Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

Mnapenda sana kupitiliza au mnaiga kweny tamthilia bila kujua wale wapo kazini wanatafuta pesa?

Baada ya kuwakuta wanagegedana nini sasa kikakupeleka barabarani? Wenge au?

Natamani nikulime bakora za maana ujinga ukutoke kichwani.
 
Hospital ni ya serikali ipo Dar ndugu yangu, ilikuwa 2008, pia sikujua kama Quinine ndiyo chanzo cha shida ya kunipunguza usikivu, maana hospitali nyingi walisema ukosefu wa Vitamin B wakaniandikia dawa zinaitwa Nurotons kama sijakosea ni mchanganyiko wa vitamin B karibu zote (B1 to B12)

walisema hizo Nurotons zitasaidia kuotesha vinyweleo ambavyo ndio vinapokea taarifa na kuifasili ieleweke na ubongo, ila shida iliendelea kadri siku zinavyoongezeka ndiyo nilivyozidi kutosikia mpaka sasa nasikia kwa shida sana masikio yote mawili.

ila kuna doctor muhimbili 2014 ndiyo alipitia taarifa zangu za nyuma vizuri akasema shida sio upungufu wa madini ila ni effect za dawa za Quinine.namimi nikavuta kumbukumbuku kuwa inawezekana Quinine ni chanzo kikuu cha tatizo langu.
Pole sana mkuu, ila hio hospitali ni ya wapi na ilikuwa mwaka gani wakakupa hio quinine, Hio quinine imefanya watu wengi sana kuwa na matatizo ya masikio, Wengine wanasikia kwa mbali, wengine wanasikia makelele masikioni wengine ndio viziwi kabisa, Ni hospitali gani na mwaka upi hao madaktari walikufanyia huu ukatili
 
pia hayo makelele kama muungurumo, nausikia pia na muda mwingine unafanya taarifa nisiielewe au nisisikie maneno yote, ila maneno yenye S na A ni ngumu zaidi kuyasikia hata uwe karibu. sio hilo tu, sauti yangu imebadilika naongea kwa sauti ya chini sana ila mimi najiona naongea sauti ya juu

mkuu pole sana, ila usikatishwe tamaa na hali yako jiamini jikubali na jisamehe kwanza wewe mwenyewe wasemehe na wengine, usibebe mizigo ndani mwako!!
 
Nashukuru kaka maana ni kweli nimebeba mzigo wa chuki na kusamehe ni ngumu. Nitaufanyia kazi ushauri wako.
 
Hospital ni ya serikali ipo Dar ndugu yangu, ilikuwa 2008, pia sikujua kama Quinine ndiyo chanzo cha shida ya kunipunguza usikivu, maana hospitali nyingi walisema ukosefu wa Vitamin B wakaniandikia dawa zinaitwa Nurotons kama sijakosea ni mchanganyiko wa vitamin B karibu zote (B1 to B12)

walisema hizo Nurotons zitasaidia kuotesha vinyweleo ambavyo ndio vinapokea taarifa na kuifasili ieleweke na ubongo, ila shida iliendelea kadri siku zinavyoongezeka ndiyo nilivyozidi kutosikia mpaka sasa nasikia kwa shida sana masikio yote mawili.

ila kuna doctor muhimbili 2014 ndiyo alipitia taarifa zangu za nyuma vizuri akasema shida sio upungufu wa madini ila ni effect za dawa za Quinine.namimi nikavuta kumbukumbuku kuwa inawezekana Quinine ni chanzo kikuu cha tatizo langu.
Haupo peke yako mkuu, nimekutana na watu kadhaa wenye hili tatizo na wengi nilipowauliza kuhusu quinine walikiri kuitumia ili kutibu malaria.

Wengi wameenda kwa waganga na kuishia kufanyiwa matambiko au dawa lakini wapi, wengi hudhani makelele ni kwamba wametupiwa majini kumbe ni quinine.

Hizi kampuni zingetumia hizi dawa ulaya nakwambia saizi kungekuwa kuna wagonjwa wamelipwa fidia ya mabilioni, Yani kampuni inatengenezaje dawa ambayo inamfanya mtu awe kiziwi kwamfano??, maana kiukweli bila maskio mtu umeshamkwa sana

vipi, simu unaskia fresh au ni mwendo wa meseji
 
pia hayo makelele kama muungurumo, nausikia pia na muda mwingine unafanya taarifa nisiielewe au nisisikie maneno yote, ila maneno yenye S na A ni ngumu zaidi kuyasikia hata uwe karibu. sio hilo tu, sauti yangu imebadilika naongea kwa sauti ya chini sana ila mimi najiona naongea sauti ya juu
Sauti kubadilika ni lazima maana unaiskia tofauti na kawaida.

huo ugonjwa wa kelele niiwahi ona jamaa mwenye tatizo hili alikua anajichanfa aende zanzibar kuna mzungu hapo zanzibar ana mitungi ile ya oxygen watu wenye magonjwa flani wanainiaga humo ndani kama kwa dakika 20 hivi kila siku kwa wiki nzima ili kutibu magonjwa yanayotolewa kwa hio gesi ya oxygen.

vp, umejaribu mafuta ya kuku??
 
ndugu simu sisikii vizuri nasikia kwa asilimia chache nikiweka loud speaker, naweza kusikia maneno 3 nisisikie maneno 8, na ule kama mwangwi wa simu ndo unanichanganya kabisa
Haupo peke yako mkuu, nimekutana na watu kadhaa wenye hili tatizo na wengi nilipowauliza kuhusu quinine walikiri kuitumia ili kutibu malaria.

Wengi wameenda kwa waganga na kuishia kufanyiwa matambiko au dawa lakini wapi, wengi hudhani makelele ni kwamba wametupiwa majini kumbe ni quinine.

Hizi kampuni zingetumia hizi dawa ulaya nakwambia saizi kungekuwa kuna wagonjwa wamelipwa fidia ya mabilioni, Yani kampuni inatengenezaje dawa ambayo inamfanya mtu awe kiziwi kwamfano??, maana kiukweli bila maskio mtu umeshamkwa sana

vipi, simu unaskia fresh au ni mwendo wa meseji
 
hapana mafuta ya kuku sijatumia, yanatumikaje.
Sauti kubadilika ni lazima maana unaiskia tofauti na kawaida.

huo ugonjwa wa kelele niiwahi ona jamaa mwenye tatizo hili alikua anajichanfa aende zanzibar kuna mzungu hapo zanzibar ana mitungi ile ya oxygen watu wenye magonjwa flani wanainiaga humo ndani kama kwa dakika 20 hivi kila siku kwa wiki nzima ili kutibu magonjwa yanayotolewa kwa hio gesi ya oxygen.

vp, umejaribu mafuta ya kuku??
 
Habarini,

Jana katika kupitia taarifa za group, la shule niliyosoma secondary, nakutana na ujumbe kuwa naima, anaolewa jumamosi ya leo, nimekosa raha ndugu zangu, kwani ni miaka takribani 13 imepita nikijitahidi kusahau, ila kila nikiangalia hali yangu ya ulemavu najikuta nakumbuka na kuyachukia mapenzi.

Mimi nilizaliwa mzima kabisa na sasa nina miaka 35, baada ya kumaliza chuo, nilikuwa na mahusiano na binti fulani ambaye tulisoma nae secondary hapa dar, nakumbuka kuonana nae ilikuwa ni kama bahati tu na kila muda naumia natamani nisingeonana nae labda leo hii ningekuwa mzima kabisa.

Mwanzo alikuwa ni mtu wa kipekee sana, nilijulikana kwao na kwetu walimjua, na kwakuwa nilikuwa na kazi private office moja hapa mjini(sitapenda kuitaja) nilijitahidi fanya uwekezaji mdogo kwake nilikopa kiasi fulani cha pesa mil 7 kwa dhamana ya kazi nikamfungulia duka kwa matumaini ya kuwa, kwakuwa sisi ni kitu kimoja mwenzangu nae asimame kwani alikuwa anashinda tu nyumbani kwao.

Nilipata misukosuko kazini na nikasimamishwa kazi na hapo ndipo nilipoanza kutoelewana na mwenzangu dharau ilikuwa kubwa, kejeli, unamuomba muonane anagoma au anakubali na hatokei kabisa na simu anazima, ndani ya miezi miwili, nilikuwa nimepata msongo mkubwa wa mawazo maana madeni na hali ngumu na mwenzangu haeleweki sikujua nifanye nini zaidi ya kunywa pombe.

Siku ya tukio jumatano ile niliamka mzima kabisa, jioni nilipanga kwenda alipopanga naima bila taarifa kwani kila nikimjulisha basi hatoi ushirikiano. Nilitaka tukubaliane tuuze duka nifund hela kidogo ya kiwanja nilichonacho nifungue biashara nyingine, inisaidie kufanya marejesho bank.

Sikuwahi fikiria kama ananisaliti nilijua tu ni kutingwa na kazi na kuwa na mood mbaya, saa 1 nilienda kwake kwakujua aliishafunga biashara nilivyofika kwake, niligonga mlango kukawa kimya, nilikuwa na funguo za kwake na yeye alikuwa nazo za kwangu nikafungua mlango.

Sikuamini macho yangu naima alikuwa na rafiki angu kipenzi salim wakifanya mepenzi pale sebuleni wakapigwa na mshangao kwani hawakunitarajia, nilirudi nyuma na kuanza kutoka pale nikiwa na maumivu zaidi na kujiona sifai nikiwa mita chache tu kutoka pale nikivuka barabara nilisikia honi ya gari mara 2 baada ya hapo sikukumbuka kitu tena.

Baada ya kuamka nilikuta ndugu zangu wakiwa hospital namimi wakiwa na huzuni, baada ya siku 2 ndiyo niligundua mguu wangu wa kushoto sina tena nilielezwa uliharibika kutokana na kusagwa na gari, nililia sana na bado nalia sana, nilijiuliza nimefanya dhambi gani kustahili adhabu hii, niliwaza nitalipaje deni la bank na nitawezaje kuanza maisha katika hali yangu ya ulemavu.

Baada mwezi 1 nanusu nikatoka hospitalini, ila ikawa kama ninamkosi kwani baada ya mwezi nilikamatwa na malaria kali sana nikajua ndio mwisho wa maisha yangu, nilikuwa naweweseka sana, hospital wakaniwekea dripu ya Quinine, masikini ningejua naenda pata ulemavu mwingine ni bora ningejitibia nyumbani, ila nilipona vizuri baada ya week tu...

Baada ya miezi 7 nilianza poteza uwezo wa kusikia taratibu na kupoteza balance ya kutembea sikugundua mapema ila baada ya kufikisha mwaka na miezi 2, nilikuwa natatizo lingine la kutosikia vizuri.

Maisha yangu yalibadilika sikuwa na furaha tena na leo hii mwanamke alieniharibia maisha yangu ambaye naamini ni chanzo cha ulemavu wangu anaenda kuolewa najiuliza nimeikosea nini dunia, muda mwingine natamani kufariki kwani ninayopitia ni mazito kushinda uwezo wangu wa kustahili.

Ewe maisha, nilikukosea nini?

Hongera sana mkuu una kipaji cha UTUNZI ,mtafute Director Bongo Movie Bishop Hiluka muandae script yake mutengeneze Movie.
 
Misfortunes never come singly (proverb) = Bad things, event, situations, outcomes, etc., almost always arrive in groups of two or more all at once or in quick succession.
 
mkuu usije ukawaonea wanawake huruma ni viumbe wasio jielewa akili zao zinafanana na kuku. Ukitaka kuwekeza wekeza kwa watoto maskini na watu wasiojiweza kama ndugu zako hawapo.
 
Back
Top Bottom