Nilifika vodacom mlimani city

Anfaal

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
1,154
113
Line yangu ya voda nilikuwa nimeismiplace. Nikaenda vodacom mlimani city ili nipatiwe namba ile ile. Nikamkuta dada mmoja na kumueleza shida yangu. Akaingiza ile line kwny computer ghafla akageuka hii line imekuwa corrupt (hakutumia neno hili ila neno linalofanana na hilo), akasema kwahiyo ili tuifanyie kazi inabidi utoe shs 2000. Hiyo pesa si tatizo, nikamuuliza, utanipa na risiti kwa pesa nitakayokupa? Akatazama na mwenzie wakaduaa kisha akasema hatutoi risiti. Nikamuuliza wapi imeandikwa ninastahili kulipa pesa hii? Akajikanyaga tu.
Hapa ninachojiuliza, hii shs 2000 ni sahihi? Wateja wataamini vipi km ni malipo halali katika mazingira ya kitapeli namna hii? Serikali inapata kodi kwenye malipo ya hivi? Nimalizie kwamba mwishoni nilipata mashaka na ukweli wa pesa hii kwa sababu dada yule alinipatia line bure nyingine tu (zikawa 2) bila malipo nikadhani huenda ndio change yangu.
 
hao walikuingiza chaka man!! mi ninavyokua kubadilishiwa line ni bure kabisa
 
Hawa ndio watoa huduma wetu. Yaani kwenye ushindani watu wanafanya masihara. Nikaingia pale wanapouza vifaa mbalimbali kwenye dirisha. Tulikuwa wateja watatu, tukawakuta wahudumu wawili wanaongea bila kujali mbele yao kuna wateja. Baada ya muda wakatugeukia na kusema hebu pangeni foleni huko. Mmoja kati yetu akawaambia nyie mnajua hatukufika hapa kuwabembeleza mtupatie huduma, tunahitaji huduma. Ndio wakastuka na kuanza kuhudumia. Yaani customer care ni mbovu imegubikwa na wizi. Hapo ndio tumekwenda physically.
 
hao walikuingiza chaka man!! mi ninavyokua kubadilishiwa line ni bure kabisa
hapana kubadili line kuna gharama kidogo nadhani iko chini ya shs 1000/= hamna kitu cha bure ndugu.
 
hapana kubadili line kuna gharama kidogo nadhani iko chini ya shs 1000/= hamna kitu cha bure ndugu.
<br />
<br />kwanini hawadisplay hizo bei? Hapa watu mnatofautiana kwasababu hawapo clear.
 
Ukienda voda com pale ohio kuna fomu unajaza na unalipia mia tano unapata risiti kwa cashier sio customer care. Hapo mlimani hawana dirisha la malipo?
 
Nimewauliza wahusika nilipopita hapo mlimani wanasema....line ikifutwa(deleted) baada miezi 6 hadi mwaka bila kutumika wala kuwekwa pesa...utalipa 2000/ ukipoteza kawaida kutengeneza 500/
 
Nimewauliza wahusika nilipopita hapo mlimani wanasema....line ikifutwa(deleted) baada miezi 6 hadi mwaka bila kutumika wala kuwekwa pesa...utalipa 2000/ ukipoteza kawaida kutengeneza 500/

basi walimstahi tu huyo jamaa. Nimeshapoteza line, line zangu zimeshakuwa corrupt ila sijawahi kuomba risit na si kama hawatoi bali mfumo wao si wa risit
 
Hata Tigo huwa wanadai elfu 2 bila risiti. Yangu ya airtel kuna mtu alinitengenezea bure; yamkini hakunipendelea.
 
Ukwakuta wanajitanuuuua na pesa za wizi, Tatizo hii industry haipo clear sana na wananchi wengi sana tunaumizwa na kwa kuwa mawasiliano ni muhimu ndo tunaumia zaidi, Nshawah kurenew Line ya Celtel enzi hizo kwa elfu 3500 Pale posta Kudadek ila sikuwabana na kitu cha risiti!
 
line unaweza hata kununua mtaani ukaenda ukaomba kubadilishwa number ili mradi tu wamejiridhisha na hiyo number. hakuna gharama kwenye kubadili number ila gharama inayotozwa ni ya kununua line nyingine
 
Nimewauliza wahusika nilipopita hapo mlimani wanasema....line ikifutwa(deleted) baada miezi 6 hadi mwaka bila kutumika wala kuwekwa pesa...utalipa 2000/ ukipoteza kawaida kutengeneza 500/
<br />
<br />
Inawezekana upo sahihi, kwanini hawadisplay bei za hii biasharra pale. Kwenye vocha wameandika ni kiasi gani, kwanini si kwahuduma hizi? Pia huwa wanaonyesha mapato ya shughuli hizi? Hapa aidha watoe risiti au waweke bei wazi.
 
hizo ndizo huduma mkuu,
je personality yako ilikuwa vipi?
tafakari/
ningekuwa mimi ..ooh wala wasingeniomba hiyo hela
 
Mm nadhan walinicharge buku kumi kama sio tano mwaka 2003 voda pale ppf tower. nilipewa risit baada ya kurenew line. those dayz was foolish age!
 
Biashara hii ina mizengwe mingi nami najaribu ku connect dots.

  1. kuna watu waliuliza humu inakuwaje mtandao namba moja haumo katika orodha ya tatu bora TRA kwa maana ya ulipaji kodi?
  2. Pia tujaribu kuwaunganisha watu wanaotajwa kuwa na hisa vodacom,RA,Ben na kuna wakati Msekwa alikuwa mwenyekiti wa board.
  3. Kuna mjadala (kipima joto) ulifanyika ITV juzi usiku na kuna watu wawili walilalamika kuwa wakati sheria inahitaji ukinunua chip isajiliwe kwanza,chip za vodacom unaweza kununua na kuanza kutumia,jamaa wa TCRA walichojibu ni kuwa "Hizi ni Changamoto"
 
Hakuna customer care bora Tanzania, WATEJA WANANYONYWA KUPINDUKIA na sasa haya makampuni yameingiza mifumo ya kibenki, NI MTAFARUKU mkubwa wa kimaslahi na hawafikirii uboreshaji wa huduma kwa wateja.
 
hao walikuingiza chaka man!! mi ninavyokua kubadilishiwa line ni bure kabisa
Meeen, hiyo 2000 ni ndogo sana ila imeniuma sana kuskia nimepigwa, nime renew vodaDuka flan hapa zenji kwa charge hiyo. Ila hii yote inaletwa na mfumo mzima hapa TZ. "Don't hate the player, Hate the Game"
 
haha natamani tufikie kama nchi fulani niliyotembelea hata sokoni utakuta wamedisplay bei ya nyanya na kila kitu unanunua kwa kupima kwa mzani sijui mwaka gani tutafika kwani hata ukiongeza hela kwenye simu wapewa risiti
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom