Niliua kwa Kukusudia--25-
ILIPOISHIA WIKIENDA:
Nilishituka baada ya kuguswa na kitu kisichokuwa cha kawaida mwilini mwangu. Nikafumbua macho kwa tabu. Sikuamini nilichokishuhudia. Ghafla ulevi ukaniisha. SASA ENDELEA…
Tulikuwa ndani ya gari kwa upande wa nyuma. Bosi alikuwa amevua suruali yake na kukomea magotini, ambapo sasa alikuwa amebaki kama alivyozaliwa. Mkono wake wa kuume ulikuwa ukijaribu kunivua sketi niliyokuwa nimevaa.
Nikajitutumua kwa kumsukuma japo sikuwa na nguvu sawia kutokana na ile hali ya ulevi.
Bosi alipoona kuwa nilijaribu kuleta kipingamizi, sasa alitaka kwa nguvu kutimiza alichokuwa amedhamiria dhidi yangu. Alikuwa akinibaka. Sikuwa tayari hata kidogo kufanyiwa kitendo kama kile bila ridhaa yangu. Nikawa naizuia mikono ya bosi Elhakimu aliyekuwa akiendelea kunivua kwa nguvu.
Purukushani iliendelea ndani ya gari huku nikijaribu kupiga kelele za kuomba msaada lakini hakuna aliyesikia kutokana na milango ya gari lile la kifahari kuwa imefungwa, vioo vyake vilikuwa vyeusi ambavyo kwa kisasa huitwa tintedi. Nikawa najaribu kumuondoa bosi maungoni mwangu lakini sikufanikiwa kutokana na kuzidiwa nguvu.
Hatimaye nikaamua kumuacha yule Mwarabu ambaye kwa wakati huo sikuwa nikimhesabu kama bosi tena kutokana na kitendo cha udhalilishaji alichokuwa akinifanyia kwa wakati huo. Katika maisha yangu sikuwahi kusikia maumivu makali kama hayo.
Maumbile makubwa ya yule Mwarabu yaliniumiza. Maumivu yalikuwa ni makali, hayasimuliki na kumbuka kuwa ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuingiliwa na mwanaume, tena kwa nguvu na bila ridhaa yangu, yaani nilikuwa nabakwa! Inauma mno, hadi sasa kila nikikumbuka juu ya tukio hilo, machozi hunitiririka.
Bila huruma huku akitoa sauti ya kuashiria kufurahishwa na kitendo kile, Mwarabu huyo aliendelea kutoa sauti ya miguno. Licha ya kulia kwa nguvu na maumivu, Elhakimu hakujali, kwa takriban saa moja na nusu aliendelea kuniingilia kwa nguvu nyingi kadiri alivyoweza.
Baada ya kumaliza kunitendea unyama huo, Elhakimu alivaa na kuniacha nyuma ya gari nikiwa nimelala, nilijaribu kuinuka lakini nikashindwa, nikatupa macho sehemu zangu za siri, machozi yalinitiririka, nilikuwa nimeharibika vibaya mno. Ghafla nikiwa katika hali ile, macho yalianza kuona giza kwa mbali, nikasikia yule Mwarabu akiwasha gari, nikawa nasikia kizunguzungu cha ajabu huku giza likizidi kutanda machoni na kizunguzungu kikazidi kunisumbua, baada ya hapo sikujua kilichoendelea.
*****
Majira ya saa kumi na moja alfajiri, fahamu zilianza kunirejea taratibu. Nikafumbua macho na kuanza kuangaza huku na kule. Nilikuwa ndani ya chumba kilichokuwa na vitanda vingi sana. Nilipojaribu kunyanyuka, nilishindwa kutokana na mikono yangu kubanwa na kitu ambacho kwa haraka sikukijua.
Nikaangaza macho vizuri na kugundua nilikuwa hospitali nikiwa nimelazwa, kwa haraka sikuweza kukumbuka nilifikaje mahali pale na kwa nini nilikuwa nimelazwa. Kumbukumbu za matukio yote ya jana yake zilianza kumiminika kichwani mithili ya filamu ya Kihindi ambapo kila kitu kilikuwa kikipita kichwani.
Katika kukumbuka, ndipo tukio la yule Mwarabu kunibaka likauvamia kwa kasi ubongo wangu. Maumivu yalirejea upya na kuanza kulia. Nilipojaribu kujitingisha, maumivu yalikuwa makali kuliko neno lenyewe!
Mikononi nilikuwa na dripu za maji. Nikaanza kulia kwa nguvu huku nikitaja majina ya wazazi wangu. Ulimwengu ulikuwa umenigeuka sasa, maisha yalikuwa yakinielemea, najaribu kujihangaikia lakini shetani anazidi kuweka kucha zake katika kila njia ninayojaribu kuipita.
Nilianza kulia taratibu, lakini kadiri kumbukumbu za tukio la kubakwa zilivyozidi kuongezeka, ndivyo sauti ya kilio ilizidi kuongezeka ndani ya wodi na kujikuta nikigeuka kero kwa wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa!
"Dokta, dokta, doktaaa," nikazidi kuita huku nikilia kwa nguvu. Mchanganyiko wa maumivu na uchungu wa kubakwa na mtu niliyemuamini kama Elhakimu, ulizidi kunifanya niione dunia kama jehanamu.
Muda mfupi baadaye, alikuja daktari kwa mwendo wa haraka hadi nilipokuwa nimelazwa na kuniinamia huku akiniangali kwa hofu kubwa.
"Mungu ni mkubwa, uliletwa hapa ukiwa hujitambui kabisa," alisema yule dokta na kunifanya nianze kukumbuka ni nani aliyelileta mahali pale.
"Nani alinileta dokta?" nikajikuta nikimuuliza kwa sauti ya kwikwi ikisindikizwa na machozi yaliyosababishwa na maumivu makali niliyokuwa nayo.
Wakati dokta akijiandaa kunijibu, ghafla mlango ulifunguliwa na kutokea mtu ambaye wote tulibaki tumemuangalia kwa mshangao!
Je, nini kiliendelea? Usikose kufuatilia simulizi hii ya kusisimua leo jioni usichoke tu....