Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, ajiuzulu

JoJiPoJi

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2009
Posts
2,988
Reaction score
3,543
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo na kustaafu siasa pamoja na utumishi wa umma.

Katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa leo, Dkt. Nchimbi amesema amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumjulisha uamuzi wake wa kuachia nafasi hiyo.

Amesema uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kujiuzulu kwake kutaanza rasmi Septemba 4, 2026.

Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa wakati alipomuahidi Rais Samia mwaka 2025 kuwa atamsaidia katika kutekeleza majukumu yake kwa uwezo na uaminifu wake wote, pia aliahidi kuwa angeachia nafasi hiyo siku ambayo Rais angeona anahitaji Makamu mwingine.

Amesema amefanya uamuzi huo pasipo shaka baada ya kubaini kuwa Rais anatarajia mabadiliko.

785599575_18617794186061326_4321667131540834046_n.jpg

Emmanuel Nchimbi aliteuliwa kuwa mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Agosti 27, 2025, na baada ya uchaguzi aliapishwa rasmi kushika wadhifa huo, Novemba 3, 2025.

Soma zaidi;
 
Back
Top Bottom