Nilimuona Bwana ameketi katika kiti cha enzi (Utukufu wake ni mkuu)

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,664
59,735
Nawasalimu wana JF

Watu wote duniani, wasio soma na waliosoma; watafiti na wasio watafiti hatujui kabla na baada ya kufa kitu gani kitatokea. Wengine wanakuja na theories za Time travel lengo lake ni kujifariji.

Nilikuwa katika ROHO siku ya Bwana, hakika siku hiyo ilikuwa siku kuu kwangu. Maana nilichukuliwa juu sana nikapita mbingu ya kwanza mpaka nikafika mbingu ile Bwana alikoketi. Nilifika katika mji unaong'aa taa zake za rangi ya zambarau, barabara zake zikiwa na rangi ya dhahabu. Kisha nilisikia sauti ikiniita, nami nikigeuka na kukutana uso kwa uso na kiumbe mwenye mabawa makubwa mawili, uso wake wa kung'aa sana kama jua.

Akaniambia Bwana amenituma kwako nikuambia habari ya mambo mengi. Nami nikamuuliza wewe ni nani na unatokea wapi. Akajibu mimi ni mtumishi wa Bwana nimetumwa na yule mzee wa miaka nikuletee habari.

Tazama mnatafuta kujua habar za ulimwengu huku mkishindwa kutafuta kujua habari za Roho ambako ndiko chemichemi za uzima zinatoka. Upendo ndilo msingi wa kuwafanya muishi kwa pamoja. Dunia hii mnaoyoishi kitambo kidogo tu itateketea. Hakuna awezae kuzuia maangamizo ya dunia. Chini na juu ya dunia nimeweka moto. Pale matetemeko yatakapoanza moto kutoka chini utaiteketeza dunia, hakuna kilicho hai kitabaki juu yake.

Sasa basi wekezeni katika Roho ili mpate maarifa.

Yule kiumbe alinichukua na kunipeleka sehemu. Nilipofika sehemu hiyo nguvu ziliniishia na kuanguka kifudi kufidi huku nikisujudu. Mbele yangu kulikuwa na kiti kikubwa, utukufu ukikizunguka kiti hicho. Ndipo sauti kuu ya Bwana nikaisikia ikisema "UMEPATA NEEMA KUYAJUA HAYA" Ndipo Bwana akaniambia nimekutuma wewe uwafungue roho zao wajue kusudi langu na mimi ni nani. Wapate kujua hakuna wa kushindana na mimi. Mimi ndiye mwanzo na mimi ndiye mwisho. Mimi ndiye niliye umba ngiza na ndiye niliye umba mwanga.

NIITE "NDIVYO NILIVYO, UTAVYO NILIVYO"

Bwana ni mwema, mawazo yake hayachunguziki. Hakuna aijuaye kesho, hakuna ajuaye kabla ya kuzaliwa alikuwaje. Hakuna ajuaye akili anapata kutoka wapi. Watu wanachunguza yale yanayoonekana. Yanayoonekana yametokana na yasiyoonekana.

Tafuta kujua mambo ya ROHO. Ukila baadae utapata njaa, ukipata mali utataka zaidi na zaidi. Hofu imetanda kwa kila mtu akiihofia kesho.

WATU WANAOGOPA WASICHOKIJUA, WANAHOFIA KESHO.
 
@genecandy.wanaanzaga hivi hivi halafu unasikia fulani kafa. Wakichokana siku hizi wanapotezana, naona kama kuna kitu tunaonywa au kukumbushwa hapa.
 
Isa 6:1-3 SUV

Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu. Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka. Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.

Be blessed
 
Katika mwili huwezi ukamwona Bwana ukaishi. Katika Roho utukufu wa Bwana ni mkuu.

Science inaongelea mambo ya Mwili. Mambo ya Roho yanajulikana kwa Elimu ya Roho.

Elimu ya Roho kwa wenye ufahamu ya dunia kwao ni upuuzi, lakini kwao wenye kujua ni uzima. Lakini kiwango cha upuuzi wa elimu ya Roho ni nguvu kubwa katika mwili.

Hakuna kinachoweza kuwako, kichopo pasipo Roho.
 
Amen.

Mambo ya rohoni bila kujihusisha na biblia ni ngumu sana kwa wahusika kuyaelewa.
 
Kisha shetani akamchukua yesu hadi katika mlima mreeefu, na huko akamwonyesha falme zote za dunia...
FLrK7nDVQAQb63a.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom