Nilishuhudia mgonjwa akijirusha toka ghorofani Hospital ya Kairuki, Dar

goldcall

JF-Expert Member
Oct 20, 2017
394
535
Kichwa chajieleza, nimeshuhudia kwa macho yangu mgonjwa akijirusha ghorofa ya juu sana, pale kairuki hospital, na kufika chini mifupa ikiwa inaonekana.

Nilishangaa kuona manesi wanaulizana kumbeba yule mgonjwa kumuweka katika gari ya wagonjwa.

Kama dakika tano hivi yule mgonjwa alipoteza maisha,

Hospitali ya Kairuki naona kabisa kuna shida mahara, sio pazuri naona Pana harufu ya kifo kifo tu, uzembe na kukosa umakini.
 
Daaaa, Ilifikia hatua akakata tamaa kabisa.

Afya ni Kati ya vitu ambavyo binafsi nachukuliaga poa lakini nikiumwa mawazo yanaenda mbali sana na kuwakumbuka watu wanao ugua miakaa.

Siku mtu ukilazwa ndio hua unakumbuka kale ka msemo
"Kikubwa uzima".

Huyu pengine ni sababu za kiuchumi,
Au ameugua kwa mda mrefu bila kupona,
Au ni kati ya magonjwa makubwa yanayokatisha uhai wa wengi,
Au ametelekezwa....

Kwa ufupi mpaka mtu anajitoa uhai, anajihisi ni hopeless.

Mungu awape nguvu wagonjwa wotee.
 
Daaaa, Ilifikia hatua akakata tamaa kabisa.

Afya ni Kati ya vitu ambavyo binafsi nachukuliaga poa lakini nikiumwa mawazo yanaenda mbali sana na kuwakumbuka watu wanao ugua miakaa.

Siku mtu ukilazwa ndio hua unakumbuka kale ka msemo
"Kikubwa uzima".

Huyu pengine ni sababu za kiuchumi
Au ameugua kwa mda mrefu bila kupona.
Au ni kati ya magonjwa makubwa yanayokatisha uhai wa wengi
Au ametelekezwa

Kwa ufupi mpaka mtu anajitoa uhai, anajihisi ni hopeless.

Mungu awape nguvu wagonjwa wotee.
Aamiin.
 
daah afya afya afya in kitu kimoja cha muhimu sana. Mgonjwa labda alishajikatia tamaa kama mkuu reyzzap alivyosema ama ile ndugu kumtelekeza kutokana na hali zao mbaya kiuchumi. Ina huzunisha ila ndio hivyo hakuna namna. Apumzike kwa amani tu. Uchungu wake wa mgonjwa aujuae mgonjwa mwenyewe.
 
dash afya afya afya in kitu kimoja cha muhimu sana. Mgonjwa lambda alishajikatia tamaa kama mkuu reyzzap alivyosema ama ile ndugu kumtelekeza kutokana na hali zao mbaya kiuchumi. Ina huzunisha ila ndio hivyo hakuna namna. Apumzike kwa amani tu. Uchungu wake wa mgonjwa aujuae mgonjwa mwenyewe.

Lamda = Labda
 
Kwa mbele ni bonge la kesi hiyo, sema kibongo bongo, na kama mgonjwa mwenyewe ni miongoni mwa akina sie, hapo watu wataishia kutoa justification za kipumbavu kv "malaria ilikuwa imepanda kichwani", and that's it!
Kwa kweli hospitali ingepigwa faini za kutosha. Mgonjwa katoka kitandani, hamna anayejua, hamna anayemsimamia.
 
Nani aliwahi kufa humu atueleze kama ni faida au hasara?

Unaweza kuta alichungulia mautini akaona kukopoa kulik huku, akaamua awahi.

Siku mkifariki mkaenda upande wa pili unaweza kujutia, kwamba kwanini ulichelewa kwenda.
 
Wewe mtu ambae Mungu amekujalia afya njema, tunajua una shida zako,lakini pindi unapokutana na mwenye shida zilizo za wazi epuka kumtolea kauli ngumu, mfano:-
1. Sina hela - Sema "Acha nipambane, nikifanikiwa nitakuwezesha"
2. Wewe huna akili - Sema "Wewe una akili sana, sema hujaamua kusoma kwa bidii"
3. Huu ugonjwa utakuua kwa ubishi wako - Sema "Watu wengi wamepona huu ugonjwa kwa kufanya 1,2,3"
Kwa kifupi, tujihadhari kutoa kauli ngumu kwa watu wenye shida.
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom