Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Nilivyomdhania Magufuli kumbe sivyo...

Hatutaki Katiba Mpya, Magufuli anatosha, na isitoshe hatuna huwo muda!

Kenya wana Katiba mpya lkn hakuna kilichobdailika, wametumia bilions na kuitangaza Dunia nzima, leo hii ufisadi umeongezeka na ni mkubwa klk hata wakati wa KANU, hakuna rule of law walioiahidi, hali ya usalama iko vile vile kama haijaharibika zaidi, deni la nchi limezidi kuongezeka na sasa siyo deni la nchi tu bali kila Jimbo pia linatengeneza deni lake, na kikubwa labda kuliko vyote hiyo tume wanaoiita huru ya uchaguzi hawana Imani nao na tayari Wapinzani wamesema hawatatambua matokeo ya Uchaguzi, sasa kwanini tuende huko??!
Magufuli asipo kuwepo ??
 
Kama hakuna namna ya kumwajibisha kiongozi mkuu wa nchi hata akistaafu, hapo hakuna tunachofanya. Kiongozi akijua madudu yake yatafuatiliwa hata akistaafu hawezi kufanya waliyofanya viongozi wetu wakuu kama Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hata Magufuli mwenyewe. Rais lazima akae akielewa kwamba hayuko juu ya sheria na kwamba akivunja Katiba aliyoapa kuilinda awe tayari kushughulikiwa kama mhalifu yeyote yule. Katiba lazima itaje atakavyoshughulikiwa.

Hiyo ni nadharia tu, Katiba haijengi nchi hata siku moja bali watu wenye nidhamu na Uzalendo wa kweli ndiyo wanaojenga nchi, mifano iko mingi juzi kati huko AK Jakob Zuma amefisadi kuliko maelezo na mwenyewe amekiri tena Bungeni haya hiyo Katiba imesaidia nini???
Kwani wakati Zuma anafisadi hakujua kwamba akitoka anaweza kushitakiwa?? Mbona ameendelea kufisadi???

Acheni kujidanganya hakuna nchi iliyoendelea eti kwa sababu ya Katiba! Kama viongozi ni mafisadi watafisadi tu hata uweke Katiba gani kwani mwisho wa siku bado unahitaji watu kusimamia hizo sheria sasa kama Kiongozi akiweka wote ni watu wake utamshitaki vipi????
 
Magufuli asipo kuwepo ??

Asipokuwepo atakuja mwingine kwani kabla ya Magufuli tulijua kama atakuja kuwa jinsi alivyo leo hii?? Ni Watanzania wangapi kama ungewauliza miezi 10 iliyopita kama Magufuli angeweza kufanya anayoyafanya leo hii wangekubali???

Ndiyo maisha hayo na ndivyo nchi zinavyokwenda zinapanda zinashuka zinapanda zinashuka kidogo zinapanda hivyo hivyo mpaka zinafika juu, cha muhimu klk vyote ni Elimu, kama tukiwekeza kwenye Elimu bora tutakuwa na wananchi ambao wanaweza kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua watu sahihi na siyo Katiba, Katiba haitasaidia kitu kama watu ni wajinga na hawana Elimu!
 
Akija kama Jakaya ?
 
Hatutaki Katiba Mpya, Magufuli anatosha, na isitoshe hatuna huwo muda!
Hivi hapa wewe unaongea kama nani? Hamtaki...wewe na nani? Huko nyuma ulipokuwa ukimtetea Kikwete, kila siku matamko yako yalikuwa tunamtaka, tunamtaka, tunamtaka. Je bado mnamtaka? Kweli una msimamo wowote wewe? Unaitaja katiba ya Kenya bila kujua hiyo katiba ndio imemwezesha hata huyo mpinzani wa serikali ya Kenya kuja Tanzania na kuteta na Rais wa Tanzania bila serikali ya Kenya kupata mhemko kama serikali yetu. Hapa kwetu si ajabu hata Makonda anaweza kumweka ndani Kiongozi Mkuu wa upinzani.
 
Mh. Magufuli ana kazi kubwa sana mbele yake. Lakini tushukuru MUNGU maana Rais anaonesha kuwa ashapata kanuni ( fomular ) ya kulikarabati taifa.
 
john-magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa baadhi yetu tuliokataa kuvingirisha mikono yetu kuunga mkono mabadiliko yaliyobinafsishwa kwa mtu mmoja tulijikuta hatuna budi kumuunga mkono Magufuli tukiamini anawakilisha mabadiliko ya kweli. Binafsi niliamini kabisa kuwa Taifa lilikuwa linamhitaji kiongozi kama Magufuli kuweza kulinasua mahali lilipo kuliko kiongozi yule mwingine toka upinzani. Niliamini kabisa kuwa Magufuli akishika madaraka atakuwa na kazi kubwa ya kulirejesha Taifa katika misingi yake ambayo inaonekana ilikuwa imepotea.

Hatua zake mbalimbali za mwanzo kushughulika na kubana matumizi, kupambana na ufisadi na kuondoa watendaji mizigo a.k.a majipu kulinifanya niamini kabisa kuwa Magufuli kazi aliyonayo akiendelea na kasi hiyo basi ndani ya miezi sita tu atakuwa ameleta heshima katika utumishi wa umma, kurejesha heshima kwa Watanzania na fahari ya taifa letu kurudishwa. Niliamini kabisa kuwa Magufuli atafanya kazi hii bila woga, huruma, husuda, wivu, au kusita sita. Kwamba, hatomwangalia yeyote, popote na kwa lolote. Ndani ya miezi sita hivi na kabla ya ujio wa bajeti ya kwanza ya serikali yake basi Magufuli atakuwa ameshaweka alama za namna gani taifa linataka kwenda na kila kiongozi atakuwa amepata ujumbe.

Nilifanya makosa.

Nilifanya makosa kwa sababu nilidhani hii ni kazi rahisi kwa Rais. Nilidhani ni kazi ya kutimua huyu, kuondoa yule na kumleta yule mwingine. Nilidhani ni kazi ambayo akimaliza teuzi mbalimbali basi atauwa ameipanga serikali yake kwa ajili ya kuchapa kazi.

Sasa najua kuwa uamuzi wake wa kushughulika na watu kwanza kabla ya mfumo ni jambo muhimu sana. Ulikuwa ni uamuzi sahihi na unajitahi kutetewa. Watu ndio hutengeneza mfumo; ni watu ndio ambao hukaa chini na kufanya maamuzi mbalimbali yenye kuathiri (kwa uzuri au ubaya) uwepo na utendaji wa mfumo wa utawala. Ukiwa na watu wabovu, wabinafsi na wenye mwelekeo wa ufisadi basi mfumo utakuwa mbovu, wa kibinafsi na wenye uelekeo wa kifisadi kwa sababu moja kubwa; wale wenye kuiwamba ngoma ngozi huivutia kwao! Mfumo wetu wa utawala wa kifisadi ulitengenezwa na watawala wenye mwelekeo wa kifisadi. Matobo (siyo matundu) kwenye sheria zetu vilitengenezwa na watu ambao walijua wakiziba na wao watakuwa wamejizibia.

Magufuli asingeweza kutengeneza mfumo mwingine kwa kutumia watu wale wale walioutengeneza mfumo huu wa sasa na hasa kama watu hao ni wanufaika wa mfumo huu. Ingelikuwa ni sawa sawa na kumtaka Rais awalazimishe watu wakate matawi ambayo wamekalia huku wakijua kwa kufanya hivyo wataangukia mtoni kwenye mamba wengi. Hakukuwa na jinsi nab ado hakuna jinsi ni lazima kuwaondoa hawa na kuwashughulikia ili kuleta watu wenye fikra zinazoakisi mwelekeo wa serikali yake.

Ni kwa sababu hiyo, kumbe kazi ile ya miezi sita kwa kweli haiwezekani. Ni kazi ambayo inapaswa kuwa endelevu na yenye matokeo bora. Tayari tumeanza kuona dalili za yaliyomo ndani ya ripot ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) na tayari inatisha kama ilivyotisha mwaka 2006 na miaka iliyofuatia. Kwa muda mrefu tumekuwa tukijulishwa juu ya uchafu wa watendaji wetu na taasisi zetu na mara karibu hizo zote tumekuwa tukionesha kushtushwa na kusikitishwa tukiamini kuwa labda mwaka unaofuatia mambo yatakua tofauti. CAG aliyepita alikuwa anarudia baadhi ya hoja mwaka baada ya mwaka na wakati mwingine kuhusiana na taasisi au watu wale wale. Na safari hii tusije kushangaa kuwa hata CAG wa sasa anaweza kujikuta amegusa maeneo yale yale; matumizi mabaya ya sheria ya manunuzi ya umma, fedha kutumiwa bila maelezo, kutopatikana kwa vitabu vya masuala ya fedha wakati wa ukaguzi, na upotevu wa fedha za umma kwa namna ambayo inadokeza tu kuwa zimeliwa.

Magufuli basi ana kazi kubwa; kushughulikia viongozi wabadhirifu, wazembe, wezi, na wenye kutumia madaraka yao vibaya na wakati huo huo kupanga na kusimamia serikali yake huku akiuunda upya mfumo uliojaribiwa na kuharibiwa.

Kwa mwendo alioanza nao hakuna shaka yoyote jambo moja lilikuwa sahihi kwa upande wangu; kuunga mkono mabadiliko haya. Wapo wanadhani hali ni ngumu sasa na kuwa serikali inabana naamini bado hatujaona hasa ugumu kwani hadi hivi sasa bado serikali inahangaika na madudu ya nyuma na yanatisha. Kusahihisha uchumi (correcting an economy) ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) haiwezekani kuwa ni jambo moja.

Ni kwa sababu hiyo naamini:

1. Kuanza kazi kwa mahakama za kushughulikia ufisadi na uhujumu uchumi kunahitajika mara moja

2. Sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema zaidi ili CAG awe na madaraka ya kutoa agizo la kusimamishwa kazi na hata kufikishwa mahakamani kwa mtendaji yeyote wa umma ambaye uchunguzi wake (CAG) unaonesha kuwa kuna uvunjaji wa sheria. Ikiwezekana ofisi ya CAG iwe na Waendesha mashtaka wake kama ilivyo kwa TAKUKURU. Haipaswi madudu yam waka mzima yanasubiri mwaka mwingine kujulikana. CAG anapofanya ukaguzi na kukuta madudu na ushahidi wa kisayansi upo (forensic evidence) basi hatua zichukuliwe mara moja. Siyo awe na uwezo wa kupeleka mashtaka lakini kwa kupendekeza kwa DPP au hata yeye mwenyewe washutumiwa watiwe mbaroni, mali zao zinazohusiwa kupatikana kwa njia haramu kukamatwa ili zije kufilisiwa wakikutwa na hatia.

3. Sheria ya Usalama wa Taifa inahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka – hili ni jambo ambalo limekuwa katika mada zangu kwa karibu miaka kumi sasa. TISS bado ni dhaifu sana na udhaifu wake umechangia sana kutamalaki kwa utamaduni wa kifisadi. Natumaini Magufuli hatochukua muda mrefu kuifumua hii taasisi kwani ndio moyo wa taifa. Ikilegea taifa liko mashakani.

Kuna na mengine mengi ambayo naamini Magufuli atayafanya kwani tayari ameshaanza kuyafanya na kuwa endapo atafanikiwa tutakapofika mwisho wa mwaka huu kama taifa tutashusha pumzi kidogo kwani angalau tutakuwa katika mazingira ya kusema “kweli hakika huyu alikuwa anahitajika”.

Ni wazi pia kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema “hapana” na waleta “vikwazo”. Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu. La maana ni kukaza mwenzo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikani, na nidhamu ili hatimaye Ujenzi Mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni Zama Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu.

Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.
.....namba tatu umegonga penyewe mkuu!!!!!
 
Hivi hapa wewe unaongea kama nani? Hamtaki...wewe na nani? Huko nyuma ulipokuwa ukimtetea Kikwete, kila siku matamko yako yalikuwa tunamtaka, tunamtaka, tunamtaka. Je bado mnamtaka? Kweli una msimamo wowote wewe? Unaitaja katiba ya Kenya bila kujua hiyo katiba ndio imemwezesha hata huyo mpinzani wa serikali ya Kenya kuja Tanzania na kuteta na Rais wa Tanzania bila serikali ya Kenya kupata mhemko kama serikali yetu. Hapa kwetu si ajabu hata Makonda anaweza kumweka ndani Kiongozi Mkuu wa upinzani.

Sasa angalia unaongea vitu vido vidogo eti ujaji wa Odinga TZ ni kwa sababu ya Katiba, mbona mambo muhimu kama Tume ya uchaguzi ambayo inaitwa huru kuwa corrupt klk hata iliyopita hausemi, Majimbo kutengeza madeni kama Serikali Kuu pmj na kuongezeka kwa gharama za uendeshwaji wa Serikali mbona hauviongelei hivyo?
hiyo Bill of rights iliyoandikwa kwenye Katiba yao mpya ina kazi gani kama wanafunzi kama uliona kwenye video wanaadhibiwa na Police kama mateka wa kivita?
Ufisadi Kenya ni mkubwa kulika hata kabla ya Katiba mpya mbona hauongelei hilo na hakuna aliye jela bora hata sisi Kitilya na Mtoto wa lowasa angalau wako Mahabusu kwa ufisadi!
 
Huwa nasema na nitarudia kusema kila siku kwamba Magufuli ni genius, watu wengi hawaamini lkn muda utaongea, mimi nilimkubali Magufuli jinsi tu alivyoweza kupenya CCM na kuibuka kuwa Mgombea wa CCM, ni mtu genius tu ndiyo anaweza kupenya kwenye mto uliojaa mamba wengi namna ile na kuibuka mshindi!
Watu kama Lowasa walijiandaa kwa zaidi miaka 20, walijenga mitandao ya watu wenye ushawishi mkubwa wa fedha na karibia kila kitu lkn hawakupita, na sababu kubwa ni kwamba watu kama Lowasa wana fedha na watu wenye fedha lkn siyo Inteligent men na ndiyo maana wanashindwa kama Lowasa angekuwa intelligent man huu uraisi ulikuwa wake kabisa!

Ikumbukwe kwambaMagufuli hakuwa na kundi, fedha wala watu wazito na wenye ushawishi kwenye Chama hivyo alitegemea Akili yake tu na ndiyo maana hata siku anaaongea na majaji alilisema hilo kwamba mtu kama yeye from now where akaweza kupenya na mwishowe kuapishwa kuwa Raisi wa JMTZ siyo jambo dogo!
Tangia hapo nikajua kwamba Magufuli siyo mtu wa kawaida, najua baadhi wanamdharau na kumdhihaki lkn siku zinavyozidi kwenda idadi yao inazidi kupungua, watu waliokuwa wanamkebehi na kumdhihaki Magufuli hapa JF mwanzoni walikuwa wengi sana leo hii wengi wao wamepotea!

Mambo aliyoyafanya Magufuli kwa nchi hii chini ya miezi 6 hata nchi za Wazungu tunazozifia viongozi wao hawawezi kufanya reforms kubwa namna hii, fikiria kupunguza utegemezi wa bajeti chini ya mwaka 1 ktk 40% mpaka 3% hii siyo kazi ndogo, uwezo tu wa kuteua watu makini kama Waziri Mpango kuwa waziri wa fedha inahitaji akili!

Hivyo kama alivyosema Kikwete hata mimi nalala usingizi kabisa tena nakoroma kwa maana najua TanZania yetu iko salama na tutavuka kama alivyosema Raisi Magufuli!
Umeongea point mkuu,unajua sisi wa Tz tunapenda kulalamika sana na hakuna anaeweza kuwaridhisha binadamu.Lakini kwa kazi jamaa amefanya mpaka sasa anastahili pongezi.Watu wamtie moyo wamuunge mkono aendelee na jitihada zake za kurudisha watu kwenye uzalendo na uajibikaji.Kazi inayomkabili nikubwa na ina risk kubwa sana ,lakini kumbuka watu wanamkwamisha wanamtegea.Kila mtu kwa nafasi yake awajibike ipasavyo amsaidie rais wetu.
 
Chukua likes 100 mzee mwanakijiji, ni juzi tu nilikua naongea na jirani the same perspective... Watu ndio wanaounda mfumo, magufuli lazima atoe watu wabovu kwanza ndio aunde mfumo akiwa na watu wenye mtazamo na wenye ku support nia yake njema kwa wa Tanzanian.

Iko wazi, hii kazi sio ndogo, nashindwa elewa watu wanavyodhihaki hizi hatua, na sijui walitegemea nini.

Rejea mfano wa marekebisho ya katiba itaelewa umuhimu wa watu bora kuunda mfumo.
Namuunga Magufuli mkono asilimia 100.

Swali la kujiuliza ni je waliomzunguka wanacheza tune moja naye??
Vigogo wa TISS hawakuwa wanufaikaji wa huo mfumo uliopita??
Atawezaje kujenga mfumo mpya kama anaowatumia kujenga mfumo wako corrupted, maana nachojua uozo wa hii nchi haujaanzia mikoani wala kwenye mashirika ya umma, uozo ulikua unaishi ndani ya jumba jeupe
 
Mkuu unamaanisha hatuwezi kabisa kutengeneza kuanzia hapa tulipofikia? Japo nakumbuka wahenga wanasema hauwezi kufika unapokwenda hadi urudi pale ulipokosea ndio uanze kutafuta ulipopanga kwenda.
Kumbe jibu unalo...!
 
Mkuu hiyo namba mbili ni hatari sana, kumpa madaraka yote hayo mtu mmoja (CAG) anaweza kuyatumia vibaya. Yani yeye afanye ukaguzi na awe na uwezo wa kushtaki na kufukuza ni hatari ukipata mtu ambaye mwehu. Lazima kuwa na segregation of duties
 
Kumbe jibu unalo...!

Hakuna jibu moja linalofaa au kutatua matatizo yote mkuu, changamoto ni nyingi na za kila aina, zinahitaji mtazamo mpya na njia tofauti kukabiliana nazo. Hilo huenda likawa mojawapo ya jibu lakini lisiwe jibu pekee.
 
N
Tunaanza na katiba nzuri iitkayotujengea mfumo ambao hautegemei mtu. Leo hii Mungu akimwita magu tunaweza tukampata kikwete mwingine
Kwa nchi changa kama hizi mfumo kufanya kazi kwa kujitegemea bila kutegemea watu bado ni ngumu sana.

Lazima awepo mtu mwenye strong political will at the top, halafu mfumo ufanye kazi yake, otherwise ni yale yale ya JK tu
 
Mkuu hiyo namba mbili ni hatari sana, kumpa madaraka yote hayo mtu mmoja (CAG) anaweza kuyatumia vibaya. Yani yeye afanye ukaguzi na awe na uwezo wa kushtaki na kufukuza ni hatari ukipata mtu ambaye mwehu. Lazima kuwa na segregation of duties

Segregation of duties kwa nchi zetu za kiafrika bado ni shida mkuu, umeona kilichotokea Afrika ya Kusini? Licha ya maamuzi ya mahakama, Rais ameendelea kutamalaki pamoja na kashafa zote zile. Safari ni ndefu sana
 
Tuache siasa pembeni. ...kwa mfano akituomba radhi halafu akafanya yale yale inatusaidia nini?
Tutasamehe na kusonga mbele pamoja lakini kwa sasa tutamuungaje mkono bila maelezo kuhusu ushiriki wake huko nyuma? Tutamwamini vipi?
Nafikiri ingekuwa vema tusukume wote gurudumu la mabadiliko. Siasa hazileti msosi juu ya meza za walio wengi isipokuwa kwa wana siasa wachache.
Afadhali kama wewe ni miongoni mwa wenye unafuu wa maisha baada ya miezi sita toka Magufuli akamate madaraka. Je mabadiliko yameweza kukuletea msosi mezani?
Walio wengi wanataka masahihisho ya makosa ya nyuma ili tusonge mbele
Usiwe na wasi wasi, tutasamehe lakini hatutasahau nusu karne ya matatizo yaliyosababishwa na watawala wetu.
 
Mkuu, uko sahihi , mifumo huundwa na watu sio mifumo huunda watu,(kwanza kinachoitwa mifumo ni nadharia tu) kwa hiyo aina ya watu waliopo kwenye mfumo au wanaounda mfumo ndio hutoa muelekeo wa mfumo wenyewe
Kweli kabisa. Mfano taasisi za umma zina mifumo mizuri tu ya internal control lakini tumewahi kujiuliza kwanini haifanyi kazi? Tusipige siasa penye kuhitaji tafakuri za kizalendo ...
 
john-magufuli.jpg
Na. M. M. Mwanakijiji

Kwa baadhi yetu tuliokataa kuvingirisha mikono yetu kuunga mkono mabadiliko yaliyobinafsishwa kwa mtu mmoja tulijikuta hatuna budi kumuunga mkono Magufuli tukiamini anawakilisha mabadiliko ya kweli. Binafsi niliamini kabisa kuwa Taifa lilikuwa linamhitaji kiongozi kama Magufuli kuweza kulinasua mahali lilipo kuliko kiongozi yule mwingine toka upinzani. Niliamini kabisa kuwa Magufuli akishika madaraka atakuwa na kazi kubwa ya kulirejesha Taifa katika misingi yake ambayo inaonekana ilikuwa imepotea.

Hatua zake mbalimbali za mwanzo kushughulika na kubana matumizi, kupambana na ufisadi na kuondoa watendaji mizigo a.k.a majipu kulinifanya niamini kabisa kuwa Magufuli kazi aliyonayo akiendelea na kasi hiyo basi ndani ya miezi sita tu atakuwa ameleta heshima katika utumishi wa umma, kurejesha heshima kwa Watanzania na fahari ya taifa letu kurudishwa. Niliamini kabisa kuwa Magufuli atafanya kazi hii bila woga, huruma, husuda, wivu, au kusita sita. Kwamba, hatomwangalia yeyote, popote na kwa lolote. Ndani ya miezi sita hivi na kabla ya ujio wa bajeti ya kwanza ya serikali yake basi Magufuli atakuwa ameshaweka alama za namna gani taifa linataka kwenda na kila kiongozi atakuwa amepata ujumbe.

Nilifanya makosa.

Nilifanya makosa kwa sababu nilidhani hii ni kazi rahisi kwa Rais. Nilidhani ni kazi ya kutimua huyu, kuondoa yule na kumleta yule mwingine. Nilidhani ni kazi ambayo akimaliza teuzi mbalimbali basi atauwa ameipanga serikali yake kwa ajili ya kuchapa kazi.

Sasa najua kuwa uamuzi wake wa kushughulika na watu kwanza kabla ya mfumo ni jambo muhimu sana. Ulikuwa ni uamuzi sahihi na unajitahi kutetewa. Watu ndio hutengeneza mfumo; ni watu ndio ambao hukaa chini na kufanya maamuzi mbalimbali yenye kuathiri (kwa uzuri au ubaya) uwepo na utendaji wa mfumo wa utawala. Ukiwa na watu wabovu, wabinafsi na wenye mwelekeo wa ufisadi basi mfumo utakuwa mbovu, wa kibinafsi na wenye uelekeo wa kifisadi kwa sababu moja kubwa; wale wenye kuiwamba ngoma ngozi huivutia kwao! Mfumo wetu wa utawala wa kifisadi ulitengenezwa na watawala wenye mwelekeo wa kifisadi. Matobo (siyo matundu) kwenye sheria zetu vilitengenezwa na watu ambao walijua wakiziba na wao watakuwa wamejizibia.

Magufuli asingeweza kutengeneza mfumo mwingine kwa kutumia watu wale wale walioutengeneza mfumo huu wa sasa na hasa kama watu hao ni wanufaika wa mfumo huu. Ingelikuwa ni sawa sawa na kumtaka Rais awalazimishe watu wakate matawi ambayo wamekalia huku wakijua kwa kufanya hivyo wataangukia mtoni kwenye mamba wengi. Hakukuwa na jinsi nab ado hakuna jinsi ni lazima kuwaondoa hawa na kuwashughulikia ili kuleta watu wenye fikra zinazoakisi mwelekeo wa serikali yake.

Ni kwa sababu hiyo, kumbe kazi ile ya miezi sita kwa kweli haiwezekani. Ni kazi ambayo inapaswa kuwa endelevu na yenye matokeo bora. Tayari tumeanza kuona dalili za yaliyomo ndani ya ripot ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) na tayari inatisha kama ilivyotisha mwaka 2006 na miaka iliyofuatia. Kwa muda mrefu tumekuwa tukijulishwa juu ya uchafu wa watendaji wetu na taasisi zetu na mara karibu hizo zote tumekuwa tukionesha kushtushwa na kusikitishwa tukiamini kuwa labda mwaka unaofuatia mambo yatakua tofauti. CAG aliyepita alikuwa anarudia baadhi ya hoja mwaka baada ya mwaka na wakati mwingine kuhusiana na taasisi au watu wale wale. Na safari hii tusije kushangaa kuwa hata CAG wa sasa anaweza kujikuta amegusa maeneo yale yale; matumizi mabaya ya sheria ya manunuzi ya umma, fedha kutumiwa bila maelezo, kutopatikana kwa vitabu vya masuala ya fedha wakati wa ukaguzi, na upotevu wa fedha za umma kwa namna ambayo inadokeza tu kuwa zimeliwa.

Magufuli basi ana kazi kubwa; kushughulikia viongozi wabadhirifu, wazembe, wezi, na wenye kutumia madaraka yao vibaya na wakati huo huo kupanga na kusimamia serikali yake huku akiuunda upya mfumo uliojaribiwa na kuharibiwa.

Kwa mwendo alioanza nao hakuna shaka yoyote jambo moja lilikuwa sahihi kwa upande wangu; kuunga mkono mabadiliko haya. Wapo wanadhani hali ni ngumu sasa na kuwa serikali inabana naamini bado hatujaona hasa ugumu kwani hadi hivi sasa bado serikali inahangaika na madudu ya nyuma na yanatisha. Kusahihisha uchumi (correcting an economy) ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) haiwezekani kuwa ni jambo moja.

Ni kwa sababu hiyo naamini:

1. Kuanza kazi kwa mahakama za kushughulikia ufisadi na uhujumu uchumi kunahitajika mara moja

2. Sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema zaidi ili CAG awe na madaraka ya kutoa agizo la kusimamishwa kazi na hata kufikishwa mahakamani kwa mtendaji yeyote wa umma ambaye uchunguzi wake (CAG) unaonesha kuwa kuna uvunjaji wa sheria. Ikiwezekana ofisi ya CAG iwe na Waendesha mashtaka wake kama ilivyo kwa TAKUKURU. Haipaswi madudu yam waka mzima yanasubiri mwaka mwingine kujulikana. CAG anapofanya ukaguzi na kukuta madudu na ushahidi wa kisayansi upo (forensic evidence) basi hatua zichukuliwe mara moja. Siyo awe na uwezo wa kupeleka mashtaka lakini kwa kupendekeza kwa DPP au hata yeye mwenyewe washutumiwa watiwe mbaroni, mali zao zinazohusiwa kupatikana kwa njia haramu kukamatwa ili zije kufilisiwa wakikutwa na hatia.

3. Sheria ya Usalama wa Taifa inahitaji kufanyiwa marekebisho ya haraka – hili ni jambo ambalo limekuwa katika mada zangu kwa karibu miaka kumi sasa. TISS bado ni dhaifu sana na udhaifu wake umechangia sana kutamalaki kwa utamaduni wa kifisadi. Natumaini Magufuli hatochukua muda mrefu kuifumua hii taasisi kwani ndio moyo wa taifa. Ikilegea taifa liko mashakani.

Kuna na mengine mengi ambayo naamini Magufuli atayafanya kwani tayari ameshaanza kuyafanya na kuwa endapo atafanikiwa tutakapofika mwisho wa mwaka huu kama taifa tutashusha pumzi kidogo kwani angalau tutakuwa katika mazingira ya kusema “kweli hakika huyu alikuwa anahitajika”.

Ni wazi pia kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema “hapana” na waleta “vikwazo”. Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu. La maana ni kukaza mwenzo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikani, na nidhamu ili hatimaye Ujenzi Mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni Zama Mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu.

Katika hili, naamini nilikuwa sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.

Upo sahihi mkuu

Bwana Pombe ameshakosea njia. Anachofanya hakuna ni maigizo tu. HAKI tu itakuwa kipengele pekee cha kumpima mwelekeo wake. HAKI kwa kila mTanzania. Mzee wetu Yohana Pombe (siyo mtembezi) ni mbaguzi, ona anavyo wafanya wapinzani. Ona anavyo shindwa hata kusema neno juu ya Zanzibar. Kuthibitisha wamewaambia viongozi wakandamizaji wa haki za demokrasia ambayo pia ni haki za msingi ya binadamu. Tumenyimwa msaada kwa sababu HAKUNA HAKI
 
Back
Top Bottom