Nilikuwa nakutega tu!!

Nilikuwa nakutega tu!!

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
6,989
Reaction score
5,066
Leo katika pita pita zangu nikakutana na mdada mmoja mtaani. Huyu dada tumeshawahi kutana mara nyingi, mi najua anafanya kazi gani ila ya alikuwa hajui kazi yangu.

Nikamweleza kuwa nina maongezi naye, akanipa namba yake ili nimtafute jioni. Ilipofika jioni nikamtafuta tukaenda pub moja tukaagiza vinywaji na nyama choma.

Tukiendelea kunywa akaniuliza nafanya kazi gani? Nikamwambia mi muuzaji wa duka la mhindi. Si akaanza kujishaua, oooh... Unajua kuna mtu nataka nimuwahi aliahidi kunipa hela leo..!., na sababu zingine kibao! Aakiwa anaendelea kujishaua kuna jamaa anayenifahamu akatukuta pale.

Katika kunisalimia akataja Dr. Nyalotsi vipi? Kusikia hivyo nikaona mdada kabadirika, akaagiza na kinywaji kingine na kuniuliza, mbona hukunambia kuwa wewe ni dr? Nikamjibu nilitaka nijue kama utavutiwa na mimi kwanza.. Bahati nzuri na simu yangu ikaita kuna jamaa yangu alikuwa zamu, alihitaji nimsaidie.

Lakini bado najiuliza, kukiwa hakuna uhakika wa hela hupendwi? Ina maana ni money for service? Duh, kazi tunayo..!
 
ndo hivyo kama ulikuwa hujui,hao binadamu,wanaruka kama kunguru,
 
mkono mtupu.........................:A S 39:
Leo katika pita pita zangu nikakutana na mdada mmoja mtaani. Huyu dada tumeshawahi kutana mara nyingi, mi najua anafanya kazi gani ila ya alikuwa hajui kazi yangu. Nikamweleza kuwa nina maongezi naye, akanipa namba yake ili nimtafute jioni. Ilipofika jioni nikamtafuta tukaenda pub moja tukaagiza vinywaji na nyama choma. Tukiendelea kunywa akaniuliza nafanya kazi gani? Nikamwambia mi muuzaji wa duka la mhindi. Si akaanza kujishaua, oooh... Unajua kuna mtu nataka nimuwahi aliahidi kunipa hela leo..!., na sababu zingine kibao! Aakiwa anaendelea kujishaua kuna jamaa anayenifahamu akatukuta pale. Katika kunisalimia akataja Dr. Nyalotsi vipi? Kusikia hivyo nikaona mdada kabadirika, akaagiza na kinywaji kingine na kuniuliza, mbona hukunambia kuwa wewe ni dr? Nikamjibu nilitaka nijue kama utavutiwa na mimi kwanza.. Bahati nzuri na simu yangu ikaita kuna jamaa yangu alikuwa zamu, alihitaji nimsaidie. Lakini bado najiuliza, kukiwa hakuna uhakika wa hela hupendwi? Ina maana ni money for service? Duh, kazi tunayo..!
 
ulisahau kwamba uko mjini?

kwa hiyo umeendelea nae au na wewe ni kick, eat and run!?
 
Kwani kazi ya kuuza duka haina hela? Hii mbôna hatari, kama issue ni hela kwanza hatuponi!

wakati mwingine huwa wanafikiria atakutambulisha vipi kwa mashosti zake... "baby yangu ni muuza duka kwa wahindi kariakoo" wenyewe wanasema 'aka bibie Inahuu!!'
 
Kwani kazi ya kuuza duka haina hela? Hii mbôna hatari, kama issue ni hela kwanza hatuponi!

Kupona mara ya ngapi????!!!!!!
Ushakuwa classified unasubiri zamu tu!!!!!
Ni endangerd specie wewe unawindwa tu 24/7 omba ukutane na safe predator!!!!
 
Na hivi madaktari wengi hawajipendi (rough rough) muonekano wako ulimlazimisha akuulize wafanya kazi gani.
Ingukuwa smart (simaanishi kichwani) asingekuuliza angekuuliza kwa vitendo na kudeduce kuwa unazo au za kuunga na gundi ya mnyaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom