Nilichokiona leo Kivuko cha Kigamboni

Inasitikisha sana!

Kupambana na system ambaye imejengwa katika msingi wa wizi sio kazi ndogo.

Inawezekana kuanzia Mkuu mpaka mwajiriwa wa mwisho kimadaraka wako kwenye system moja ya wizi(criminal cartel).

TAKUKURU kama hawapo au hawaoni!
 
Nijuavyo mimi....ile tiket inakuwa scanned ili isitumuke mara mbili....kwamba mapato yanapotea kwa kutoscan sidhan kama ni dhana sahihi. Itakuwa sahihi tu kama hizo tiket zitaenda kuuzwa tena...hapo mapato yatapotea.
Mkuu vyovyote vile. Jmaa yetu kasema alikusanya ticket kama kumi halafu akashughulikia moja tu. Sasa huoni zilizobaki zinakwenda kuuzwa tena? Nitashangaa sana kama hakutakuwa na wizi pale.
 
Njia bora zaidi wangeweka hizo mashine kwenye maduka na ukitaka unanunua tickets za wiki, mwezi na au mwaka mzima unapewa kadi yenye picha yako na detail zako zote kwenye kadi (bus pass) ikiisha unaenda ongeza hii itasaidia kukusanya mapato vizuri zaidi kuliko huu mfumo wa nani ale
 
Nijuavyo mimi....ile tiket inakuwa scanned ili isitumuke mara mbili....kwamba mapato yanapotea kwa kutoscan sidhan kama ni dhana sahihi. Itakuwa sahihi tu kama hizo tiket zitaenda kuuzwa tena...hapo mapato yatapotea.

Kama lengo ni kuiscan hiyo tiketi ili usitumike tena kulikuwa hakuna maana ya kununua hiyo mashine ila tu wangeweka mtu wa kuchana tu alitosha
 
Leo wakati nipo ferry nimeshuhudia kitu cha kusikitisha, licha raisi wetu anajitahidi kudhibiti rushwa na kukusanya mapato, lakini kuna watz wachache wamethibitisha mtoto wa haramu hata umfiche ndani ya chupa atatoa kidole tu ili kuonyesha uwepo wake, ni hivi nimefika ferry mwazoni kabisa nakutana na geti na kibanda cha kukatia tiketi, nikalipa nauli nikapewa tiketi iliyochapwa kwa kompyuta, nikaingia ndani nakutana na kijana ambaye anakusanya zile tiketi na kuzimulika ( jina silijui) na kitu kama sensor fulani ambazo husoma zile tarakimu na kuziingiza kwenye mfumo wa ukusanyaji mapato pale kivukoni, sasa huyu jamaa anachokifanya ni kukusanya tiketi kama kumi halafu anaimulika ya juu tu halafu anazichana, kwa hiyo zile tisa za chini zinakuwa hazijaingizwa kwenye kompyuta kuonyesha kuwa tiketi zile zimenunuliwa, nashauri kuwe na mashine ambazo ikitoa tiketi isome moja kwa moja bila kuhitaji mtu wa pili wa kumulika kama zile za madukani
kama zilisaidia ushindi wa ........usitegemee chochote (ESCROW)
 
Wafanye hivi, ifanywe research ya mapato halisi kwa siku, kisha akabidhiwe wakala na apangiwe kiasi cha kurejesha, ambacho kwa vyovyote kitamfanya awe makini kukusanya ili apate marejesho, lakini vya machine wala mimi siviamini kabisa, nchi hii ina uwezo wa kukusanya trilion tatu kwa mwezi, nenda stend ubungo uone , watu wanaoingia na kutoka wote wanalipa, lakini mwisho wa siku ni story za kijinga, mimi nadhani tuweke pembeni siasa, let us try AMIN STYLE FOR ONE YEAR
 
Leo wakati nipo ferry nimeshuhudia kitu cha kusikitisha, licha raisi wetu anajitahidi kudhibiti rushwa na kukusanya mapato, lakini kuna watz wachache wamethibitisha mtoto wa haramu hata umfiche ndani ya chupa atatoa kidole tu ili kuonyesha uwepo wake, ni hivi nimefika ferry mwazoni kabisa nakutana na geti na kibanda cha kukatia tiketi, nikalipa nauli nikapewa tiketi iliyochapwa kwa kompyuta, nikaingia ndani nakutana na kijana ambaye anakusanya zile tiketi na kuzimulika ( jina silijui) na kitu kama sensor fulani ambazo husoma zile tarakimu na kuziingiza kwenye mfumo wa ukusanyaji mapato pale kivukoni, sasa huyu jamaa anachokifanya ni kukusanya tiketi kama kumi halafu anaimulika ya juu tu halafu anazichana, kwa hiyo zile tisa za chini zinakuwa hazijaingizwa kwenye kompyuta kuonyesha kuwa tiketi zile zimenunuliwa, nashauri kuwe na mashine ambazo ikitoa tiketi isome moja kwa moja bila kuhitaji mtu wa pili wa kumulika kama zile za madukani
ulichukua hatua gani
 
Hilo wezi walilijua ila hawakutaka kununua kwa kuwa hawata iba, usifikiri wamenunua hiki kimashine kimakosa ila wanajua wanachokifanya, chunga sana binadamu wakati unajitahidi kujenga kuna wajinga wanajitahidi kubomoa
Kuna kitu kina tuchelewesha kufikia malengo yetu nacho ni HAKI ZA BINADAMU! Yaani third world countries ina bidi kuweka pembeni hii kitu badala yake ni kupiga risasi mtu anae vunja sheria na kutaka kujinufaisha binafsi kama huyo jamaa. Anajua kabisa kuwa analiibia Taifa lake halafu akikamatwa tunampeleka wapi sijui mahakamani wakati fedha za kuhonga anazo!Dawa ni shaba tu tuna achana nae tunasonga mbele.
 
Tiba ni kuweka zile machine za ku scan hiyoticket unavyoingia. hatua ya kwanza ni kununua ticket halafu unaenda kwenye gate la kuzunguka ambalo litakuwa na sehemu ya kuscan hiyo ticket na baada ya kuscan ndipo gate hufunguka na kuweka record ya watu walioingia
 
Tatizo Magu yupo peke yake. Wanaomzunguka wote ni wapiga dili kama kakaake dadaake
 
Mbona kuna kipindi hata uwa hawascan kabisa wanakuwa wanachana tu...ni nadhani sababu ya kuscan ni ticket ustumie ticket Mara mbili..
 
anaokoa muda akianza kuscan kila kamoja mtalaumu anawachelewesha yeye pia ni binadamu kuna kipindi anachoka, hata mwalimu akisahisha mitihani kuna wanafunzi huwa wanapata maksi za chee, au kuonewa kwa kuwa msahishaji kachoka
 
Leo wakati nipo ferry nimeshuhudia kitu cha kusikitisha, licha raisi wetu anajitahidi kudhibiti rushwa na kukusanya mapato, lakini kuna watz wachache wamethibitisha mtoto wa haramu hata umfiche ndani ya chupa atatoa kidole tu ili kuonyesha uwepo wake, ni hivi nimefika ferry mwazoni kabisa nakutana na geti na kibanda cha kukatia tiketi, nikalipa nauli nikapewa tiketi iliyochapwa kwa kompyuta, nikaingia ndani nakutana na kijana ambaye anakusanya zile tiketi na kuzimulika ( jina silijui) na kitu kama sensor fulani ambazo husoma zile tarakimu na kuziingiza kwenye mfumo wa ukusanyaji mapato pale kivukoni, sasa huyu jamaa anachokifanya ni kukusanya tiketi kama kumi halafu anaimulika ya juu tu halafu anazichana, kwa hiyo zile tisa za chini zinakuwa hazijaingizwa kwenye kompyuta kuonyesha kuwa tiketi zile zimenunuliwa, nashauri kuwe na mashine ambazo ikitoa tiketi isome moja kwa moja bila kuhitaji mtu wa pili wa kumulika kama zile za madukani
Hongera kwa kugundua ufisadi huo. Naamini mamlaka husika zitalifanyia kazi.
 
Nijuavyo mimi....ile tiket inakuwa scanned ili isitumuke mara mbili....kwamba mapato yanapotea kwa kutoscan sidhan kama ni dhana sahihi. Itakuwa sahihi tu kama hizo tiket zitaenda kuuzwa tena...hapo mapato yatapotea.

Hasa wanapokuwepo watu wengi huwa wanazikusanya, mimi binafsi alichosema mtoa mada nimewahi kukiona kwa macho, hasa traffic inapokua kubwa, lakini nimewahi kuona wanazichana. Sasa kama wanaenda kuuza tena sina uhakika!
 
Wadau hao jamaa wa ferry tupite hapo tuwachunguze halafu tupeane mirejesho hapa ili hata kama ikigundulika wanaiba halafu hawachukuliwi hatua basi wajue tu kwamba watu tunajua huo mchezo wao.
 
Back
Top Bottom