Nilikamatwa na Polisi na kufichwa Kituo kilichopo Dar kwa siku tatu bila kula nikipewa vitisho

impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
8,425
2,000
Sitaandika yote kuficha kujulikana Kwasababu za usalama wangu na sitataja Kituo (mojawapo ya vituo vya police DSM) Kwasababu walio nifanyia hayo mateso, wapo na wanaendelea na utumishi wao kuumiza wa Tanzania.

Sitosahau mwaka 2021 mwezi March nilipokea simu ya mtu aliyejitambulisha kuwa ni mpemba ana kazi ya Ujenzi wa ghorofa nane anahitaji kuonana na mimi ili kunipa Sub-contract Kwasababu main contract wanatumia kampuni ya nje, tuliahidiana kukutana kesho yake DSM.

Siku ya pili saa 3:15 nilifika sehemu tuliyoahidiana, kukutana.
Nilikutana na watu wawili walijitambulisha kwangu kuwa mmoja ni Askari Polisi kutoka DODOMA amepata maelekezo kwa mkuu wa police Dodoma kuja kunikamata na mwingine (Bonge la mtu) alijitambulisha kuwa ni Afisa wa Mkubwa wa Usalama wa Taifa KUTOKA MAKAO MAKUU DODOMA kwa hiyo nipo chini ya ulinzi nisifurukute chochote la sivyo watanifumua ubongo na risasi.

Niliuliza kosa langu sikuambiwa ilikuwa ni vitisho tu niliomba vitambulisho wakanitisha wao ni maalumu hawana vitambulisho.

Walinipeleka mojawapo ya kituo cha Polisi kilicho karibu ambacho wengi wanaoshikiliwa katika hicho kituo wengi ni vibaka.

Nilikabidhiwa kwa mpelelezi akaniandika jina na kunisweka lockup bila hata kupokelewa mapokezi na nikaambiwa kuna mtu atanifuata ndiye ataniambia kosa langu.

Nilikaa lockup na vibaka hao (niliponea chupu kubakwa na nikawaahidi kuwapa hela ndio wakaniacha kidogo wanishughulikie, Polisi wao hawana muda)

Nilishinda njaa, mchana ulikwisha kiza kilianza na nilianza kuhisi, njaa Kali kila nilipoomba Askari vijana wanaoleta chakula cha wafungwa kuwa naomba kuongea nao walinitisha kunivunja vunja na kuniambia niangalie vibaka wenzangu walivyo vunjwa vunjwa. Nilijitahidi kuwaambia kuwa sijui kosa langu niliambua matusi na vitisho.

Usiku mwingi (sijui saa ngapi) kukadiria Kama saa 7. Niliitwa Mara moja sogea huku cha kunishangaza alikuwa ni polisi akiambatana na mtu ambaye ni (Achtect) MFANYAKAZI WA TARURA ambaye tumewahi kuwa na UGOMVI kwa kutompa RUSHWA aliyoniomba tangu 2019.

Nilimuuliza hivi Sheikh wewe ndiye umefanya mchongo wote huu kunitesa hivi akacheka kwa dharau na kuniambia hiyo hela (RUSHWA) umeshindwa kulipa, milioni Saba sasa utalipa milioni 20 la sivyo hao vibaka watakubaka humo.

Aliniuliza una milioni 20 kwenye gari nikuachie au niruhusu ushughulikiwe na hao vibaka, niliumia sana nilitamani geti lifunguliwe nimrukie nimtafune hata meno na aliniambia hivyo mbele ya Polisi.

Alinitisha atanisafirisha katika buti na kunipeleka Kigoma kituo chake cha kazi kama sina hela atanitupa ziwa Tanganyika au atatoa ruhusa nifungwe jela miaka 10.

Nilimuuliza wewe ni nani mpaka unitishe hivi?

Alijibu: hapo upo wapi? Mimi nina hela sina Sheria.

Ningependa niendelee ila Sina muda Kama nitapata mda nitamalizia kwa siku nyingine.

MWENDELEZO WA MWISHO
Nilimuuliza wewe ni nani mpaka unitishe hivi?

Alijibu: hapo upo wapi? Mimi nina hela sina Sheria.

Alinitisha na kuniambia iwapo sina hela ya RUSHWA niliyo muahidi akaongeza na Dau milioni 20 au nimpe gari tuandikshane gari yangu niliyokuja nayo iliyokuwa imezuiwa kituoni na au atanisafirisha hadi kigoma na katika buti na atakwenda kunitupa ziwa Tanganyika hakuna ndugu atakaye fahamu ni wapi nilipo hata MAITI YANGU HAITAONEKANA ITALIWA NA MIGEBUKA.

Usiku huo liniacha selo na kuondoka ndipo kijana mmoja mwenye makovu mengi na miraba minne (nyampala) alinifuata na kuniambia tulielekezwa tukutese lakini sasa mtu mwenyewe hata unaonekana dhaifu niambie kuna nini nisiendelee kukuumiza? nilimwambia tatizo langu ni kuninyanyasa wameomba RUSHWA nimewakatalia, akaniambia nikisikia askari anakuja lango linafunguliwa nitapiga vibao ukutani wewe piga kelele kuugulia maumivu ili mimi nipate ujira wangu.

Asubuhi ilifika ukweli kituo kile wengi ni vibaka polisi walileta mikate mikavu na kurusha kupitia katika geti na vijana kugombania mimi nilianza kukata tamaa maana sikujua hatima yangu.

Katika madrisha madogo ya lockup nilianza kuona kiza kinaingia siku ya pili sijaweka chochote tumboni nilihisi utumbo kukatika.

Ilifika usiku wa manane nikasikia geti likifunguliwa kwa kasi niliitwa wewe MHANDISI NJOO HAPA !!!!

Ilikuwa ni sauti ya huyu mtesi wangu kutoka TARURA aliniuliza bado haujakoma tu unatoa hela hiyo milioni 20 nimekuja na Mwanasheria nipe gari tuandikishane hata kama gari haina thamani hiyo nitachukua tu au hautoi chochote?

Nilimjibu kuwa Gari si mali yangu ninatumia gari ya Rafiki yangu ila hela ninadai kwenye moja ya taasisi za umma ninategemea malipo ndani ya siku saba labda niwaandikie HUNDI (CHECK) malipo yakiingia wachukue hiyo millioni 20 waniachie uhai wangu.

Walitoka pembeni na Mwanasheria wao wakazungumza baadae wakaniuliza ninathibitishaje kuwa kuna malipo yapo karibu ili wanielewe.

Niliwaambia kuwa katika simu yangu kuna majibizano ya barua nilifanya na mhasibu pia kuna document zinaonyesha hilo.
Waliondoka na alfajiri wakarudi na kuniletea simu yangu pale selo niwaonyeshe hizo document lakini nisifanye mawasiliano yoyote.

Waliniwashia WIFI ili nipate mtandao wa ku access kwenye internet wakaona document wakakubali kuwa niwape hundi twende bank nisaini Afisa wa Bank afanye ulinganisho hapo wataweza kuniachia.

Nilikubali na kuwaambia hundi zipo ofisini wanisaidie kufanya mawasiliano ili hundi iletwe

Nilipewa ruksa nikawapa namba nikampigia kijana mmoja wa Ofisini kwa shariti la kutosema kuwa nimempigia nikaongea nae na kumwambia alete kitabu cha hundi DSM Katika kituo hicho cha POLIS Na awapigie familia yangu kuwa sina shida nilipata dharura nina kazi siku hiyo jioni nitarudi.

Alileta hundi tukaenda CRDB BANK Nikaandika na maofisa waka hakiki nikaruhusiwa kutoka kituoni kwa shariti la kutosema chochote vinginevyo nitapotea.
fAMILIA yangu tayari walifungua jarada polis kunitafta bila mafanikio.

Nilirudi nyumbani nikiwa nimekonda nikaumwa lakini baada ya kupata nafuu nilienda
TAKUKURU = SIKUPATA MAFANIKIO
POLISI= SIKUPATA MAFANIKIO
TARURA= MAKAO MAKUU NILIWAANDIKIA BARUA, NILIPIGA SIMU BILA MSAADA
TARURA= TAARIFA KWA REGIONAL COOR-DNATOR NA COUNCIL MENEJA SIKUPATA MSAADA

MWISHO: Hakuweza kupata hiyo PESA mpaka sasa kwasababu tayari AKAUNTI ZANGU ZILIZUILIWA NA TRA KWASABABU YA MADENI Pesa yote inayoingia kwenye akaunti zangu hupelekwa TRA kulipa madeni.

Jeshi la Polisi lijitafakari je ni kweli wanalinda Raia na Mali zao au ni watesi wa Raia na Mali zao.

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA
 

Gambino Crime Family

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
3,745
2,000
Eti nusu ubakwe, mwanaume unakubali kweli kwamba ilikua kidogo ubakwe😂😂. Kukuweka sawa, mwanaume habakwi, mwanaume anafirwa ama kulawitiwa mwanamke ndio anabakwa.

Mwanaume kitu ulichonacho cha thamani kuliko vyote na ambacho unatakiwa kukilinda hata kwa maisha yako ni marinda, huwezi kukubali mtu akutishie kwamba atakufira ama kukulawiti na wewe umchekee tu haijalishi uko mazingira gani.

Mwanaume hupaswi ku negotiate kuhusu kufirwa, hapo hakuna negotiations. Eti unaomba jamani naomba msinifire nitawapa hela, serious?

Anyway, Pole sana mkuu kwa yaliyokukuta.
 

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
5,260
2,000
Eti nusu ubakwe, mwanaume unakubali kweli kwamba ilikua kidogo ubakwe😂😂.

Pole sana mkuu.
image_search_1643135538488.jpg
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
45,022
2,000
Kwa hiyo ulitaka afiche uovu unaofanyika huko?
Mwanaume unaanzaje kusema ulitaka kubakwa kituo cha Polisi?

Hadithi yake ina gapes kibao, kwanza Usalama wa Taifa hawajishughulishi na mambo ya arrest.

Na ikitokea Afisa usalama wa Taifa yuko joint venture na Polisi basi ujuwe hicho ni kikosi kazi kwa kazi maalum na hapo hakuna mizaha kama hii anayohadithia huyu jamaa.
 

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
5,260
2,000
Sitaandika yote kuficha kujulikana Kwasababu za usalama wangu na sitataja Kituo (mojawapo ya vituo vya police DSM) Kwasababu walio nifanyia hayo mateso, wapo na wanaendelea na utumishi wao kuumiza wa Tanzania.
Sitosahau mwaka 2021 mwezi March nilipokea simu ya mtu aliyejitambulisha kuwa ni mpemba ana kazi ya Ujenzi wa ghorofa nane anahitaji kuonana na mimi ili kunipa Sub-contract Kwasababu main contract wanatumia kampuni ya nnje tuliahidiana kukutana kesho yake DSM.
Siku ya pili saa 3:15 nilifika sehemu tuliyoahidiana, kukutana.
image_search_1643157258309.jpg
 

Watu8

Platinum Member
Feb 19, 2010
60,630
2,000
Mwanaume unaanzaje kusema ulitaka kubakwa kituo cha Polisi?

Hadithi yake ina gapes kibao, kwanza Usalama wa Taifa hawajishughulishi na mambo ya arrest.

Na ikitokea Afisa usalama wa Taifa yuko joint venture na Polisi basi ujuwe hicho ni kikosi kazi kwa kazi maalum na hapo hakuna mizaha kama hii anayohadithia huyu jamaa.

Yes, kutaka kulawitiwa ni jambo la fedheha kwa mwanaume yoyote (isipokuwa mapunga)

Lakini kwa kuwa jamaa kakosa mahali pa kwenda kuutaja uovu wote aliotakatendewa na aliotendewa ni vyema ataje kila kitu wazi...

Kupitia kila atachokitaja, ndipo itaweza kujulikana jinai zote alizotendewa, na ukisoma kwa makini utagundua kuna mtu mmoja tu wa TANROAD ndiye aliyemsababishia nongwa yote hii kwa sababu zao za kudaiana pesa.
 

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
2,575
2,000
Sitaandika yote kuficha kujulikana Kwasababu za usalama wangu na sitataja Kituo (mojawapo ya vituo vya police DSM) Kwasababu walio nifanyia hayo mateso, wapo na wanaendelea na utumishi wao kuumiza wa Tanzania.
Sitosahau mwaka 2021 mwezi March nilipokea simu ya mtu aliyejitambulisha kuwa ni mpemba ana kazi ya Ujenzi wa ghorofa nane anahitaji kuonana
Kwanini unaficha uonevu na unyama kama huu. Inatakiwa useme una utaje kila baya walilokufanyia ili hao watu wajulikane. Wanakuingiza selo bila kuandikishwa mapokezi. Kiongozi ww una tatizo sana. Ushahidi unao huyo jamaa wa TARURA hao walitaka kukuua.
 

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
2,804
2,000
Sitaandika yote kuficha kujulikana Kwasababu za usalama wangu na sitataja Kituo (mojawapo ya vituo vya police DSM) Kwasababu walio nifanyia hayo mateso, wapo na wanaendelea na utumishi wao kuumiza wa Tanzania.
Sitosahau mwaka 2021 mwezi March nilipokea simu ya mtu aliyejitambulisha kuwa ni mpemba ana kazi ya Ujenzi wa ghorofa nane anahitaji kuonana kwa dh
Mkuu,Mimi ningekuwa wewe,HUYO TARURA na HAO ASKARI wote wangekuwa .............
 

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
2,575
2,000
Mwanaume unaanzaje kusema ulitaka kubakwa kituo cha Polisi?

Hadithi yake ina gapes kibao, kwanza Usalama wa Taifa hawajishughulishi na mambo ya arrest.

Na ikitokea Afisa usalama wa Taifa yuko joint venture na Polisi basi ujuwe hicho ni kikosi kazi kwa kazi maalum na hapo hakuna mizaha kama hii anayohadithia huyu jamaa.
Nina uhakika kwenye fuvu lako la kichwa kuna ufa kiasi unashindwa kuweka ubongo wako sawa. Sijui umsoma jamaa na kumuelewa ama unaandika upupu bila kuelewa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom