Nilimkaribisha rafiki kwangu kanipandia kichwani

STABILIZER

Member
Joined
Jan 7, 2013
Posts
10
Reaction score
13
Jamani kuna watu hawana heshima kabisa,

Mimi ni mwanaume, nina mke na watoto wawili. Pia nafanya kazi sehemu moja na rafiki yangu (pia mwanaume, naye ana familia). Hajahamisha familia yake, kwa hiyo anakaa kwangu. Kwa sasa mke wangu yuko masomoni na watoto ameenda nao. Nimebaki na huyu jamaa, ambaye wakati mwingine mke wake huja kumsalimia na nimewatengea chumba chao.

Nimekerwa na tabia ya huyu jamaa. Analeta wanawake nyumbani kwangu anasema ni marafiki zake tuu. Kuna siku nilienda church yeye akabaki home akamwita msichana amfulie na wakafanya mapenzi nyumbani kwangu na kwenye kitanda changu. Mwanzoni aligoma, lakini baadaye nikamtega kwenye kupiga stori akakiri.

Leo asubuhi tumekuja kazini, mimi nikiwa nimepewa majukumu fulani hapa kazini, jamaa akijua kuwa siwezi kutoka, akaniomba funguo na kusema kasahau kitu fulani. Kumbe mwenzangu ameenda na msichana na baada ya muda akarudi kazini. nikamwomba anirudishie key akasema ameacha home kuna mtu anamfulia nguo. Nimemwuliza ni nani kagoma kuniambia ni nani.

Namweleza uhalisia wa athari zake ananibishia

Moja, huyo mtu ameachiwa funguo, je akienda kuchonga na tukiibiwa in the future itakuwaje?
Pili, amemwambia amfanyie na usafi kwa maana ya kudeki nyumba, je usalama uko wapi?
Privacy ya nyumbani kwangu iko wapi?
Mimi ni kiongozi wa kanisa na wakati mwingine ninakaa na fedha za kanisa. Kwa sababu kanisa lenyewe ni dogo, huwa siendi BENKI kila wiki, at least ikifika kuanzia millioni moja na kuendelea ndo nazipeleka benki. Sasa je, nikiibiwa atakuwa tayari kuwajibuka?

Amebaki tuu kuuchuna hata kuomba msamaha hataki, anaona alilofanya ni sawa.

Nishaurini wazoefu nimfanyeje huyu mtu? Nafikiria kumwambia atafute chumba apange ili awe huru
 
Mimi sioni sababu ya kujiuliza, au kuomba ushauri, ure a real Men, Mwite mwambie hali halisi ya jinsi unavyokereka na Tabia yake, Pia mwambie atafute chumba chake ambaho atakuwa huru kufanya mambo yake hayo, machafu, usilee kidonda kitakuumbua, kwa sababu siku mkeo akirudi akamkuta huyo mdada hapo ndani utamweleza nn akuelewe? Je utamshauri vipi kuwa na wewe hukuwa unaingiza na wewe wanawake yeye akiwa hayupo? Maana ndege wanaofanana huruka pamoja. So kama Tabia yako haiendani na huyo Rafiki yako better umwambie aondoke kuokoa ndoa yako na Amani iliyokuwepo
 
Hili suala wala halikuhitaji kufuata ushauri hapa JF ni kutumia akili tu ya kawaida na kumwambia "ONDOKA NENDA KAPANGE". Inamaana hata room moja anashindwa kupanga wakati akijipanga, this is too much bana, ukiendelea kumchekea mtakuja kugombana vibaya na ukawa mwisho wa ushikaji wetu, shauri yako!
 
Ubest gharama.. Vaa sura ya kazi!! Mwambie unampa muda wa week, aondoke au umwambie wazazi wako ama ndugu zako kijijin wanakuja kusoma mjini na chumba ni kile kile anacholala,kama unamwonea huruma kumpa za uso.
 
Siku ukiibiwa ndio uje kuomba ushauri,sawa mtumishi wa Mungu eeh!
Hivi huko unakofanya kazi ndio mnavyofundishwa kulea mambo ya uzinzi?Maana haiwezekani unaona mambo machafu yanafanyika nyumbani kwako na wewe umekaa tu kulalalmika na kutaka ushauri bila kuchukua hatua.

Dah kazi kweli kweli binadamu tunajisahau sana .wewe unakaajer na huyo jamaa kwani halipwi mshahara ?mwambie akapange
 
Jamani kuna watu hawana heshima kabisa,

Mimi ni mwanaume, nina mke na watoto wawili. Pia nafanya kazi sehemu moja na rafiki yangu (pia mwanaume, naye ana familia). Hajahamisha familia yake, kwa hiyo anakaa kwangu. Kwa sasa mke wangu yuko masomoni na watoto ameenda nao. Nimebaki na huyu jamaa, ambaye wakati mwingine mke wake huja kumsalimia na nimewatengea chumba chao.

Nimekerwa na tabia ya huyu jamaa. Analeta wanawake nyumbani kwangu anasema ni marafiki zake tuu. Kuna siku nilienda church yeye akabaki home akamwita msichana amfulie na wakafanya mapenzi nyumbani kwangu na kwenye kitanda changu. Mwanzoni aligoma, lakini baadaye nikamtega kwenye kupiga stori akakiri.

Leo asubuhi tumekuja kazini, mimi nikiwa nimepewa majukumu fulani hapa kazini, jamaa akijua kuwa siwezi kutoka, akaniomba funguo na kusema kasahau kitu fulani. Kumbe mwenzangu ameenda na msichana na baada ya muda akarudi kazini. nikamwomba anirudishie key akasema ameacha home kuna mtu anamfulia nguo. Nimemwuliza ni nani kagoma kuniambia ni nani.

Namweleza uhalisia wa athari zake ananibishia

Moja, huyo mtu ameachiwa funguo, je akienda kuchonga na tukiibiwa in the future itakuwaje?
Pili, amemwambia amfanyie na usafi kwa maana ya kudeki nyumba, je usalama uko wapi?
Privacy ya nyumbani kwangu iko wapi?
Mimi ni kiongozi wa kanisa na wakati mwingine ninakaa na fedha za kanisa. Kwa sababu kanisa lenyewe ni dogo, huwa siendi BENKI kila wiki, at least ikifika kuanzia millioni moja na kuendelea ndo nazipeleka benki. Sasa je, nikiibiwa atakuwa tayari kuwajibuka?

Amebaki tuu kuuchuna hata kuomba msamaha hataki, anaona alilofanya ni sawa.

Nishaurini wazoefu nimfanyeje huyu mtu? Nafikiria kumwambia atafute chumba apange ili awe huru

Mfukuze nyumbani kwako. Hana Adabu hata kidogo. Anakuona wewe ni Juha. Leo ukitoka kazini mchane "live", na ikiwezekana tupa nje ya nyumba yako mazagazaga yake. Watu wengine hawana heshima kabisa.
 
... Kwa sasa mke wangu yuko masomoni na watoto ameenda nao. Nimebaki na huyu jamaa, ambaye wakati mwingine mke wake huja kumsalimia na nimewatengea chumba chao ...

.... Nimekerwa na tabia ya huyu jamaa. Analeta wanawake nyumbani kwangu anasema ni marafiki zake tuu. Kuna siku nilienda church yeye akabaki home akamwita msichana amfulie na wakafanya mapenzi nyumbani kwangu na kwenye kitanda changu ...

Pole sana mkuu kwa yaliyokukuta. Naamini ulimkaribisha kwa nia njema ya kumsaidia kama rafiki na nafikiri haukujua kuwa pamoja na yeye kuwa na familia kama wewe bado mwenzio ana vitabia vya uzinzi!!!

Hapo nilipobold umenichanganya sana, umesema kuwa uliwatengea chumba chao na baadaye pia ukasema kuwa alimwita msichana akafanya naye mapenzi chumbani kwako!!! Sasa hapa inamaana aliacha chumba chake na kuingia chumbani kwako? Ina maana huwa hufungi chumba chako? Ina maana pia kuwa rafiki yako umempa mamlaka ya kuona na kulalia kitanda ancholalia mkeo? Siku mkeo akirudi ukamkuta na rafiki yako utamkasirikia nani? Na hizo sadaka huwa unazitunzia wapi? Nahisi kuna aina fulani ya ka-uzembe kalikupita ktk kumkaribisha huyo mgeni wako!

Nafikiri kwa hizo tabia za kihuni alizoanza, zinaweza kukufanya na wewe uonekane muhuni na kukuharibia kazi yako ya kuchunga kondoo wa Bwana. Kama ni kweli haya usemayo, nakushauri kama mtu mzima, si jambo jema kulea tatizo na ni bora kufanya maamuzi mapema kabla mambo hayajawa mabaya zaidi, vinginevyo utakuwa unahatarisha usalama wa ndoa na familia yako pia. Mtu mzima kama huyo huwezi kumuonya na wala hawezi kubadili tabia kama ndo mchezo aliouzoea.
 
Duh, ndugu yangu huo wema wako sasa unapitiliza na hujitendei haki hata wewe mwenyewe, hayo anayoyafanya huwa yanafanywa na vijana wanaojiita masela, mi nisingekubali, huyo aondoke tu akapange chumba cha kufanyia huo uchafu wake!

NB: Isijekuwa na wewe una tabia ya kuleta wanawake home hivyo anakuiga, au anakufahamu ulikuwa na tabia hiyo kabla ya kuoa na anaona huwezi kumshangaa!
 
siwezi kukushauri ila siku nyingine jifunze utakaaje n jamaa ambaye ana familia?
 
Fukuzia mbali mayala huyo!!!! Atakuletea matatizo!! Just urafiki tu. To hell with him.
 
Pole sana mkuu kwa yaliyokukuta. Naamini ulimkaribisha kwa nia njema ya kumsaidia kama rafiki na nafikiri haukujua kuwa pamoja na yeye kuwa na familia kama wewe bado mwenzio ana vitabia vya uzinzi!!!

Hapo nilipobold umenichanganya sana, umesema kuwa uliwatengea chumba chao na baadaye pia ukasema kuwa alimwita msichana akafanya naye mapenzi chumbani kwako!!! Sasa hapa inamaana aliacha chumba chake na kuingia chumbani kwako? Ina maana huwa hufungi chumba chako? Ina maana pia kuwa rafiki yako umempa mamlaka ya kuona na kulalia kitanda ancholalia mkeo? Siku mkeo akirudi ukamkuta na rafiki yako utamkasirikia nani? Na hizo sadaka huwa unazitunzia wapi? Nahisi kuna aina fulani ya ka-uzembe kalikupita ktk kumkaribisha huyo mgeni wako!

Nafikiri kwa hizo tabia za kihuni alizoanza, zinaweza kukufanya na wewe uonekane muhuni na kukuharibia kazi yako ya kuchunga kondoo wa Bwana. Kama ni kweli haya usemayo, nakushauri kama mtu mzima, si jambo jema kulea tatizo na ni bora kufanya maamuzi mapema kabla mambo hayajawa mabaya zaidi, vinginevyo utakuwa unahatarisha usalama wa ndoa na familia yako pia. Mtu mzima kama huyo huwezi kumuonya na wala hawezi kubadili tabia kama ndo mchezo aliouzoea.

siyo kitanda changu kwa maana ya bed room yangu. Namaanisha hicho chumba nilichowapa wanatumia kitanda changu, yaani kaja na begi lake tuu.
 
Acha kumuonea haya,we hapo ni kwako

mwambie ukweli,jiamini kama mwanume asile upumbavu ndani ya nyumba yako
 
Sasa mbona mwenyewe umesha sema unafikiria kumfukuza? na sababu zote za kumfukuza unazo?
 
Ndg yangu, ndio umeamua kwa dhati kbs kuja kunidharirisha huku? Mbona wewe kipindi hujapata kazi uliishi kwetu na ulikuwa unavusha madem kama upo kwenu? Haya nashkr, ila hata hivyo nilikuwa nimepanga mwisho wa mwezi huu nikajitegemee. Asante sana!
 
Yaani huwa upo urafiki wa kubebana ila mara nyingi unategemea ustaarabu wa mbebwaji.
Na wengi tumeacha mambo hayo ya kumkaribisha rafiki au hata mashosti kwa kinadada kwa mambo ya kijinga ya "kutonata na beat" zako. Na mtu asiponata na beat inakera sana utatamani hata UMTAFUNE!
Kwa wengine inakuwa taabu kuongea naye kutokana na msingi wa urafiki wenyewe...
Usimwesabie makosa yake, wala nini,ila mkalishe chini,muulize atakaa bila familia mpaka lini! Kisha mwambie unahitaji kukaa peke yako,na anayezidi,basi familia yako. Na akuombe muda ambao ukifika tu,awe ameshahama.
 
Yaani huwa upo urafiki wa kubebana ila mara nyingi unategemea ustaarabu wa mbebwaji.
Na wengi tumeacha mambo hayo ya kumkaribisha rafiki au hata mashosti kwa kinadada kwa mambo ya kijinga ya "kutonata na beat" zako. Na mtu asiponata na beat inakera sana utatamani hata UMTAFUNE!
Kwa wengine inakuwa taabu kuongea naye kutokana na msingi wa urafiki wenyewe...
Usimwesabie makosa yake, wala nini,ila mkalishe chini,muulize atakaa bila familia mpaka lini! Kisha mwambie unahitaji kukaa peke yako,na anayezidi,basi familia yako. Na akuombe muda ambao ukifika tu,awe ameshahama...
 
Waswahili wanasema "ufanze muhali na chako unacho, sefanza muhali na chako hunacho"
 
Ndg yangu, ndio umeamua kwa dhati kbs kuja kunidharirisha huku? Mbona wewe kipindi hujapata kazi uliishi kwetu na ulikuwa unavusha madem kama upo kwenu? Haya nashkr, ila hata hivyo nilikuwa nimepanga mwisho wa mwezi huu nikajitegemee. Asante sana!

Duu ni ya kweli haya au unamchemsha tu ? na yeye aje ajibu hapa kama aliwahi kufanya kitendo hiki.
 
Back
Top Bottom