Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,110
Awali nawatakieni happy boxing day. Bila shaka jukwaa hili ni kitovu cha hoja mbalimbali za kisiasa hivyo nami naweka rekodi yangu katika historia yangu, kwa upande wa pili nawasilisha mtazamo wangu juu ya umuhimu wa kuheshimu taasisi (chama) badala ya watu binafsi nikiwemo mimi. Mpaka sasa nimeamini na ndivyo ilivyo kwamba mimi si zaidi ya chama na katika harakati zangu nimethibitisha kwamba image ya CHADEMA ni kubwa na ni zaidi ya yeyote ndani/nje ya chama na ndiyo maana kauli ya Wassira kwamba chama kitasambaratika mwaka 2013 imekuwa kinyume.Tofauti na wengine, nimejiunga CHADEMA nikiwa nimejitambua ningali chuo kikuu na siyo kama vijana wengine waliolazimishwa na peer groups, wazazi au just foolish age motivations ambapo vijana hujitumbukiza kwenye makundi fulani bila kujitambua na wengine huwa hivyo hadi ukubwani kwani wanakuwepo katika makundi kimazoea badala ya kuangalia malengo.Maudhui yangu ni kwamba tuheshimu katiba na malengo ya CHADEMA bila kujali umri. Happy New Year to all PRO-CHADEMA.