Nilikamatwa na Polisi na kufichwa Kituo kilichopo Dar kwa siku tatu bila kula nikipewa vitisho

Nilimuuliza wewe ni Nani mpaka unitishe hivi?
Alijibu: hapo upo wapi? Mimi Nina hela Sina Sheria.
Hii Dunia wakati mwingine ina manyanyaso ndio maana wengi hukochukulia Sheria mkononi inapo bidi
 
Yes, kutaka kulawitiwa ni jambo la fedheha kwa mwanaume yoyote (isipokuwa mapunga)

Lakini kwa kuwa jamaa kakosa mahali pa kwenda kuutaja uovu wote aliotakatendewa na aliotendewa ni vyema ataje kila kitu wazi...

Kupitia kila atachokitaja, ndipo itaweza kujulikana jinai zote alizotendewa, na ukisoma kwa makini utagundua kuna mtu mmoja tu wa TANROAD ndiye aliyemsababishia nongwa yote hii kwa sababu zao za kudaiana pesa.
Jamaa ni wa TARURA siyo TANROAD?
 
Kwanini unaficha uonevu na unyama kama huu. Inatakiwa useme una utaje kila baya walilokufanyia ili hao watu wajulikane. Wanakuingiza selo bila kuandikishwa mapokezi. Kiongozi ww una tatizo sana. Ushahidi unao huyo jamaa wa TARURA hao walitaka kukuua.
Nimeficha kwasababu za kiusalama kwasababu bado wananisakama
 
Kiongozi pamoja na kuwa tuna mapolisi wasiokuwa na maadili lakini hakuna vitendo hivyo kwenye vituo vya Polisi.

Hata magerezani wanaolawitiwa ni kwa hiyari yao wala si kwa kulazimishwa au kuwekwa mtu kati na kufanyiwa kinguvu, si kweli na hakuna kitu kama hicho.
Kwa Kuwa hayaja kukuta omba Mungu iendelee kua simulizo kwako
 
Ila hicho kisa alicho andika jamaa kama ni kweli halafu initokee mimi, hao polisi na huyo mtu waniue. Nikitoka mzima watajua WW1 na hata WW2 ilikuwa vita ya kitoto.

Nasema labda waniue, wakiniacha salama hakuna cha nani wala nani ilimradi wote ni binadamu na tunakanyaga ardhi.

Kama ni kweli polisi waache hiyo mambo mara moja.
Huu ni ukweli
 
Jeshi la polisi Lina mapungufu mengi Sana, wengi hatujatedewa haki, lakini mtu anaeleza yaliyomkuta watu ambao ndio waathirika wanamdhihaki mlalamikaji badala ya kuchangia mawazo ya kulirekebisha. Sasa hivi inaonekana jeshi la polisi Kuna vikundi vya kuwapora fedha wafanyabiashara wa madini na kuwaua, kwa utani tunaofanya hili genge litaimarika sana.Pole Sana mtoa Mada.
 
Jeshi la polisi Lina mapungufu mengi Sana, wengi hatujatedewa haki, lakini mtu anaeleza yaliyomkuta watu ambao ndio waathirika wanamdhihaki mlalamikaji badala ya kuchangia mawazo ya kulirekebisha. Sasa hivi inaonekana jeshi la polisi Kuna vikundi vya kuwapora fedha wafanyabiashara wa madini na kuwaua, kwa utani tunaofanya hili genge litaimarika sana.Pole Sana mtoa Mada.
Huyu siyo wa kumpa pole Mkuu maaana ni tapeli. Arudishe pesa waliyokubaliana na mwenzake Mil 20 aone kama wataendelea kumfuata fuata. Vinginevyo anakoelekea ni kupotea mazima
 
Mimi pia niliwekwa rumande siku tatu,vitisho vingi,,ila sikuteswa...kisa tu polisi alikua anataka Laptop yangu ambayo nimenunua kihalali,Bali sikua na risiti,nilinunua kwa jamaa yangu alitoka nayo China...mwisho wa siku nikawaachia Laptop,na elfu 60..nikatoka...mpaka leo anaitumia MacBook air
 
Back
Top Bottom