Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Mzee Mwanakijiji, nadhani tuna haja ya kurejea jalalani, tukacharure takataka mpaka tuikute ile katiba tuliyo itupa kule, katiba ya yule Waziri Mkuu wa zamani.
Tuzifuate zile tunu za Taifa, Taifa letu kitakuwa limepata chanjo, tiba na kinga

You have said it all. Katiba mbovu haiwezi kuzaa mifumo mizuri.
Utendaji wa Rais na wasaidizi wake huzingatia katiba.
Sheria hutungwa kuzingatia katiba.
Katiba mbovu huzaa sheria mbovu, mifumo mibovu, uwajibikaji mbovu. Mbaya pia huwafanya raia washindwe kuiwajibisha serikali na watawala.
 
Kwa mgeni unaweza kuona hatuna mbadala.Kwa wazoefu wanajua tunasema nini

Miaka michache iliyopita tulikemea safari za Rais. Tulisema tunazo resources za kutosha hatuhitaji kuhemea vibaba. Akina Mh Magufuli wakasema ziara za Rais zina manufaa, hivi karibuni baada ya MCC wanasema tuanze kujitegemea!!!

Tliwahi kusema bandari yetu ina operate chini ya kiwango na kwamba tuna bandari ambazo tukizutumia vyema tutanufaika. Walioshindwa kutuelewa walisema nadharia tu, leo akina Magufuli wanafanya tulichokizungumza miaka 5 iliyopita

Tunasema hivi, lazima kwanza ufumue mfumo mzima, uweke structure itakayohakikisha kila mmoja ana wajibika, ana maadili na uzalendo. Huo ni mbadala wa majipu.
Hilo jaliwezekani kwasababu wakati tunazungumzia katiba mpya, Magufuli alikuwa upande wa mfumo, of course bado yupo. Hivyo kutumbua majipu ni njia ya mkato,haina suluhusisho la kudumu

Huwezi kutumbua majipu ukiwa huna taratibu endelevu za kuzuia isitokee tena na ikitokea wahusika wanawajibishwa. Huo ndio mbadala si kuhangaika na issue moja moja

Magufuli alipokwenda Muhimbili na kumfukuza mkurugenzi, wengi walisema jipu limetumbuliwa.
Tuliokuwa na mawazo tofauti tulisema kuwa haiwezekani tatizo liwe mkurugenzi pekee.
Je hazina walifanya kazi yao? Je wizara ya afya walifanya kazi yao?

Miezi miwili Mgufuli karudi muhimbili na kukuta akina mama wakilala karibu na maji ya chooni.
Tatizo si mashine za MRI au maji, ni kwanini hayo yanatokea? Tukamwambia aangalie mfumo mzima kwanini akiondoka mambo yanarudi kama zamani.

Nimekupa mifano hiyo michache kati ya mingi kukuonyesha kuwa sisi wengine hatuimbi tuu !

Nimalizie kwa kukuambia kuwa, tulimwambia suala la ZNZ litatugharimu sote, wakati huo tukaonekana wana harakati. Je, hali ipoje sasa? Si kweli yametokea?

Sisi wenye uchungu na nchi na wazalendo tunashangilia jema na tunakosoa ubovu, hatushangilii tuu
Hii mifano yako haijibu maswali yangu ambayo yako kwenye bandiko namba 127.

Haya unayoyasema ni masuala ambayo lazima yatokee kwa sababu mfumo haushuki kutoka mbinguni na walinzi wa kuulinda.

Unajaribu kuwaaminisha wanaJF kuwa mfumo ni kama kitu fulani ambacho ukikiweka kila kitu kinakuwa absolutely perfect.

Uingereza pamoja na kuwepo kama taifa kwa miongo mingi, kila mara kunatokea scandal ndani ya serikali na kwenye vyama vya siasa. Siyo muda mrefu, wabunge wengi walifanikiwa kugushi risiti za malipo mbali mbali kwa miaka mingi bila kugunduliwa na kile unakiita mfumo.

Marekani nayo vivyo hivyo. Tumeshuhudia siyo mara moja dunia inajikuta kwenye matatizo ya kiuchumi yanayotikisa dunia na kujikuta mamilioni ya watu wanakosa kazi pamoja na uwepo wa mfumo.

...And the list goes on and on

Halafu unaposema tulisema hiki na kile kitatokea na kilitokea ni kupotosha wale ambao hawaangalii mantiki ya kile unakisema.

Hivi nikisema, Tanzania itafanya Uchaguzi Mkuu baada ya miaka mitano na kweli baada ya miaka mitano ikafanya Uchaguzi Mkuu. Ninaamini kuna watu wanaweza kunisifia kuwa nilichosema kimetokea lakini ukweli ni kuwa sheria na taratibu zinataka nchi kufanya Uchaguzi Mkuu baada ya miaka mitano.

Eti mtu anasema huyu mtoto baada ya mwaka atatembeana na kweli baada ya mwaka anatembea halafu anaanza kujisifu kuwa alisema atatembea baada ya mwaka. Kwa mtu asiyefahamu utaratibu wa maisha ya mtoto katika ukuaji anaweza kukusifu.

Matatizo ya Zanzibar yanafahamika miaka na miaka. Hata matokeo ya Uchaguzi huwa yanafahamika miaka na miaka kutokana na mazingira ya siasa za Zanzibar. Huwezi kuja hapa na kujidai eti ulitabiri mambo fulani yatatokea Zanzibar wakati inafahamika hata kabla ya kutokea.

Bado nasubiri majibu ya maswali yangu kwenye bandiko la 127.
 
Mungu akulinde na akupe maisha marefu Rais wangu.....! JPM uweze kurekebisha hi nchi!.....imeoza kabisa!
 
john-magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa baadhi yetu tuliokataa kuvingirisha mikono yetu kuunga mkono mabadiliko yaliyobinafsishwa kwa mtu mmoja tulijikuta hatuna budi kumuunga mkono Magufuli tukiamini anawakilisha mabadiliko ya kweli. Binafsi niliamini kabisa kuwa Taifa lilikuwa linamhitaji kiongozi kama Magufuli kuweza kulinasua mahali lilipo kuliko kiongozi yule mwingine toka upinzani. Niliamini kabisa kuwa Magufuli akishika madaraka atakuwa na kazi kubwa ya kulirejesha Taifa katika misingi yake ambayo inaonekana ilikuwa imepotea.

Hatua zake mbalimbali za mwanzo kushughulika na kubana matumizi, kupambana na ufisadi na kuondoa watendaji mizigo a.k.a majipu kulinifanya niamini kabisa kuwa Magufuli kazi aliyonayo akiendelea na kasi hiyo basi ndani ya miezi sita tu atakuwa ameleta heshima katika utumishi wa umma, kurejesha heshima kwa Watanzania na fahari ya taifa letu kurudishwa. Niliamini kabisa kuwa Magufuli atafanya kazi hii bila woga, huruma, husuda, wivu, au kusita sita. Kwamba, hatomwangalia yeyote, popote na kwa lolote. Ndani ya miezi sita hivi na kabla ya ujio wa bajeti ya kwanza ya serikali yake basi Magufuli atakuwa ameshaweka alama za namna gani taifa linataka kwenda na kila kiongozi atakuwa amepata ujumbe.

Nilifanya makosa.

Nilifanya makosa kwa sababu nilidhani hii ni kazi rahisi kwa Rais. Nilidhani ni kazi ya kutimua huyu, kuondoa yule na kumleta yule mwingine. Nilidhani ni kazi ambayo akimaliza teuzi mbalimbali basi atakuwa ameipanga serikali yake kwa ajili ya kuchapa kazi.

Sasa najua kuwa uamuzi wake wa kushughulika na watu kwanza kabla ya mfumo ni jambo muhimu sana. Ulikuwa ni uamuzi sahihi na unajitahi kutetewa. Watu ndio hutengeneza mfumo; ni watu ndio ambao hukaa chini na kufanya maamuzi mbalimbali yenye kuathiri (kwa uzuri au ubaya) uwepo na utendaji wa mfumo wa utawala. Ukiwa na watu wabovu, wabinafsi na wenye mwelekeo wa ufisadi basi mfumo utakuwa mbovu, wa kibinafsi na wenye uelekeo wa kifisadi kwa sababu moja kubwa; wale wenye kuiwamba ngoma ngozi huivutia kwao! Mfumo wetu wa utawala wa kifisadi ulitengenezwa na watawala wenye mwelekeo wa kifisadi. Matobo (siyo matundu) kwenye sheria zetu vilitengenezwa na watu ambao walijua wakiziba na wao watakuwa wamejizibia.

Magufuli asingeweza kutengeneza mfumo mwingine kwa kutumia watu wale wale walioutengeneza mfumo huu wa sasa na hasa kama watu hao ni wanufaika wa mfumo huu. Ingelikuwa ni sawa sawa na kumtaka Rais awalazimishe watu wakate matawi ambayo wamekalia huku wakijua kwa kufanya hivyo wataangukia mtoni kwenye mamba wengi. Hakukuwa na jinsi nab ado hakuna jinsi ni lazima kuwaondoa hawa na kuwashughulikia ili kuleta watu wenye fikra zinazoakisi mwelekeo wa serikali yake.

Ni kwa sababu hiyo, kumbe kazi ile ya miezi sita kwa kweli haiwezekani. Ni kazi ambayo inapaswa kuwa endelevu na yenye matokeo bora. Tayari tumeanza kuona dalili za yaliyomo ndani ya ripot ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) na tayari inatisha kama ilivyotisha mwaka 2006 na miaka iliyofuatia.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukijulishwa juu ya uchafu wa watendaji wetu na taasisi zetu na mara karibu hizo zote tumekuwa tukionesha kushtushwa na kusikitishwa tukiamini kuwa labda mwaka unaofuatia mambo yatakua tofauti. CAG aliyepita alikuwa anarudia baadhi ya hoja mwaka baada ya mwaka na wakati mwingine kuhusiana na taasisi au watu wale wale. Na safari hii tusije kushangaa kuwa hata CAG wa sasa anaweza kujikuta amegusa maeneo yale yale; matumizi mabaya ya sheria ya manunuzi ya umma, fedha kutumiwa bila maelezo, kutopatikana kwa vitabu vya masuala ya fedha wakati wa ukaguzi, na upotevu wa fedha za umma kwa namna ambayo inadokeza tu kuwa zimeliwa.

Magufuli basi ana kazi kubwa; kushughulikia viongozi wabadhirifu, wazembe, wezi, na wenye kutumia madaraka yao vibaya na wakati huo huo kupanga na kusimamia serikali yake huku akiuunda upya mfumo uliojaribiwa na kuharibiwa.

Kwa mwendo alioanza nao hakuna shaka yoyote jambo moja lilikuwa sahihi kwa upande wangu; kuunga mkono mabadiliko haya. Wapo wanadhani hali ni ngumu sasa na kuwa serikali inabana naamini bado hatujaona hasa ugumu kwani hadi hivi sasa bado serikali inahangaika na madudu ya nyuma na yanatisha. Kusahihisha uchumi (correcting an economy) ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) haiwezekani kuwa ni jambo moja.

Ni kwa sababu hiyo naamini:

1. Kuanza kazi kwa mahakama za kushughulikia ufisadi na uhujumu uchumi kunahitajika mara moja

2. Sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema zaidi ili CAG awe na madaraka ya kutoa agizo la kusimamishwa kazi na hata kufikishwa mahakamani kwa mtendaji yeyote wa umma ambaye uchunguzi wake (CAG) unaonesha kuwa kuna uvunjaji wa sheria. Ikiwezekana ofisi ya CAG iwe na Waendesha mashtaka wake kama ilivyo kwa TAKUKURU. Haipaswi madudu yam waka mzima yanasubiri mwaka mwingine kujulikana. CAG anapofanya ukaguzi na kukuta madudu na ushahidi wa kisayansi upo (forensic evidence) basi hatua zichukuliwe mara moja. Siyo awe na uwezo wa kupeleka mashtaka lakini kwa kupendekeza kwa DPP au hata yeye mwenyewe washutumiwa watiwe mbaroni, mali zao zinazohusiwa kupatikana kwa njia haramu kukamatwa ili zije kufilisiwa wakikutwa na hatia.

3. Sheria ya Usalama wa Taifa inahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka – hili ni jambo ambalo limekuwa katika mada zangu kwa karibu miaka kumi sasa. TISS bado ni dhaifu sana na udhaifu wake umechangia sana kutamalaki kwa utamaduni wa kifisadi. Natumaini Magufuli hatochukua muda mrefu kuifumua hii taasisi kwani ndio moyo wa taifa. Ikilegea taifa liko mashakani.

Kuna na mengine mengi ambayo naamini Magufuli atayafanya kwani tayari ameshaanza kuyafanya na kuwa endapo atafanikiwa tutakapofika mwisho wa mwaka huu kama taifa tutashusha pumzi kidogo kwani angalau tutakuwa katika mazingira ya kusema “kweli hakika huyu alikuwa anahitajika”.

Ni wazi pia kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema “hapana” na waleta “vikwazo”. Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu. La maana ni kukaza mwenzo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikani, na nidhamu ili hatimaye Ujenzi Mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni Zama Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu.

Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.

Asante kwa uzalendo wako, hata hivyo CAG hawezi kuyafanya hayo unayosema, hawezi kuwa mshauri na mtoa hukumu, kazi yake ni kutoa maoni ya kitaalamu kuhusu mifumo na kutoa mapendekezo.Vyombo vingine vya kimamlaka zinatekeleza mapendekezo ya CAG.sEGREGATION OF DUTIES must be observed in a good Governance environment.
Labda ushauri wa kurekebisha sheria ya CAG uwe kwamba; CAG shall report administratively to the President and Functionally shall report to the Parliament na uteuzi wake uthibitishwe na bunge
 
Mungu amemuweka Magufuli kwa ajili ya kuvunja, kuharibu, kubomoa na kisha kujenga.
 
Hana la kufanya kwa makosa yaliyofanyika akiwa madarakani. Ila kama ni makosa baada ya kutoka madarakani Sheria inafuata mkondo wake.
Acha uongo mbona tulichukua mgodi wetu wa kiwira na mnunuzi alinunua akiwa madarakani.Fuatilia comments ujifunze badala ya ku-comment
 
Hii mifano yako haijibu maswali yangu ambayo yako kwenye bandiko namba 127.

Haya unayoyasema ni masuala ambayo lazima yatokee kwa sababu mfumo haushuki kutoka mbinguni na walinzi wa kuulinda.

Unajaribu kuwaaminisha wanaJF kuwa mfumo ni kama kitu fulani ambacho ukikiweka kila kitu kinakuwa absolutely perfect.

Uingereza pamoja na kuwepo kama taifa kwa miongo mingi, kila mara kunatokea scandal ndani ya serikali na kwenye vyama vya siasa. Siyo muda mrefu, wabunge wengi walifanikiwa kugushi risiti za malipo mbali mbali kwa miaka mingi bila kugunduliwa na kile unakiita mfumo.

Marekani nayo vivyo hivyo. Tumeshuhudia siyo mara moja dunia inajikuta kwenye matatizo ya kiuchumi yanayotikisa dunia na kujikuta mamilioni ya watu wanakosa kazi pamoja na uwepo wa mfumo.

...And the list goes on and on

Halafu unaposema tulisema hiki na kile kitatokea na kilitokea ni kupotosha wale ambao hawaangalii mantiki ya kile unakisema.

Hivi nikisema, Tanzania itafanya Uchaguzi Mkuu baada ya miaka mitano na kweli baada ya miaka mitano ikafanya Uchaguzi Mkuu. Ninaamini kuna watu wanaweza kunisifia kuwa nilichosema kimetokea lakini ukweli ni kuwa sheria na taratibu zinataka nchi kufanya Uchaguzi Mkuu baada ya miaka mitano.

Eti mtu anasema huyu mtoto baada ya mwaka atatembeana na kweli baada ya mwaka anatembea halafu anaanza kujisifu kuwa alisema atatembea baada ya mwaka. Kwa mtu asiyefahamu utaratibu wa maisha ya mtoto katika ukuaji anaweza kukusifu.

Matatizo ya Zanzibar yanafahamika miaka na miaka. Hata matokeo ya Uchaguzi huwa yanafahamika miaka na miaka kutokana na mazingira ya siasa za Zanzibar. Huwezi kuja hapa na kujidai eti ulitabiri mambo fulani yatatokea Zanzibar wakati inafahamika hata kabla ya kutokea.

Bado nasubiri majibu ya maswali yangu kwenye bandiko la 127.
Sirudi nyuma kuongelea jambo moja kila siku. Kama sieleweki au hawaelewi tuendelee kibubusa

Sikiliza ndugu yangu, katibu mkuu wa wizara anapokamatwa kwa rushwa akashindwa kushtakiwa maana yake nini? Vyombo husika vinafanya kazi zake?

Unajua wanyama walipitia KIA kwa mkono wa katibu'' mkuu'' mstaafu.

Kwasababu mfumo una matatizo, tumbili nao wamechukua pipa.

Maana yake ni kuwa ya KIA ilikuwa bahati mbaya, suala la wanyama lipo katika mfumo mahususi. Na hilo Magu hakugusi hata siku moja

Huwezi kuwa na DCI, DPP, TAKUKURU, IGP,CAG wasio na nguvu ukasema una mfumo sahihi.. Hawa wanapowajibika kwa mtu, wao si mfumo, mfumo ni mtu. Unaelewa hapa!

Mfumo hauwezi kuwa 100% lakini lazima tukubaliane na tunakubaliane kuwa mfumo uiopo umeoza karibu na 99% . Tutengeneze ambao ni 99% perfect

Hakuna mafanikio na ni tanuru la kufeli kama tutafikiri mfumo ni mtu na huu uliopo ni mzuri sana

Watu wale wale na mfumo ule ule hauwezi kutupa jibu tofauti.

Naenda kutafuta fanusi nitarudi saa sita mchana kuwamulikia baadhi yetu, nina uhakika jua linawaka lakini.....
 
Mwanakijiji nina tamani Magufuli angeiona hii thread yako. inatia moyo sana.
Pia niseme kuwa ndugu zangu kama Magufuli akishindwa kuitia hii mizizi ya rushwa na ufisadi, basi Tanzania haitapata kutokea kiongozi atakaetfanikiwa na tujue kuwa sisi na Tanzania yetu hatutafika popote na wala tusiwe na ndoto za kuendelea. Naamini Magufuli anaweza tumuunge mkono. tuwe na moyo wa kizalendo.
 
Sirudi nyuma kuongelea jambo moja kila siku. Kama sieleweki au hawaelewi tuendelee kibubusa

Sikiliza ndugu yangu, katibu mkuu wa wizara anapokamatwa kwa rushwa akashindwa kushtakiwa maana yake nini? Vyombo husika vinafanya kazi zake?

Unajua wanyama walipitia KIA kwa mkono wa katibu'' mkuu'' mstaafu.

Kwasababu mfumo una matatizo, tumbili nao wamechukua pipa.

Maana yake ni kuwa ya KIA ilikuwa bahati mbaya, suala la wanyama lipo katika mfumo mahususi. Na hilo Magu hakugusi hata siku moja

Huwezi kuwa na DCI, DPP, TAKUKURU, IGP,CAG wasio na nguvu ukasema una mfumo sahihi.. Hawa wanapowajibika kwa mtu, wao si mfumo, mfumo ni mtu. Unaelewa hapa!

Mfumo hauwezi kuwa 100% lakini lazima tukubaliane na tunakubaliane kuwa mfumo uiopo umeoza karibu na 99% . Tutengeneze ambao ni 99% perfect

Hakuna mafanikio na ni tanuru la kufeli kama tutafikiri mfumo ni mtu na huu uliopo ni mzuri sana

Watu wale wale na mfumo ule ule hauwezi kutupa jibu tofauti.

Naenda kutafuta fanusi nitarudi saa sita mchana kuwamulikia baadhi yetu, nina uhakika jua linawaka lakini.....
Mkuu, bado uko pale pale tu unajaribu kuainisha matatizo halafu unamalizia kwa kusema mfumo umeoza.

Nikikuuliza ni mfumo upi hauna matatizo unaniambia huwezi kuzungumza tena kuhusu mfumo.

Hakuna anayekataa kuwa Tanzania kama nchi tuna matatizo. Ieleweke pia hata nchi zilizoendelea zina matatizo pamoja na uwepo wake ndani ya mfumo kama nchi kwa miaka mingi kabla yetu.

Kujenga mfumo imara ni mchakato endelevu. Hata nchi zilizoendelea bado mpaka sasa zinajenga na kujaribu kuimarisha mifumo yake.

Tulianza kuujenga mfumo wetu tokea siku tulipopata uhuru na tunaendelea kuujenga na kuuimarisha.

Tuacheni siasa za kinadharia na porojo.

Bado ninasubiri majibu yangu ya bandiko namba 127
 
Mwanakijiji umekua msahaulifu sana na siasa za nchi hii, nakumbuka miaka kumi nyuma kila mtanzania aliiona Tanzania ya maishabora kwa wote iko mbeleyake ,hata sisi tuliokua wapinzani wa ccm tuliona mara hii kweli nchi itabadilika
Na pale JK alivyojaribu kubadilisha mawaziri kila baada ya muda ili kukabiliana na changamoto ambazo tulidhani zilimfanya Rais asifikie malengo ya maisha bora tulipata tamaa zaidi.

Lakini hatimayake nikuongezeka umasikini mitaani na kupanda uchumi ndani ya vitabu sio kwa wanachi wakawaida.

Nakusudia kusema Tanzania haitabadilika kama mfumo haujabadilika.
CCM bado ni kikwazo kwa Tanzania

Kila kiongozi anaekuja watu hupatatamaa kwa zile hadaa za miaka ya mwanzo.
Rudisha kumbukumbu tena miaka ishirini ya iliopita (Mkapa) utanielewa pengine.

Maneno haya yaweke kumbukumbu ili uje unisute baada ya muda wa magufuli kuisha.

Na natanguliza tena maneno 2025 ataibuliwa malaika mwengine kutoka ccm tutalisha maneno haya haya.

Kwakutumia vitendo ya miaka ya mwanzo vya Rais mtarajiwa.

Watanzania wenzangu mbona tunadanganywa kila siku na watu hawa hawa na sisi wengi tuliokosa elimu tunaburuza ila chakusikitisha na wasomi wetu pia huburuzwa tena wao ndio wanajifunga minyororo wenyewe,inakua afadhali ya sisi tusio na elimu !

Watanzania tunamatatizo gani?

hata usijali mkuu uchaguzi tu unaokuja utakuwa moto tofauti na matarajio ya wengi
 
Kwa maoni yangu JK kama binadamu mwingine yeyote ana haki ya kuwa na mapenzi na soka.Na akipata nafasi si vibaya kufurahisha nafsi yake kama alivyofanya.Siyo kwamba unapokuwa Rais basi wewe unaondoka na kujitenga na hobby zako.Iwapo tunajitahidi kutafuta mapungufu ya Kikwete,basi tufanye utafiti kwanza.Si vizuri kumtafutia mtu ubaya kwa hoja za kitoto.

Hivi vigezo vyako vya kumwita mtu genius ni vipya.
 
MMM Uchaguzi umeisha, huna haja ya kuendelea na maneno yako kuzungusha mikono sijui... Ni muda sasa umefika kutumia ule weledi wako kumshauri JPM kwa kiwango kile ulichokuwa unakitumia kuwashauri CDM.
Naamini JPM anahitaji sana ushauri wako kwa sasa Kwani ameonyesha nia kwa kiasi kikubwa ya kuisaidia nchi hii.
Nilikuwa na bado naikataa CCM kwa sababu bado naamini CCM ni ile ile... Ili hii nchi ivuke nliwahi kusema ni lazima JPM awageuke jamaa zake wa CCM... Hilo angalau anaelekea kuthubutu... Akiwaonea haya CCM wenzie then Hii kazi itamshinda. Tutaendelea kuimba kile kiwimbo chetu... Mbeleee kwa mbeleee...Wapinzani nchi hii baada ya Uchaguzi hawana madhara tena.
 
Muda ndo utakuwa mwamuzi!

Hakuna cha muda kuwa mwamuzi ulipaswa tu kutoa like kwa mwanakijiji kwa umahiri wake kwenye uzi huu.Pia nasema raisi Magufuli aufumue utaratibu na mamlaka makubwa ya DPP kwani hapa napo ni kichaka kingine cha rushwa kubwa kubwa.Hayo mamlaka haramu ya kuamua kuifuta au kutopeleka mashtaka yoyote mahakamani kwa uamuzi wake tu na bila kuhojiwa yalikuwa mamlaka haramu ya uongozi uliopita na tuseme wazi kwa tawala zote baada ya kifo cha Kambarage. Vinginevyo nami nimponge sana Mwanakijiji kwa uzi wake murua na wote tuendelee kumwombea raisi Magufuli kwa zoezi hili gumu na Mungu alie sirini amsimamie.
 
Well said MMM.

Queen Esther

john-magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa baadhi yetu tuliokataa kuvingirisha mikono yetu kuunga mkono mabadiliko yaliyobinafsishwa kwa mtu mmoja tulijikuta hatuna budi kumuunga mkono Magufuli tukiamini anawakilisha mabadiliko ya kweli. Binafsi niliamini kabisa kuwa Taifa lilikuwa linamhitaji kiongozi kama Magufuli kuweza kulinasua mahali lilipo kuliko kiongozi yule mwingine toka upinzani. Niliamini kabisa kuwa Magufuli akishika madaraka atakuwa na kazi kubwa ya kulirejesha Taifa katika misingi yake ambayo inaonekana ilikuwa imepotea.

Hatua zake mbalimbali za mwanzo kushughulika na kubana matumizi, kupambana na ufisadi na kuondoa watendaji mizigo a.k.a majipu kulinifanya niamini kabisa kuwa Magufuli kazi aliyonayo akiendelea na kasi hiyo basi ndani ya miezi sita tu atakuwa ameleta heshima katika utumishi wa umma, kurejesha heshima kwa Watanzania na fahari ya taifa letu kurudishwa. Niliamini kabisa kuwa Magufuli atafanya kazi hii bila woga, huruma, husuda, wivu, au kusita sita. Kwamba, hatomwangalia yeyote, popote na kwa lolote. Ndani ya miezi sita hivi na kabla ya ujio wa bajeti ya kwanza ya serikali yake basi Magufuli atakuwa ameshaweka alama za namna gani taifa linataka kwenda na kila kiongozi atakuwa amepata ujumbe.

Nilifanya makosa.

Nilifanya makosa kwa sababu nilidhani hii ni kazi rahisi kwa Rais. Nilidhani ni kazi ya kutimua huyu, kuondoa yule na kumleta yule mwingine. Nilidhani ni kazi ambayo akimaliza teuzi mbalimbali basi atakuwa ameipanga serikali yake kwa ajili ya kuchapa kazi.

Sasa najua kuwa uamuzi wake wa kushughulika na watu kwanza kabla ya mfumo ni jambo muhimu sana. Ulikuwa ni uamuzi sahihi na unajitahi kutetewa. Watu ndio hutengeneza mfumo; ni watu ndio ambao hukaa chini na kufanya maamuzi mbalimbali yenye kuathiri (kwa uzuri au ubaya) uwepo na utendaji wa mfumo wa utawala. Ukiwa na watu wabovu, wabinafsi na wenye mwelekeo wa ufisadi basi mfumo utakuwa mbovu, wa kibinafsi na wenye uelekeo wa kifisadi kwa sababu moja kubwa; wale wenye kuiwamba ngoma ngozi huivutia kwao! Mfumo wetu wa utawala wa kifisadi ulitengenezwa na watawala wenye mwelekeo wa kifisadi. Matobo (siyo matundu) kwenye sheria zetu vilitengenezwa na watu ambao walijua wakiziba na wao watakuwa wamejizibia.

Magufuli asingeweza kutengeneza mfumo mwingine kwa kutumia watu wale wale walioutengeneza mfumo huu wa sasa na hasa kama watu hao ni wanufaika wa mfumo huu. Ingelikuwa ni sawa sawa na kumtaka Rais awalazimishe watu wakate matawi ambayo wamekalia huku wakijua kwa kufanya hivyo wataangukia mtoni kwenye mamba wengi. Hakukuwa na jinsi nab ado hakuna jinsi ni lazima kuwaondoa hawa na kuwashughulikia ili kuleta watu wenye fikra zinazoakisi mwelekeo wa serikali yake.

Ni kwa sababu hiyo, kumbe kazi ile ya miezi sita kwa kweli haiwezekani. Ni kazi ambayo inapaswa kuwa endelevu na yenye matokeo bora. Tayari tumeanza kuona dalili za yaliyomo ndani ya ripot ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) na tayari inatisha kama ilivyotisha mwaka 2006 na miaka iliyofuatia.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukijulishwa juu ya uchafu wa watendaji wetu na taasisi zetu na mara karibu hizo zote tumekuwa tukionesha kushtushwa na kusikitishwa tukiamini kuwa labda mwaka unaofuatia mambo yatakua tofauti. CAG aliyepita alikuwa anarudia baadhi ya hoja mwaka baada ya mwaka na wakati mwingine kuhusiana na taasisi au watu wale wale. Na safari hii tusije kushangaa kuwa hata CAG wa sasa anaweza kujikuta amegusa maeneo yale yale; matumizi mabaya ya sheria ya manunuzi ya umma, fedha kutumiwa bila maelezo, kutopatikana kwa vitabu vya masuala ya fedha wakati wa ukaguzi, na upotevu wa fedha za umma kwa namna ambayo inadokeza tu kuwa zimeliwa.

Magufuli basi ana kazi kubwa; kushughulikia viongozi wabadhirifu, wazembe, wezi, na wenye kutumia madaraka yao vibaya na wakati huo huo kupanga na kusimamia serikali yake huku akiuunda upya mfumo uliojaribiwa na kuharibiwa.

Kwa mwendo alioanza nao hakuna shaka yoyote jambo moja lilikuwa sahihi kwa upande wangu; kuunga mkono mabadiliko haya. Wapo wanadhani hali ni ngumu sasa na kuwa serikali inabana naamini bado hatujaona hasa ugumu kwani hadi hivi sasa bado serikali inahangaika na madudu ya nyuma na yanatisha. Kusahihisha uchumi (correcting an economy) ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) haiwezekani kuwa ni jambo moja.

Ni kwa sababu hiyo naamini:

1. Kuanza kazi kwa mahakama za kushughulikia ufisadi na uhujumu uchumi kunahitajika mara moja

2. Sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema zaidi ili CAG awe na madaraka ya kutoa agizo la kusimamishwa kazi na hata kufikishwa mahakamani kwa mtendaji yeyote wa umma ambaye uchunguzi wake (CAG) unaonesha kuwa kuna uvunjaji wa sheria. Ikiwezekana ofisi ya CAG iwe na Waendesha mashtaka wake kama ilivyo kwa TAKUKURU. Haipaswi madudu yam waka mzima yanasubiri mwaka mwingine kujulikana. CAG anapofanya ukaguzi na kukuta madudu na ushahidi wa kisayansi upo (forensic evidence) basi hatua zichukuliwe mara moja. Siyo awe na uwezo wa kupeleka mashtaka lakini kwa kupendekeza kwa DPP au hata yeye mwenyewe washutumiwa watiwe mbaroni, mali zao zinazohusiwa kupatikana kwa njia haramu kukamatwa ili zije kufilisiwa wakikutwa na hatia.

3. Sheria ya Usalama wa Taifa inahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka – hili ni jambo ambalo limekuwa katika mada zangu kwa karibu miaka kumi sasa. TISS bado ni dhaifu sana na udhaifu wake umechangia sana kutamalaki kwa utamaduni wa kifisadi. Natumaini Magufuli hatochukua muda mrefu kuifumua hii taasisi kwani ndio moyo wa taifa. Ikilegea taifa liko mashakani.

Kuna na mengine mengi ambayo naamini Magufuli atayafanya kwani tayari ameshaanza kuyafanya na kuwa endapo atafanikiwa tutakapofika mwisho wa mwaka huu kama taifa tutashusha pumzi kidogo kwani angalau tutakuwa katika mazingira ya kusema “kweli hakika huyu alikuwa anahitajika”.

Ni wazi pia kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema “hapana” na waleta “vikwazo”. Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu. La maana ni kukaza mwenzo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikani, na nidhamu ili hatimaye Ujenzi Mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni Zama Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu.

Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.
 
Kwani tunaelekea wapi? Maana naona majipu tu no dira hata mpango wa miaka mitano umemshinda
 
Mtu ambaye hana principle iliyokuwa based kwenye rule of law and the right economic theory hawezi kutengeneza mfumo sahihi.
 
Kwani tunaelekea wapi? Maana naona majipu tu no dira hata mpango wa miaka mitano umemshinda
Hizo dira zishawekwa sana ila wajanja wachache wanakwamisha.

Anachofanya sasa rais ndio kitu sahihi kwa wakati sahihi. Ni kukata mirija kwanza then dira na mengineyo yatafuata.
 
Back
Top Bottom