Nilichokiona bado sijakitambua mpaka leo..

Kuna watu wanadhani mtu ukiwa mtoto basi ulikuwa unaota! duh! kuwa mtoto sio sababu wkt huo nilikuwa darasa la nne kwahiyo mnataka kuniambia mtu wa darasa la nne mwaka 2006 mpk leo hawezi kukumbuka kitu..?
nimekuwa hata nikimsimulia mama baadhi ya matukio kipindi nipo mdogo lkn hata yeye amekuwa akishangaa maana anadhani kwa umri ule(hata chekechea nilikuwa sijaanza) nisingeweza kukumbuka matukio mengine!

Nyie mnaosema umri kama kikwazo ndo mnaambiwa kitu na watoto wenu kisha mnapuuzia but inakuja kuwa tatizo mbeleni..
 
Kuna mdada nilimuhoji na yeye akasema alishawahi kuona kitu kama hicho nikamuuliza mwaka akasema ilikuwa ni 2006! lkn hakuwa interest sana kuniambia ilikuwaje kiundani zaidi.
kuna vitu watu huviona lkn huwa tunapuuzia tu..
 
Ha ha ha mkuu kama kitu kukumbuka ni ngumu hiyo ni ngumu kwako! hili tukio nalikumbuka vizuri zaidi ya unavyodhani..!
 
Nimekuwa na maswali.
1. Je wale maarusi wapo? isije kuwa kuna mila mlivunja.
2, Kuisha mafuta gari ilikuwa sababu maalim ili muone hiyo kitu.
3. Wazee.wa kisukuma watajuwa angea nao.
4. Wakati mwingine wanasema kuna nyoka kubwa huwa inaruka inaweza toka sehemu yenye ziwa au bahari ikaenda juu sana na kuangukia kwingine.
5.Nyota pia zinaruka. ila nyota maalum.
6, roket labda toka nchi jirani.
7. Mungu alionesha miujiza kuwa huko ni sehemu teule na mwaka atamwinua mtu wake kutawala

Ongea na wazee.
 
kwetu viko vingi sana hivyo tunaviita namasata vinatumiwa sana na walozi
 
Kuna mdada nilimuhoji na yeye akasema alishawahi kuona kitu kama hicho nikamuuliza mwaka akasema ilikuwa ni 2006! lkn hakuwa interest sana kuniambia ilikuwaje kiundani zaidi.
kuna vitu watu huviona lkn huwa tunapuuzia tu..
Kabisa mkuuu sisi tulikuwa watatu, tulipoona baadae kila tuliyekuwa tunamuhadithia anatupuuza. Lilikuwa ni tukio la ajabu sana.
 
Maharusi bado wapo
 
Mkuu The Boss nami nahisi itakuwa ni UFO. Palikuwa na mjadala mzito sana kuhusu mambo ya UFOs miaka ya nyuma kidogo, japo wajuvi wa maswala ya aviation wanasema haya mambo yalikuwa ni mwiko kuyazungumza kipindi hicho. Lakini baadaye imekuja kupata nafasi kidogo na watu wengi wakiwemo pilots wa commercial liners na military aircraft wamesema wanewahi kutana na jambo hilo.

Japo wataalam nao husema pia muda mwingine kuna watu waliona nyota ambazo zina miale mikali na ziko mbali na uso wa dunia na kutengeneza illusion kuwa ziko karibu na ni UFOs. Ila wapo ma pilots wa kijapani ambao walisema walishuhudia kabisa hiyo object na hadi kwenye rada ya ndege yao waliione lakini bado swala hili limekuwa ni utata.

Kwa wapenzi wa discovery channel kuna kipindi walikuwa wanaonyesha sana the hidden truth/conspiricay behind the UFOs. Wengi wakikataa kuhusu hizo objects na wengine wakitoa shuhuda kuwahi ziona na pia yuko pilot aliyeshuhudia kuwahi kuifuata hiyo object na kujaribu kuipiga risasi akiwa na fighter jet miaka hiyo.

Wengine wataongezea.
 
Petroli ilikuja saa ngapi mkuu, mlifika saa ngapi nyumbani, mlifika salama
 
Na wewe umekua sasa usipeleke watoto wako kwenye harusi usiku haya ndio madhara ya kelele za miziki ukumbini' kifup ni mwanga wa zile taa za rang ukumbini zilikua zinajirudia kichwani kwako ulipokurupushwa ukiwa umelala baada ya gari kuisha mafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…