Nilikuwa napuuza 'Chuma Ulete', leo yamenikuta

Nilikuwa napuuza 'Chuma Ulete', leo yamenikuta

Binamu yetu aliachwa dukani ( m pesa kiosk)
Jioni alivoulizwa pesa ziko wapi kasema kuna mtu kaja kaomba chenji na baadae pesa kama laki tatu zikapotea kichuma ulete

"Mimi sijawahi kuamini kama ni kweli zilipotea au alitumia tu "
Nilikuwa natia shaka muuzaji wa kibanda changu huenda ananiibia. Siku moja nikaamua nikomae mwenyewe. Kama kawaida nimefungua asubuhi na kazi ikaenda. Mauzo murua haijawahi kutokea. Nikajua dogo alikuwa ananipiga. Hadi saa kumi hivi akaja mteja kununua mahitaji kama ya sh. 69,300/= hivi. Droo yangu ikasoma 260,000/= hivi. Nikiwa na furaha ya kazi, nikawa niko nje ya kibanda natia story na waliokuwepo hapo nje. Nikapata wazo kuwa nitenganishe ile hela kwa kuondoa 250,000/= niweke mfukoni nianze kudunduliza upya. Ninakwenda kuhesbu ile hela ninakuta imebaki 190,000/=. Yaani yale mauzo ya mwisho hayapo. Nililia kiaina.

Huu mchezo upo. Amini usiamin. Kama haijakitokea shukuru Mungu tu.

Nililazimika kutafuta msaada wa wahenga. Nikapata just for trial maana sikuwa na imani.

Yule mteja alikuja tena. Nikamhudumia kama kawaida. Alipoondoka, nikawa ninatoka nilikosimama kwenda sehemu ya kusimama wateja. Nikaona pamelowa yaani maji yamemwagika. Sikupata jibu haraka. Nikachukua tambara nifute, nikagundua ni mkojo na aliyesimama hapo katoka nao kwa nyayo.

Nini kilijiri hata sijui na hakuja tena pale kibandani badala yake akihitaji kitu alikuwa anapiga simu nimwagizie na baada ya muda mfupi alihamisha biashara yake kwenda mbali.
 
Weekend moja ungeenda kukaa hapo ili ujiridhishe.
Nilishaenda sana na actualy nilikua hapo mda mwingi na wana,tunakula na kunywa ila wala dogo simsumbui.
Nikimaliza naondoka, tunaonana tu Siku ya mrejesho.
Na nia kuonana alipe ilikua nzuri tu,ili tukuze mtaji aongezee biashara yake.
(Mwongozo)
Kwasababu hata anipe mimi hiyo hela ningemrudishia tu na kumshauri ongeza hiki na hiki.
Weka hii siku ya kodi tulipe
Ilikua hivyo tu mkuu.
Badae ningemuachia mazima angekua vizuri.
 
Binamu yetu aliachwa dukani ( m pesa kiosk)
Jioni alivoulizwa pesa ziko wapi kasema kuna mtu kaja kaomba chenji na baadae pesa kama laki tatu zikapotea kichuma ulete

"Mimi sijawahi kuamini kama ni kweli zilipotea au alitumia tu "
Chuma ulete haichukui kiasi kikubwa hivyo
 
Kuna dogo mama yake ni mfyabiashr pia mwanasiasaa ana pesa ndefu.
Sasa dogo napiga nae mishe ndogo ndogo sana nikamuuliza sasa kwa nini usimwambie mama akupe mtaji ufanye biashr nzuri.

Dogo akanijibu, mama kasema mimi bado mdogo.!
Nikamuuliza mdogo kivipi wakati tunawaona wadogo zaidi yako wanakimbiza biashara na wewe una advantage ni msomi?

Kimsingi dogo ni mtu mzima na kamaliza degree yake miaka 3 iliyopita.

Dogo akaishia kucheka.! Baada ya sekunde 10 nikapata jibu.

Nimejifunza, ukitaka kufanya biashara aisee usiwe neutral, utaumia utakua mtu wa kuwekeza mtaji wako kila siku.

Muamini Mungu, au nenda kapikwe uwe mtu mkubwa hawezi mtu kukuchezea kizembe.
Mimi nimechagua kumuomba Mungu, biblia sijui sehemu gani ile inasema " Mimi Mungu nitamkemea yule alaye" halafu sehemu nyingine anasema ukiwa hutoi sadaka unakua unaweka pesa kwenye mifuko iliyo toboka.

Kiufupi kutoboa maisha ukiwa neutral ni kazi kubwa sana.
 
Back
Top Bottom