Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Leo umeongea kizalendo sana Mzee Mwanakijiji Rais anakazi ngumu sana, tatizo juhudi zake zinapata upinzani mkubwa sana. Wale tunaompinga tungejitahidi kupongeza hizi jitihada na kushauri nini kifanyike badala ya kubeza na kudharau kila jitihada anazozifanya. Tukumbuke kwamba kila kitu kina hatua na hauwezi kuleta maendeleo au kubadilisha hali mbaya kuwa hali nzuri kwa usiku mmoja.
Tusipokosoa tutakula wapi ndugu angu. Unataka tufe njaa...hii ndio kazi inayotuweka mjini kaka...
 
john-magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa baadhi yetu tuliokataa kuvingirisha mikono yetu kuunga mkono mabadiliko yaliyobinafsishwa kwa mtu mmoja tulijikuta hatuna budi kumuunga mkono Magufuli tukiamini anawakilisha mabadiliko ya kweli. Binafsi niliamini kabisa kuwa Taifa lilikuwa linamhitaji kiongozi kama Magufuli kuweza kulinasua mahali lilipo kuliko kiongozi yule mwingine toka upinzani. Niliamini kabisa kuwa Magufuli akishika madaraka atakuwa na kazi kubwa ya kulirejesha Taifa katika misingi yake ambayo inaonekana ilikuwa imepotea.

Hatua zake mbalimbali za mwanzo kushughulika na kubana matumizi, kupambana na ufisadi na kuondoa watendaji mizigo a.k.a majipu kulinifanya niamini kabisa kuwa Magufuli kazi aliyonayo akiendelea na kasi hiyo basi ndani ya miezi sita tu atakuwa ameleta heshima katika utumishi wa umma, kurejesha heshima kwa Watanzania na fahari ya taifa letu kurudishwa. Niliamini kabisa kuwa Magufuli atafanya kazi hii bila woga, huruma, husuda, wivu, au kusita sita. Kwamba, hatomwangalia yeyote, popote na kwa lolote. Ndani ya miezi sita hivi na kabla ya ujio wa bajeti ya kwanza ya serikali yake basi Magufuli atakuwa ameshaweka alama za namna gani taifa linataka kwenda na kila kiongozi atakuwa amepata ujumbe.

Nilifanya makosa.

Nilifanya makosa kwa sababu nilidhani hii ni kazi rahisi kwa Rais. Nilidhani ni kazi ya kutimua huyu, kuondoa yule na kumleta yule mwingine. Nilidhani ni kazi ambayo akimaliza teuzi mbalimbali basi atauwa ameipanga serikali yake kwa ajili ya kuchapa kazi.

Sasa najua kuwa uamuzi wake wa kushughulika na watu kwanza kabla ya mfumo ni jambo muhimu sana. Ulikuwa ni uamuzi sahihi na unajitahi kutetewa. Watu ndio hutengeneza mfumo; ni watu ndio ambao hukaa chini na kufanya maamuzi mbalimbali yenye kuathiri (kwa uzuri au ubaya) uwepo na utendaji wa mfumo wa utawala. Ukiwa na watu wabovu, wabinafsi na wenye mwelekeo wa ufisadi basi mfumo utakuwa mbovu, wa kibinafsi na wenye uelekeo wa kifisadi kwa sababu moja kubwa; wale wenye kuiwamba ngoma ngozi huivutia kwao! Mfumo wetu wa utawala wa kifisadi ulitengenezwa na watawala wenye mwelekeo wa kifisadi. Matobo (siyo matundu) kwenye sheria zetu vilitengenezwa na watu ambao walijua wakiziba na wao watakuwa wamejizibia.

Magufuli asingeweza kutengeneza mfumo mwingine kwa kutumia watu wale wale walioutengeneza mfumo huu wa sasa na hasa kama watu hao ni wanufaika wa mfumo huu. Ingelikuwa ni sawa sawa na kumtaka Rais awalazimishe watu wakate matawi ambayo wamekalia huku wakijua kwa kufanya hivyo wataangukia mtoni kwenye mamba wengi. Hakukuwa na jinsi nab ado hakuna jinsi ni lazima kuwaondoa hawa na kuwashughulikia ili kuleta watu wenye fikra zinazoakisi mwelekeo wa serikali yake.

Ni kwa sababu hiyo, kumbe kazi ile ya miezi sita kwa kweli haiwezekani. Ni kazi ambayo inapaswa kuwa endelevu na yenye matokeo bora. Tayari tumeanza kuona dalili za yaliyomo ndani ya ripot ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) na tayari inatisha kama ilivyotisha mwaka 2006 na miaka iliyofuatia. Kwa muda mrefu tumekuwa tukijulishwa juu ya uchafu wa watendaji wetu na taasisi zetu na mara karibu hizo zote tumekuwa tukionesha kushtushwa na kusikitishwa tukiamini kuwa labda mwaka unaofuatia mambo yatakua tofauti. CAG aliyepita alikuwa anarudia baadhi ya hoja mwaka baada ya mwaka na wakati mwingine kuhusiana na taasisi au watu wale wale. Na safari hii tusije kushangaa kuwa hata CAG wa sasa anaweza kujikuta amegusa maeneo yale yale; matumizi mabaya ya sheria ya manunuzi ya umma, fedha kutumiwa bila maelezo, kutopatikana kwa vitabu vya masuala ya fedha wakati wa ukaguzi, na upotevu wa fedha za umma kwa namna ambayo inadokeza tu kuwa zimeliwa.

Magufuli basi ana kazi kubwa; kushughulikia viongozi wabadhirifu, wazembe, wezi, na wenye kutumia madaraka yao vibaya na wakati huo huo kupanga na kusimamia serikali yake huku akiuunda upya mfumo uliojaribiwa na kuharibiwa.

Kwa mwendo alioanza nao hakuna shaka yoyote jambo moja lilikuwa sahihi kwa upande wangu; kuunga mkono mabadiliko haya. Wapo wanadhani hali ni ngumu sasa na kuwa serikali inabana naamini bado hatujaona hasa ugumu kwani hadi hivi sasa bado serikali inahangaika na madudu ya nyuma na yanatisha. Kusahihisha uchumi (correcting an economy) ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) haiwezekani kuwa ni jambo moja.

Ni kwa sababu hiyo naamini:

1. Kuanza kazi kwa mahakama za kushughulikia ufisadi na uhujumu uchumi kunahitajika mara moja

2. Sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema zaidi ili CAG awe na madaraka ya kutoa agizo la kusimamishwa kazi na hata kufikishwa mahakamani kwa mtendaji yeyote wa umma ambaye uchunguzi wake (CAG) unaonesha kuwa kuna uvunjaji wa sheria. Ikiwezekana ofisi ya CAG iwe na Waendesha mashtaka wake kama ilivyo kwa TAKUKURU. Haipaswi madudu yam waka mzima yanasubiri mwaka mwingine kujulikana. CAG anapofanya ukaguzi na kukuta madudu na ushahidi wa kisayansi upo (forensic evidence) basi hatua zichukuliwe mara moja. Siyo awe na uwezo wa kupeleka mashtaka lakini kwa kupendekeza kwa DPP au hata yeye mwenyewe washutumiwa watiwe mbaroni, mali zao zinazohusiwa kupatikana kwa njia haramu kukamatwa ili zije kufilisiwa wakikutwa na hatia.

3. Sheria ya Usalama wa Taifa inahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka – hili ni jambo ambalo limekuwa katika mada zangu kwa karibu miaka kumi sasa. TISS bado ni dhaifu sana na udhaifu wake umechangia sana kutamalaki kwa utamaduni wa kifisadi. Natumaini Magufuli hatochukua muda mrefu kuifumua hii taasisi kwani ndio moyo wa taifa. Ikilegea taifa liko mashakani.

Kuna na mengine mengi ambayo naamini Magufuli atayafanya kwani tayari ameshaanza kuyafanya na kuwa endapo atafanikiwa tutakapofika mwisho wa mwaka huu kama taifa tutashusha pumzi kidogo kwani angalau tutakuwa katika mazingira ya kusema “kweli hakika huyu alikuwa anahitajika”.

Ni wazi pia kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema “hapana” na waleta “vikwazo”. Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu. La maana ni kukaza mwenzo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikani, na nidhamu ili hatimaye Ujenzi Mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni Zama Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu.

Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.
Hongera Mwanakijiji kwa maoni ambayo leo nahisi umeondoa ushabiki.
Nakubaliana na yote uliyosema na kwa kweli amegusa hata ambapo hatukutegemea.
Hofu yangu na nikiri kuwa hofu ndiyo iliyosababisha nishabikie mabadiliko hata ikiwa ni kumpa kura mgonjwa ni hili la Chama chake ambacho kwa kweli uozo wote unaoonekana leo ni udhaifu wa chama tawala ambacho kilishindwa kuisimamia serikali yake.
Hivyo hofu ni ya mtu aliyeengwa na mfumo huo atakuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko ambayo ni sustainable?
Siamini na sitaamini kuwa wa kupata U raisi amekuwa saint na kuna mambo ambayo hata yeye yatamgusa kama hili la kivuko cha Bagamoyo,nyumba za serikali n.k.
Nahisi ya kuwa atafikia mahali dhamira itamsuta.
Ni Raisi nami namwombea ayafanyayo yawe endelevu.
 
Yote sawa lakini akikosea aachwe?? Na nyie mnayempongeza je mliwahi kumkosoa mtangulizi wake ? Au kwa wote ni makofi tu!!!!
 
Napingana na maoni yako. Nyumba imara huanzia kweye msingi. Nyumba yetu imechakaa, Ina nyufa, na unatikisika. Anachofanya magu ni kuondoa baadhi ya bâti ailizooza sana, kupaka rangi kuta zenye nyufa na kuwaita wanakijiji waje kupiga picha na kushangilia.
Hivi magufuri ana ubavu Wa kuvunja mitandao ya kiharifu inayoongozwa na viongozi Wakuu Wa chama chake Kama ujangiri , mdawa ya kulevya nk. Tusidanganyane, mfumo ndio msingi kwanza mengine yatafuata. Tuache kushangilia maigizo.
Hivi mwenzetu kuna uwezekano unaandika ukiwa mapango ya Amboni?
 
Chukua likes 100 mzee mwanakijiji, ni juzi tu nilikua naongea na jirani the same perspective... Watu ndio wanaounda mfumo, magufuli lazima atoe watu wabovu kwanza ndio aunde mfumo akiwa na watu wenye mtazamo na wenye ku support nia yake njema kwa wa Tanzanian.

Iko wazi, hii kazi sio ndogo, nashindwa elewa watu wanavyodhihaki hizi hatua, na sijui walitegemea nini.

Rejea mfano wa marekebisho ya katiba itaelewa umuhimu wa watu bora kuunda mfumo.
 
CAG angewezeshwa kwa kupewa rasimali watu na fedha,ili watu wake wafanye kazi kwa weledi,kuliko kusikia kashfa za rushwa kutoka kwenye taasisi yake.Pia watafute njia ambazo whistle blowers wangesaidia CAG kupata inputs za kutosha.Pia serikali itumie report zake maana bila hivyo itakuwa kazi bure
 
Napingana na maoni yako. Nyumba imara huanzia kweye msingi. Nyumba yetu imechakaa, Ina nyufa, na unatikisika. Anachofanya magu ni kuondoa baadhi ya bâti ailizooza sana, kupaka rangi kuta zenye nyufa na kuwaita wanakijiji waje kupiga picha na kushangilia.
Hivi magufuri ana ubavu Wa kuvunja mitandao ya kiharifu inayoongozwa na viongozi Wakuu Wa chama chake Kama ujangiri , mdawa ya kulevya nk. Tusidanganyane, mfumo ndio msingi kwanza mengine yatafuata. Tuache kushangilia maigizo.


Mfumo ni nini? Tuanzie hapo kwanza kwa maana isije kuwa tunanukuu tu mambo bila ya kuelewa hasa maana yake ni nini!
 
Ni nani waliomo serikalini hawakuwa katika mfumo uliopo?
 
Chukua likes 100 mzee mwanakijiji, ni juzi tu nilikua naongea na jirani the same perspective... Watu ndio wanaounda mfumo, magufuli lazima atoe watu wabovu kwanza ndio aunde mfumo akiwa na watu wenye mtazamo na wenye ku support nia yake njema kwa wa Tanzanian.
The likes of Makonda, Nape, Makamba, Mwigulu, Kigwangala, Kilango, Magembe, Mulugo...
Iko wazi, hii kazi sio ndogo, nashindwa elewa watu wanavyodhihaki hizi hatua, na sijui walitegemea nini.
Hatudhihaki, tunakosoa. Magufuli si malaika, je umeshuhudia chaguzi za Mameya wa Halmashauri zilivyoendeshwa? Bila shaka utasema hazimhusu lakini siku alipotoa kauli tu (miezi mitano baada ya kuapishwa) Dar wakampata Meya.
Rejea mfano wa marekebisho ya katiba itaelewa umuhimu wa watu bora kuunda mfumo.
Kwa hiyo hapo unalaumu watu na si mfumo unaoruhusu ujinga kama tulivyoshuhudia?
 
Mawazo haya ni mazuri pamoja na kuwa watu huunda mfumo ila ni ukweli usiopingika pia kuna utaratibu wa kufanya muundo huo ufanye kazi na katiba ni moja ya utaratibu huo ,hivi kuna sababu gani ya kila mara kuziba vitobo vilivyopo kwenye katiba yetu hii ya sasa ? Badala ya kuziba kwanini tusifumue katiba hiyo na kuiunda upya ile iendane na mfumo mpya unajengwa kwa kutumia watu wapya ??

Ikitokea raisi mstaafu anatakiwa kupelekwa mahakamani Magufuli atafanyaje ??


Hatutaki Katiba Mpya, Magufuli anatosha, na isitoshe hatuna huwo muda!

Kenya wana Katiba mpya lkn hakuna kilichobdailika, wametumia bilions na kuitangaza Dunia nzima, leo hii ufisadi umeongezeka na ni mkubwa klk hata wakati wa KANU, hakuna rule of law walioiahidi, hali ya usalama iko vile vile kama haijaharibika zaidi, deni la nchi limezidi kuongezeka na sasa siyo deni la nchi tu bali kila Jimbo pia linatengeneza deni lake, na kikubwa labda kuliko vyote hiyo tume wanaoiita huru ya uchaguzi hawana Imani nao na tayari Wapinzani wamesema hawatatambua matokeo ya Uchaguzi, sasa kwanini tuende huko??!
 
Huwa nasema na nitarudia kusema kila siku kwamba Magufuli ni genius, watu wengi hawaamini lkn muda utaongea, mimi nilimkubali Magufuli jinsi tu alivyoweza kupenya CCM na kuibuka kuwa Mgombea wa CCM, ni mtu genius tu ndiyo anaweza kupenya kwenye mto uliojaa mamba wengi namna ile na kuibuka mshindi!
Watu kama Lowasa walijiandaa kwa zaidi miaka 20, walijenga mitandao ya watu wenye ushawishi mkubwa wa fedha na karibia kila kitu lkn hawakupita, na sababu kubwa ni kwamba watu kama Lowasa wana fedha na watu wenye fedha lkn siyo Inteligent men na ndiyo maana wanashindwa kama Lowasa angekuwa intelligent man huu uraisi ulikuwa wake kabisa!

Ikumbukwe kwambaMagufuli hakuwa na kundi, fedha wala watu wazito na wenye ushawishi kwenye Chama hivyo alitegemea Akili yake tu na ndiyo maana hata siku anaaongea na majaji alilisema hilo kwamba mtu kama yeye from now where akaweza kupenya na mwishowe kuapishwa kuwa Raisi wa JMTZ siyo jambo dogo!
Tangia hapo nikajua kwamba Magufuli siyo mtu wa kawaida, najua baadhi wanamdharau na kumdhihaki lkn siku zinavyozidi kwenda idadi yao inazidi kupungua, watu waliokuwa wanamkebehi na kumdhihaki Magufuli hapa JF mwanzoni walikuwa wengi sana leo hii wengi wao wamepotea!

Mambo aliyoyafanya Magufuli kwa nchi hii chini ya miezi 6 hata nchi za Wazungu tunazozifia viongozi wao hawawezi kufanya reforms kubwa namna hii, fikiria kupunguza utegemezi wa bajeti chini ya mwaka 1 ktk 40% mpaka 3% hii siyo kazi ndogo, uwezo tu wa kuteua watu makini kama Waziri Mpango kuwa waziri wa fedha inahitaji akili!

Hivyo kama alivyosema Kikwete hata mimi nalala usingizi kabisa tena nakoroma kwa maana najua TanZania yetu iko salama na tutavuka kama alivyosema Raisi Magufuli!
umeandika kwa hisia sana......
 
N
Mfumo ni nini? Tuanzie hapo kwanza kwa maana isije kuwa tunanukuu tu mambo bila ya kuelewa hasa maana yake ni nini!
Tunaanza na katiba nzuri iitkayotujengea mfumo ambao hautegemei mtu. Leo hii Mungu akimwita magu tunaweza tukampata kikwete mwingine
 
Mzee Mwanakijiji, katika bandiko naona umetaja uchumi ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) kama tatizo kubwa linalolikabili taifa. Nafurahi kuwa umekiri uwepo wa utamaduni ambao ni wazi haukuzuka tu ghafla bin vuu...ulipandwa, ukalelewa, ukakomaa na sasa unampa taabu hata Magufuli, mtumbuaji wa majipu! Unachosahau ni kwamba huyo Magufuli pia alikuwa sehemu ya uongozi wa zama zile uliolea, kulinda na kutetea kwa nguvu huo utamaduni.

Je Magufuli toka akamate madaraka amewahi kutuomba radhi Watanzania kwa ushiriki wake katika uongozi serikalini kwa miaka zaidi ya ishirini. Wengine tulisema toka awali kabisa kwamba mathalan katangazwa mshindi apate ujasiri wa kuomba radhi Watanzania kwa niaba yake na ya chama chake, CCM, ambacho kimekuwa madarakani wakati wote wa huu utamaduni wa kifisadi. Vitendo vyote vya kifisadi vilivumiliwa na kulindwa na uongozi uliokuwa madarakani kwa sababu ndio ulikuwa ni utamaduni wao.

Umesema ni vigumu mtu kukata tawi alokalia, true, na kwamba kazi ya kwanza ya Magufuli ni kukata matawi (watu) wa zama zile ili kuanza na zama mpya, mbona tawi alokalia Magufuli ni la mti ule ule? Unapotaja kuanza upya una maana gani kama katiba inayotuongoza ni ile ile ya zamani na sera tunazofuata ni za chama kile kile cha zamani. Ningeelewa kama ungemshauri Magufuli kuanza kutawala kwa kuitupilia mbali katiba na kuachana na maelekezo ya chama chake, hapo japo ungeweza kueleweka.

Wengine tunapolaumu mfumo wewe unasema, hapana, si mfumo ni utamaduni. Tukisema mfumo ndio hujenga mazingira yasiyo ya maadili mema wewe unasema, hapana, tabia ndiyo tatizo. Tukilaumu mfumo kwa kutuletea utamaduni wa kifisadi, wewe unasema, hapana, watu ndio hujenga utamaduni wa kifisadi. Sawa tukubaliane kwamba tatizo ni watu na si mfumo, je tutafanikishaje ujenzi mpya wa taifa jipya chini ya viongozi wale wale ambao wengi wao walikuwa kwenye uongozi wa zama zile zile?


Tuache siasa pembeni. ...kwa mfano akituomba radhi halafu akafanya yale yale inatusaidia nini?

Nafikiri ingekuwa vema tusukume wote gurudumu la mabadiliko. Siasa hazileti msosi juu ya meza za walio wengi isipokuwa kwa wana siasa wachache.

Walio wengi wanataka masahihisho ya makosa ya nyuma ili tusonge mbele
 
Tuliposema kuwa yote haya bila ya kubadirisha mfumo ni maigizo tu, hamkutuelewa mkabaki mnatushambulia.
Ni vizuri kwamba hivi sasa mmeanza kugutuka
 
N
Tunaanza na katiba nzuri iitkayotujengea mfumo ambao hautegemei mtu. Leo hii Mungu akimwita magu tunaweza tukampata kikwete mwingine


Ni nani alikwambia Katiba inazuia hilo??
 
Ni nani alikwambia Katiba inazuia hilo??
Kama hakuna namna ya kumwajibisha kiongozi mkuu wa nchi hata akistaafu, hapo hakuna tunachofanya. Kiongozi akijua madudu yake yatafuatiliwa hata akistaafu hawezi kufanya waliyofanya viongozi wetu wakuu kama Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hata Magufuli mwenyewe. Rais lazima akae akielewa kwamba hayuko juu ya sheria na kwamba akivunja Katiba aliyoapa kuilinda awe tayari kushughulikiwa kama mhalifu yeyote yule. Katiba lazima ioainishe atakavyoshughulikiwa.
 
Back
Top Bottom