Rais Samia tupia jicho kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli, Mbezi

MUSHEKY

JF-Expert Member
May 9, 2014
2,812
2,754
Kwanza nianze kukubaliana na walio wengi kuhusu kupanda kwa gharama za maisha kupita kiasi kutokana na sababu mbali mbali hasa zile za kiulimwengi hususani tokea mlipuko wa corona na sasa vita vya Russia na Ukraine

Ikumbukwe pia baada tu ya kutangazwa bei mpya za mafuta bei za vitu pamoja na nauli za mabasi ziliongezeka ghafla na mzigo huu mzito wananchi tukaubeba kwa kua sisi ndio "wanyamwezi"

Lengo la kuandika haya ni hujuma wanazofanya watendaji wa kituo hiki cha mabasi hususani wale wanaokaa mlangoni kukusanya mapato wanapomlipisha abiria kwa mara ya pili pindi anapoingia getini kupanda gari hata kama amekata risiti ya basi anayo mkononi

Ikumbukwe utaratibu wa awali ilikua kwa abiria mwenye tiketi mkononi anaingia kwa kutumia tiketi yake kwa kua dhahili inafahamika anachokwenda kukifanya ni safari kwa mujibu wa tiketi yake ambalo ndio lengo kuu la kituo chenyewe "kusafirisha abiria''

Aidha kumlipisha abiria mlangoni hata kama kashika tiketi ya basi "yenye machungu ya nauli iliyopanda" ni kumkosanisha mheshimiwa rais na wapigakura wake kwa kua ukiachilia mbali kupanda kwa gharama za maisha kiasili, zipo pia sababu za kiuzembe kama hizi ambazo naamini mamlaka za juu hazijabariki unyonyaji huu zaidi ya kua ni utashi wa kifisadi wa baadhi ya watendaji huku wakiamini hawatafanywa lolote

Kilichonishangaza baada ya kuwakomalia kwa nini nilipe wakati nina tiketi ya gari mkononi eti wananiambia kwa sababu hiyo tiketi ya gari sio za kielectroniki!! Sasa hilo ni kosa langu?

Na je kama sio za kielekteoniki leo miaka yote ya nyuma zilikua za kielektroniki?

Naamini mheshmiwa rais utatupia jicho kwenye kituo hiki kikubwa cha mabasi na kuuondoa mzigo huu mpya ambao wananchi wako tumebebeshwa tena

Ahsanteni
 
Hii ni too much sasa,mnatulazimisha tuwachukie.
Mwisho wake ikakubidi ulipe au ulikomaa nao?
Nalog off  Z
 
Kama wewe ni mwanaume na huwezi kuingia stand yoyote ya mabasi hadi ulipie 200 wakati huo una ticket ya 50,000 Dar Mwanza..naomba ujitafakari sana mkuu..tafadhari
 
Kama wewe ni mwanaume na huwezi kuingia stand yoyote ya mabasi hadi ulipie 200 wakati huo una ticket ya 50,000 Dar Mwanza..naomba ujitafakari sana mkuu..tafadhari
Mkuu mimi sikuwalipa ila wananchi waliowengi wameshaanzishiwa tozo hii mpya na wanalipa na wengi kwa sababu ya haraka kuwahi usafiri wanaamua kukubali yaishe
 
Kama wewe ni mwanaume na huwezi kuingia stand yoyote ya mabasi hadi ulipie 200 wakati huo una ticket ya 50,000 Dar Mwanza..naomba ujitafakari sana mkuu..tafadhari

Hivi hizi akili mnaweka wapi wakati mnaandika hapa JF? Unaona 200/300 ni pesa ndogo? Sawa wewe unaweza kutoa unajua kile kituo kina hudumia watu wangapi wenye hali gani za uchumi? Pia sio sababu ya kuwa na uwezo wakulipia huduma ndio ulipe tuu bila utaratibu! Unaandika kwa sifa kwa kuwa una vi change vinakuwasha labda; ila yule mama muuza matunda anapigania apate hiyo 200/300 kwa machozi jasho na damu. Mungu akurehemu. Nonsense!
 
Ni wizi aisee. Ukifika getini na tiketi ya safari wanakuuliza ulikatia wapi hiyo tiketi, ukisema kwenye booking offices nje ya stendi wanakutaka ulipe Tshs. 300, ili usilipe basi sema umekata ghorofa ya pili zilipo office za mabasi ndani ya magufuli terminal.

Haya sasa, maana ya kiingilio ni kuwa kuna huduma ndani utazipata bila kulipia tena, huduma kama choo, kunawa mikono nk lakini sasa hapo Magufuli bado ukienda chooni unatakiwa kulipa tena kwa huduma ya choo, sasa kiingilio ni cha nini ikiwa huduma bado unazilipia? Wizi

Hongera sana MUSHEKY kwa uzi huu na kwa kukomaa kutetea haki na msimamo wako kutoporwa hela kizembe. Taifa linajitaji watu kama wewe wa kuhoji uhalali wa mambo na siyo wale wa ndio mzee au bora liende tu.
 
Ni wizi aisee. Ukifika getini na tiketi ya safari wanakuuliza ulikatia wapi hiyo tiketi, ukisema kwenye booking offices nje ya stendi wanakutaka ulipe Tshs. 300, ili usilipe basi sema umekata ghorofa ya pili zilipo office za mabasi ndani ya magufuli terminal.

Haya sasa, maana ya kiingilio ni kuwa kuna huduma ndani utazipata bila kulipia tena, huduma kama choo, kunawa mikono nk lakini sasa hapo Magufuli bado ukienda chooni unatakiwa kulipa tena kwa huduma ya choo, sasa kiingilio ni cha nini ikiwa huduma bado unazilipia?? Wizi

Hongera sana MUSHEKY kwa uzi huu na kwa kukomaa kutetea haki na msimamo wako kutoporwa hela kizembe. Taifa linajitaji watu kama wewe wa kuhoji uhalali wa mambo na siyo wale wa ndio mzee au bora liende tu.
Ni kwa vile wameshatuona watz tu wajinga. Wanatuibia kila kona hatulalamiki.

Ukiingia stand kama hotelini, huduma ya Choo ilitakiwa iwe inahesabiwa katika kiingilio chako. Lakini wapi!
 
Back
Top Bottom