Nilichokishuhudia leo...!


Mkuu dunia inatumikiwa na nguvu mbili, moja yatoka kwa yule muovu ibilisi na Nyingine kwa Mungu....haya mambo yapo tena kuna makubwa zaidi ya hayo, na hata ya ki Mungu pia yapo yanayompatia sifa Mungu, ila mara nyingi ni ugumu wa mioyo ya wanadamu wa kutokuamini vitu ambavyo hawajavishuhudia kwa macho.
 
Ndugu poleni, kweli mlifikwa sawasawa. Naomba nikuambie, nyumba kama hizo mpelekeni MLOKOLE wa kwelii. Atakaa humo, bila shida na mwisho wa yote mwenye nyumba atashika adabu.
Pale K/koo kuna mwuza nyama mmoja aliipata fresh. Alimhonga nyama mlokole akidhani jioni ni kwenda tu kumgegeda. We, amefika kaambiwa, fedha nilikupa ukazitupa, sikuziokota nemda kaziokote pale buchani kwako. Mimi na Yesu baasi. Mwuza nyama akadhani ni mchezo, alipotuma majitu yake, we, yakamrudi mwenyewe. Mpemba kapiga yowe, Naliwa kibog jamanii.
Natamani kama nyumba hiyo ingekuwa karibu ningeenda leo kuikaa
 

Hakika mkuu
 
Uchawi upo mbna mkuu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 

Mkuu kwani ukitafuta pa kujenga hicho kiwanja unajua anaekuuzia alikipataje na aliweka maagano gani?
 
Ukisikia 'Utamu wa Yesu' ndo kwenye matukio kama hayo, ukiwa na Yesu walaaa,,utayasikia tu!!
 
Hata huyu jamaa yangu hakudai kodi
Unadhani ujasiri wa kudai kodi utautoa wapi?


Halafu unadhani ni Bugando tu?
Hii makitu ya kuuza maji ya maiti niliwahi kukutana nayo mahili kwingi sana na mikoa tofauti tofauti!
maji ya maiti ni dili sana hasa kwa waganga ambao wanataka kuwarudisha watu kazini waliofukuzwa , vile vile fimbo ya kipofu , kucha za mwehu nk , yaani ni majanga tu
 
bora wewe ulikuta na ukaona mauza uza kama hayo , kigoma ujiji kulikuwa na nyumba kama hiyo ikifika usiku mnachapwa fimbo na wanao wachapa hamuwaoni na kelele hazisikiki mnazopiga, yaani ilikuwa kila siku watu wanahama na kuingia , sijui ilikuwa wanaogopa kuambiana . dawa ni kumpata mchungaji kama ni mkiristo kufanya maombi , na kama muislam dua na mafusho inaweza kukimbiza hizo roho chafu
 
Yaani hivi vituko ni vingi sana
Unaweza kuhamia kisha ukaambiwa wanaume humo huliwa kibog sijui inakuwaje aisee!!!!!!

hii sasa kali aisee...unaweza jikuta umelala huku umevaa jinzi kama nane kuhofia kugeuzwa rostmaini!!!
 
Mwenye jukumu la kufanya hayo si mwenye nyumba mkuu?
Sasa wapangaji watahusikaje?

Inawezekana kwa aina moja au nyingine mwenye nyumba anahusika au anapenda hali hiyo kwa wapangaji wake!
Kama angekuwa hapendi angekuwa amechukua hatua!

Je huyo rafiki yako aliwasiliana na mwenye nyumba wake na kumweleza hayo matatizo?
 
Jamaa na yeye nahisi aliingiliwa kingono ndo maana wakafanya maamuzi ya gafla ya kuhama.

......hahahaha, popobawa?!
Halafu ndio miezi yake hii mwisho wa mwaka!
 
maji ya maiti ni dili sana hasa kwa waganga ambao wanataka kuwarudisha watu kazini waliofukuzwa , vile vile fimbo ya kipofu , kucha za mwehu nk , yaani ni majanga tu

.....hehehe, "mtaalamu!" Wewe!
 
Mnahamiaje nyumba mpya bila kufanya dua ama maombi? Mdogo wangu eiyer, huyo mana tayari keshaingiwa jini mahaba. Hawana ujanja hapo, kama ni wakristo ama waislamu ni muhimu waende kwa ajili ya maombi/dua.

Bwana asipoulinda mji wakeshao wafanya kazi bure.
 
Eiyer poleni sana kwa yaliyowakuta , umenikumbusha niliwahi kuishi mtaa flani hapa bongo na ndio kwanza tulikua tumefunga pingu za maisha. Basi kumbe mtaa tuliopanga wamama walikua kila atakaeshika ujauzito alikua hapati mtoto i.e ilikua lazima atajifungua bahati mbaya tu. Na niliwahi tembelewa mara kadhaa na vigogo wa mtaa ule. Tuliamua kutohama mtaa ule na nilisema wa kwangu atazaliwa na atakua tu. Ngoja nifupishe habari , mara baada ya kuutambua vituko vya mtaa ule tulifanya maombi na tulipata ushindi . HAkuna madhara yoyote yaliyotupata maana Bwana alitupa ulinzi tosha. Sasa huyo ndugu yako mfahamishe kuwa uchawi haujawahi kuizidi nguvu ya Mungu cha msingi ni kufanya maombi na kukemea nguvu za yule muovu.
 
Last edited by a moderator:
Dah!!!! Hii inatisha sana!!! Bora ilikuwa ni nyumba ya kupanga, fikiria kama jamaa ndio alikuwa ameinunua hiyo nyumba kwa mamilioni chungu nzima!!!....ingekula kwake.
 

Kweli kaka. Naona nchi ambayo naishi hivi sasa, watu wanapotea kiajabu ajabu nyumba baadhi zina vibweka vya kufa mtu, lkn Kama ulivyosema, kwa vile wenzetu wabishi wanaamua kuzama kwenye uchunguzi lkn juu ya hilo bado wanaambulia patupu. Mwisho wake nao wanarudi kwenye Kalumanzira wao. Dunia hii tunayoishi ina mambo sana.
 
dawa ni yesu tu mwaminini alafu tumia jina la yesu kukemea uchawi soma biblia yatakusaidia bila yesu popote utayakuta coz wachaw wapo kila sehemu na wanaweza kukufuata popote mi usiku wa leo walimbana mtoto wangu nilizani anaumwa toka saa 5 mpaka saa 8 mtoto analia bembeleza wapi ndipo niliposikia omba nikawakemea kwa jina la yesu wakatoweka mtoto palepale akalala mpaka asubuh hii bado kalala jina la yesu lina magic power
 
Mara nyingi wanapatwa na hayo huwa wanajihusisha nayo kwa nmna moja au nyingine.
 
Dah!!!! Hii inatisha sana!!! Bora ilikuwa ni nyumba ya kupanga, fikiria kama jamaa ndio alikuwa ameinunua hiyo nyumba kwa mamilioni chungu nzima!!!....ingekula kwake.
Me ndo maana siafiki hili swala la kununua nyumba,maana zina mengi sana
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…