Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Magufuli anafanya vizuri, tatizo kubwa Ni kuegemea said kwenye ujamaa, mfumo ambao ulifel kabla hata ya Nyerere kutoka madarakani, kingine Ni kupingana na nguvu zinazoendesha chumi za dunia....Magufuli needs strong minds and
smart advisers, ajenge system Mpya kabisa, anzia kwenye manunuzi ya umma, TISS, police, na public services..otherwise muda anaotumia kutoa huyu na kuweka yule utakuwa Ni kazi bure......
 
Watu wanaozungusha mikono wanapenda saana kuongelea kuhusu mfumo bila kuongelea committment, lakini tatizo la tz sio Suala la mfumo Bali committment, na ku prove this tuangalie Suala la Zuma na kashfa ya ujenzi wa nyumba yake binafsi kwa kutumia fedha za umma, ingawa mfumo wao ni mzuri kuliko wetu lakini kutokana na kutokuwepo kwa political will / committment ya wabunge wa ANC etc Ndio Maana impunity na mazagazaga yake yapo Huko SA
 
Mimi siwezi sema sana kwa Sasa, tarehe 30 mwezi wa Saba nitatoa ya moyoni, kwanza nione ataongeza ngapi kwa walimu kama yuko serious kweli. Naungana na Tundu Lissu kuwa ni mapema sana kumsifia Magufuli, sikilizeni wimbo wa kampeni ya CCM ulio sema CCM mbele kwabele, cccm ni ile ile na watu ni wale wale
 
Lakini Hiyo pay kwa waalimu si iendane na quality ya hao waalimu upe vs Voda fast vs failures Ndio wanakuwa waalimu ku wafundisha wengine vs quality ones
 
Ukiachilia hilo la kuwaombea wengine vifo, naunga mkono dua lako kwamba Mungu amsaidie kutekeleza majukumu yake bila upendeleo kwa haki na ampe hekima namna ya kupanga mipango endelevu kwa ukuaji wa uchumi wa taifa letu na maisha bora Ndg,natambua si busara kuomba kifo kwa ajili ya wengine.Nikili kughafirika.Lkn yote hayo nasababishwa na wao(WACHONGA NEEMA WASIOMAANISHA).Wanarubuni vijana kukili IMANI zao OVU.Wapo radhi lolote lile wafanye ili kujipatia madaraka.Wachafu ki-maadili na watuamishao ni wema na watetezi wetu.Hakika,mm nasononeshwa sana na wao!
 
Mzee M.M nakuunga mkono kwa asilimia zote.Nasubiri kwa hamu sana kuona JPM atafanya nini baada ya kuzipitia kwa ufasaha reports za CAG hasa kuhusu NSSF.I'm terribly heartbroken!
 
Magufuli anafanya vizuri, tatizo kubwa Ni kuegemea said kwenye ujamaa, mfumo ambao ulifel kabla hata ya Nyerere kutoka madarakani, kingine Ni kupingana na nguvu zinazoendesha chumi za dunia....Magufuli needs strong minds and
smart advisers, ajenge system Mpya kabisa, anzia kwenye manunuzi ya umma, TISS, police, na public services..otherwise muda anaotumia kutoa huyu na kuweka yule utakuwa Ni kazi bure......

Uko sahihi mkuu, kuna usemi wa Kichina unasema "Samaki huanza kuoza kwenye kichwa.." sasa nafikiri hizo idara zote ulizozitaja zimeharibika kutokana na awamu iliyopita, sasa hivi kila upande watu wanajitahidi kwenda na mwendo wa aliyeko madarakani. Naamini akiendelea kuonyesha hali hii ya kutokuvumilia uvundo na ufisadi, taratibu tutaanza kupiga hatua japo kazi ni kubwa.
 
Mzee M.M nakuunga mkono kwa asilimia zote.Nasubiri kwa hamu sana kuona JPM atafanya nini baada ya kuzipitia kwa ufasaha reports za CAG hasa kuhusu NSSF.I'm terribly heartbroken!

Huwezijua mkuu, huenda hiyo report ya CAG ndio imepelekea aliyekuwa DG wa NSSF kuhojiwa na TAKUKURU ikiashiria kwamba kuna uwezekano wa kufunguliwa mashtaka.
 
john-magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa baadhi yetu tuliokataa kuvingirisha mikono yetu kuunga mkono mabadiliko yaliyobinafsishwa kwa mtu mmoja tulijikuta hatuna budi kumuunga mkono Magufuli tukiamini anawakilisha mabadiliko ya kweli. Binafsi niliamini kabisa kuwa Taifa lilikuwa linamhitaji kiongozi kama Magufuli kuweza kulinasua mahali lilipo kuliko kiongozi yule mwingine toka upinzani. Niliamini kabisa kuwa Magufuli akishika madaraka atakuwa na kazi kubwa ya kulirejesha Taifa katika misingi yake ambayo inaonekana ilikuwa imepotea.

Hatua zake mbalimbali za mwanzo kushughulika na kubana matumizi, kupambana na ufisadi na kuondoa watendaji mizigo a.k.a majipu kulinifanya niamini kabisa kuwa Magufuli kazi aliyonayo akiendelea na kasi hiyo basi ndani ya miezi sita tu atakuwa ameleta heshima katika utumishi wa umma, kurejesha heshima kwa Watanzania na fahari ya taifa letu kurudishwa. Niliamini kabisa kuwa Magufuli atafanya kazi hii bila woga, huruma, husuda, wivu, au kusita sita. Kwamba, hatomwangalia yeyote, popote na kwa lolote. Ndani ya miezi sita hivi na kabla ya ujio wa bajeti ya kwanza ya serikali yake basi Magufuli atakuwa ameshaweka alama za namna gani taifa linataka kwenda na kila kiongozi atakuwa amepata ujumbe.

Nilifanya makosa.

Nilifanya makosa kwa sababu nilidhani hii ni kazi rahisi kwa Rais. Nilidhani ni kazi ya kutimua huyu, kuondoa yule na kumleta yule mwingine. Nilidhani ni kazi ambayo akimaliza teuzi mbalimbali basi atauwa ameipanga serikali yake kwa ajili ya kuchapa kazi.

Sasa najua kuwa uamuzi wake wa kushughulika na watu kwanza kabla ya mfumo ni jambo muhimu sana. Ulikuwa ni uamuzi sahihi na unajitahi kutetewa. Watu ndio hutengeneza mfumo; ni watu ndio ambao hukaa chini na kufanya maamuzi mbalimbali yenye kuathiri (kwa uzuri au ubaya) uwepo na utendaji wa mfumo wa utawala. Ukiwa na watu wabovu, wabinafsi na wenye mwelekeo wa ufisadi basi mfumo utakuwa mbovu, wa kibinafsi na wenye uelekeo wa kifisadi kwa sababu moja kubwa; wale wenye kuiwamba ngoma ngozi huivutia kwao! Mfumo wetu wa utawala wa kifisadi ulitengenezwa na watawala wenye mwelekeo wa kifisadi. Matobo (siyo matundu) kwenye sheria zetu vilitengenezwa na watu ambao walijua wakiziba na wao watakuwa wamejizibia.

Magufuli asingeweza kutengeneza mfumo mwingine kwa kutumia watu wale wale walioutengeneza mfumo huu wa sasa na hasa kama watu hao ni wanufaika wa mfumo huu. Ingelikuwa ni sawa sawa na kumtaka Rais awalazimishe watu wakate matawi ambayo wamekalia huku wakijua kwa kufanya hivyo wataangukia mtoni kwenye mamba wengi. Hakukuwa na jinsi nab ado hakuna jinsi ni lazima kuwaondoa hawa na kuwashughulikia ili kuleta watu wenye fikra zinazoakisi mwelekeo wa serikali yake.

Ni kwa sababu hiyo, kumbe kazi ile ya miezi sita kwa kweli haiwezekani. Ni kazi ambayo inapaswa kuwa endelevu na yenye matokeo bora. Tayari tumeanza kuona dalili za yaliyomo ndani ya ripot ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) na tayari inatisha kama ilivyotisha mwaka 2006 na miaka iliyofuatia. Kwa muda mrefu tumekuwa tukijulishwa juu ya uchafu wa watendaji wetu na taasisi zetu na mara karibu hizo zote tumekuwa tukionesha kushtushwa na kusikitishwa tukiamini kuwa labda mwaka unaofuatia mambo yatakua tofauti. CAG aliyepita alikuwa anarudia baadhi ya hoja mwaka baada ya mwaka na wakati mwingine kuhusiana na taasisi au watu wale wale. Na safari hii tusije kushangaa kuwa hata CAG wa sasa anaweza kujikuta amegusa maeneo yale yale; matumizi mabaya ya sheria ya manunuzi ya umma, fedha kutumiwa bila maelezo, kutopatikana kwa vitabu vya masuala ya fedha wakati wa ukaguzi, na upotevu wa fedha za umma kwa namna ambayo inadokeza tu kuwa zimeliwa.

Magufuli basi ana kazi kubwa; kushughulikia viongozi wabadhirifu, wazembe, wezi, na wenye kutumia madaraka yao vibaya na wakati huo huo kupanga na kusimamia serikali yake huku akiuunda upya mfumo uliojaribiwa na kuharibiwa.

Kwa mwendo alioanza nao hakuna shaka yoyote jambo moja lilikuwa sahihi kwa upande wangu; kuunga mkono mabadiliko haya. Wapo wanadhani hali ni ngumu sasa na kuwa serikali inabana naamini bado hatujaona hasa ugumu kwani hadi hivi sasa bado serikali inahangaika na madudu ya nyuma na yanatisha. Kusahihisha uchumi (correcting an economy) ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) haiwezekani kuwa ni jambo moja.

Ni kwa sababu hiyo naamini:

1. Kuanza kazi kwa mahakama za kushughulikia ufisadi na uhujumu uchumi kunahitajika mara moja

2. Sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema zaidi ili CAG awe na madaraka ya kutoa agizo la kusimamishwa kazi na hata kufikishwa mahakamani kwa mtendaji yeyote wa umma ambaye uchunguzi wake (CAG) unaonesha kuwa kuna uvunjaji wa sheria. Ikiwezekana ofisi ya CAG iwe na Waendesha mashtaka wake kama ilivyo kwa TAKUKURU. Haipaswi madudu yam waka mzima yanasubiri mwaka mwingine kujulikana. CAG anapofanya ukaguzi na kukuta madudu na ushahidi wa kisayansi upo (forensic evidence) basi hatua zichukuliwe mara moja. Siyo awe na uwezo wa kupeleka mashtaka lakini kwa kupendekeza kwa DPP au hata yeye mwenyewe washutumiwa watiwe mbaroni, mali zao zinazohusiwa kupatikana kwa njia haramu kukamatwa ili zije kufilisiwa wakikutwa na hatia.

3. Sheria ya Usalama wa Taifa inahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka – hili ni jambo ambalo limekuwa katika mada zangu kwa karibu miaka kumi sasa. TISS bado ni dhaifu sana na udhaifu wake umechangia sana kutamalaki kwa utamaduni wa kifisadi. Natumaini Magufuli hatochukua muda mrefu kuifumua hii taasisi kwani ndio moyo wa taifa. Ikilegea taifa liko mashakani.

Kuna na mengine mengi ambayo naamini Magufuli atayafanya kwani tayari ameshaanza kuyafanya na kuwa endapo atafanikiwa tutakapofika mwisho wa mwaka huu kama taifa tutashusha pumzi kidogo kwani angalau tutakuwa katika mazingira ya kusema “kweli hakika huyu alikuwa anahitajika”.

Ni wazi pia kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema “hapana” na waleta “vikwazo”. Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu. La maana ni kukaza mwenzo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikani, na nidhamu ili hatimaye Ujenzi Mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni Zama Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu.

Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.
Wasomaji wa riwaya na tamthilia, huwa kuna dhima ya Ujenzi wa jamii mpya. Naamini sasa tunaijenga jamii mpya.
 
Big up mleta uzi. Time will tell.

Pia, mimi naamini kabisa kuwa kama POLISI, TAKUKURU, na MAHAKAMA wataenda sambamba na kasi ya Rais Magufuli, basi itawezekana kusafisha huu uozo ulipo kwenye utumishi wa umma.

Almost kila sector ya umma tunaona ufisadi unaibuliwa. Ni kazi nzito sana
 
Mawazo haya ni mazuri pamoja na kuwa watu huunda mfumo ila ni ukweli usiopingika pia kuna utaratibu wa kufanya muundo huo ufanye kazi na katiba ni moja ya utaratibu huo ,hivi kuna sababu gani ya kila mara kuziba vitobo vilivyopo kwenye katiba yetu hii ya sasa ? Badala ya kuziba kwanini tusifumue katiba hiyo na kuiunda upya ile iendane na mfumo mpya unajengwa kwa kutumia watu wapya ??

Ikitokea raisi mstaafu anatakiwa kupelekwa mahakamani Magufuli atafanyaje ??
 
JPM was not JK's preference. Just a point of correction,comrade!
JK na CCM yake kama sio JK basi CCM ilihusika chini ya Mwenyekiti JK akapitishwa na akatafutiwa kura za kutosha kwa baraka zote za chama.
 
Mungu ni mwema. Ibariki nchi yangu na uongozi mpya. Ni kazi kubwa, tuwaunge mkono wanaoifanya kazi hiyo ngumu. Penye nia pana njia. ALUTA CONTINUA MAPAMBANO BADO YANAENDELEA. The battle is for the strong!!!!!
 
Hizi ni Zama Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu. Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.
Mzee Mwanakijiji, katika bandiko naona umetaja uchumi ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) kama tatizo kubwa linalolikabili taifa. Nafurahi kuwa umekiri uwepo wa utamaduni ambao ni wazi haukuzuka tu ghafla bin vuu...ulipandwa, ukalelewa, ukakomaa na sasa unampa taabu hata Magufuli, mtumbuaji wa majipu! Unachosahau ni kwamba huyo Magufuli pia alikuwa sehemu ya uongozi wa zama zile uliolea, kulinda na kutetea kwa nguvu huo utamaduni.

Je Magufuli toka akamate madaraka amewahi kutuomba radhi Watanzania kwa ushiriki wake katika uongozi serikalini kwa miaka zaidi ya ishirini. Wengine tulisema toka awali kabisa kwamba mathalan katangazwa mshindi apate ujasiri wa kuomba radhi Watanzania kwa niaba yake na ya chama chake, CCM, ambacho kimekuwa madarakani wakati wote wa huu utamaduni wa kifisadi. Vitendo vyote vya kifisadi vilivumiliwa na kulindwa na uongozi uliokuwa madarakani kwa sababu ndio ulikuwa ni utamaduni wao.

Umesema ni vigumu mtu kukata tawi alokalia, true, na kwamba kazi ya kwanza ya Magufuli ni kukata matawi (watu) wa zama zile ili kuanza na zama mpya, mbona tawi alokalia Magufuli ni la mti ule ule? Unapotaja kuanza upya una maana gani kama katiba inayotuongoza ni ile ile ya zamani na sera tunazofuata ni za chama kile kile cha zamani. Ningeelewa kama ungemshauri Magufuli kuanza kutawala kwa kuitupilia mbali katiba na kuachana na maelekezo ya chama chake, hapo japo ungeweza kueleweka.

Wengine tunapolaumu mfumo wewe unasema, hapana, si mfumo ni utamaduni. Tukisema mfumo ndio hujenga mazingira yasiyo ya maadili mema wewe unasema, hapana, tabia ndiyo tatizo. Tukilaumu mfumo kwa kutuletea utamaduni wa kifisadi, wewe unasema, hapana, watu ndio hujenga utamaduni wa kifisadi. Sawa tukubaliane kwamba tatizo ni watu na si mfumo, je tutafanikishaje ujenzi mpya wa taifa jipya chini ya viongozi wale wale ambao wengi wao walikuwa kwenye uongozi wa zama zile zile?
 
Mkuu unamaanisha hatuwezi kabisa kutengeneza kuanzia hapa tulipofikia? Japo nakumbuka wahenga wanasema hauwezi kufika unapokwenda hadi urudi pale ulipokosea ndio uanze kutafuta ulipopanga kwenda.
Unataka taunzie ule upuuzi wa CCM wenyewe wanaita Katiba pandikizwa!
 
Back
Top Bottom