Nilikua siijui jamii Forums

Nzuri tu mkuu, za chama, tunaendelea kukisafisha chama.
 

Karibu ndugu! huku ndiko wenye upeo mkubwa wa kufikiri waliko. Mabaya na mazuri yote yako huku.
ila vyama vilivyoko huku ni viwili tu ukiendelea kusoma utavijua ni chama gani na chama gani.
 
Hivi kulipia tangazo kwenye vyombo vya habari ni shilingi ngapi mpaka hii jamiiforumu inashindwa kujitangaza?
Wengi hawaijui kabisa.
 
Umechagua jina zuri, suprise karibu and be ready to be suprised!
 

acha uongo wewe, umejiunga leo masaa machache haya umeishasoma na kumaliza post zote?

unajua JF ina post ngapi hadi sasa? angalia statistics na usirudie tena kudanganya great thinkers!
 
Karibu sana Suprise jamvini..
Hapa hakuna uchochezi wala nini ni malumbano ya hoja tu, wanaoshindwa kutetea hoja zao ndio hao wanaokimbilia kusema kuwa kuna uchochezi.
 
karibu sana JF ila hapo nilipo bold maneno sijui ulikuwa una maanisha nini
 
Kumbe ni ya tangu 2006, halafu haifahamiki.

Asante makamu mwenyekiti wangu kwa kunifungua macho.
 
Unajua ccm wanajifanya kujua sana.
Yani fikira zao ni mgando mi nadhani. Sasa mtu mzima kama Msekwa anawezaje kusema jamii forum ndio adui wa CCM? Je humu yanayojadiliwa ni ya uongo? Wao kama CCM then only way ya kujiweka salama ni ku-prove wrong yale yote yanasemwa lakini wanashindwa, sasa jamii ambayo inatumika na watu wasiozidi 40,000, wengi wakiwa mijini na nje ya nchi wanawezaje kukipaka CCM matope...chama kilicho na mizizi hadi huko ambapo barabara hakuna kama Loliondo?
Hapa badala ya kujenga ndio wameharibu sana, mana sasa ndio watanzania wengi, wenye access ya internet, ndio watataka kujua jamii forum, na watakapoingia watajua mambo mengi.... bora wangekaa kimya.

Kwa nini CCM wasianzishe forum yao? si wanatumia vyombo vya habari kama Uhuru, Daily News etc....je hivyo vimeshindwa kukijenga chama?
 
Sijatumwa na mtu ila jana niliambiwa kuwa jamiiforums inauchochezi.
 
Kwani kunaubaya gani watanzania wakiijua jamiiforums?


The issue hapa ni juu ya 'great thinkers', hapa pumba huwa hazina nafasi ilhali chama tawala hakiwataki magreat thinkaz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…