Wachawi tunajua siri moja kuu: upepo ukivuma vibaya na tunguli zikakataa kuongea, hata sisi tunalegeza magoti. Nguvu ikipungua, unyenyekevu unakuwa ndio ngao ya kujificha ili tusije tukaangamizwa na walio juu yetu. Mafanikio yakirudi na usiku ukiwa wetu tena, hapo ndipo utajua kama magoti haya yatawahi kugusa ardhi tena!Hongera sana lakini je mambo yangekuwa yanakwenda vizuri sana ulipokuwa unapiga ramli, ungekuwa na huo unyenyekevu wa kupiga magoti leo?
Kuvunja nazi njiapanda ni tambiko la kale linalofanyika kwenye makutano ya njia, mahali panapoaminika kuwa kitovu cha kukutana kwa mizimu, majini, na nguvu za giza.Nimecheka sana! Kuna siku jamaa yangu aliniomba nimpe lifti mpaka njia panda akavunje nazi! π
Sirudi huko tena maana hakuna nilichosahauπͺπΏπ₯ππΏMoja ya dhambi nzito kwa Mungu muumbaji ni ushirikina,umefanikiwa kuomba toba inshaallah Mungu husamehe haraka sana,hongera ila kikubwa tu usirudie katu hiyo dhambi.
Yah Mshana Jr .Wengi humu jf tulikufahamu kwa nyuzi za aina hii,Jambo zuri kufanya toba.Lakini kama hutojali kuna mada moja uliwahi kuizungumzia huko nyuma kuhusu milango ya kuzimu hapa Tanzania,na mazindiko yaliyowekwa kwa nchi mfano mwenge,kwa faida ya watu fulani, unaweza kuturudisha darasani tena kuhusu hizo mada?
Kwakweli Mimi sasa ni wa nuruni nitaweka link ya ile uzi lakini pia nitaongeza maelezo kidogo leoWengi humu jf tulikufahamu kwa nyuzi za aina hii,Jambo zuri kufanya toba.Lakini kama hutojali kuna mada moja uliwahi kuizungumzia huko nyuma kuhusu milango ya kuzimu hapa Tanzania,na mazindiko yaliyowekwa kwa nchi mfano mwenge,kwa faida ya watu fulani, unaweza kuturudisha darasani tena kuhusu hizo mada?
Can u show me a magic?Ni kweli kabisa Ila Mimi nimeshapita hizo level na naishi kwenye toba, maombi na msamahaπͺπΏππΏ
Ulichofeli ni kutomuachia mrithi wa mikoba yako ya urogajiNiliroga mchana nikaroga usiku, niliroga kushoto nikaroga kulia, niliroga mashariki nikaroga magharibi, niliroga kaskazini nikaroga kusini. Niliroga chini nikaroga juu, niliroga mbele nikaroga nyuma, niliroga jua nikaroga mwezi, niliroga nyota nikaroga mawingu.
Niliroga milima nikaroga mabonde, niliroga bahari nikaroga nchi kavu, niliroga mito nikaroga chemchemi, niliroga upepo nikaroga dhoruba. Niliroga moto nikaroga majivu, niliroga masika nikaroga kiangazi, niliroga kila pembe nikaroga dunia nzima, lakini bado siri haikufunuka wala moyo wangu haukutulia.
Lakini mwisho nilitubu na kumrudia mola wangu, nikaacha giza na kufuata mwanga, nikavunja vibuyu na kutupa matunguli. Nilisafisha mikono yangu kwa maji ya toba, nikapiga magoti kwa unyenyekevu mkuu, nikapokea amani ambayo dunia isingeweza kunipa. Yale yote niliyoyatafuta kwa waganga na ramli, nikayapata bure kwa neema na rehema zake, kwani hakuna mkuu zaidi ya Muumba wa mbingu na ardhi.
Sasa mimi ni mpya na wa nuruni, giza limepita na mambo yote yamekuwa mapya, ninasimama imara katika mstari wa haki. Tabia za kale zimezikwa katika kaburi la historia, mavazi ya huzuni yamevuliwa na nimevikwa vazi la sifa na utukufu. Hatua zangu sasa zinaongozwa na mwanga wa kimungu, kila neno langu linajenga badala ya kubomoa, na moyo wangu umejaa amani tele, furaha isiyo na kifani, na tumaini la milele.