Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

Pole sana nakupa tu maneno ya faraja tu ila ya ukweli utaumia sana jinsi ulivyo.

Samehe mara 700 na utalipwa mbinguni na Mungu
 
Dah Pole sana kaka.
Mi naamua kulipiza kwa Hawa wengine kwa Niaba yako .
It’s beyond the Human pains.
Mungu mkubwa, huyo Dada hatadumu kwenye ndoa yake.
 
nipo Dodoma mkuu,nimesomea education pia sina shughuli yoyote ndio kwanza nimepata mtaji wa laki 6 nataka nijitahidi biashara ya mtumba pia nimeulizia humu mkoa mzuri nikaanze upya

Pole sana, pambana utafanikiwa tu baadaye.

Ulemavu wa mguu baadaye unaweza kupata mguu wa bandia or motorized wheel chair to help with mobility.

Masikio, hearing aids zinaweza kukusaidia.

Ni kanuni nzuri ya maisha not to spend zaidi ya 10% in any one thing or deal (even like cars or houses).
 
Nitazungumzia Hilo eneo la kusimamishwa kazi na kuanza kuyumba kiuchumi. Kwakuwa hujui siku Wala saa ya kuondolewa kazini, wewe uliyeajiriwa, wekeza vitega uchumi, na si lazima mwanamke wako ajue vilipo. Kiukweli, asilimia kubwa ya wanawake wanatumbea helaaaa.
 
Pole Kaka,.wanawake ndivyo walivyo..mi ndo Mana mpka Leo siwaamini.
Mungu Ni mwema ipo siku utasimama Tena.
 
Habarini,

Jana katika kupitia taarifa za group, la shule niliyosoma secondary, nakutana na ujumbe kuwa naima, anaolewa jumamosi ya leo, nimekosa raha ndugu zangu, kwani ni miaka takribani 13 imepita nikijitahidi kusahau, ila kila nikiangalia hali yangu ya ulemavu najikuta nakumbuka na kuyachukia mapenzi.

Mimi nilizaliwa mzima kabisa na sasa nina miaka 35, baada ya kumaliza chuo, nilikuwa na mahusiano na binti fulani ambaye tulisoma nae secondary hapa dar, nakumbuka kuonana nae ilikuwa ni kama bahati tu na kila muda naumia natamani nisingeonana nae labda leo hii ningekuwa mzima kabisa.

Mwanzo alikuwa ni mtu wa kipekee sana, nilijulikana kwao na kwetu walimjua, na kwakuwa nilikuwa na kazi private office moja hapa mjini(sitapenda kuitaja) nilijitahidi fanya uwekezaji mdogo kwake nilikopa kiasi fulani cha pesa mil 7 kwa dhamana ya kazi nikamfungulia duka kwa matumaini ya kuwa, kwakuwa sisi ni kitu kimoja mwenzangu nae asimame kwani alikuwa anashinda tu nyumbani kwao.

Nilipata misukosuko kazini na nikasimamishwa kazi na hapo ndipo nilipoanza kutoelewana na mwenzangu dharau ilikuwa kubwa, kejeli, unamuomba muonane anagoma au anakubali na hatokei kabisa na simu anazima, ndani ya miezi miwili, nilikuwa nimepata msongo mkubwa wa mawazo maana madeni na hali ngumu na mwenzangu haeleweki sikujua nifanye nini zaidi ya kunywa pombe.

Siku ya tukio jumatano ile niliamka mzima kabisa, jioni nilipanga kwenda alipopanga naima bila taarifa kwani kila nikimjulisha basi hatoi ushirikiano. Nilitaka tukubaliane tuuze duka nifund hela kidogo ya kiwanja nilichonacho nifungue biashara nyingine, inisaidie kufanya marejesho bank.

Sikuwahi fikiria kama ananisaliti nilijua tu ni kutingwa na kazi na kuwa na mood mbaya, saa 1 nilienda kwake kwakujua aliishafunga biashara nilivyofika kwake, niligonga mlango kukawa kimya, nilikuwa na funguo za kwake na yeye alikuwa nazo za kwangu nikafungua mlango.

Sikuamini macho yangu naima alikuwa na rafiki angu kipenzi salim wakifanya mepenzi pale sebuleni wakapigwa na mshangao kwani hawakunitarajia, nilirudi nyuma na kuanza kutoka pale nikiwa na maumivu zaidi na kujiona sifai nikiwa mita chache tu kutoka pale nikivuka barabara nilisikia honi ya gari mara 2 baada ya hapo sikukumbuka kitu tena.

Baada ya kuamka nilikuta ndugu zangu wakiwa hospital namimi wakiwa na huzuni, baada ya siku 2 ndiyo niligundua mguu wangu wa kushoto sina tena nilielezwa uliharibika kutokana na kusagwa na gari, nililia sana na bado nalia sana, nilijiuliza nimefanya dhambi gani kustahili adhabu hii, niliwaza nitalipaje deni la bank na nitawezaje kuanza maisha katika hali yangu ya ulemavu.

Baada mwezi 1 nanusu nikatoka hospitalini, ila ikawa kama ninamkosi kwani baada ya mwezi nilikamatwa na malaria kali sana nikajua ndio mwisho wa maisha yangu, nilikuwa naweweseka sana, hospital wakaniwekea dripu ya Quinine, masikini ningejua naenda pata ulemavu mwingine ni bora ningejitibia nyumbani, ila nilipona vizuri baada ya week tu...

Baada ya miezi 7 nilianza poteza uwezo wa kusikia taratibu na kupoteza balance ya kutembea sikugundua mapema ila baada ya kufikisha mwaka na miezi 2, nilikuwa natatizo lingine la kutosikia vizuri.

Maisha yangu yalibadilika sikuwa na furaha tena na leo hii mwanamke alieniharibia maisha yangu ambaye naamini ni chanzo cha ulemavu wangu anaenda kuolewa najiuliza nimeikosea nini dunia, muda mwingine natamani kufariki kwani ninayopitia ni mazito kushinda uwezo wangu wa kustahili.

Ewe maisha, nilikukosea nini?
Sitaki kuamini kuwa kiss hiki ni Cha kweli
 
Pole sana,mtukuze Mungu na kumshukuru kwa kila jambo,mgeukie yeye utaiona amani na furaha kwani kuna wanaopitia magumu kuliko hata yako...
 
hiyo movie nimeisahau jina kidogo ila kacheza Ray Kigosi na Aunt Ezekiel . sema kwa badae ulemavu wake ulipona akapata kazi na dem aliemsaliti akaja kumuomba msamaha tena

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Asante sana ndugu, Mungu atasaidia kwangu japo hearing aid ninayo ila siitumii kwasababu inaongeza makelele, nahisi ni sababu ya brand kuwa low quality, ila Mungu akisaidia nitajaribu phonac hearing aid maana ndio bora kwasasa na kuna dada anatumia anasema ni nzuri sana kuliko brand za kawaida..
Pole sana, pambana utafanikiwa tu baadaye.

Ulemavu wa mguu baadaye unaweza kupata mguu wa bandia or motorized wheel chair to help with mobility.

Masikio, hearing aids zinaweza kukusaidia.

Ni kanuni nzuri ya maisha not to spend zaidi ya 10% in any one thing or deal (even like cars or houses).
 
Pole sana,mtukuze Mungu na kumshukuru kwa kila jambo,mgukie yeye utaiona amani na furaha kwani kuna wanaopitia magumu kuliko hata yako...
ndugu naamini matatizo yangu sio makubwa ila kukaa na hali hii ya ulemavu ndiko kunaniletea simanzi na kunikumbusha, Mungu atanisaidia naimani
 
Pole sana nakupa tu maneno ya faraja tu ila ya ukweli utaumia sana jinsi ulivyo.

Samehe mara 700 na utalipwa mbinguni na Mungu
ni kweli kaka kusahau kabisa ni ngumu sababu nitasahau dakika mbili ila nikinyanyuka na mguu au nikiitwa nisiposikia nitarudi kwenye simanzi yangu.
 
100 Reactions
Reply
Back
Top Bottom