Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

Habarini,

Jana katika kupitia taarifa za group, la shule niliyosoma secondary, nakutana na ujumbe kuwa naima, anaolewa jumamosi ya leo, nimekosa raha ndugu zangu, kwani ni miaka takribani 13 imepita nikijitahidi kusahau, ila kila nikiangalia hali yangu ya ulemavu najikuta nakumbuka na kuyachukia mapenzi.

Mimi nilizaliwa mzima kabisa na sasa nina miaka 35, baada ya kumaliza chuo, nilikuwa na mahusiano na binti fulani ambaye tulisoma nae secondary hapa dar, nakumbuka kuonana nae ilikuwa ni kama bahati tu na kila muda naumia natamani nisingeonana nae labda leo hii ningekuwa mzima kabisa.

Mwanzo alikuwa ni mtu wa kipekee sana, nilijulikana kwao na kwetu walimjua, na kwakuwa nilikuwa na kazi private office moja hapa mjini(sitapenda kuitaja) nilijitahidi fanya uwekezaji mdogo kwake nilikopa kiasi fulani cha pesa mil 7 kwa dhamana ya kazi nikamfungulia duka kwa matumaini ya kuwa, kwakuwa sisi ni kitu kimoja mwenzangu nae asimame kwani alikuwa anashinda tu nyumbani kwao.

Nilipata misukosuko kazini na nikasimamishwa kazi na hapo ndipo nilipoanza kutoelewana na mwenzangu dharau ilikuwa kubwa, kejeli, unamuomba muonane anagoma au anakubali na hatokei kabisa na simu anazima, ndani ya miezi miwili, nilikuwa nimepata msongo mkubwa wa mawazo maana madeni na hali ngumu na mwenzangu haeleweki sikujua nifanye nini zaidi ya kunywa pombe.

Siku ya tukio jumatano ile niliamka mzima kabisa, jioni nilipanga kwenda alipopanga naima bila taarifa kwani kila nikimjulisha basi hatoi ushirikiano. Nilitaka tukubaliane tuuze duka nifund hela kidogo ya kiwanja nilichonacho nifungue biashara nyingine, inisaidie kufanya marejesho bank.

Sikuwahi fikiria kama ananisaliti nilijua tu ni kutingwa na kazi na kuwa na mood mbaya, saa 1 nilienda kwake kwakujua aliishafunga biashara nilivyofika kwake, niligonga mlango kukawa kimya, nilikuwa na funguo za kwake na yeye alikuwa nazo za kwangu nikafungua mlango.

Sikuamini macho yangu naima alikuwa na rafiki angu kipenzi salim wakifanya mepenzi pale sebuleni wakapigwa na mshangao kwani hawakunitarajia, nilirudi nyuma na kuanza kutoka pale nikiwa na maumivu zaidi na kujiona sifai nikiwa mita chache tu kutoka pale nikivuka barabara nilisikia honi ya gari mara 2 baada ya hapo sikukumbuka kitu tena.

Baada ya kuamka nilikuta ndugu zangu wakiwa hospital namimi wakiwa na huzuni, baada ya siku 2 ndiyo niligundua mguu wangu wa kushoto sina tena nilielezwa uliharibika kutokana na kusagwa na gari, nililia sana na bado nalia sana, nilijiuliza nimefanya dhambi gani kustahili adhabu hii, niliwaza nitalipaje deni la bank na nitawezaje kuanza maisha katika hali yangu ya ulemavu.

Baada mwezi 1 nanusu nikatoka hospitalini, ila ikawa kama ninamkosi kwani baada ya mwezi nilikamatwa na malaria kali sana nikajua ndio mwisho wa maisha yangu, nilikuwa naweweseka sana, hospital wakaniwekea dripu ya Quinine, masikini ningejua naenda pata ulemavu mwingine ni bora ningejitibia nyumbani, ila nilipona vizuri baada ya week tu...

Baada ya miezi 7 nilianza poteza uwezo wa kusikia taratibu na kupoteza balance ya kutembea sikugundua mapema ila baada ya kufikisha mwaka na miezi 2, nilikuwa natatizo lingine la kutosikia vizuri.

Maisha yangu yalibadilika sikuwa na furaha tena na leo hii mwanamke alieniharibia maisha yangu ambaye naamini ni chanzo cha ulemavu wangu anaenda kuolewa najiuliza nimeikosea nini dunia, muda mwingine natamani kufariki kwani ninayopitia ni mazito kushinda uwezo wangu wa kustahili.

Ewe maisha, nilikukosea nini?
Samahan Kaka ang njoo pm
 
hongera ndugu yangu kwa ajira na pole kwa tatizo la masikio, najua jinsi unavyoumia na unayopitia, yani tatizo la masikio ndo limefanya hata nje nisitake kutoka mtu anakwambia hujambo unasema salama inaumiza sana, mazungumzo unapata kwa asilimia 40 tu hizo nyingine unabaki kusema ndio hivyo au kucheka inaumiza sana,

nandio kikwazo kikubwa kwangu kuanza kujiajiri nawaza nitahudumiaje wateja wa hizo nguo au ndio nitaulizwa hii bei gani nitasema salama tena Mungu anihurumie tu.
Kaka acha kabisa ni hatar labda watu hwajanizoea naona karaha sitaki kuongea hata na demu
 
Pole kaka na ulemavu wakupatia ukubwani inachukua muda sana kuukubali, muda mwingine simu inaita unaacha hadi ikate tunapoteza pesa na watu wa karibu ila Mungu ni mwema mkuu yatakwisha sikumoja.
 
Mi sishakubali na kazi napiga ila sipend kusemeshwa kabisa itakavyokuwa ndo ivyo ivyo sina tabu na mtu nishakubali najikubali sana wapo wanaonikubali but kuna watu wananipa simanzi nilimaliza nao mda sana wengine msingi wengine sekondari basi nikuktana nao wanasema una dharau tunakuita hugeuki naona maisha bora yaendelea pesa ninayo mshallah, navaa kila kitu 😋😋😋😊😊😊sio kesi ndhani mke wangu atakuja nielewa tu
 
Habarini,

Jana katika kupitia taarifa za group, la shule niliyosoma secondary, nakutana na ujumbe kuwa naima, anaolewa jumamosi ya leo, nimekosa raha ndugu zangu, kwani ni miaka takribani 13 imepita nikijitahidi kusahau, ila kila nikiangalia hali yangu ya ulemavu najikuta nakumbuka na kuyachukia mapenzi.

Mimi nilizaliwa mzima kabisa na sasa nina miaka 35, baada ya kumaliza chuo, nilikuwa na mahusiano na binti fulani ambaye tulisoma nae secondary hapa dar, nakumbuka kuonana nae ilikuwa ni kama bahati tu na kila muda naumia natamani nisingeonana nae labda leo hii ningekuwa mzima kabisa.

Mwanzo alikuwa ni mtu wa kipekee sana, nilijulikana kwao na kwetu walimjua, na kwakuwa nilikuwa na kazi private office moja hapa mjini(sitapenda kuitaja) nilijitahidi fanya uwekezaji mdogo kwake nilikopa kiasi fulani cha pesa mil 7 kwa dhamana ya kazi nikamfungulia duka kwa matumaini ya kuwa, kwakuwa sisi ni kitu kimoja mwenzangu nae asimame kwani alikuwa anashinda tu nyumbani kwao.

Nilipata misukosuko kazini na nikasimamishwa kazi na hapo ndipo nilipoanza kutoelewana na mwenzangu dharau ilikuwa kubwa, kejeli, unamuomba muonane anagoma au anakubali na hatokei kabisa na simu anazima, ndani ya miezi miwili, nilikuwa nimepata msongo mkubwa wa mawazo maana madeni na hali ngumu na mwenzangu haeleweki sikujua nifanye nini zaidi ya kunywa pombe.

Siku ya tukio jumatano ile niliamka mzima kabisa, jioni nilipanga kwenda alipopanga naima bila taarifa kwani kila nikimjulisha basi hatoi ushirikiano. Nilitaka tukubaliane tuuze duka nifund hela kidogo ya kiwanja nilichonacho nifungue biashara nyingine, inisaidie kufanya marejesho bank.

Sikuwahi fikiria kama ananisaliti nilijua tu ni kutingwa na kazi na kuwa na mood mbaya, saa 1 nilienda kwake kwakujua aliishafunga biashara nilivyofika kwake, niligonga mlango kukawa kimya, nilikuwa na funguo za kwake na yeye alikuwa nazo za kwangu nikafungua mlango.

Sikuamini macho yangu naima alikuwa na rafiki angu kipenzi salim wakifanya mepenzi pale sebuleni wakapigwa na mshangao kwani hawakunitarajia, nilirudi nyuma na kuanza kutoka pale nikiwa na maumivu zaidi na kujiona sifai nikiwa mita chache tu kutoka pale nikivuka barabara nilisikia honi ya gari mara 2 baada ya hapo sikukumbuka kitu tena.

Baada ya kuamka nilikuta ndugu zangu wakiwa hospital namimi wakiwa na huzuni, baada ya siku 2 ndiyo niligundua mguu wangu wa kushoto sina tena nilielezwa uliharibika kutokana na kusagwa na gari, nililia sana na bado nalia sana, nilijiuliza nimefanya dhambi gani kustahili adhabu hii, niliwaza nitalipaje deni la bank na nitawezaje kuanza maisha katika hali yangu ya ulemavu.

Baada mwezi 1 nanusu nikatoka hospitalini, ila ikawa kama ninamkosi kwani baada ya mwezi nilikamatwa na malaria kali sana nikajua ndio mwisho wa maisha yangu, nilikuwa naweweseka sana, hospital wakaniwekea dripu ya Quinine, masikini ningejua naenda pata ulemavu mwingine ni bora ningejitibia nyumbani, ila nilipona vizuri baada ya week tu...

Baada ya miezi 7 nilianza poteza uwezo wa kusikia taratibu na kupoteza balance ya kutembea sikugundua mapema ila baada ya kufikisha mwaka na miezi 2, nilikuwa natatizo lingine la kutosikia vizuri.

Maisha yangu yalibadilika sikuwa na furaha tena na leo hii mwanamke alieniharibia maisha yangu ambaye naamini ni chanzo cha ulemavu wangu anaenda kuolewa najiuliza nimeikosea nini dunia, muda mwingine natamani kufariki kwani ninayopitia ni mazito kushinda uwezo wangu wa kustahili.

Ewe maisha, nilikukosea nini?
Amini Mungu, huyu kibaka aliyekuharibia maisha ana yake na usikute pengine ni Mungu huyo huyo aliyetaka kukuepusha na huyu mwanamke. Time will tell.
 
Malipo yote ni hapa hapa....

Huyo binti na yeye siku zake zinahesabika...

Ngoja tuone...
 
hongera ndugu yangu kwa ajira na pole kwa tatizo la masikio, najua jinsi unavyoumia na unayopitia, yani tatizo la masikio ndo limefanya hata nje nisitake kutoka mtu anakwambia hujambo unasema salama inaumiza sana, mazungumzo unapata kwa asilimia 40 tu hizo nyingine unabaki kusema ndio hivyo au kucheka inaumiza sana,

nandio kikwazo kikubwa kwangu kuanza kujiajiri nawaza nitahudumiaje wateja wa hizo nguo au ndio nitaulizwa hii bei gani nitasema salama tena Mungu anihurumie tu.
Pole sana braza yan bora ungekatwa miguu miwili afu masikio yabaki vizuri..

Ulemavu wa kusikia mbaya sana huwezi kakaa popote kwa amani kama husikii vizuri
 
mkuu japo kwa miguu ningeteseka pia ila kwa masikio napata tabu sana kwa muda mchache ambao nafanya conversation na watu naambulia asilimia 40 tu na kwenye simu naambulia 20 kama sio 10 tena kwa loud speaker, Mungu ni mwema muda mwingine tunaweza ongea tu vizuri hata dakika 30 ila milio ikianza masikioni na ukiwa mbali hata jina siwezi kuitika.

Back
Top Bottom