Nilichokitafuta nimekipata!!!!!!!!

Nilichokitafuta nimekipata!!!!!!!!

jidanganye kumuacha uone wengine wanavyochukua nafasi fasta. Mungu anisamehe natembea na mke wa mtu na hayuko tayari kumuacha mumewe, sema anahudumia......ndo mana siwazi kuoa maisha!!
 
Nilichokitafuta nimekipata,hii imenitokea jana;
Mimi niliolewa miaka mitatu iliyopita,tuliishi kwa furaha na upendo mimi na mume wangu.Mwaka jana nilianza kuhisi mahusiano ya mume wangu na secretary wake si ya kawaida,niliamua kumuuliza mume wangu kwa utaratibu ila alikana na kunitoa wasiwasi kuwa hakuna kitu kama hicho.Tuliendelea ila nilikua bado naona movement zisizoeleweka za mume wangu na secretary wake.
Juzi usiku nikaamua kubadilisha(edit) no ya huyo secretary wake;nilichofanya nilizifuta nikaweka no.zangu kwenye jina lake na kwenye jina langu nikaweka no.za secretary.Jana asbh nikiwa ofisini nikapata msg ya kwanza kutoka kwa mume wangu akijua anamtext secretary na chat ziliendelea kama ifuatavyo;
Mume wangu:Gmorning darling leo nitachelewa kufika ofisini
Secretary (mimi):morng to u hny unapitia wapi?
Mume wangu:Napitia mjini kuna kikao nikiwahi nitakuja kukuchukua twende lunch then............
Secretary (mimi):Siku hizi umenitosa sana au mke wako kakubana?
Mume wangu:Aaaaah wapi yule hawezi kunibana mimi kwani hakufikii kabisa
Secretary(mimi):MMMH hanifikii kwa lipi?
Mume wangu: yeye si mtamu kama wewe,baby you are so sweet,cant wait to hold and .......you hardly.

Nilitetemeka jasho likanitoka nikaomba ruhusa ofisini nikarudi nyumbani,jioni anafika nikamuonyesha zile msg zake hakuongea chochote na mpaka sasa hajibu chochote wala haongei na mimi.

Wanajamii mmekua wa kwanza kuelezewa huu mkasa na sitarajii kumueleza mtu mwingine yeyote.
Nawaomba ushauri nifanyeje???


Nawala usimweleze mtu mwingine. Don't worry your secret is safe with us!
 
mimi kwa uzoefu wangu, naona wanaume wengi si waaminifu kwenye ndoa. nataka kukuthibitishia kuwa hayo maneno kuwa sec ni mtamu kuliko wewe si kweli, ni lugha wanaume wanatumia kudanganya wanawake wa nje, ila ukweli ni kuwa mumeo anakupenda, na ndio maana amekuoa wewe. sema tu anazini na huyo sec, msamehe, na umuombee kwa Mungu aache uzinzi, do not even feel bad, the husband loves you!

royna unatujua Dah! Hongera kwa aliyeko na wewe!
 
Hii ni fundisho kwa wanawake wote, kila mara nimekuwanasema, "hakuna mwanaume asiyeruka fensi" kinachotakiwa ni kujitahidi usigundue na kumsihi afanye kwa heshima.
 
jamani pole sana mwanamke mwenzagu kuna wanaume huwa hawatoshiki mpaka wakale na nje ndio wanakamilisha uanaume wao, kwani ye sio member wa humu?namaanisha akijua umeleta uzi hapa hutapata kichapo heavy?
 
hayo ni mapito tu dada angu!!hakuna ambaye ni msafi kwa maana ya dhambi.sote tu wadhambi.kabla hujafanya maamuzi mazito,tafakari ,ulisha fanya dhambi ngapi?then uchukue hatua.otherwise msamee bure.
 
ni worse kwa mwanamke kucheat kuliko mwanaume
 
We,tulia acha papara za wazazi,kwani alikuambia wewe ulikuwa wa kwanza? Mpikie chakula kizuri,acha kulala na chupi? Ndiyo maana akasema wewe siyo mtamu. Unalala mno. Sisi wanaume tunataka mchakamchaka kila siku,asubuhi na jioni.Niye wanwake wa maofisini mnajifanya busy saa zote,haya ndiyo matokeo. Ila usimwambie mtu mwingine ili aone ulivyomlindia heshima,mpe kitu rohoo inapenda,tena mlazimishe,na akikubali mpelekee moto mpaka atamke mwenyewe kuwa hatarudia na kwamba wewe ni mtamu kuliko yule secretaty. Mungu akuongoze,mdumu kwenye ndoa yenu
 
Mume wangu: yeye si mtamu kama wewe,baby you are so sweet,cant wait to hold and .......you hardly.
Dah!! Huyo mumeo wala hana adabu hata kidogo!! Yaani sipati picha angetoa jibu gani endapo ungeuliza "kwani yake ina nini?"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom