Niliuwa kwa kukusudia-1

Niliuwa kwa kukusudia-1

Niliua kwa Kukusudia--28-


ILIPOISHIA:
Kwa ushahidi niliokuwa nao niliamini Elhakimu angepatikana na hatia, angenilipa fidia kwa kitendo alichonifanyia na kufungwa jela miaka thelathini ili iwe fundisho kwa wanaume wenye tabia kama yake.

Pale kituoni nilimkuta mkuu wa kituo, nikamweleza shida yangu lakini baada ya kumtajia kuwa mhusika alikuwa ni Elhakimu yule Mwarabu, mkuu wa kituo alishtuka na kutamka maneno yaliyonifanya niishiwe nguvu.
SASA ENDELEA…


likiri wazi kuwa kama kweli mhusika alikuwa ni Elhakimu, ilikuwa ni vigumu mno kumtia hatiani kutokana na nguvu kubwa aliyokuwa nayo kwa baadhi ya viongozi wakubwa serikalini. Nguvu iliyotokana na ushawishi wa fedha aliyokuwa nayo.

Mara nyingi kila alipokuwa akifanya maovu, hakusita kumwaga fedha chafu na kuwahonga viongozi. Katika hali ya kushangaza, mkuu wa kituo alikuwa mkali na kunigeuzia kibao kwa madai kuwa huenda natumiwa na wabaya wa Elhakimu ili kumchafulia jina, kauli ambayo ilinikata maini na kunifanya nimuangalie yule mkuu wa kituo kwa jicho kali na la chuki.
"Wewe binti wewe, usitake kuhatarisha maisha yako kwa pesa ndogo na za kijinga ulizohongwa na maadui wa Elhakimu wanaotaka kumharibia sifa nzuri ya jina lake," alisema yule mkuu wa kituo kwa sauti ya ukali na kufoka huku akinikazia macho yake mekundu.
"Hapana afande, hakika Elhakimu amenibaka, tena akanitupa mtaroni baada ya kunifanyia unyama huo, naomba unisaidie ili haki itendeke na kumfikisha mbele ya sheria, naomba baba yangu," nilisema kwa sauti iliyochanganyika huruma na hasira, hakika chuki niliyokuwa nayo dhidi ya Elhakimu haikuwa na mfano wa kusimulika hata kwa chembe.
"Ushahidi wa kuwa umebakwa na Elhakimu uko wapi," aliniuliza huku akinisogelea mahali nilipokuwa nimesimama karibu kabisa na meza ya mapokezi ya kituo hicho kidogo cha polisi.
"Kama ulivyoona vipimo vya daktari hivi hapa," nikamjibu na kumyooshea kwa vidole vipimo na maelezo ya daktari aliyokuwa ameyashikilia mkononi.

"Sawa, haya ni maelezo tu nataka ushahidi kwamba aliyekubaka ni Elhakimu."
"Lakini baba, nimekuja kuripoti jinsi nilivyobakwa, pia nikakutajia mhusika sasa mbona ninageuka mtuhumiwa kwa kunihojiwa rundo la maswali magumu namna hii?" nilijikuta nikitamka maneno hayo mazito mbele ya mkuu huyo wa kituo huku nikijishangaa mwenyewe kwa ujasiri mkubwa nilioutumia.

"Kwa hiyo unanifundisha kazi siyo," akahoji tena kwa kufoka.
"Sasa sikiliza, kwa leo nafungua maelezo yako kwenye kitabu cha kutoa taarifa, yaani Reporting Book (RB)," alisema na kuchukua daftari kubwa lilikokuwa na maandishi makubwa ya rangi ya bluu kwa juu.
Kwa muda wa dakika saba, alikuwa akiandika kitu ambacho sikukijua, alipomaliza aliniangalia huku akiwa kimya.
"Haya, sasa anza kueleza upya huku nikiandika maelezo yako kwenye daftari hili."

Nikaanza kusimulia jinsi ambavyo nilikutana na Elhakimu, alivyonigonga hadi kuanza kufanya kazi hotelini kwake, nikasimulia hadi siku hiyo ya tukio ambapo alinialika kwa chakula cha jioni na kunieleza nia yake ya kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mimi.
Pia, nikaeleza namna ambavyo nilimkatalia kwa msimamo wa hali ya juu, hata tulivyoanza kunywa pombe mimi Redd's na yeye Grants.
Kila nilichokuwa nikieleza, yule mkuu wa kituo alikuwa akiandika na kunitazama usoni kila mwisho wa sentensi.

Baada ya maelezo, yule afande aliniambia niende nyumbani ambapo alinitaka kurudi kesho yake kwa ajili ya taratibu nyingine za kisheria. Akaahidi kunikutanisha na Elhakimu.
Sikujua nia na lengo la yeye kunikutanisha na Elhakimu ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mtuhumiwa wa ubakaji.

"Sasa huyu ana maana gani, kwa nini asikamatwe huyo Elhakimu ili ajibu mbele ya mahakama?" niliwaza huku nikiondoka kituoni hapo.
"Sikiliza wewe binti, hakikisha kuwa kila ulichokisema kina ukweli na uhakika halisi, huyu mtu si wa mchezo," alisema yule afande lakini sikujibu chochote zaidi ya kumkazia macho na kuanza kuondoaka kituoni hapo.
Moyoni niliamini kuwa yule afande alikuwa ni miongoni mwa watumishi wa serikali waliokuwa wakimuogopa na kumhusudu Elhakimu kutokana na jeuri ya fedha aliyokuwa nayo, ndiyo maana alikuwa akitoa kauli mbaya na chungu za kunikatisha tamaa kabisa.
Wakati nakata kona ya kuelekea nyumbani kwangu, ghafla lilikuja gari moja la kifahari jeusi lililokuwa na vioo vyeusi visivyoonesha ndani na kupaki karibu kabisa na miguu yangu.

Je, nini kitafuata? Usikose
leo jioni

 
Niliua kwa Kukusudia - 29
[h=1]ILIPOISHIA [/h]Wakati nakata kona ya kuelekea nyumbani kwangu, ghafla lilikuja gari moja la kifahari jeusi lililokuwa na vioo vyeusi visivyoonesha ndani na kupaki karibu kabisa na miguu yangu.
SASA ENDELEA…



Nilishituka na kusogea pembeni kidogo ambapo nilianza kuchungulia kwa umakini ili kujua ni nani aliyekuwa ndani ya gari hilo.

Nikiwa naendelea kusumbua ubongo wangu juu ya hilo, ghafla niliona kioo cha upande wa dereva kikianza kushuka taratibu, nikatoa macho nikiwa na hamu ya kujua ni nani aliyekuwa ndani. Bila kutarajia alishuka yule mdogo wake na Elhakimu aliyekuwa akiishi na mdogo wangu Inana.
"Habari za kwako?" alinisabahi huku akionesha uso wa uchangamfu wa hali ya juu. Sikumjibu kwa furaha kama siku zote, hali iliyomlazimu ashuke haraka ndani ya gari na kuja hadi nilipokuwa nimesimama. Akaanza kuniangalia kuanzia miguuni hadi utosini mwa kichwa na kushusha tena macho taratibu huku akionesha dalili zote za kunishangaa.
"Vipi Tunu, kulikoni?"
"Hapana, niko sawa na mdogo wangu anaendeleaje?"
"Anaendelea salama, lakini ni kama una tatizo, naweza kukusaidia tafadhali!"
"Aah, hapana lakini naomba ukifika nyumbani umwambie kuwa namhitaji aje kwangu, sawa?"
"Sawa lakini chukua hii kama nauli maana jua linaanza kuwa la utosi sasa," alisema Ashraf ndipo nikagundua wazi kwamba hakuwa akijua unyama alionitendea kaka yake Elhakimu.

Akaingiza mkono mfukoni na kutoa pochi lake la kutunzia fedha, haraka akatumbukiza mkono na kutoa noti nyekundu kama tano hivi.
Baada ya kunipa akarejea kwenye gari lake akaondoka huku akiniacha nikiwa nimesimama wima.
Japo hapakuwa mbali sana na mahali nilipokuwa nikiishi, Ashraf hakulijua hilo, nikajikongoja kuelekea nyumbani kwangu.

Maumivu yalikuwa ni makali ambapo licha ya kupewa dawa nyingi zikiwemo zile za kuzuia maambukizi lakini niliendelea kupata maumivu makali sehemu zangu za siri na kiunoni.
Kadiri maumivu yalivyozidi kushamiri kila nilipokuwa nikipiga hatua, ndivyo chuki dhidi ya Elhakimu zikazidi kunipanda, kwa mara ya kwanza maishani mwangu nikatamani kulipiza kisasi kwa kuua!

Yalikuwa ni mawazo mabaya mno kwa mtoto wa kike tena binti mdogo kama mimi kuyawaza, lakini sikuwa na jinsi, hakika nikajikuta nikidhamiria kuua japo hadi wakati huu sikujua nitaua kwa njia gani.
"Lakini kwani lazima uue, hakuna njia nyingine ya kulipiza kisasi tofauti na kuua," nilisikia sauti ikijirudia nafsini mwangu. Nikazidi kubaki njia panda.

Wakati nausogelea mlango, ghafla sauti ya marehemu mama yangu ikaanza kusikika moyoni.
"Hakika usilipize baya kwa baya, siku zote epuka maisha ya visasi kwa wakukoseao, kamwe usilipe kisasi kwa yoyote akutendeaye kosa, hata kama ni kubwa namna gani," ilikuwa ni sauti ya mama ikijirudia kwa kasi ya umeme, maneno ambayo alipenda kuniambia mara kwa mara enzi za uhai wake.

"Hapana mama, kwa hili utanisamehe, siwezi kuacha kulipiza kisasi kwa mtu kama Elhakimu, hapana mama, nisamehe mama yangu popote ulipo, lazima nilipe uovu huu, tena kwa sasa natamani kuua, nisamehe mama, hata Allah anisamehe kwa hili.
"Kwani si uliamua kutegemea sheria, subiri akamatwe na haki yako itapatikana ndipo sheria ichukue mkondo wake, kuliko hiyo hatua mbaya ya kuua unayotaka kuichukua," sauti nafsini mwangu ikazidi kuchukua nafasi kubwa. Nilikuwa katika wakati mgumu na mbaya mno.
Kwa hapa naomba niweke wazi kitu kimoja kabla sijaendelea na simulizi hii ya kuumiza.
Maumivi juu ya tukio hilo la kubakwa na Elhakimu yalikuwa ni mara mbili, mosi alikuwa amenivunjia malengo yangu ambayo nilikuwa nimejiwekea kuwa ni lazima mume wangu aikute heshima yake ya ndoa. Lazima awe wa kwanza kukipasua kikombe changu, sasa ndoto na malengo hayo yalikuwa yamefutwa na Elhakimu. Hakika nilimchukia kuliko kiumbe chochote kinachoishi chini ya jua.

Pili, sikuwahi kufikiri kama kuna siku nitadhalilishwa kama alivyonitendea Elhakimu, hakika moyo wangu ulikuwa umejawa na maumivu makali yasiyosimulika kwa maneno wala maandishi.
Mateso, maumivu, simanzi, huzuni na masononeko yalikuwa ni sehemu ya maisha yangu kwa wakati huo, hakika sikujua ni kwa nini Elhakimu ambaye nilimheshimu na kumchukulia kama mzazi wangu alifikia hatua ya kunifanyia unyama ule bila ya chembe ya huruma.
"Lazima niue," nilijikuta nikitamka maneno hayo kwa sauti ya juu.


Je, nini kitaendelea? Fuatilia
Usiku mwingi...
 
Mchunie tu,
Kumdedisha haiondoi ukweli kua alikubaka.

Halafu pengine ungemkubalia angeweza kufanya kiulaini tu then usiumie kihivyo. Mi wakati unakula hela zake mbona nlishahisi hatari mbeleni?
 
Mmmhmmh!!! Japo kuwa inauma sn lkn angejaribu kipinguza hasira na kumuachia mungu coz hatutakiwi kulipiza kisasi!!! Je km mungu angekuwa anatulipiza cc kwa yt tunayokosea!!!! Tujifunze kulia na mungu wetu coz yy alikuwa anayajua hy tng mwnz na angeweza kuzuia lkn alikuwa lzm apitie hk
 
Back
Top Bottom