Niliuwa kwa kukusudia-1

Niliuwa kwa kukusudia-1

Niliua kwa Kukusudia -22-

ILIPOISHIA

Niliingia ofisini, lakini nilishtuka kumkuta bosi akiwa ameshika bastola huku akiifuta kwa kitambaa, nikabaki nimetoa macho.

SASA ENDELEA…


PAMOJA na kwamba ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuona bastola ana kwa ana, hali ile ilinishtua sana. Nishtuka kwa mengi, kwanza sikuwahi kuwaza au kufikiria kuwa yule Mwarabu alikuwa akimiliki silaha ya aina hiyo.

Nikabaki nimetoa macho mithili ya mjusi aliyekuwa amebanwa na mlango. Huku mwili ukinitetemeka, nilijikaza na kumuamkia.
"Shikamoo bosi."

"Marahaba," aliitikia huku akiendelea kuifuta ile bastola na kuigeuza mara kwa mara. Hakuonekana kabisa kujali uwepo wangu ofisini kwake.
Kila mara, uoga wangu ulizidi kuongezeka. Hali hiyo ilichangiwa na kumuona akiwa katika uso wa hasira sana. Hakika niliogopa kuliko maelezo.

"Vipi, mbona unashtuka na kuonesha woga kiasi hicho?" aliniuliza na kunisogelea kitendo kilichozidisha woga maradufu moyoni mwangu. Bila kutarajia nikaanza kutetemeka.
"Hii inaitwa bastola aina ya Beretta, inanisaidia kujilinda kwa mambo mengi sana," akasema na kuisogeza karibu yangu. Ilitisha kwa kuitazama tu. Akazidi kunisogelea, aliponifikia akanishika begani kwa kutumia mkono mmoja. Hapo nikazidi kujawa na hofu kubwa. Kijasho chembamba kikawa kinanichuruzika.
"Usiogope, hii ni silaha ya kawaida sana, ukitaka kuitumia unafanya hivi," alianza kunielekeza namna ya kuitumia.
Akanifundisha kila kitu. Nikajikuta nikivutiwa na jinsi ya kuitumia ile bastola. Ghafla hofu na woga wa awali ulianza kunitoka. Sijui ni kwa nini lakini huenda ni kutokana na lugha laini ambayo alikuwa akiitumia huyo Mwarabu yaani bosi Elhakimu.
Baada ya maelekezo yake, nikamweleza shida yangu ambapo tofauti kabisa na matarajio yangu, alikubali kirahisi mno kunisaidia kiasi cha pesa kilichohitajika kukamilisha upangaji wa chumba.
Akarudi kwenye kiti chake. Taratibu akafungua droo iliyokuwa chini kabisa ya meza yake. Akaiweka ile bastola kisha akanitazama usoni huku akitabasamu.
Alinitazama sana usoni hali ambayo ilinifanya nione aibu na kuishia kuinama na kuanza kupikicha vidole vyangu.
Akachukua kalamu na kikaratasi kidogo na kuanza kuandika maandishi ambayo sikuyaelewa kutokana na umbali uliokuwepo kati yetu.
"Sikiliza Tunu, mimi siwezi kukukopesha pesa ila nimeamua kukusaidia, sawa binti mzuri?" akasema na kunifanya nishtuke tena. Kilichonishtua si kitendo cha kunisaidia ila ni ile kauli ya kuniita binti mzuri. Kwa jinsi ambavyo nilikuwa nikiheshimiana na huyo Mwarabu, tena akiwa bosi wangu, hakuwahi kuniita jina kama hilo tofauti na Tunu.
Akachukua simu yake ya mezani na kupiga namba fulani. Muda mfupi baadaye, aliingia msichana mrefu mwembamba, mweupe na mchangamfu sana.
"Tunu," aliniita yule bosi.

"Bee," nikaitika na kumtamza usoni.
"Huyu ni mhasibu wetu, anaitwa Zulekha, naomba uongozane naye ili akupatie hiyo pesa ambayo naamini itasaidia mahitaji yako."

Licha ya kutomtajia bosi ni kiasi gani cha pesa nilichohitaji, nilishangaa akisema kuwa anaamini kitasaidia kukidhi mahitaji yangu. Nikaongozana na yule mhasibu hadi ofisini kwake.
Wakati tunaondoka, yule bosi Mwarabu akaniambia nipitie tena ofisini kwake kuna maagizo aliyotaka kunipa.

Tulipofika ofisini kwa mhasibu huyo, alichukua bahasha na kuanza kunihesabia pesa alizoagizwa na bosi anipatie. Akanikabidhi kisha nikaondoka. Nilipofika nje, nikaanza kuzihesabu zile pesa ambazo zilikuwa ni shilingi laki mbili na nusu. Sikuamini hata kidogo. Kwa mbali nikaanza kumuona yule Mwarabu kama mkombozi wangu maishani. Niliamini hata kitendo chake cha kunigonga na gari kule Chalinze, ulikuwa ni mpango wa Mungu.
"Nimeamini kila jambo hutokea kwa makusudi, kumbe huyu Mwarabu kunigonga na gari ulikuwa ni mpango mkubwa wa Mungu, ahsante Mola wangu," nilijikuta nikitamka maneno hayo.
Baada ya kuzihesabu, nikazirudisha kwenye bahasha kisha nikaelekea ofisini kwa bosi ili nikamsikilize tena alichoniitia. Moyoni nilijawa na furaha ya ajabu mno.

Kila aliyeniona kwa wakati huo, aliweza kung'amua kwa haraka sana furaha niliyokuwa nayo. Hakika nilifurahi, nashindwa hata kuelezea ni furaha ya kiwango gani.
Nikafungua mlango wa bosi na kumkuta akizungumza na simu. Alipomaliza alinigeukia akiwa na uso wa huzuni.

Usinione nina uso wa huzuni hivi, nina habari kutoka kwa yule mdogo wangu, zinamhusu mdogo wako," akasema na kunikazia macho kauli iliyonifanya nishtuke kwa nguvu.

Je, Inana amepatwa na nini? Fuatilia



 
Mbona inahuzunisha sana hii story? Mwisho wake ni nini? Unataka tujifunze nini kutokana na kisa hiki?????
 
MziziMkavu nilikuwa nasubiri ck nzima ya leo bahati mbaya nilipitiwa na usingiz kbl hujapost!!! Ss nimeshtuka saiz kupunguza maji mwilin nikasema hebu nichungulie huenda ikawa tayari keshapost duuuh nimefurahi sn bt mbona km inahuzunisha??? Nn unataka tujifunze?? Cjui km nitalala tena bt bd mapema mmmh kesho kusinzia kwa ofs ni lzm samahan boss!!!!
 
Niliua kwa Kukusudia--23-

ILIPOISHIA :
Usinione nina uso wa huzuni hivi, nina habari kutoka kwa yule mdogo wangu zinamhusu mdogo wako," akasema na kunikazia macho kauli iliyonifanya nishituke.
SASA ENDELEA…

Kauli ya bosi ilinifanya nikae vyema kwenye kiti na kuanza kumsikiliza kwa umakini mkubwa kuliko ule wa awali. Kengele ya hatari ilikuwa imeshaanza kugonga kichwani mwangu. Nikahisi huenda mdogo wangu Inana amepatwa na janga lingine, jambo ambalo hakika sikuwa tayari kulisikia kabisa.
"Mdogo wako anaendelea vizuri, ila kuna mambo yangu ya kibiashara hayajakaa sawa ndiyo maana unaona niko katika hali hii," alisema na kunikazia macho.
Nilishusha pumzi kwa nguvu. Angalau nikawa na ahueni kwani nilikuwa nimeshaanza kuchanganyikiwa. Nilimpenda sana mdogo wangu. Baada ya kuniambia hivyo, tuliagana ambapo niliondoka nikiwa na furaha ya kupewa ile pesa. Haraka sana nikaenda kuonana na yule mama mwenye nyumba ambayo nilitakiwa nihamie. Nikakamilisha taratibu zote muhimu zilizokuwa zikihitajika.
Siku hiyohiyo nilienda kununua godoro na kuliweka ndani. Nikanunua na baadhi ya vitu muhimu kama jiko na vyombo vya kutekea na kuhifadhia maji pamoja na karai la kufulia nguo.
Kwa kuwa sikuwa nimemuaga shangazi, nikapanda gari hadi Buguruni kumuaga shangazi. Licha ya kuonekana kunichoka, shangazi alishituka sana nilipomueleza juu ya suala la kuhama na kuanza kujitegemea.

"Sasa maisha ya kujitegemea utayaweza kweli Tunu? Au umepata bwana wa kukuoa na hutaki kunieleza ukweli?"
"Hapana shangazi, nimeamua kujitegemea."
"Mbona hukuniambia mapema?"

"Nilikuwa nakamilisha taratibu zote muhimu shangazi, hata hivyo sioni kama kuna kosa," nikazidi kujieleza kwa shangazi.
"Hata hivyo, kuhusu sijui mwanaume, sina hata wa dawa shangazi," nikaongeza na kumfanya shangazi abaki kimya na kunitazama kwa macho ya kuibia kwa chini.

Baada ya mazungumzo hayo mafupi, nilimuaga. Nikaingia ndani na kuchukua vitu vyangu muhimu ikiwemo nguo.
Nikaondoka nikiwa na furaha hadi kwenye kituo cha mabasi ya kuelekea Mwananyamala. Nilifika majira ya saa mbili na nusu na kufikia nyumbani kwa kuwa hapakuwa mbali na kituo cha mabasi. Niliingia ndani nikiwa mwenye furaha isiyokuwa na kifani.

Kwa mara ya kwanza maishani nilikuwa naanza kulala kwenye nyumba ambayo nitakuwa naigharamia kwa pesa na jasho langu. Nikaweka sawa godoro langu na kulala. Nililala kwa usingizi wa pono. Nilishituka ikiwa ni asubuhi na kushangaa kuwa nilikuwa nimelala na nguo.
"Mmh! Hiki chote ni kiherehere cha makazi mapya," nilijisemea moyoni huku nikitabasamu.

Nikatoka nje nikiwa na ndoo ambapo niliteka maji na kwenda bafuni kuoga. Nikajiandaa kwenda kazini. Nikafunga mlango huku nikiimba nyimbo za kaswida. Hakika furaha niliyokuwa nayo haielezeki.
Nikaondoka hadi kazini. Nilifika na kubadili nguo na kuvaa za kazi, nikaanza kuwajibika kama kawaida.

Nikiwa naendelea na kazi, kwa mbali nilimuona meneja akija upande wangu. Moyo ulinilipuka na kuongeza bidii ya kazi. Alipofika bila hata kunijulia hali alinitaarifu kuwa bosi yule Mwarabu alikuwa akiniita ofisini kwake.
Nikajiuliza maswali kadhaa, kikaanza kujihoji juu ya tabia ya bosi kuniiita ofisini kwake mara kwa mara. Hata hivyo, sikwenda mbali zaidi kimawazo kutokana na jinsi ambavyo bosi huyo nilikuwa nikimuamini.
Nikaenda hadi ofisini kwake na kumkuta akiongea na simu. Aliponiona kwa mbali alininyooshea ishara ya kunitaka kutoingia kwanza na kuashiria kuwa alikuwa na mazungumzo ya faragha ambayo hayakuhitaji uwepo wa mtu yeyote zaidi yake.

Nikarudi hadi ofisini kwa katibu muhtasi na kukaa kwenye kochi la wageni. Baada ya nusu saa, simu ya mapokezi ilipigwa na baada ya kuongea, yule dada alinipa maelekezo kuwa bosi alikuwa akinihitaji sasa.
Nikanyanyuka na kuelekea ofisini kwake. Nilipofika alinikaribisha kwa furaha na tabasamu la bashasha. Na mimi nikajikuta nikiachia tabasamu bila kujizuia.
"Leo naomba twende pamoja matembezi ya jioni kwa ajili ya chakula cha jioni kama hutajali," bosi aliniambia akiwa ananiangalia kwa mkazo bila hata kupepesa macho.
Kutokana na kitendo cha kumuamini kupita kiasi, nilimkubalia kwa haraka bila hata kuonesha wasiwasi wa aina yoyote.

Jioni ya siku hiyo, tulikuwa kwenye ufukwe wa Coco.
"Sikukuita huku kwa bahati mbaya, kuna jambo nataka nikuambie," alisema bosi na kusimama.


Je, bosi huyo alitaka kumwambia nini? Usikose kufuatilia leo jioni.....
 
Tatizo la mwarabu kamfundisha Tunu namna ya kutumia pisto, na sasa anataka kumtumia vibaya yeye pamoja na Inana, itakula kwake! MziziMkavu, naomba umshauri huyo mwarabu!
 
Last edited by a moderator:
Ila kaka we c mstaarabu kabisa huwezi kuona watu wapo to the climax then u stop to do ur duties....?????
 
Back
Top Bottom