Nilikuwa napuuza 'Chuma Ulete', leo yamenikuta

Chuma Ulete ipo tena ya kisasa, Iko hiv, , , Pesa ya chuma ulete kwanza inatolewa kwa mkono wa kushoto mara nyingi, mpokeaji wake akitumia Right hand umeisha, ila ukipokea kwa Left haina madhara, , , tena mwenye nayo siku hiyo hafanyi tena kazi hadi siku inayofuata.

Mimi ilinikuta mwaka 2006 nikifundishwa huo mchezo, , , sasa kilichokea nilienda dukani asbh abh na kumbuka muda wa asbh kinakuwa hakuna mauzo mazuri sana, sasa nikiwa na sarafu ya shilingi 100 nikampa muuzaji "Nipe jojo moja" niya yangu anipe chenji, , , maana ukishatoa chenji umeisha, basi bana kumbe yule jamaa naye alipata hilo duka kupitia mchezo kama huo, cha ajabu alipokea kwa mkono wa kushoto jambo ambalo si kawaida, akaitazamaaaa akanambia "Kijana ulipokatia kamba mimi nimechumia kuni" dah sikumwelewa akaendelea kusema "Achana na huu mchezo unaona hili duka nimepatia kutokana na hii, kama unataka sema wapi nikuelekeze ambapo unaweza pata zaidi ya hii kuliko unavjokifanya"

Hapo nimelowa jasho mwili mzima unajua, siku hiyo nilishinda nimelala.

Tatizo la chuma ulete ni kwamba fedha yoyote unayopata unatakiwa kuitumia kabla ya siku kuisha, yaani haitakiwi kilala na hutakiwi kumsaidia mtu, ndo maana unakuta mtu anayetumia huyo hawezi tajirika kwani anapata pesa ya kutumia kwa siku husika tu.

Ngoja nikupe kisa

Sitasahau siku ambayo nilipiga kama elf 6 hivi, afu jioni nimekwenda kucheza mpira, imefika saa moja usiku ile tunamaliza kujicheki mara hela mfukoni, dah si ndo nikakumbuka hela niliipiga alafu haitakiwi kulala, , ,

Wakati huo wenzangu wameanza kuondoka, sasa napiga hesabu elf 6 ninunue nini cha haraka haraka kiliwe kiishe, , , nakumbuka nilinunu miwa ya elf 4 yakutoshanikaanza kugawia watu kila anayepita "Chukua muwa" ingine iliyobaki nikanunua vitumbua alafu 50/50 dah kila mtu kula vutumbua hadi pesa iishe, , , kumbe ndo nilikuwa ninaharibu masharti yake.

Sasa naendelea

Na baada ya kutumia hiyo pesa inaonshwa na dawa maalumu ili kuifanya iendelee kuwa na mvuto.

Angalizo ni kwamba kama ukipewa pesa ambayo unamashaka nayo ipokee kwa left hadi na ikiwa inatakiwa kurudisha chenji pia fanya hivyo, hutachukuliwa fedha zako, , , ,

Kuna siku nitaeleza hii kinagaubaga, amini usiamini Chuma ulete ipo aise!

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
Dah, tulikua tunasubir ushuhuda wa aliyewahi kupitia upigaji wa hii mission, nafikir tumekupata mtu sahihi wa kutufumbua macho zaidi.

Tunaomba mwendelezo zaidi mkuu.!
 
Wengine wanasema pesa ni jini, hujawahi kuona mtu akipata pesa nyingi gafra, anachachawa akili zinahama kabisa, atafanya mambo ya ajabu ajabu mpaka mengine yanampelekea umauti?

Nimejifunza, pesa huwa haiji kwa mtu kizembe zembe.
Ni lazima mtu uwe na power ya ku contain pesa nyingi.

Kuna pande mbili zinazotoa nguvu ya kupata pesa/utajili.

Nguvu itokayo kwa Mungu sawa na ile Kumbukumbu la torati 8: 17 -18 inasema ..........Bali utamkumbuka BWANA Mungu wako , maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri.........
Mathayo 4:7-10..,.......kisha ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamuonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, akamwambia haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia, .....,.......

Kwa hiyo utaona shetani anatoa utajiri/pesa pia ukimtegemea Mungu naye anatoa uwezo wa kumiliki pesa au utajiri.

Katika maisha ya kusaka pesa lazima uchague upande mmoja, ikitokea humuombi Mungu akusaidie pamoja na kufuata maagizo yake mengine mfano kutoa sadaka n.k basi heri uchague kwenda kwa waganga wakupe masharti uyafuate ili upate utajiri.

Ukibaki katikati shetan atakuchezea, ukipata pesa inapotea bila sababu ya msingi. Kuna watu akitoka kupata pesa ndo matatizo/majanga yanaanzia hapo hapo, utasikia mtoto mgonjwa mala wezi wamemuibia kitu flani na muda mwingine kama hivi chuma ulete wanakufilisi.
Utatumia nguvu nyingi mafanikio kiduchu, utalipwa mshahara mkubwa lkn still unaishi maisha ya magumu.

That's why biblia inasema ni bora kuwa moto au baridi kuliko kuwa vuguvugu.
Nimejifunza jambo chief.
Ubarikiwe
 
Kuna vitu naweza kuvikataa na kuvitetea kwamba havipo kwa nguvu zote lakin sio chuma ulete...jaman hii kitu usiombe ikutokee inakumaliza taratibu..hata mauzo na kila pesa unayoitumia uirecord mahali still utapigwa tu lkn kitu nimejifunza ni kwamba watu wengi wanaopinga masuala ya uchawi huwa wanashiriki sana hata hili la chuma ulete kuna watu wanapinga lkn wanajua kabisa lipo lengo la kupinga ni kuona watu wengine wanaendelea kula za uso but kwa upande wao wanazo njia za kulizuia hili......
Sio mwandishi mzuri lkn suala hili lilitaka kunigombanisha na wife baada ya kumfungulia biashara na wateja wanajaa lkn hakuna siku amekuja na faida ya hata elfu 10 nikaamua kwenda kukaa pale kusimamia kila kitu ndani ya week moja nilimwomba msamaha.
 
Mnaoamini chuma ulete kupiga hatua huwa ndoto!
Anyways!
Dada yangu let me tell you in polite way dunia hii tunayo yafahamu ni 0.5% hizo percent zingine hutokaa ufahamu nlikua mbishi kama wewe nilikuja kuelewa baada ya kufungua microfinance tuli share na jamaa yangu tulipigwa sana pesa mpka kuja kulipata tundu linalovuja akili zili kaa sawa
 
Dada yangu let me tell you in polite way dunia hii tunayo yafahamu ni 0.5% hizo percent zingine hutokaa ufahamu nlikua mbishi kama wewe nilikuja kuelewa baada ya kufungua microfinance tuli share na jamaa yangu tulipigwa sana pesa mpka kuja kulipata tundu linalovuja akili zili kaa sawa
Ilikuwaje mkuu, tunaomba uzoefu wako nasi tupate somo.!
 
Dada yangu let me tell you in polite way dunia hii tunayo yafahamu ni 0.5% hizo percent zingine hutokaa ufahamu nlikua mbishi kama wewe nilikuja kuelewa baada ya kufungua microfinance tuli share na jamaa yangu tulipigwa sana pesa mpka kuja kulipata tundu linalovuja akili zili kaa sawa
Haya mambo yapo kaka tena kwa kiwango kikubwa sana
 
Mazingira aliyokuw anapitia huyo mwamba daah ni kama umenikumbusha niliyoyapitia ni noma sana hao watu
Kuna dogo nilipata goli la chips, yai, vyuku, mishkaki na wenzie Obay huko nikaona si mbaya nimuweke ajiongeze maana alikua mzigo tu home. Goli lilikua linatema, Nikamuwekea mtaji mzuri tu vyombo, misosi na wasaidizi ye kazi yake adeal na malipo tu. Baada ya kuuza.

Na ilikua mi tukutane once a week niende kujua ngapi kaweka duh🤔.
Mwezi tu dogo kaleta hesabu mara 2.
Haya ukimuuliza ok mzigo ulikua nao wa kilo 3, kwa wiki tupate 5 we unakuja na 2 inakuaje?
Na sawa labda biashara ilikua mbovu viko wapi vitu vyote?
Vimeisha Bro.
Hela? anajibu hata mi sijui
Namboost tena tunanunua mazagazaga yote tunaweka golini.
Mara karibia 4 same shit,
kumbuka kuna kodi hapo inatakiwa ilipwe miezi mi3. na ni hela ndefu.
Ilifika mwisho nikimbananisha anaanza kulia kuomba misamaha mingi.
Nikaona kama namwonea tu.
Ilifika mahali mwenyewe akasema bro labda mi sihitajiki kufanya biashara.
Nilimwonea huruma lakini kumforce aendelee ingekua torture.
Kuna siku niliamka tu nikaenda beba kila kitu
Piga mnada,
Nikamrudisha home tutafute la kufanya.
Ilibidi ila hata mimi iliniuma.
Dogo mwenyewe sio mtu wa mademu wala kilevi.
Ndo naamini chuma ulete inawezekana kabisa walikuwepo pale.
Hiyo 2000+
 
Mfanyakaz unamuweka dukan halafu aibe pesa zote kabisa kisha abakie hapo hapo.

Haiji akilini atakua kweli alipigwa.!

Mtu ukimuweka kwenye biashar huwa anaiba kidogo kidogo ili kibarua kiendelee kuwepo.!
Ni binamu/ndugu
 
Mazingira aliyokuw anapitia huyo mwamba daah ni kama umenikumbusha niliyoyapitia ni noma sana hao watu
Nilikua hata sijali pesa iliyopotea ila dogo alikua anajuta sana,ni mdogo wangu kanifatia na alikua tu anakaa nyumbani nyumba ya urithi.
Anavuta mibangi tu na msosi basi.

Mpaka namfumbua akili kaja kule nikamkabidhi kila kitu analoose yaani ye mwenyewe alikua down sana.
 
Hii dunia ni pana sana zaidi ya tuijuavyo

Especially sehemu za njiapanda watu huweka majaba (ndoo kubwa) kishirikina ....,ambapo kila ukipita lazima uchangie ........
Bila kujua kuwa umechangia
embu fafanua hii kidogo tujue tunayakwepaje majaba ya kilozi
 
Dada yangu let me tell you in polite way dunia hii tunayo yafahamu ni 0.5% hizo percent zingine hutokaa ufahamu nlikua mbishi kama wewe nilikuja kuelewa baada ya kufungua microfinance tuli share na jamaa yangu tulipigwa sana pesa mpka kuja kulipata tundu linalovuja akili zili kaa sawa
Mie mwenyew naendesha hiyo ila sijawah pigwa..polen
 
Sio kweli nakuambia kuna mtu alimuibia humo ndani kwake
Hata mm kuiba hela kwa kibubu nakuweza mnoo na hutajua ng'oooooo..hawa Hawajui kuna watu akili zinachaji 1000times ..mie huniibii as hizonishu tumefanya sana hom miaka hiyo ..yaan huniibii..kwanza mie hata nikikaa na mwizi namgundua mapema sana .ila kuna watu wazito sana akili zao aise
 
Back
Top Bottom