Nilimshirikisha mama yangu mafanikio yangu nikadhani amefurahi, baada ya muda kila nikiwasiliana naye ananiambia isijekuwa naenda kwa waganga

Mr Why

JF-Expert Member
Nov 27, 2019
1,353
2,351
Mimi nikijana wa miaka 27 nilishinda betting kiasi kikubwa tu cha pesa lakini sikuwahi kumweleza mwanafamilia yeyote na wala hakuna anayefahamu, nikaamua kujenga nyumba kupitia zile pesa za betting kwahiyo nikawa na nyumba ya ghafla

Sikutaka kumshirikisha ndugu au mwanafamilia kwa haraka
Nikaanza kumshirikisha mama yangu mzazi nikajua atafurahi

Jambo la kushangaza akashtuka sana baada ya muda kidogo kila nikiongea nae ananambia kuna utajiri wa kafara isijekuwa nimejiunga nikadhani labda ameongea tu lakini kila mara anasema maeneno hayo hayo
Kwahiyo leo nagundua kuwa tayari ananiita mchawi

Kuna kaka yangu naye ni mlokole kwa miaka yote na mwamini lakini huwezi kuamini siku anakuja kwangu alipoondoka alianza kunizungumzia habari za kafara

Naona jinsi gani familia yangu nitavunja nao uhusiano kwasababu ya kunipakazia mambo makubwa kiasi hiki
Inawezekanaje mama yako mzazi anathubutu kukutamkia maneno kama haya ni dhahiri nimezaliwa familia yenye laana ya mafanikio

Unathubutuje kumshutumu mtu kuwa ana mali za kafara wakati pesa kapata kupitia betting akiwa kama mtu mzima kwanini asingetulia akaambiwa taratibu badala ya kutapika maneno machafu kama haya
Watu wengi wanasema kuzaliwa bongo ni nuksi kwakweli nimeona
 
Unapomuambia mtu kuwa una mradi basi jitahidi pia kumueleza chanzo cha fedha zako.

Haiwezekani kijana amemaliza tu chuo, alafu mwezi unaofata una nyumba tayari na gari la kutembelea.

Mzazi atakayefurahia bila ya kujua chanzo cha mapato yako, hakupendi. Na pengine wazazi wetu wa kiafrika mawazo yao yataenda huko kwenye ulozi.

Hivyo, ungepaswa kumuambia mama nilishinda mkeka. Nikapata kiasi kadhaa na nikaamua kujenga nyumba hii. Angekuwa na amani na chanzo cha mapato yako.
 
Elewa kwamba mafanikio ya haraka lazima yatiliwe shaka. Hivi unafikiri ni rahisi mama yako ghafla tu aone una nyumba then unakuwa na jibu rahisi kwamba nilishinda betting akubaliane na hilo?

Inawezekana ni kweli umeshinda na umeamua kujenga, usiwalaumu wao kuwa na Mashaka na wewe, endelea kuongea nao polepole tu mwisho mtaelewana,....hiyo kitu hata kama ni wewe mwanao anakuletea habari hiyo lazime uwe na wasiwasi unaweza kuhisi wewe ndo upo kwenye mpango wa kafara itakayofanyika.
 
Back
Top Bottom