Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

mimi ni mpenzi wa ngoma za asili. Siku moja nilihudhuria tamasha moja la ngoma hizo sehemu fulani.
yalikuwepo makundi mengi yaliyoalikwa, hata hivyo kuna kundi moja lilinivutia kwa jinsi lilivyoingia kwenye stage.
kwanza wasanii wake waliingia kwa mbwembwe nyingi.......mavazi ya kiasili yaliyovutia sana hadhira nikiwemo mimi pia.........ngoma na vifaa vilivyonakishiwa kiustadi sana...........hadhira iliwashangilia sana tena sana, sababu walikuwa tofauti na makundi mengine......kila mtu alivutiwa na Performance yao.
Kila kundi lilipewa muda maalum wa kutumbuiza. hili kundi lilipoanza 'kufanya vitu vyake', kelele za kushangilia zilizidi kutoka kwa hadhira........... wasanii wake walitumia nusu ya muda waliopangiwa......wakawa hoi!. Kama povu la Fursana.
nilijilaumu, kumbe ningesubiri hadi wahitimishe muda wao ndipo nishangilie.......Siku nyingine nikienda kwenye show, nitaangalia performance kimya kimya ili niache nguvu za kushangilia mbeleni.
 
Mzee Mwanakijiji, katika bandiko naona umetaja uchumi ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) kama tatizo kubwa linalolikabili taifa. Nafurahi kuwa umekiri uwepo wa utamaduni ambao ni wazi haukuzuka tu ghafla bin vuu...ulipandwa, ukalelewa, ukakomaa na sasa unampa taabu hata Magufuli, mtumbuaji wa majipu! Unachosahau ni kwamba huyo Magufuli pia alikuwa sehemu ya uongozi wa zama zile uliolea, kulinda na kutetea kwa nguvu huo utamaduni.

Je Magufuli toka akamate madaraka amewahi kutuomba radhi Watanzania kwa ushiriki wake katika uongozi serikalini kwa miaka zaidi ya ishirini. Wengine tulisema toka awali kabisa kwamba mathalan katangazwa mshindi apate ujasiri wa kuomba radhi Watanzania kwa niaba yake na ya chama chake, CCM, ambacho kimekuwa madarakani wakati wote wa huu utamaduni wa kifisadi. Vitendo vyote vya kifisadi vilivumiliwa na kulindwa na uongozi uliokuwa madarakani kwa sababu ndio ulikuwa ni utamaduni wao.

Umesema ni vigumu mtu kukata tawi alokalia, true, na kwamba kazi ya kwanza ya Magufuli ni kukata matawi (watu) wa zama zile ili kuanza na zama mpya, mbona tawi alokalia Magufuli ni la mti ule ule? Unapotaja kuanza upya una maana gani kama katiba inayotuongoza ni ile ile ya zamani na sera tunazofuata ni za chama kile kile cha zamani. Ningeelewa kama ungemshauri Magufuli kuanza kutawala kwa kuitupilia mbali katiba na kuachana na maelekezo ya chama chake, hapo japo ungeweza kueleweka.

Wengine tunapolaumu mfumo wewe unasema, hapana, si mfumo ni utamaduni. Tukisema mfumo ndio hujenga mazingira yasiyo ya maadili mema wewe unasema, hapana, tabia ndiyo tatizo. Tukilaumu mfumo kwa kutuletea utamaduni wa kifisadi, wewe unasema, hapana, watu ndio hujenga utamaduni wa kifisadi. Sawa tukubaliane kwamba tatizo ni watu na si mfumo, je tutafanikishaje ujenzi mpya wa taifa jipya chini ya viongozi wale wale ambao wengi wao walikuwa kwenye uongozi wa zama zile zile?
Brother nikisoma maandiko yenu siku hizi nashindwa kabisa kuvumilia. Kuomba radhi kwa Magufuli kuna tusaidia nini zaidi ya hatua anazochukua ambazo kila siku mnatafuta namna ya kukosoa tu badala ya constructive criticism? Hivi kweli kama kuombana msamaha kunasafisha umewahi kuhoji hili hata upinzani wanaopaswa kuwa mfano? Chadema tumesahau ya Mahanga na uchaguzi wa 2010? Please tuwe na huruma kwa taifa hili kwa kuwa wakweli ....
 
Kama hakuna namna ya kumwajibisha kiongozi mkuu wa nchi hata akistaafu, hapo hakuna tunachofanya. Kiongozi akijua madudu yake yatafuatiliwa hata akistaafu hawezi kufanya waliyofanya viongozi wetu wakuu kama Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hata Magufuli mwenyewe. Rais lazima akae akielewa kwamba hayuko juu ya sheria na kwamba akivunja Katiba aliyoapa kuilinda awe tayari kushughulikiwa kama mhalifu yeyote yule. Katiba lazima ioainishe atakavyoshughulikiwa.
Hata kama Magufuli atakubali ipigiwe kura katiba ya Warioba mtahamisha magoli naapa ...mnachosha kwakweli
 
Umeongea saana hivi hiyo ripoti ya CAG uliyoisifia umeisoma tayari nikuulize kunamahala umekuta matumizi mabaya ya fedha wizara ya ujenzi mwaka jana 2015-2016?au tayari ndo imetoka hiyo ikirudi pancha. Hahaaa, hiihiihiii kijijiii mtoto
 
Mkuu MM
Kuna mahali nimechanganyikiwa kidogo na bandiko lako

1. ''Ni lazima kubadili watu kwanza kabla ya mfumo. Huwezi kutumia watu wale wale kubadili mfumo kwasababu mfumo unatengenezwa na watu'' Fair enough

2. ''Sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema..., na sheria ya TISS ifanyiwe mabadiliko haraka.....''

Tukisema mfumo, CAG na TISS ni viungo muhimu sana

Kwanini basi usikubaliane na wale wanaosema tufumue mfumo kwanza?

Au unaaminisha wakati anaendelea ku deal na watu, tuweke viraka katika mfumo?

Msaada
 
mi sijaona cha maana ambacho magufuli amekifanya kwani kila mtawala akiingia huwa anaweka watu anao wazania watakao fanya kutokana na matakwa yake au malengo ya chama.tatizo ni kuwa wanao tolewa post zao kwenye kipindi cha magufuli wanatuhuma za ubadilifu tofauti na uongozi uliopita ambapo watawala walikuwa wanabadilisha watu lakini hawana tuhuma za ubadhilifu.

Aiseee watu wengine ni zaidi ya bomu la nuclear
 
Mkuu MM
Kuna mahali nimechanganyikiwa kidogo na bandiko lako

1. ''Ni lazima kubadili watu kwanza kabla ya mfumo. Huwezi kutumia watu wale wale lkubadili mfumo kwasababu mfumo unatengenezwa na watu'' Fair enough

2. ''Sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema..., na sheria ya TISS ifanyaiwe mabadiliko haraka.....''

Tukisema mfumo, CAG na TISS ni viungo muhimu sana

Kwanini basi usikubaliane na wale wanaosema tufumue mfumo kwanza?

Au unaaminisha wakati anaendelea ku deal na watu, tuweke viraka katika mfumo?

Msaada
Si wewe peke yako unayetatizwa...yawezekana na huko CAG na TISS kunahitaji timua timua tu na siyo sheria kufanyiwa mabadiliko. Tukisema tatizo ni mfumo tunaulizwa mfumo ni nini lakini hapo hapo tunaambiwa tatizo ni utamaduni wa kifisadi. Je huo utamaduni umeletwa na nini?

Tunaambiwa tatizo ni watu kwa hiyo jambo la msingi ni timua timua. Tukiuliza mbona Kikwete alivunja rekodi ya dunia kwa kubadilisha Baraza la Mawaziri kama anavyobadilisha shati? Tunaambiwa alikuwa anaangushwa na watu aliokuwa anawateua yeye mwenyewe kwa ushauri wa Waziri wake Mkuu.

Sasa Magufuli ameamua kuanza upya kwa kuwateua watu wapya. Tukiuliza hawa watu wapya ambao hawajaathirika na utamaduni wa kifisadi anawatoa wapi na hasa pale sura zinapokuwa zile zile? Tunalaumiwa kwa kuambiwa tunatafuta tu namna ya kukosoa badala ya kutoa constructive criticism!

Mag3, nachoka...
 
Si wewe peke yako unayetatizwa...yawezekana na huko CAG na TISS kunahitaji timua timua tu na siyo sheria kufanyiwa mabadiliko. Tukisema tatizo ni mfumo tunaulizwa mfumo ni nini lakini hapo hapo tunaambiwa tatizo ni utamaduni wa kifisadi. Je huo utamaduni umeletwa na nini?

Tunaambiwa tatizo ni watu kwa hiyo jambo la msingi ni timua timua. Tukiuliza mbona Kikwete alivunja rekodi ya dunia kwa kubadilisha Baraza la Mawaziri mara kwa mara? Tunaambiwa alikuwa anaangushwa na watu aliokuwa anawateua yeye mwenyewe kwa ushauri wa Waziri wake Mkuu.

Sasa Magufuli ameamua kuanza upya kwa kuwateua watu wapya. Tukiuliza hawa watu wapya ambao hawajaathirika na utamaduni wa kifisadi anawatoa wapi na hasa pale sura zinapokuwa zile zile? Tunalaumiwa kwa kuambiwa tunatafuta tu namna ya kukosoa badala ya kutoa constructive criticism!

Mag3, nachoka...
Ukishasema utamaduni tayari umezungumzia utaratibu wa jamii fulani yaani mfumo wa jamii husika

Watu wanaogopa hili neno mfumo kukwepa yanayoambatana na neno.

Na wala watendaji hawajawa kikwazo. Sioni bwana shamba au afisa afya anashiriki vipi katika mfumo wa kifIsadi kama tuliyowahi kuona ikitikisa taifa

Ninachokiona ni ufisadi ulio katika mfumo unaoratibiwa na kundi nje ya wafanyakazi Uzembe kazini si ufisadi, una sheria zake.

Ufisadi wa mabilioni unaratibiwa kwa ufundi katika ''mfumo'' usio rasmi wenye nguvu sana

Kuna kashfa ya wabunge, hili wataita 'utamaduni' sisi wengine tutaita mfumo wa kifisadi

Ukiangalia wabunge walioshiriki ni wazoefu wa CCM kwasababu wanajua utamaduni wao

Hapa ndipo tunakuja kwenye hoja kuwa, bila kubadili mfumo ili uweze kukabiliana na genge linalomzunguka, ni kutwanga maji kwenye kinu. Pinda laisema ni genge hatari sana

Wabunge waliitisha kikao eti kashfa zinachafua chama. Kikao si kujadili kashfa kwa Taifa, la hasha! ni kwa chama katika 'utamaduni' murua a.k.a mfumo wa kulindana

Sasa ninapoambiwa tufumue CAG haraka sana, tufumue TISS mapema iwezekanavyo halafu tunaambiwa mfumo uachwe kwanza ili timu timua ikamilike, natatizika kidogo
 
Ikitokea raisi mstaafu anatakiwa kupelekwa mahakamani Magufuli atafanyaje ??

Hana la kufanya kwa makosa yaliyofanyika akiwa madarakani. Ila kama ni makosa baada ya kutoka madarakani Sheria inafuata mkondo wake.
 
Hana la kufanya kwa makosa yaliyofanyika akiwa madarakani. Ila kama ni makosa baada ya kutoka madarakani Sheria inafuata mkondo wake.
Kwa hiyo kesho na mimi nikiingia Ikulu ,nikauchukua mgodi wa Tanzanite basi ni sawa kwa sababu ni makosa niliyoyafanya nikiwa madarakani ?
 
Mzee Mwanakijiji, nadhani tuna haja ya kurejea jalalani, tukacharure takataka mpaka tuikute ile katiba tuliyo itupa kule, katiba ya yule Waziri Mkuu wa zamani.
Tuzifuate zile tunu za Taifa, Taifa letu kitakuwa limepata chanjo, tiba na kinga
Hapo ndio penye mtihani mkubwa sana,tunapangoja kwa hamu
 
Kwa nchi changa kama hizi mfumo kufanya kazi kwa kujitegemea bila kutegemea watu bado ni ngumu sana.

Lazima awepo mtu mwenye strong political will at the top, halafu mfumo ufanye kazi yake, otherwise ni yale yale ya JK tu
hiyo ni Kama mama Wa nyumbani anatetegemea mmewe 100%, siku Mme akikatika, anajililia mwenyewe kabla ya kumlilia mme
 
Angeanza nankurekebisha katiba kwa kucopy na kipaste ile ya warioba ingesaidoa sana kupunguza sarakasi
 
Magufuli amekuja kwa wakati muafaka kwani amekuwa kama daktari Bingwa aliepewa mgonjwa mahututi ambaye wamtegemeao wamekata tamaa naye na maisha yao kwa ujumla, magufuli nitamkumbuka kwa kurejesha vitu vifuayavyo :-

1. Hali ya uzalendo

2. wajibu na uwazi

3. Ari ya kujitegemea

4. Nidhamu na ari ya kazi

5. tumaini kwa wanyonge

Ingawa ni mapema sana kutoa hitimisho lakini rais wetu amejitahidi sana hadi sasa...naisubiria bajeti ya mwaka huu na pia suluhu ya katiba mpya

**** TANZANIA KWANZA ****
 
Kweli kabisa. Mfano taasisi za umma zina mifumo mizuri tu ya internal control lakini tumewahi kujiuliza kwanini haifanyi kazi? Tusipige siasa penye kuhitaji tafakuri za kizalendo ...
Unachanganya muundo na mfumo...miundo ya mashirika ni mizuri, mifumo ni ya hovyo.
 
Mkuu hiyo namba mbili ni hatari sana, kumpa madaraka yote hayo mtu mmoja (CAG) anaweza kuyatumia vibaya. Yani yeye afanye ukaguzi na awe na uwezo wa kushtaki na kufukuza ni hatari ukipata mtu ambaye mwehu. Lazima kuwa na segregation of duties

Of course humpi yote.. bado kutakuwa na judicial reviews na judicial process.. OF course hatokuwa na uwezo wa kufukuza mtu kazi lakini awe na uwezo wa kumzuia mtu asiendelee na kazi na hata kumkamata...
 
john-magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa baadhi yetu tuliokataa kuvingirisha mikono yetu kuunga mkono mabadiliko yaliyobinafsishwa kwa mtu mmoja tulijikuta hatuna budi kumuunga mkono Magufuli tukiamini anawakilisha mabadiliko ya kweli. Binafsi niliamini kabisa kuwa Taifa lilikuwa linamhitaji kiongozi kama Magufuli kuweza kulinasua mahali lilipo kuliko kiongozi yule mwingine toka upinzani. Niliamini kabisa kuwa Magufuli akishika madaraka atakuwa na kazi kubwa ya kulirejesha Taifa katika misingi yake ambayo inaonekana ilikuwa imepotea.

Hatua zake mbalimbali za mwanzo kushughulika na kubana matumizi, kupambana na ufisadi na kuondoa watendaji mizigo a.k.a majipu kulinifanya niamini kabisa kuwa Magufuli kazi aliyonayo akiendelea na kasi hiyo basi ndani ya miezi sita tu atakuwa ameleta heshima katika utumishi wa umma, kurejesha heshima kwa Watanzania na fahari ya taifa letu kurudishwa. Niliamini kabisa kuwa Magufuli atafanya kazi hii bila woga, huruma, husuda, wivu, au kusita sita. Kwamba, hatomwangalia yeyote, popote na kwa lolote. Ndani ya miezi sita hivi na kabla ya ujio wa bajeti ya kwanza ya serikali yake basi Magufuli atakuwa ameshaweka alama za namna gani taifa linataka kwenda na kila kiongozi atakuwa amepata ujumbe.

Nilifanya makosa.

Nilifanya makosa kwa sababu nilidhani hii ni kazi rahisi kwa Rais. Nilidhani ni kazi ya kutimua huyu, kuondoa yule na kumleta yule mwingine. Nilidhani ni kazi ambayo akimaliza teuzi mbalimbali basi atakuwa ameipanga serikali yake kwa ajili ya kuchapa kazi.

Sasa najua kuwa uamuzi wake wa kushughulika na watu kwanza kabla ya mfumo ni jambo muhimu sana. Ulikuwa ni uamuzi sahihi na unajitahi kutetewa. Watu ndio hutengeneza mfumo; ni watu ndio ambao hukaa chini na kufanya maamuzi mbalimbali yenye kuathiri (kwa uzuri au ubaya) uwepo na utendaji wa mfumo wa utawala. Ukiwa na watu wabovu, wabinafsi na wenye mwelekeo wa ufisadi basi mfumo utakuwa mbovu, wa kibinafsi na wenye uelekeo wa kifisadi kwa sababu moja kubwa; wale wenye kuiwamba ngoma ngozi huivutia kwao! Mfumo wetu wa utawala wa kifisadi ulitengenezwa na watawala wenye mwelekeo wa kifisadi. Matobo (siyo matundu) kwenye sheria zetu vilitengenezwa na watu ambao walijua wakiziba na wao watakuwa wamejizibia.

Magufuli asingeweza kutengeneza mfumo mwingine kwa kutumia watu wale wale walioutengeneza mfumo huu wa sasa na hasa kama watu hao ni wanufaika wa mfumo huu. Ingelikuwa ni sawa sawa na kumtaka Rais awalazimishe watu wakate matawi ambayo wamekalia huku wakijua kwa kufanya hivyo wataangukia mtoni kwenye mamba wengi. Hakukuwa na jinsi nab ado hakuna jinsi ni lazima kuwaondoa hawa na kuwashughulikia ili kuleta watu wenye fikra zinazoakisi mwelekeo wa serikali yake.

Ni kwa sababu hiyo, kumbe kazi ile ya miezi sita kwa kweli haiwezekani. Ni kazi ambayo inapaswa kuwa endelevu na yenye matokeo bora. Tayari tumeanza kuona dalili za yaliyomo ndani ya ripot ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) na tayari inatisha kama ilivyotisha mwaka 2006 na miaka iliyofuatia.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukijulishwa juu ya uchafu wa watendaji wetu na taasisi zetu na mara karibu hizo zote tumekuwa tukionesha kushtushwa na kusikitishwa tukiamini kuwa labda mwaka unaofuatia mambo yatakua tofauti. CAG aliyepita alikuwa anarudia baadhi ya hoja mwaka baada ya mwaka na wakati mwingine kuhusiana na taasisi au watu wale wale. Na safari hii tusije kushangaa kuwa hata CAG wa sasa anaweza kujikuta amegusa maeneo yale yale; matumizi mabaya ya sheria ya manunuzi ya umma, fedha kutumiwa bila maelezo, kutopatikana kwa vitabu vya masuala ya fedha wakati wa ukaguzi, na upotevu wa fedha za umma kwa namna ambayo inadokeza tu kuwa zimeliwa.

Magufuli basi ana kazi kubwa; kushughulikia viongozi wabadhirifu, wazembe, wezi, na wenye kutumia madaraka yao vibaya na wakati huo huo kupanga na kusimamia serikali yake huku akiuunda upya mfumo uliojaribiwa na kuharibiwa.

Kwa mwendo alioanza nao hakuna shaka yoyote jambo moja lilikuwa sahihi kwa upande wangu; kuunga mkono mabadiliko haya. Wapo wanadhani hali ni ngumu sasa na kuwa serikali inabana naamini bado hatujaona hasa ugumu kwani hadi hivi sasa bado serikali inahangaika na madudu ya nyuma na yanatisha. Kusahihisha uchumi (correcting an economy) ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) haiwezekani kuwa ni jambo moja.

Ni kwa sababu hiyo naamini:

1. Kuanza kazi kwa mahakama za kushughulikia ufisadi na uhujumu uchumi kunahitajika mara moja

2. Sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema zaidi ili CAG awe na madaraka ya kutoa agizo la kusimamishwa kazi na hata kufikishwa mahakamani kwa mtendaji yeyote wa umma ambaye uchunguzi wake (CAG) unaonesha kuwa kuna uvunjaji wa sheria. Ikiwezekana ofisi ya CAG iwe na Waendesha mashtaka wake kama ilivyo kwa TAKUKURU. Haipaswi madudu yam waka mzima yanasubiri mwaka mwingine kujulikana. CAG anapofanya ukaguzi na kukuta madudu na ushahidi wa kisayansi upo (forensic evidence) basi hatua zichukuliwe mara moja. Siyo awe na uwezo wa kupeleka mashtaka lakini kwa kupendekeza kwa DPP au hata yeye mwenyewe washutumiwa watiwe mbaroni, mali zao zinazohusiwa kupatikana kwa njia haramu kukamatwa ili zije kufilisiwa wakikutwa na hatia.

3. Sheria ya Usalama wa Taifa inahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka – hili ni jambo ambalo limekuwa katika mada zangu kwa karibu miaka kumi sasa. TISS bado ni dhaifu sana na udhaifu wake umechangia sana kutamalaki kwa utamaduni wa kifisadi. Natumaini Magufuli hatochukua muda mrefu kuifumua hii taasisi kwani ndio moyo wa taifa. Ikilegea taifa liko mashakani.

Kuna na mengine mengi ambayo naamini Magufuli atayafanya kwani tayari ameshaanza kuyafanya na kuwa endapo atafanikiwa tutakapofika mwisho wa mwaka huu kama taifa tutashusha pumzi kidogo kwani angalau tutakuwa katika mazingira ya kusema “kweli hakika huyu alikuwa anahitajika”.

Ni wazi pia kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema “hapana” na waleta “vikwazo”. Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu. La maana ni kukaza mwenzo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikani, na nidhamu ili hatimaye Ujenzi Mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni Zama Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu.

Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.

Mnadanganyana,hawez kufanya lolote bila Katiba Mpya(ile ya warioba) ambayo chama chake hakiitaki hvyo haweI kuipitisha..
Na katika hyo katiba mpya aweke na sheria ya kunyonga.
Hayo mengine ni mbwembwe tu hayana tofauti na Fagio la Chuma la mwinyi..
 
Back
Top Bottom