Anfaal
JF-Expert Member
- Jan 19, 2010
- 1,154
- 113
Line yangu ya voda nilikuwa nimeismiplace. Nikaenda vodacom mlimani city ili nipatiwe namba ile ile. Nikamkuta dada mmoja na kumueleza shida yangu. Akaingiza ile line kwny computer ghafla akageuka hii line imekuwa corrupt (hakutumia neno hili ila neno linalofanana na hilo), akasema kwahiyo ili tuifanyie kazi inabidi utoe shs 2000. Hiyo pesa si tatizo, nikamuuliza, utanipa na risiti kwa pesa nitakayokupa? Akatazama na mwenzie wakaduaa kisha akasema hatutoi risiti. Nikamuuliza wapi imeandikwa ninastahili kulipa pesa hii? Akajikanyaga tu.
Hapa ninachojiuliza, hii shs 2000 ni sahihi? Wateja wataamini vipi km ni malipo halali katika mazingira ya kitapeli namna hii? Serikali inapata kodi kwenye malipo ya hivi? Nimalizie kwamba mwishoni nilipata mashaka na ukweli wa pesa hii kwa sababu dada yule alinipatia line bure nyingine tu (zikawa 2) bila malipo nikadhani huenda ndio change yangu.