Nilishuhudia mgonjwa akijirusha toka ghorofani Hospital ya Kairuki, Dar

Hyo hospital ya kairuki wazembe kwanini wasiweke madirisha ambayo mgonjwa hawezi kupita, hafu watu hukimbilia hyo hospital wakati ubora wake sio kivile hata usafi huwa ka inanuka hivi, mazingira yake tu ukienda unazidiwa
 
Wewe mtu ambae Mungu amekujalia afya njema, tunajua una shida zako,lakini pindi unapokutana na mwenye shida zilizo za wazi epuka kumtolea kauli ngumu, mfano:-
1. Sina hela - Sema "Acha nipambane, nikifanikiwa nitakuwezesha"
2. Wewe huna akili - Sema "Wewe una akili sana, sema hujaamua kusoma kwa bidii"
3. Huu ugonjwa utakuua kwa ubishi wako - Sema "Watu wengi wamepona huu ugonjwa kwa kufanya 1,2,3"
Kwa kifupi, tujihadhari kutoa kauli ngumu kwa watu wenye shida.

tumaini ni tiba zaidi 60% kuliko dawa anayopewa mtu.

kama uliishaugua hata kichwa ukisafiri ile hali ya kuiona farmacy tu mjini karibu na stand huwa kuna nguvu inakuingia na kujikuta kama kichwa kinapuuza maumivu hivi.
 
daah afya afya afya in kitu kimoja cha muhimu sana. Mgonjwa labda alishajikatia tamaa kama mkuu reyzzap alivyosema ama ile ndugu kumtelekeza kutokana na hali zao mbaya kiuchumi. Ina huzunisha ila ndio hivyo hakuna namna. Apumzike kwa amani tu. Uchungu wake wa mgonjwa aujuae mgonjwa mwenyewe.
Uyo sababu ya kiuchumi sidhani,inasemekana sababu za kiafya,ndugu yake anasema maleria Kali ilimpanda kichwani,Rest in peace
 
Hyo hospital ya kairuki wazembe kwanini wasiweke madirisha ambayo mgonjwa hawezi kupita, hafu watu hukimbilia hyo hospital wakati ubora wake sio kivile hata usafi huwa ka inanuka hivi, mazingira yake tu ukienda unazidiwa
Hiyo hospital ya ovyo .sitasahau bado kidogo nimpoteze Kaka yangu kwa uzembe wao
 
Daaaa, Ilifikia hatua akakata tamaa kabisa.

Afya ni Kati ya vitu ambavyo binafsi nachukuliaga poa lakini nikiumwa mawazo yanaenda mbali sana na kuwakumbuka watu wanao ugua miakaa.

Siku mtu ukilazwa ndio hua unakumbuka kale ka msemo
"Kikubwa uzima".

Huyu pengine ni sababu za kiuchumi,
Au ameugua kwa mda mrefu bila kupona,
Au ni kati ya magonjwa makubwa yanayokatisha uhai wa wengi,
Au ametelekezwa....

Kwa ufupi mpaka mtu anajitoa uhai, anajihisi ni hopeless.

Mungu awape nguvu wagonjwa wotee.
Umenena. Kosa yoote lakini uombe uwe na afya njema. Kama hujaugua kisawasawa huwezi kujua umuhimu wa afya au dhiki wanazokumbana anazokumbana nazo mtu mgonjwa.
 
Uyo sababu ya kiuchumi sidhani,inasemekana sababu za kiafya,ndugu yake anasema maleria Kali ilimpanda kichwani,Rest in peace
Unajua mgonjwa inatakiwa mda wote alindwe na kufarijiwe mwenyewe nimewahi kulazwa, ikafika mda nawaza nipande juu nijirushe uzuri dirishani nilikuwa siwezi kupita, so wagonjwa Wana haki ya kuangaliwa mda wote na hospital iweke madirisha ambayo mtu hapiti
 
Wewe mtu ambae Mungu amekujalia afya njema, tunajua una shida zako,lakini pindi unapokutana na mwenye shida zilizo za wazi epuka kumtolea kauli ngumu, mfano:-
1. Sina hela - Sema "Acha nipambane, nikifanikiwa nitakuwezesha"
2. Wewe huna akili - Sema "Wewe una akili sana, sema hujaamua kusoma kwa bidii"
3. Huu ugonjwa utakuua kwa ubishi wako - Sema "Watu wengi wamepona huu ugonjwa kwa kufanya 1,2,3"
Kwa kifupi, tujihadhari kutoa kauli ngumu kwa watu wenye shida.

Umeniongzea kitu mkuu.
 
tumaini ni tiba zaidi 60% kuliko dawa anayopewa mtu.

kama uliishaugua hata kichwa ukisafiri ile hali ya kuiona farmacy tu mjini karibu na stand huwa kuna nguvu inakuingia na kujikuta kama kichwa kinapuuza maumivu hivi.

Kweli hope ndo Kila kitu.
 
Hakika afya njema na ilyo bora ndio mtaji mkubwa na kila kitu kwa mwanadamu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom