Nililala hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nililala hapa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Luteni, Jan 22, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  LILIKUWA BWENI LANGU HILI![​IMG]


  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa katika bweni la Mapinduzi One, alilolala wakati akiwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Pugu, nje kidogo ya Dara es Salaam kwenye miaka ya 1960.Wazri Mkuu alitembelea shule hiyo jana wakati wa mahafali ya kidato cha Sita.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  My take, hii picha inakufundisha nini wewe kama mwana JF.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  MAFUNZO:
  INAUMIZA MACHO! huh!
   
 3. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2010
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  [FONT="Century Gothic"] Daah [/FONT]Kantalamba au ......?????
   
 4. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Afanye kitu, asishangae sana.. Hiyo ndio shule yenye majengo mazuri zaidi!
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  nahitaji mafunzo kweli hii picha imenishinda kui-edit ni kubwa mno nisaidieni
   
 6. O

  Omumura JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sasa anachoshangaa ni nini?kama ilivo kawaida yake unaweza sikia ameanza kulalamika, mambo ya huyo mtoto wa mkulima bwana!!
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Shule zetu tulizosoma zinatisha ni hivi karibuni zitakuwa magofu. Serikali haitoi hata senti tano kwa ajili ya maintanace ya shule hizo. Hii yote inatokana na donor dependence syndrome tuliyojijengea tunasubiri wafadhili, wawekezaji wakati hela ambayo tunayo tutumia kupuyanga nje ya nchi na kununulia Matoyota vx, nyumba za mawaziri na magavana wamabenki.

  Can anyone imagine toka mradi wa Danida wa school maintanance project ulivyokwisha shule zinaendeshwa bila matenegenezo hata kidogo. Last year nilipata nafasi ya kutembelea shule nilizosoma A level na O level. Najaribu kuzipost nashindwa zikiwa posted hapa ni aibu naomba hii thread iendelezwe kwa yoyote mwenye picha ya shule aliyosoma enzi hizo ili tuone madudu na maajabu.

  Halafu matokeo yakitoka mabaya serikali inajiuliza wakati jibu ni wazi kabisa. Watanzania tuna nini.

  Mkuu wa nchi badala ya kutembelea shule hizi aone madudu na uozo na aweke mikakati nini kifanyike yeye anaenda kufungua shule ya mtu binafsi sijui inaitwa Savvanah something ambayo ada yake mtanzania wa kawaida ataisikia tu kwenye gazeti.

  Hakielimu ya wakati huo ilikuwa sawa na matangazo yake ya KAYUMBA this is KAYUMBALISATION of the education system in the country.
   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Bila watanzania kubadilika ki-mtazamo na kujali zaidi ukarabati........ni sawa na kazi bure. Ukiangalia vyuo na ofisi za wenzetu huku ng'ambo yaani matengenezo/ukarabati wa majengo na vifaa vingine ni kila mwaka lakini kwa Tanzania unakuta bajeti kubwa ni ya matumizi ya mkuu wa idara/sehemu na ukiuliza hela za matengenezo unaambiwa hakuna pesa lakini magari ya wakubwa yote hayawezi kukosa pesa ya mafuta kwa mwakak mzima.
   
 9. D

  Darwin JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hii ni kweli au waandishi wa habari tu?
   
 10. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kinachonisikitisha zaidi ni kuwa Wizara husika zinaongozwa na ma-Professor! Mimi huwa najiuliza sisi watanzania huwa tunaenda shule hadi kufikia uprofessor kwa ajili ya nini?
  hule za primary zinasikitisha zaidi maana ziko mjini hazina fensi vibaka wanaingia wafanya wanachotaka mle wakati mwingine hata madawati huibiwa kwenda kuuzia vitu. Professor kakaa kwenye kiyoyozi tu! Ufisadi huu unaweza kuwa mbaya kuliko wa akina Richmond!
   
 11. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kinachonisikitisha zaidi ni kuwa Wizara husika zinaongozwa na ma-Professor! Mimi huwa najiuliza sisi watanzania huwa tunaenda shule hadi kufikia uprofessor kwa ajili ya nini?
  shule za primary zinasikitisha zaidi maana ziko mjini hazina fensi vibaka wanaingia wafanya wanachotaka mle wakati mwingine hata madawati huibiwa kwenda kuuzia vitu. Professor kakaa kwenye kiyoyozi tu! Ufisadi huu unaweza kuwa mbaya kuliko wa akina Richmond!
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  MpendaTz,

  Nafuu umeliongelea hili la maprofesa. Mi nashindwa kuwaelewa hawa watu, utakuta mtu profesa lakini hana hata website wala hajulikani ni profesa wa nini na currently anajishughulisha na nini kulimngana na uprofesa wake, maana maisha ya kielimu tayari yameshawashinda. Sasa wanabaki kuganga njaa kwenye siasa na kusema mambo ya kijinga ajabu. Chukulia mfano wa Kapuya na ajira 1 M. Ni upuuzi mtupu!
   
 13. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Uoga na maslahi ndio tatizo. Hope mmenipata
   
 14. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Sina nia ya kuwakashfu maprofesa wetu lakini siku hizi siasa za CCM zimewalemaza sana na kuwapelekea kupoteza mwelekeo. Siamini kama mtu kweli umeelimika utakubali kuacha kazi muhimu ya kuelimisha na na kutafiti ukakae unapiga domo tena bila mafanikio yoyote kama tunavyowaona na wakivumilia uongo na ujinga mwingi namna ilivyo sasa. CCM imeufanya uprofesa kuwa chaguo lao siku hizi kutoka kwenye taasisi muhimu ili kupamba siasa zao kama kuchagua sekretari mrembo wa kupamba ofisi! Nalaani kitendo hiki hakisaidii ujenzi wa taifa letu.
   
 15. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #15
  Jan 24, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  WHAT??? Hii ndio ilikuwa moja ya shule za "vichwa" enzi hizo!!
  Mimi ninazo picha za shule niliyosoma zamani, nilienda, sikuamini, nitazipost karibuni, nadhani kuna mtakaoitambua shule hiyo!!
   
 16. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni serikali au wazazi? Nani anatakiwa kugharamia elimu na mahitaji ya mtoto wake? Tusitupe kila jambo kwa serikali. Karo ya sekondari ni 20,000 kwa mwaka napo watu wanalalamika kuwa ni nyingi. Tutegemee nini? Waliosoma nje wanajua karo zao! Mtoto wangu anasoma Isamilo International school yuko grade II primary school na karo ni Pauni 2000 kwa mwaka. Kaitembelee Shule uone ilivyo bomba....

  Fanyeni kazi kwa bidii mlipie gharama za huduma siyo kulalamika tu!
   
 17. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  so what d'you need? go and paste u'r old feelings and lets did what is the next
   
 18. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu hata bajeti ya chai tu ikaachwa ifanye kazi hii kwa miaka mitatu mabadiliko lazima yataonekana.
  Suala ni who cares?
   
 19. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Jitolee basi hata kulikarabati tuweke kumbukumbu yako hapo.
   
 20. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #20
  Jan 25, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Watanzania hatuna utamaduni wa maintenance wala hata hatukuwa na neno la kiswahili lenye maana hiyo. Neno ukarabati tumelibuni miaka ya hivi karibuni tu, nadhani mwanzoni mwa miaka ya tisini tu, na wala hatujaweza kujenga tabia hiyo akilini mwetu. Mtu akimaliza kujenga nyumba yake na kuipaka rangi akahamia basi inabaki hivyo hivyo miaka yote mpaka inapata ukuku.
   
Loading...