Nilikuwa napuuza 'Chuma Ulete', leo yamenikuta

Nilikuwa napuuza 'Chuma Ulete', leo yamenikuta

Kwanza kabisa niwape pole kwa msiba mzito wa rais wetu Jpm.
Binafsi nimehuzunika sana kumpoteza mtetezi wa wanyonge, mzalendo, mkweli, mchapa Kazi, mbunifu, mcha Mungu, jasiri.

Niende direct kwenye Mada,

Aisee nimekua nashangaa watu nikiwaomba chenji wanapata wasiwasi na kuniuliza, pesa yako haina miguu??

Wengine wamekua wakinyima chenji kabisa mpaka unakasirika na kuwaona wana roho mbaya.!

Ipo hivii, kuna eneo la stend nikiwa nimetulia nasubiri wateja waje, akaja dogo amempakia abiria kwenye boda.
Walisimama Karibu yangu na kuomba chenji ya elfu 10 nikasema ninayo ila ni elfu tano tano, dereva boda akasema hiyo hiyo.
Nikazama mfukoni nikatoa kitita cha elfu 60. Elfu 10, kumi zilikua 3 nyingine zilikua elfu tano tano tu.
Nikatoa elfu tano mbili nikampa ile elfu 10 yake nikaikunja na zile nyingine, kwa hiyo elfu kumi kumi nikawa nazo 4.
Hee, baada ya muda kidogo kupita nikaenda mpesa nimtumie mtu elfu 20.

Kuchomoa kitita changu nakuta elfu kumi aliyonipa siioni, niliikariri maana zangu zilikua mpya nahisi second au first hand kabisa kutoka zitengenezwe ila ile ten yake ilionesha imetumika zaidi.
Nilijisachi mpaka kwenye soksi nikavua viatu lkn wapi.

Nilishangaa sana, ile narudi nikamcheki aliposhuka yule jamaa, akawa hayupo na wakati hakuna bus limepita na abiria wengine walikuwa wamekaa kwenye banda la kungojea usafiri.

Nikaja kuconnect na jinsi walivyofika pale nikaamini walikuwa kitu kimoja maana walipofika walikuwa wanaongea kwa sauti ya chini kabla ya kunifuata, sikuwafikiria sana mi nikawa busy tu na smart yangu nafuatilia matukio ya msiba wa taifa.

Wanaonyima chenji nimeamini hawajipendei, imewapasa kufanya hivyo kutokana na mambo ya kihuni kama hivi.

Kama una kisa cha kuibiwa pesa kimazingara kama hivi, tunaomba ushuhuda na jinsi ya kuzuia hawa chuma ulete.!
Basi wafanyabiashara vituo vya mafuta ya petroli watakua wanapigwa sana hawa jamaa nimewaza tu maana wanaombwa sana chenji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuaje mpaka wakakunyosha wakati nawe huwa unaendaga kwa waganga nauliza tu[emoji1][emoji1][emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2019 kuna jamaa wana kikampuni chao niliwafanyia kazi ikawa nawadai laki sita na nusu tukakubaliana jumatatu watanilipa maana ilikuwa weekend,,kweli juma tatu majira ya saa kumi akanipigia simu meneja kuwa hela wamemuachia dada mmoja alikuwa mfanyakazi wao wa pale,,kwa kuwa yule manzi nishawahi kumgonga nikaona nikiziacha akae zimzoee hata kwa lisaa anaweza zitaifisha nikampigia nikamwelekeza aniletee mahali maana kuna mtu nataka mlipa nae ananidai.

Nilikuwa baa muda huo napata bia kidogo akaja kweli akanikabidhi mzigo wangu wote,,mfukoni nilikuwa na cash kamaaki tatu,,jumla ikawa laki tisa na nusu,,nikaona kukaa na kiasi kikubwa hivi cha pesa baa ni hatari,,home hapakuwa mbali nikatoa 50 nikaweka kwenye walet laki tisa nikaipeleka home na nilikuwa naishi mwenyewe hela nikaiweka mahali ambapo ndo nawekaga hela zangu mara zote,,then nikarudi kuendelea na mambo mengine,,saa sita narudi home nacheki droo haina hata mia *****

Niliitafuta hadi chooni wapi,,hangaika holaa sikulala kwa kweli,,asubuhi nikatafuta eeeh hakuna,,nikaomba ushauri kwa jamaa yangu akanielekeza kwa mtaalamu mmoja nikaenda nikamuelezea yale mazingira jamaa akacheki akanambia alokufanyia hili tukio ni mtu wa karibu na anaekujua sana ila kusema hela zirudi hivi hivi ni ngumu zaidi nitatengeneza dawa nimtupie mikosi itamuandama hadi akijapata jibu ni ww ndo chanzo akija kukuomba msamaha utampa gharama zako akikulipa yataisha,,sema hakutaka nambia ni nani kabisa akasema hizo ramli chonganishi hafanyi basi bwana akafanya mambo yake nikasepa zangu

Yule demu nilimpigia kumuelezea ile hali akawa anasikitika tu hakunijibu la maana,,,baada ya muda bwana ile kampuni wakapata hasara kubwa ikasadikika yule binti kapora milioni tano,,na shida sasa walikuwa ndugu ndugu wakasumbuana ww badae yule meneja akamtimu yule binti akaendelea hivo hivo badae kampuni ikafa,,,baada ya muda nasikia aliuza eneo lake na akakopa bank akaanza tena kwa nguvu kubwa mwaka jana kwenye agost kijana anapeleka hela bank milioni 12 akatekwa zikaporwa zote hadi ninavoandika hapa yule meneja anahangaika na kulima lima,,gari alikuwa nayo imekufa kapaki,,yule demu nae nasikia ka anapoajiriwa ni wiki mbili anatimuliwa

Mwisho sijajua hadi leo kama ndo wao walinipa hela zenye miguu zikarudi kwao au la maana hadi leo hawajaja kuniomba radhi,,na yule mtaalamu hakuniweka wazi kabisa ila kwa watu wangu wa karibu ambao mikosi imewaandama ni hao jamaa na huyo sister,,nasubiri siku waje kuomba radhi
Duh hela hujaipata ni nini kuwapitisha huko kote, lengo si ulikua upate hela yako ni vyema ungetumia njia nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaan ni vile wabongo hatupend kuchunguzaga mambo...siku ungekuja jua ungebak unashika tama....kuna watu wanakupiga in a sec tu ushaibiwa...chunguza .afu usiusemee moyo mkuu...narudia usiusemee moyo ..heheheee...mie niliwah muibia hubby hela nikainyaka yote na sio tabia yangu lakini niliiba niliona nimechoka...mpk leo anaamini ameangushaga ofisini ...imagine ss iweje huyo umuamini km Mungu! Usimuamini mtu wewe ...amkaaa
Hoja yako ni kuwa huamini kama kuna chuma ulete? Manabii, wachungaji huwa wanaombea waumini roho za chuma ulete ziwakae mbali...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo biashara za waswahili hazina hesabu, kila akipata shida kidogo hela anachukua kwenye droo baada ya muda anasahau km alichukua hela anaanza kusingizia chuma ulete
I had this mentality, mpaka siku nilipoonyeshwa maana ya chuma ulete.

Nilikuwa nataka kuanzisha kibanda so nikaenda kununua mbao. Nilikuwa na elfu kumi mbili, na shilingi elfu mbili. So nikanunua mbao za buku Saba na kutoa teni moja.
Wakati anataka kunirudishia chenji kuna jamaa alikuwa anampa buku muuzaji, so yule jamaa akaona anipe ile buku tatu Kama chenji ya muuzaji lakini muuzaji alikataa Bali akanipa pesa aliyokuwa amefunga kwenye kitenge chake. Nikapeleka nyumbani ambapo palikuwa karibu tu.

Nikiwa njiani kwenda kutafuta banzi niajisachi kuangalia pesa, ile teni nyingine sikuikuta, wakati yenyewe ndiyo ilikuwa chini kabisa, so Kama ni kudondoka Basi zingetangulia zingine. Nikachanganyikiwa sana na kuamua kurudi nyumbani kumuambia wife kwamba nimepoteza pesa. Basi akachukua ile buku 2 niliyopewa Kama chenji akaenda nayo sokoni kwa ndugu yake na wakati anatoka akakisahau kitenge ambacho kilikuwa na ile buku mbili.
Ile buku mbili yangu nikaenda na kununua banzi.

Aliporudi akagundua ile pesa kaisahau dukani, ile kuwapigia wamuangalizie ile pesa wakamwambia kitenge kimefungwa ndiyo lakini pesa haipo. Tukahisi kwamba tushaingia kwenye chuma ulete.

Tukashauriana hii buku iliyobaki nikanunue misumari haraka. Kufika kwenye lile duka wakaniambia watanipa misumari Ila ile pesa hawataichukua, nikiipata pesa nyingine niwapelekee. Kumbe wameshaiona ile pesa kuwa ni chuma ulete. Basi nikaondoka kwa aibu sana. Lakini nikasema lazima niitumie tu.
Na bahati nzuri nikapata duka moja ambalo waliipokea..

Aisee usiombee ukakutana na hichi kisanga
 
Ni mara ngapi umekua ukienda sokoni hasa pale Ilala au K koo na pesa yako nzuri tu lakini unarudi ukiwa na nguo au bidhaa yeyote ile ambayo ulienda kununua ukiwa huelewi elewi yaani, Mfano umeenda zako na 50k lakini vitu ulivyorudi navyo ukiangalia thamani yake ni kama umeibiwa maana haiendani na thamani ya pesa ambayo umeenda nayo, Bhasi iko hivii kwa kawaida katika haya masoko mawili jambo la chuma ulete sio geni masikioni mwa wa wafanyabiashara wa masoko haya, Chuma ulete hua ni jambo la kupuuza sana miongoni mwa wateja wa haya masoko, Niliwahi kuambiwa kua ukienda nunua chochote katika masoko haya pindi ikatokea ukarudishiwa chenji maeneo haya usithubutu kuchanganya na pesa zako zilizoko mfukoni maana kitakachofuata ni kilio na maswali yasiyo kua na majibu kua mbona kama nilikua na kiasi fulani cha pesa lakini sahii nimebaki na kiasi hiki, Ndugu zangu chuma ulete ipoo sio utanii nami pia ni muhanga wa chuma ulete nimewahi kufunga biashara yangu mara mbili japo namshukuru Mungu kaniinua tena na nimerudi kupambana kutafuta ridhiki huku nikiwa na funzo hili kuhusu chuma ulete.
 
Yaan ni vile wabongo hatupend kuchunguzaga mambo...siku ungekuja jua ungebak unashika tama....kuna watu wanakupiga in a sec tu ushaibiwa...chunguza .afu usiusemee moyo mkuu...narudia usiusemee moyo ..heheheee...mie niliwah muibia hubby hela nikainyaka yote na sio tabia yangu lakini niliiba niliona nimechoka...mpk leo anaamini ameangushaga ofisini ...imagine ss iweje huyo umuamini km Mungu! Usimuamini mtu wewe ...amkaaa
Ndiyo tabia zenu nyie hata buku kumi kwenye kufua suruali mnazuiagaaa.Acha wizi.
 
Day moja mida ya jioni nlikua napiga stori na mama fulani hapa jirani yangu, stori zilipo fika tamati nika muaga naondoka, akasema chukua hi Mai mbili(Karume) mpelekee mkeo jana aliniazima hela ya kibiriti, nikaichukua nikaitia mfukoni nikasepa zangu kuelekea home, nlipofika home wife sikumkuta, Basi kwakua ilikua ni jioni nikaona ngoja niende bar ya jirani hapo nikapate ku- refresh mind yangu, Basi nikachuka buku nane (note ya buku5, buku2 na buku) nikazikunja kama wengi tufanyavyo ukipewa note kuweka mfukoni;nikatia mfukoni mmoja na ileMia mbili niliyopewa, nikatoka huyo naelekea bar, nafika mbele kidogo wakati natembea nikaona buku tano chini(imekunjwa Mara nne) ile kama nime ikwaa hivi kwa mguu, kamoyo kakastuka nikajua nimeokota buku tano leo, haraka nikaiokota nikaitia mfukoni mwingine sikuchanganya na zangu, Basi nafika pale baa nikaitoa ile buku tano nlioiokota nikaikunjua fresh then nikatoa na zile zangu mfukoni mwingine; khaaa nashangaa nakuta buku tatu tu na miambili ya yule mama, asee nilijipiga Sachi mpaka Basi, nikaona isiwe kesi ngoja niitumie hi niloiokota...nilipo Rudi home nikamuelezea wife hadithi nzima, wife akasema hapo ndo alikua anavuta sema ukashituka kabla hajaichukua ndo maana ilidondoka chini...nilipo enda kwa mtaalamu kufahamu zaidi akasema yule jirani yangu huvuta Sana pesa za watu.
 
Dawa ya pesa Ni kuihesabu tu mkuu,,,! Mchawi hawez kuiba hela iliyohesabiwa hata sikumoja, ndio maana ba
nk huwa hawagusi
 
Binamu yetu aliachwa dukani ( m pesa kiosk)
Jioni alivoulizwa pesa ziko wapi kasema kuna mtu kaja kaomba chenji na baadae pesa kama laki tatu zikapotea kichuma ulete

"Mimi sijawahi kuamini kama ni kweli zilipotea au alitumia tu "
Mfanyakaz unamuweka dukan halafu aibe pesa zote kabisa kisha abakie hapo hapo.

Haiji akilini atakua kweli alipigwa.!

Mtu ukimuweka kwenye biashar huwa anaiba kidogo kidogo ili kibarua kiendelee kuwepo.!
 
Back
Top Bottom