Niliupenda Muungano...

Niliupenda Muungano...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,097
Reaction score
43,309
Mimi sasa nimekuwa muumini wa Serikali Moja; Moja ya kwao na Moja ya kwetu, tukutane Umoja wa Mataifa kama ndugu wamoja! Undugu haung'ang'aniwi na ndugu akishalalamika kuwa unamzibia ni wakati wa kumtakia kila la kheri... Niliupenda Muungano lakini Mungu ameupenda zaidi..
 
Mkuu Mwanakijiji, hivi umekaa ukatafakari kujua madhara yatakayojitokeza ikiwa Muungano utavunjika? Hivi uliwahi kuwafikiria wale wafanyabiaahara wenye asili ya Pekba ambao wamejazana pale Tandika, Ilala, Kariakoo na Buguruni? Vipi wataishi ikiwa Muungano utavunjika? Mkuu Mwanakijiji, hivi uliwahi kufikiria juu ya hawa watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao wametoka pande zote za muungano na wapo kila upande? Mkuu, hivi uliwahi kutafakari mathalan juu ya kuvunjika kwa ndoa yako ambayo imesumu zaidi ya miaka 50 mkiwa mmezaa watoto na wajukuu, mmechuma mali nyingi na kikubwa zaidi mmejenga udugu wa kifamilia?
 
chabruma watafuta vita mkuu. wakikusikia watu ukiufananisha na ndoa shauri yako. Hili lilitaka kuleta tifu hata bungeni
 
Mkuu Mwanakijiji, hivi umekaa ukatafakari kujua madhara yatakayojitokeza ikiwa Muungano utavunjika? Hivi uliwahi kuwafikiria wale wafanyabiaahara wenye asili ya Pekba ambao wamejazana pale Tandika, Ilala, Kariakoo na Buguruni? Vipi wataishi ikiwa Muungano utavunjika? Mkuu Mwanakijiji, hivi uliwahi kufikiria juu ya hawa watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao wametoka pande zote za muungano na wapo kila upande? Mkuu, hivi uliwahi kutafakari mathalan juu ya kuvunjika kwa ndoa yako ambayo imesumu zaidi ya miaka 50 mkiwa mmezaa watoto na wajukuu, mmechuma mali nyingi na kikubwa zaidi mmejenga udugu wa kifamilia?

Hatuna ugomvi na wazanzibari. Itabidi wachague tu uraia wa nchi mojawapo na kuendelea na shughulu zao kama kawaida. Mbona wakenya wengi na waganda na wahindi wapo hapa hatuna shida nao? Ulidhani muungano ukivunjika wazanzibari watafukuzwa tanganyika? hapana kuna sheria za kimataifa zinawalinda. kwani wageni wanaoendesha maisha yao hapa tanzania hawana ndugu huko kwao? Kuvunjika kwa muungano sio kuvunjika kwa undugu ila wazanzibari tena nadhani tutawapa preferential treatment waendelee kuenjoy rights fulani fulani. Pia wabara walioko kwao itakuwa hivyo hivyo. Ila wakidhubutu tu kuwafanyia fujo, watakiona cha moto. Na wakijua wana ndugu zao wamejazana huku hawatadhubutu.Mimi napendekeza tushirikiane na zanzibar kwenye mambo ya ulinzi na usalama peke yake mengine kila mtu asepe kivyake. Huu muungano tunaongangania utakuja kuiletea hii nchi sifa mbaya ya umwagaji mkubwa wa damu. Mwalimu kwa mnaopenda kumquote aliweza kusema zanzibar wakitaka kujitenga basi waende tu ila isiwe ni kwa ugomvi. alisema hatawalzimisha kwa majeshi na vifaru kubaki kwenye muungano.
 
Na je mtagawana vipi udugu na upendo mlioujenga kwa muda mrefu?
Mkuu Chanruma, hakika inahitaji tafakuri ya kina kabla ya kuuvunja muungano. Kwangu naona kuwa kitendo cha kuuvunja muungano ni kama kumchinja mtu kwa msumeno
 
Mkuu, hizo ni hisia zako na chiki ulizonazo kwa wazanzibari
sio chuki tatizo waznz hawajui wanachokitaka. sasa wameona t/nyika wanadai nchi yao wamelowa. ila kabla ya hapo walikuwa wakifura eti tunawatawala. hawa watu wana akili ya ajabu sana
 
Kwa hiyo tulianza na Nchi 1, Serikali 2 baadaye Nchi 2, Serikali 2 na sasa tunaelekea kwenye Nchi 1, Serikali 1, lakini kwa kuvunja Muungano! Kweli Waafrika tumelaaniwa maana wakati mataifa makubwa yanaungana, (hata Crimea ilivyojitenga na Ukraine imeungana na Russia), vinchi vidogo vidogo vya kiafrika vinatengana!
 
Mkuu Mwanakijiji, hivi umekaa ukatafakari kujua madhara yatakayojitokeza ikiwa Muungano utavunjika? Hivi uliwahi kuwafikiria wale wafanyabiaahara wenye asili ya Pekba ambao wamejazana pale Tandika, Ilala, Kariakoo na Buguruni? Vipi wataishi ikiwa Muungano utavunjika? Mkuu Mwanakijiji, hivi uliwahi kufikiria juu ya hawa watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao wametoka pande zote za muungano na wapo kila upande? Mkuu, hivi uliwahi kutafakari mathalan juu ya kuvunjika kwa ndoa yako ambayo imesumu zaidi ya miaka 50 mkiwa mmezaa watoto na wajukuu, mmechuma mali nyingi na kikubwa zaidi mmejenga udugu wa kifamilia?

Watachagua uraia wa nchi mojawapo. Kama watachagua kuwa raia wa Tanganyika, basi wataendelea na biashara kama kawaida pale Tandika, Kariakoo, Kibaigwa na maeneo mengine. Kama watachagua uraia wa Zanzibar, itabidi wafuate taratibu za uhamiaji ili waweze kuendelea na biashara kama wawekezaji wengine wa kigeni. Na muungano kati ya nchi na ndoa kati ya mume na mke ni nonsense. Hata hivyo, mmoja kati ya wanandoa akidai uhuru wake na kukataa kufungamana na upande mwingine, basi ndoa lazima ivunjike.
 
Mimi sasa nimekuwa muumini wa Serikali Moja; Moja ya kwao na Moja ya kwetu, tukutane Umoja wa Mataifa kama ndugu wamoja! Undugu haung'ang'aniwi na ndugu akishalalamika kuwa unamzibia ni wakati wa kumtakia kila la kheri... Niliupenda Muungano lakini Mungu ameupenda zaidi..

jamani hatuna muungano tena mjue kama nchi ila kuna muungano wa kisiasa tu yani kwavile ccm iko bara na pwani baaaaaaaass
 
Mimi naendelea na msimamo wangu wa serikali moja,nchi moja.Zanzibar ife kama tanganyika.mtasemaje mmeoana halafu mmoja hataki kuondoka kwao?miaka 50 ya kuungana halafu bado mnazungumzia uzanzibari na utanganyika?you can't be serious aisee unless mniambie muungano ni unfinished business ya marehemu na sasa biashara Hugo imewashindeni watoto wa marehemu matokeo yake mnaua biashara.laiti
marehemu wazazi wenu wangekuwepo?!
 
Mi sikuwahi kuupenda muungano hata siku moja, kama kufa mi ulishakufa siku nyingi tu ila nasubiri siku ya kuanua matanga RIP MUUNGANO.
MUNGU IBARIKI TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom