Nilichokitafuta nimekipata!!!!!!!!

Nilichokitafuta nimekipata,hii imenitokea jana;
Mimi niliolewa miaka mitatu iliyopita,tuliishi kwa furaha na upendo mimi na mume wangu.Mwaka jana nilianza kuhisi mahusiano ya mume wangu na secretary wake si ya kawaida,niliamua kumuuliza mume wangu kwa utaratibu ila alikana na kunitoa wasiwasi kuwa hakuna kitu kama hicho.Tuliendelea ila nilikua bado naona movement zisizoeleweka za mume wangu na secretary wake.
Juzi usiku nikaamua kubadilisha(edit) no ya huyo secretary wake;nilichofanya nilizifuta nikaweka no.zangu kwenye jina lake na kwenye jina langu nikaweka no.za secretary.Jana asbh nikiwa ofisini nikapata msg ya kwanza kutoka kwa mume wangu akijua anamtext secretary na chat ziliendelea kama ifuatavyo;
Mume wangu:Gmorning darling leo nitachelewa kufika ofisini
Secretary (mimi):morng to u hny unapitia wapi?
Mume wangu:Napitia mjini kuna kikao nikiwahi nitakuja kukuchukua twende lunch then............
Secretary (mimi):Siku hizi umenitosa sana au mke wako kakubana?
Mume wangu:Aaaaah wapi yule hawezi kunibana mimi kwani hakufikii kabisa
Secretary(mimi):MMMH hanifikii kwa lipi?
Mume wangu: yeye si mtamu kama wewe,baby you are so sweet,cant wait to hold and .......you hardly.

Nilitetemeka jasho likanitoka nikaomba ruhusa ofisini nikarudi nyumbani,jioni anafika nikamuonyesha zile msg zake hakuongea chochote na mpaka sasa hajibu chochote wala haongei na mimi.

Wanajamii mmekua wa kwanza kuelezewa huu mkasa na sitarajii kumueleza mtu mwingine yeyote.
Nawaomba ushauri nifanyeje???
Yani mke wangu mambo haya umeamua kuyaweka hadhalani wakati nilikwambia yamekwisha na nikakuomba msamaha?anyway kupitia jukwaa hili naomba unisamehe na walah sintarudia kugawa "OGO" lako tena I promise!
Your lovely husband!
 
Pole sana kwa hilo lililokukuta..umefanya vyema kubaini hilo.
Muombe Mungu akupe ujasiri na uvumilivu katika kutatua conflict hii iliyopo kati yenu, vinginevyo ndoa yako itakuwa ktk hali tete.
Busara yahitajika zaidi hapo.
 
Sasa we ulikua unatafuta kujua haya ili uafanye nini?
jamani siku zote ukimdoubt mwenziio lazimatu utaprove hzo doubt zako.hata kama proof
utakazokua nazo si sahihi ila utajiridhisha, na hapa ndipo matatizo huanzia.
sasa umebadiisha namba na umeprove. sis tufanye nini?
Pole, hiyo ni ndoa. kuna mambo menngi tofauti na mapenzi kati yenu,
fikiriatu ukipata jibu tutaliheshimu.
 
Naipenda sana JF kwa kuwa ina watu wenye mitazamo tofauti na tunabaki kushangaana.

Yani mtu ukiwa kwenye ndoa hupaswi kufanya uchunguzi? Uchunguzi pekee ni wa daktari pale unapoanza kuharisha mara 65 kwa wiki? Hata mkeo akiwa anatoka nje kupokea simu kila siku u relax tu ndoa isivunjike?

Kwa mtaji huu I would opt kuwa single aisee!

Sasa we ulikua unatafuta kujua haya ili uafanye nini?
jamani siku zote ukimdoubt mwenziio lazimatu utaprove hzo doubt zako.hata kama proof
utakazokua nazo si sahihi ila utajiridhisha, na hapa ndipo matatizo huanzia.
sasa umebadiisha namba na umeprove. sis tufanye nini?
Pole, hiyo ni ndoa. kuna mambo menngi tofauti na mapenzi kati yenu,
fikiriatu ukipata jibu tutaliheshimu.
 
Pole sana Ila kwakuwa yuko kimya na hasemi chochote jua there is something running in his mind so nakushauri na wewe uwe SILENT as you are planning something (but not) then utajua nini kitakachoendelea ila usiendelee kuchokoza coz hujui anapanga au kufikiria nini. Njia ya kushinda uovu.....

Umejibu kwa usahihi kabisa. Ila kwa kmshauri mleta mada, hili tatizo la mapenzi nje ya ndoa limekuwepo miaka kwa miaka. tangu dunia ilipoumbwa. La msingi ni kutochokonoa kila lifanywalo na mume au mke. simu zimeleta tatizo kubwa zaidi. Wanandoa wengi wanapenda kuchokonoa simu za wenzi wao. Hiyo ni hatari kabisa. Nimuulize mtoa mada. Akikujibu kuwa alikuwa anajua kuwa umebadilisha namba hizo na alituma meseji kwa makusudi kabisa akijua ni wewe ili akurushe roho, ukome. Utasemaje?
 
shida iko wapi... umetaka kujua how bad upo kwenye mapenzi ukajua

usiingilie yasiyokuhusu aisee

Mimi nimeoa, ila hat siku moja sintopenda kujua ananipimaje, kwani sikuoa kupimana wala kuchunguzana

ILA NIKIPATA SABABU YA KUMUACHA SITAULIZA MTU JF

kuna msemo abiria chunga mzigo wako.
kutomchunguza mkeo/mmeo japo kidogo jua humpendi.
wivu pia ni kipimo cha upendo. ukijiona huna wivu kabisa na mke wako anza kujiuliza kama unampenda kweli
 
yaani just because wana watoto ndio mtu akae kwenye ndoa ya mateso au kutokua na raha aah wapi...mtoto or no mtoto ajiondokee zake...atakapopewa ukimwi akafa ndio wenziwe watahamia hapo nyumbani kwake kabisa

Umeolewa??? au Umeoa????....kama una moja kati ya hayo, na bado una mtazamo huo...kaa chini tafakari zaidi...chukua uhusika wa huyu dada aliyeomba ushauri...

Ushauri wangu kwa wanaume na wanawake...TUACHE KUCHUNGUZANA.....MUNGU ndiye anatulinda kwa yote...hata huo UKIMWI.....

Je, unajua kama utakufa kwa kugongwa na gari...au vinginevyo.... HAKUNA ANAYEJUA SAFARI YAKE YA MWISHO HAPA DUNIANI ITAKUWAJE...

TAASISI YA NDOA,.. ili isimame .....ni kombinasheni ya mambo mengi lkn komponenti kubwa ni ...UVUMILIVU

POLE DADA
 
let me begin by saying I empathize with u...
Hilo la kwanza, pili; Marriage is a bitter sweet institution...

wewe ni wife yule ni kishtobe...naomba ukusanye nguvu zako na usideclare kushindwa na kishtobe. viapo vinavyowekwa siku ya kufunga pingu ya maisha ni vizito ndio maana zinaitwa vows na sio promises. tena unazifanya mbele ya watu na mbele ya Mungu, alafu leo hii udeclare kushindwa na kishtobe? Naomba uikatae hiyo tokea ndani ya moyo. u r the queen, don't u dare leave ur territory for some low life to take lead NEVER.

Narudia wewe ni wife wa jamaa yule ni kishtobe...wakati jamaa anaamua kukuoa wewe haiingii kabisa akilini kuwa wanawake wenye "ladha" ya huyo secretary hawakuwepo...walikuwepo, ila akaona wewe ndiye unayemvutia na mwenye hekima ya kutosha kujenga naye familia na kumpa "riziki" yake ya "kila siku", wewe ndiyo ubavu wake, upo hapo?
suala la yeye kumuambia huyo kishtobe kuwa ni mtamu kuliko wewe ndugu hiyo ni kawaida. unafikiri akisema vinginevyo huyo kishtobe ataendelea kuwepo? lazima kidanganywe ili kiendelee kutoa "first aid" ila huyo siyo mke...kama ni hayo maneno hata vibinti vya shule vinapewa na wababa watu wazima ili vijione vya maana wkt vinalaghaiwa tu...hata ingekuwa mimi nna kishtobe lazima ningemwambia hivyo huku namng'ong'a!

mwanaume mpaka afanye uamuzi wa kuoa anaweka vigezo vingi tu mpaka unapita kwa asilimia nyingi, anakuwa amekuangalia kwa macho ya moyo wake na kuunganisha na facts za kichwa kufikia uamuzi. lakini kufikia uamuzi wa kuwa na kishtobe, inahitaji macho ya kichwa kile kidogo kisicho na brains.

suala la mtoto: jamaa huyo anaplay role zaidi ya moja ndani ya familia, ni mume na pia ni baba. katika role ya kuwa mume amefanya ambalo linafanywa na wengi tu. je katika kuwa baba? how much does he care when it comes to the child's welfare? if he cares much, then he is a good father. don't let ur bedroom drama with ur husband affect ur child!

usithubutu kwenda kustareheka kwingineko, hutostarehe badala yake zitakupata fedheha nzito baadae...i dnt knw how it happens ila the fact is when a woman cheats, it becomes stinky more than when a man does it, don't ask me how that happens, na mie nimeyakuta hivyo hivyo...

tulizana ukae kimya tu kama vile hakuna lililotokea, usitoe "riziki" akiihitaji chomeka suala la kupima coz hujui secretary ni kishtobe wa wangapi mama. akikuomba msamaha, consider kumsamehe maisha mafupi sana haya. endelea kukeep silence...trust me in such situations it is louder than a thousand hurting words.

usifikirie kukubali kushindwa na kishtobe. wewe ndio wife yule ni kishtobe...hata kama ana the so called utamu...kwani hata ice cream na cake ni vitamu kuliko vyakula vingi sana ila havijengi mwili na hata cku moja havishauriwi na daktari ingawa ni vitamu saaaaana....
otherwise Mungu akusaidie in these trying times of the bitter sweet institution we call MARRIAGE!
 
Ushauri mzuri wa kupambana na "vishtobe"
 
Salaam magreat thinkers wote mliotumia muda wenu kusoma uzi wangu na kutoa maoni mbalimbali,nimesoma kwa umakini sana comments zenu na zilikua zinanipa faraja sana.Kwa wale wote waliokua wananizodoa kuhusu kumchunguza mume wangu pia nimewaelewa japo siwezi kukubali kutomchunguza mwenzangu,as long as he said I do kwa vile viapo vyote mbele ya Mungu na mbele ya watumishi wa Mungu,ndg, jamaa na marafiki hilo la kumuacha tu ajiachie asahau.

Feedback:Ukimya kumbe alikua anatafuta njia ya kuyazungumza. Ijumaa asbh nikiwa ofisini aliniomba kupitia njia ya simu kwamba jioni twende znz alikua ameshafanya booking zote zinazohitajika na muda huo yeye nilimuacha nyumbani akasema anaanza kupack kwa ajili ya safari,alikua anaongea kwa utaratibu wa hali yajuu na mimi ikanibidi kumjibu kwa utaratibu huohuo kuwa sawa tutakwenda.Tumeyaongelea kwa undani sana na contract ya secretary itaisha mwezi wa kumi hakuna kurenew.Tumerudi jana namshukuru Mungu na nawashukuru sana wanajamii forum MMU kwa kunifariji.Mungu awabariki woooote waliochangia kwenye uzi huu iwe ni kwa ushauri hasi,chanya au utani.
 
hongera mamiie!MUNGU AKUBARIKI NA NDOA YAKO IWE NA AMANI MILELE.HAPO SASA ANZA UPYA,PITIAS KILA ENEO ULILOHISI UMELIACHA AU UMEZEMBEA,MSAMEHE TOKA MOYONI NA JENGA UPYA NDOA YAKO.wote tuliopita kwenye hayo mazingira tutakwambia ndoa zetu zilikuwa tamu vipi baada ya hayo kuisha!DHAHABU HAIWI SAFI MPAKA IPITE KWENYE MOTO MKALI!
 
Snowhite nashukuru sana ,kwa kweli jiwe la dhahabu likipita kwenye moto huzidi kung'ara ila jiwe la kawaida likipita kwenye moto lazima litapasuka,Mungu ni mwema na pia nafurahia uamuzi wangu wa kuwamwagia wana MMU huu mzigo bila kumueleza mtu mwingine yeyote hata wazazi,sasa mambo yameisha na imekua siri yetu ya chumbani.

mimi naamini katika kuyamaliza mwenyewe au kama hivi kuomba ushauri bila kujulikana,unajua ukishamshirikisha mzazi au rafiki mattizo ya ndoa yako,mawazo yao kwa kweli yanaweza yasiwe sawa na nini unataka kwa wakti huo.hilo umelimaliza kike mamii,na hicho ndo kifua cha mwanamke kinatakiwa kuwa hivyo.hakuna haja ya kuwaeleza wazazi kwani ungezidi kujidhalilisha since mapungufu yanayotokea kwenye ndoa mengi huwa tunatupia wanawake,so hapo na hubby chubby wako anh!wenyewe kimya kimya!na ye atazidi kukuheshimu!
 
Hongera shosti.

Nakupongeza kwa kutobweteka. Upelelezi wako umeokoa ndoa yako. Am sure kwa sasa wala hujutii uamuzi wako wa kumpeleleza mumeo. Usingejua dear ungeletewa watoto na magonjwa juu. Na usitegemee mumeo angemtimua huyo secretary kazi bila wewe kugundua huo mchezo mchafu. Kwangu wewe ni mpambanaji... na umeshinda na kufanikiwa kurudisha ndoa yako kwenye mstari.

Jitahidi kusahau yalopita...muendeleze furaha ya ndoa yenu. All the best
 
Snowhite si wote tuna feel kudhalilika kwa makosa ya waume zetu; including me.

AIBU YAKE AIBU YANGU? AIBU YAKE MWENYEWE! kuchiti achiti yeye aibu nipate mie, kasema nani????
Mi nilishasemaga nitawajibika kwa makosa yangu si ya mtu mwingine.

Na nadhani wanawake wengi these days hawana hizo za ku feel aibu kwa uzinzi wa waume zao.

[/COLOR]

ndio mana nimesema wengi nikijua wapo wengine hili hwalichukulii hivi,na nilichokimaanisha ni kuwa matatizo mengi yanayotokea kwenye ndo tunatupiwa lawama wanawake
 
Hongera shosti.

Nakupongeza kwa kutobweteka. Upelelezi wako umeokoa ndoa yako. Am sure kwa sasa wala hujutii uamuzi wako wa kumpeleleza mumeo. Usingejua dear ungeletewa watoto na magonjwa juu. Na usitegemee mumeo angemtimua huyo secretary kazi bila wewe kugundua huo mchezo mchafu. Kwangu wewe ni mpambanaji... na umeshinda na kufanikiwa kurudisha ndoa yako kwenye mstari.

Jitahidi kusahau yalopita...muendeleze furaha ya ndoa yenu. All the best
si kila upelelezi wa mume huishia kwa kuokoa ndoa nyumba kubwa!
 
Nakubali...ndoa inaokoka kama penzi bado lipo...sababu ya uzinzi ilikuwa ni mhemko tu.

Kwa upande mwingine wa shilingi kama ndoa itasambaratika yote kwangu mimi ni heri...kwa kuwa nikisema Mungu anakuwa amekunusuru si lazima nusuru hiyo iwe ndoa kuimarika...hata kuvunjika wakati mwingine ni heri tu.

Back
Top Bottom