi kiitikadi unaleta post ya akili namna hii, naamini vijana wengine tubadilike, tukosoe pale tunapoina pana kosa na kupongeza pale inapofamywa cha maana na pia tushauri pale tunapoona ikiwa hivi itafaa.....
Big up kaka...
 
Leo umeongea kizalendo sana Mzee Mwanakijiji Rais anakazi ngumu sana, tatizo juhudi zake zinapata upinzani mkubwa sana. Wale tunaompinga tungejitahidi kupongeza hizi jitihada na kushauri nini kifanyike badala ya kubeza na kudharau kila jitihada anazozifanya. Tukumbuke kwamba kila kitu kina hatua na hauwezi kuleta maendeleo au kubadilisha hali mbaya kuwa hali nzuri kwa usiku mmoja.
kuchallenge ni moja ya vitu vya muhimu sana kwa ufanyaji kaz wa kiongoz wa juu wa nchi fulani aliyemadarakani.....
haiwezekani kila mtanzania akawa anasifu tu juhudi za jpm kisa ni rais wa nchi yetuuuu.........
kupitia kupondwa kwake ndo kutamfanya, afanye kazi kwa weledi na tathmini kubwa ili watu wale wanaomponda na kumchallenge wasipate nafas ya kumchallenge,.hapo ndipo rais wetu atakapofanya kazi vizuri na kwa weledi uliotukuka
na kuleta vitu tofauti tofauti na kumridhisha kila mTZ mwenye haki na taifa lake...............
 
Mtu ambaye hana principle iliyokuwa based kwenye rule of law and the right economic theory hawezi kutengeneza mfumo sahihi.
Exactly ! ndicho wengi wasichoelewa . Tunajukumu la kusaidiana katika weledi

Twiga walipandishwa 'business class' kuelekea Qatar.
Wakakamatwa walinzi tukaambiwa issue inashughulikiwa.

Majuzi, Tumbili nao wakaona no way pori linaboa lazima wachukue 'First class' kuelekea uholanzi.

Kwa mtu anayefikiri lazima ajiulize, kwanini haya yanajirudia?
Ni lazima ajiulize, tuna mfumo wa kubaini tatizo na kulizuia ?

Mwenye fikra atajiuliza, hivi walinzi wa mageti ndiyo tatizo la wanyama kupelekwa nje ?
Hatujiulizi, mfumo wetu wa usalama upo sahihi?

Jipu likatumbuliwa muhimbili , miezi miwili jipu likaiva muhimbili kwa akina mama
Mtu mwenye fikra atajiuliza, tatizo ni kitu gani hali hii inajirudia?

Tunaambiwa PCCB wamefanya kazi yao, mafaili yapo kwa DPP.
DPP hawezi kuwashughulikia waliobainika na PCCB. Tatizo ni nini?

Rais anapambana na rushwa, wabunge wanatuhuma za rushwa.
Tujiulize mapambano yanahusu nini? Na kwanini wapo wasio tii sheria au kuziogopa?

Lazima tujiulize, tunachofanya ni sustainable? Na kwanini mambo yanajirudia?

Hawataki kusikia habari hizi, wanataka tufunge manyanga na kushangilia tu
 
Nguruvi3, huyo MsemajiUkweli anao ule unaoitwa ubishi wa kitoto. Kuna wakati kulitokea ndani ya CCM kundi lililojitambulisha Kama wapiganaji wa ndani. Tupo tuliowaomba waache usanii kwani hakuna mwenye akili anayeamua kukata tawi alokalia.

Yako matamshi ambayo Magufuli kayatoa ambayo moja moja yanaonesha kwamba naye, kama waliomtangulia, katanguliza maslahi ya CCM badala ya taifa. Ametamba alivyo tayari kuwapa madaraka wanaolalamikiwa na wananchi na hasa wapinzani!

Kwa kushindwa kuwa unifier hakuna namna atafanikiwa kwani, ingawa wapinzani wanamkosoa hadharani, watakaomkwamisha ni hao hao makada wenzake ndani ya CCM kimya kimya. Magufuli anatuhitaji sisi tunaohoji utendaji wake wazi wazi kuliko wanafiki wanaomsifia hata pale anapoteleza.
 
Ni rahisi kuubadilisha mfumo lakini hauwezi kuubomoa mfumo.
Mfumo utabadilishwa na kubomolewa na KATIBA! Twansubiria Mheshimiwa Raisi AIIBUE katiba ya Wananchi (ile ya Warioba). Kila kitu kimewekwa WAZI. Kwa mfano moja ya maeneo yanayozungumziwa ni TUNU za Taifa. Hii yafanana na MIIKO ya Mwanachama wa CCM.Haya siyo tu yaesiginwa, yamepuuzwa na ciongozi wenyewe.. Tuanzie hapo...
 
Akili za wanaccm hizi,mfumo unaozungumzwa ni pamoja na namna tunavyowapata viongozi wetu,mfano huyu maraika wako Magufuli ilikuwaje hakuja 2005?
Watu wanaozungusha mikono wanapenda saana kuongelea kuhusu mfumo bila kuongelea committment, lakini tatizo la tz sio Suala la mfumo Bali committment, na ku prove this tuangalie Suala la Zuma na kashfa ya ujenzi wa nyumba yake binafsi kwa kutumia fedha za umma, ingawa mfumo wao ni mzuri kuliko wetu lakini kutokana na kutokuwepo kwa political will / committment ya wabunge wa ANC etc Ndio Maana impunity na mazagazaga yake yapo Huko SA
 
Nguruvi3, huyo MsemajiUkweli anao ule unaoitwa ubishi wa kitoto. Kuna wakati kulitokea ndani ya CCM kundi lililojitambulisha Kama wapiganaji wa ndani. Tupo tuliowaomba waache usanii kwani hakuna mwenye akili anayeamua kukata tawi alokalia.

Yako matamshi ambayo Magufuli kayatoa ambayo moja moja yanaonesha kwamba naye, kama waliomtangulia, katanguliza maslahi ya CCM badala ya taifa. Ametamba alivyo tayari kuwapa madaraka wanaolalamikiwa na wananchi na hasa wapinzani!

Kwa kushindwa kuwa unifier hakuna namna atafanikiwa kwani, ingawa wapinzani wanamkosoa hadharani, watakaomkwamisha ni hao hao makada wenzake ndani ya CCM kimya kimya. Magufuli anatuhitaji sisi tunaohoji utendaji wake wazi wazi kuliko wanafiki wanaomsifia hata pale anapoteleza.
Mkuu ukitaka kuwatwala Watanzania ni kuwaeleza habari wanzotaka kusikia wao

Wenzetu hutafuta chanzo na kukifanyia kazi. Mdororo wa uchumi wa 2008(Recession) waliohusika 'wametumbuliwa.

Hiyo haikuwa habari kubwa kama Dodd-Frank act , sheria inayolenga kuzuia madhara

Visa zilipogundulika kwa passport feki, wenzetu hawakuhangaika kukamata waliofoji, waliweka electronic chips.

Nazo wameona zina walakini, sasa hivi ni Biometric

Hawahangaiki na wafoji passport, wanaangalia mfumo mzima umelegea wapi

Sisi wanyama wamekamatwa kiwanja cha KIA. Hatukuangalia mfumo mzima kuwa inakuwaje Polisi, usalama wa Taifa, askari wanyama pori, mkuu wa hifadhi, kamati ya mkoa ya ulinzi na usalama, wizara, uhamiaji, jeshi , wakashindwa kubaini dege kutua KIA?

Kwavile hatuangalii nyuma, Juzi tumbili wamekamatwa pale pale KIA.

Badala ya kujiuliza imekuwaje, tulijifunza nini, tupo bize kushangilia majipu

Tumepigwa Richmond, Dowans, Kagoda n.k. Hatujifunzi kuwa kuna tatizo katika mfumo

Wajanja wakaturudi kwa Escrow. Hatujiulizi tu, tunafunga manyanga vifua mbele

Rais yupo bize na majipu, wabunge wanatenda yao.

Tena walitumia siku 2 kujadili hotuba yake na kumsifia.
Kumbe, wana mng'ong'a wanajua udhaifu wa mfumo

Tupo bize tukihimiza akina mama wafunge vibwebwe tuselebuke kwa rythm ya majipu

Ukitaka kuona ubaya wa mfumo, jiulize uhuni uliotokea visiwani
Mtu anageuka kuwa katiba, nchi inaendeshwa kwa maoni ya mtu si katiba

Wabaya ni wanao onyesha tatizo, ''wazalendo'' wametulia Dodoma wanavuta rushwa
 
Napingana na maoni yako. Nyumba imara huanzia kweye msingi. Nyumba yetu imechakaa, Ina nyufa, na unatikisika. Anachofanya magu ni kuondoa baadhi ya bâti ailizooza sana, kupaka rangi kuta zenye nyufa na kuwaita wanakijiji waje kupiga picha na kushangilia.
Hivi magufuri ana ubavu Wa kuvunja mitandao ya kiharifu inayoongozwa na viongozi Wakuu Wa chama chake Kama ujangiri , mdawa ya kulevya nk. Tusidanganyane, mfumo ndio msingi kwanza mengine yatafuata. Tuache kushangilia maigizo.

Asante Mkuu, hakika wanaoshangilia hawaifahamu CCM. Pia nimependa mchango mmoja hapo juu "Muda utatuambia"
 
Naomba muitafakari hii mifano miwili;
  1. Marekani Raisi Obama hana mamlaka ya kuamuru vyombo vya dola kumkamata raia hata akiwa kibaka, lakini hapa Tanzania Makonda DC wa Kinondoni anaweza kuwaamuru Polisi kumkamata raia hata kama ni Mbunge na kumsweka ndani!
  2. Polisi wa Tanzania atasita kumkamata balozi wa nyumba kumi wa CCM hata akiwa kibaka mpaka apate idhini ya Wakubwa zake lakini hatasita kumkamata Kiongozi wa upinzani kwa kosa dogo hata kama ni Mwakilishi wa kitaifa.
Nimetoa hii mifano miwili tu katika mingi hapa Tanzania na yote inasababishwa na mfumo mbovu.
 
Gazeti la kila wiki liliwahi kuandika, sakata la KIA kwa undani. Mmoja wa waliotoa vibali ni katibu mkuu wa kitengo nyeti. Watanzania wajiulize, DCI, DPP,IGP, PCCB kwa pamoja wanaweza kufanya uchunguzi wa katibu huyo?

Watanzani wakitaka kujua mfumo wetu ni mbovu sana wajiulize. Mkuu wa mkoa anawajibika kwa nani? Na kwanini.

Katibu tawala na Mkurugenzi wana kazi zipi tofauti katika maeneo yao

Watanzania na wale wasiaomini mfumo ni tatizo, watueleze kuna 'guideline' gani za kumpata mkuu wa mkoa, mkuu wa Wilaya?

Kama hakuna guideline, hao wanaingiaje katika system? (Mfumo). Hapa wajiulize, hawa ni sehemu ya 'mfumo mzuri tulio nao' wameingia kwa vigezo gani?

Kama hakuna vigezo Watanzania wajiulize, mfumo unatengenezwajwe? I mean mtu mmoja hawezi kutengeneza mfumo wa nchi. Mfumo unatengeneza na wananchi
Je ndivyo ilivyo ?

Mtakumbuka wakuu wa Wilaya ni nafasi za shukrani.
Wasiojua mfumo ni mbovu kwa kiasi gani waangalie ukuu wa Wilaya

Kwavile hakuna mfumo, yule Dr aliyeandika katiba mpya akapewa zawadi ya ujumbe wa bodi 'bahari'. Yule dada aliyeandika katiba pendekezwa kama mwanasheria akazawadiwa ujumbe ya bodi hiyo

Wote wawili ni washiriki wa timu iliyoua ''bahari''
Waliula Taifa likaingia hasara, kisha majipu tunashangilia. Hatujiulizi tulifikaje pale
 
john-magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa baadhi yetu tuliokataa kuvingirisha mikono yetu kuunga mkono mabadiliko yaliyobinafsishwa kwa mtu mmoja tulijikuta hatuna budi kumuunga mkono Magufuli tukiamini anawakilisha mabadiliko ya kweli. Binafsi niliamini kabisa kuwa Taifa lilikuwa linamhitaji kiongozi kama Magufuli kuweza kulinasua mahali lilipo kuliko kiongozi yule mwingine toka upinzani. Niliamini kabisa kuwa Magufuli akishika madaraka atakuwa na kazi kubwa ya kulirejesha Taifa katika misingi yake ambayo inaonekana ilikuwa imepotea.

Hatua zake mbalimbali za mwanzo kushughulika na kubana matumizi, kupambana na ufisadi na kuondoa watendaji mizigo a.k.a majipu kulinifanya niamini kabisa kuwa Magufuli kazi aliyonayo akiendelea na kasi hiyo basi ndani ya miezi sita tu atakuwa ameleta heshima katika utumishi wa umma, kurejesha heshima kwa Watanzania na fahari ya taifa letu kurudishwa. Niliamini kabisa kuwa Magufuli atafanya kazi hii bila woga, huruma, husuda, wivu, au kusita sita. Kwamba, hatomwangalia yeyote, popote na kwa lolote. Ndani ya miezi sita hivi na kabla ya ujio wa bajeti ya kwanza ya serikali yake basi Magufuli atakuwa ameshaweka alama za namna gani taifa linataka kwenda na kila kiongozi atakuwa amepata ujumbe.

Nilifanya makosa.

Nilifanya makosa kwa sababu nilidhani hii ni kazi rahisi kwa Rais. Nilidhani ni kazi ya kutimua huyu, kuondoa yule na kumleta yule mwingine. Nilidhani ni kazi ambayo akimaliza teuzi mbalimbali basi atakuwa ameipanga serikali yake kwa ajili ya kuchapa kazi.

Sasa najua kuwa uamuzi wake wa kushughulika na watu kwanza kabla ya mfumo ni jambo muhimu sana. Ulikuwa ni uamuzi sahihi na unajitahi kutetewa. Watu ndio hutengeneza mfumo; ni watu ndio ambao hukaa chini na kufanya maamuzi mbalimbali yenye kuathiri (kwa uzuri au ubaya) uwepo na utendaji wa mfumo wa utawala. Ukiwa na watu wabovu, wabinafsi na wenye mwelekeo wa ufisadi basi mfumo utakuwa mbovu, wa kibinafsi na wenye uelekeo wa kifisadi kwa sababu moja kubwa; wale wenye kuiwamba ngoma ngozi huivutia kwao! Mfumo wetu wa utawala wa kifisadi ulitengenezwa na watawala wenye mwelekeo wa kifisadi. Matobo (siyo matundu) kwenye sheria zetu vilitengenezwa na watu ambao walijua wakiziba na wao watakuwa wamejizibia.

Magufuli asingeweza kutengeneza mfumo mwingine kwa kutumia watu wale wale walioutengeneza mfumo huu wa sasa na hasa kama watu hao ni wanufaika wa mfumo huu. Ingelikuwa ni sawa sawa na kumtaka Rais awalazimishe watu wakate matawi ambayo wamekalia huku wakijua kwa kufanya hivyo wataangukia mtoni kwenye mamba wengi. Hakukuwa na jinsi nab ado hakuna jinsi ni lazima kuwaondoa hawa na kuwashughulikia ili kuleta watu wenye fikra zinazoakisi mwelekeo wa serikali yake.

Ni kwa sababu hiyo, kumbe kazi ile ya miezi sita kwa kweli haiwezekani. Ni kazi ambayo inapaswa kuwa endelevu na yenye matokeo bora. Tayari tumeanza kuona dalili za yaliyomo ndani ya ripot ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) na tayari inatisha kama ilivyotisha mwaka 2006 na miaka iliyofuatia.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukijulishwa juu ya uchafu wa watendaji wetu na taasisi zetu na mara karibu hizo zote tumekuwa tukionesha kushtushwa na kusikitishwa tukiamini kuwa labda mwaka unaofuatia mambo yatakua tofauti. CAG aliyepita alikuwa anarudia baadhi ya hoja mwaka baada ya mwaka na wakati mwingine kuhusiana na taasisi au watu wale wale. Na safari hii tusije kushangaa kuwa hata CAG wa sasa anaweza kujikuta amegusa maeneo yale yale; matumizi mabaya ya sheria ya manunuzi ya umma, fedha kutumiwa bila maelezo, kutopatikana kwa vitabu vya masuala ya fedha wakati wa ukaguzi, na upotevu wa fedha za umma kwa namna ambayo inadokeza tu kuwa zimeliwa.

Magufuli basi ana kazi kubwa; kushughulikia viongozi wabadhirifu, wazembe, wezi, na wenye kutumia madaraka yao vibaya na wakati huo huo kupanga na kusimamia serikali yake huku akiuunda upya mfumo uliojaribiwa na kuharibiwa.

Kwa mwendo alioanza nao hakuna shaka yoyote jambo moja lilikuwa sahihi kwa upande wangu; kuunga mkono mabadiliko haya. Wapo wanadhani hali ni ngumu sasa na kuwa serikali inabana naamini bado hatujaona hasa ugumu kwani hadi hivi sasa bado serikali inahangaika na madudu ya nyuma na yanatisha. Kusahihisha uchumi (correcting an economy) ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) haiwezekani kuwa ni jambo moja.

Ni kwa sababu hiyo naamini:

1. Kuanza kazi kwa mahakama za kushughulikia ufisadi na uhujumu uchumi kunahitajika mara moja

2. Sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema zaidi ili CAG awe na madaraka ya kutoa agizo la kusimamishwa kazi na hata kufikishwa mahakamani kwa mtendaji yeyote wa umma ambaye uchunguzi wake (CAG) unaonesha kuwa kuna uvunjaji wa sheria. Ikiwezekana ofisi ya CAG iwe na Waendesha mashtaka wake kama ilivyo kwa TAKUKURU. Haipaswi madudu yam waka mzima yanasubiri mwaka mwingine kujulikana. CAG anapofanya ukaguzi na kukuta madudu na ushahidi wa kisayansi upo (forensic evidence) basi hatua zichukuliwe mara moja. Siyo awe na uwezo wa kupeleka mashtaka lakini kwa kupendekeza kwa DPP au hata yeye mwenyewe washutumiwa watiwe mbaroni, mali zao zinazohusiwa kupatikana kwa njia haramu kukamatwa ili zije kufilisiwa wakikutwa na hatia.

3. Sheria ya Usalama wa Taifa inahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka – hili ni jambo ambalo limekuwa katika mada zangu kwa karibu miaka kumi sasa. TISS bado ni dhaifu sana na udhaifu wake umechangia sana kutamalaki kwa utamaduni wa kifisadi. Natumaini Magufuli hatochukua muda mrefu kuifumua hii taasisi kwani ndio moyo wa taifa. Ikilegea taifa liko mashakani.

Kuna na mengine mengi ambayo naamini Magufuli atayafanya kwani tayari ameshaanza kuyafanya na kuwa endapo atafanikiwa tutakapofika mwisho wa mwaka huu kama taifa tutashusha pumzi kidogo kwani angalau tutakuwa katika mazingira ya kusema “kweli hakika huyu alikuwa anahitajika”.

Ni wazi pia kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema “hapana” na waleta “vikwazo”. Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu. La maana ni kukaza mwenzo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikani, na nidhamu ili hatimaye Ujenzi Mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni Zama Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu.

Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.
Na yeye alivyokudhania kumbe sivyo
 
Ole Sendeka amshukia Lowassa, asema ni muongo

Hapo kuna barua na tamko la CCM kutoka kwa Bw Sendeka
Sina tatizo na hoja au maoni ya CCM kwasababu ni maoni yao na wana haki ya kusema

Nilichotaka ni kumkumbusha Mzee Mwanakijiji kuwa CCM wanaamini mfumo ni mzuri sana na unafanya kazi vizuri kama tulivyowahi kusema, wamethibitisha

Wakati CCM wakiamini mfumo ni imara, MM anataka sheria ya CAG ifanyiwe kazi haraka na TISS mapema sana. Naiona hoja ya MM japo siafiki kutia viraka

Ni kwa mantiki hii tunasema, watu wale wale waliotufikisha hapa hawawezi kuona jambo tofauti kwasababu wamezoea kuishi kwa mazoea katika mazingira waliyozoea ambayo kwao ni mazuri tangu tupate uhuru, kwasababu tu matumbo yanavimba

Katika hali hii, Magufuli atatumbua majipu mfululizo, hoja za MM hata zile za viraka akina Sendeka hawazifikirii kabisa, mfumo ni mzuri tuendelee kama tulivyoachiwa na waasisi!!!

MsemajiUkweli Mag3
 
Mimi binafsi ingawa ninayafurahia haya yanayofanywa na Magufuri ingawa sikumpa kura yangu....lakini bado ninaamini kuwa mabadiliko ya kweli kwenye nchi hayatapatikana mpaka pale tutakapokuwa na katiba mpya itakayowawajibisha viongozi wasio waadirifu.....

Nchi hii ina mifumo mibovu ya utoaji na sheria kiasi kwamba hadi mshitakiwa wa kosa kubwa kama la utakatishaji wa fedha chafu lakini akifikishwa mahakamani anatabasamu......
Unaweza kukuta kuna kesi nzito sana ambayo itaunguruma kwa zaidi ya mwaka lakini utakuja kustaajabu hiyo hukumu yake.....wengine tumewaona wakikutwa na hatia za matumizi mabaya ya ofisi za umma lakini wanakuja kupewa adhabu za kufagia mahospitalini....

Haya ni baadhi ya madhaifu ya sheria zetu.....ni dhahiri kuwa hatupo makini na suala zima ufisadi na ndio matatizo haya yamekuwa sugu kwa kuwa yanafugwa na mifumo yetu mibovu iliyojaa rushwa.....
 
Penye Blue hawana habari kabisa kuwa Magufuli katokea wapi? wanjuta ila ndio hivyo mkuu!!!!!
Acha kujifaliji kwani Magufuli sio CCM? CCM ilikaa na kuchambua wagombea wake akaonekana Magufuli anafaa sasa sijui we mwenzetu unajua vipi kwamba CCM na JK hawamtambui Magufuli au vipi[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Mkuu, bado uko pale pale tu unajaribu kuainisha matatizo halafu unamalizia kwa kusema mfumo umeoza.

Nikikuuliza ni mfumo upi hauna matatizo unaniambia huwezi kuzungumza tena kuhusu mfumo.

Hakuna anayekataa kuwa Tanzania kama nchi tuna matatizo. Ieleweke pia hata nchi zilizoendelea zina matatizo pamoja na uwepo wake ndani ya mfumo kama nchi kwa miaka mingi kabla yetu.

Kujenga mfumo imara ni mchakato endelevu. Hata nchi zilizoendelea bado mpaka sasa zinajenga na kujaribu kuimarisha mifumo yake.

Tulianza kuujenga mfumo wetu tokea siku tulipopata uhuru na tunaendelea kuujenga na kuuimarisha.

Tuacheni siasa za kinadharia na porojo.

Bado ninasubiri majibu yangu ya bandiko namba 127

Msemakweli, nadhani kuna ujumbe unaufunika kwa sababu fulani au kwa makusudio fulani. Kitu kunachosisitizwa hapa ni hicho ulichokitaja kuwa kujenga mfumo imara nimchakato endelevu, lakini tunachosisitiza wengine hapa ni siyo tu ni mchakato endelevu bali ili mfumo ufanikiwe na uende haraka ni lazima uwe SHIRKISHI.
Kwa sasa hivi imeonekana wazi kuwa kasi ya kuimarisha mfumo haipo na kama ikitokea umesonga mbele, husonga hatua sita na kurudi nyuma hatua kumi. Na hii inasababishwa na ukweli kuwa hatuna katiba ya nchi bali Itikadi ya chama iliyobatizwa na kuitwa Katiba ya Nchi na mfumo hali kadhalika siyo wa Taifa ni wa Chama!
 
Back
Top Bottom