Nilichokigundua Kutoka Simba Mpya - Simba 0 - 1 TP Mazembe

Ninachoona hapa ni kwamba umeshajengeka mtazamo kuwa Simba anatakiwa afanye vizuri, akifanya vibaya kuna jambo la kuchunguzwa, lakini Yanga huwa hakuna kipya, maana tayari huwa anatazamiwa kufanya vibaya
Yaaah
 
Leo nilipata wasaa wa kushuhudia Tamasha la Vichekesho kutoka kwa watani zangu pale Taifa.

Maana ilikuwa sio Tamasha bali ni vibweko tosha, hata ilikuwa bado kidogo nisahau kuwa ninapaswa kutazama Mwanajangwani aliyepoteza uelekeo kule Port Harcout - Nigeria. Kiufupi kichekesho kimojawapo kilikuwa ni kuwaona Mascots 4 kiwanjani. Hahaha.

Anyways tuachane na hilo.

Matarajio ya walio wengi leo pale Taifa ni kuona kama Usajili Mpya umefanikiwa kuziba mapengo au lah. Mwisho wa mechi imefahamika kuwa licha ya kuwa TP Mazembe haiko kwenye ubora wake bado usajili mpya haukuweza kufaa vya kutosha hata kuleta ushindi kwenye siku ya tukio kubwa kama ile. (Kuna mtu alininong'oneza kuwa pengine ni ujio wa Mgeni rasmi ndio ulisababisha ushindi kwa TP Mazembe), lakini haikuwan kweli.

Usajili wa Simba ulifanywa kwa lengo la kubahatisha ili kuona kama inawezekana kuziba mapengo ya Chama & Miqquie.

1. Benard Morrison

Huyu dogo ameacha kucheza mpira uwanjani na sasa amekuwa anaucheza mpira mwingi sana nje ya uwanja kuliko ndani ya uwanja. Ila kwa umachachari wake bado atawaweka benchi wakina Migomba.

2. Kanoute
Kijana ana kiwango cha kawaida na wala sio cha kutisha. Hajamfikia Chama hata nusu. Uwezo wake unafanana na mdogo wangu wa Baraka Majogoro wa Polisi Tanzania. Hapa pengo la chama halijazibwa.

3. Kibu
Kijana alihitaji muda zaidi wa kufanya vyema kwingine. Ni aina ile ile ya washambuliaji wa kibongo (Kama Ditram Nchimbi) ambao wana nguuuvu nyingi ila akili hazijai kisoda mara walisogeleapo lango la mpinzani.

4. P.O Sakho
Ana uwezo mguuuni ila ata struggle sana kufikia uweko wa Miqqiesone kwa sababu mpira wake hauna tofauti na Benard Morrison/Konde boy aliyekuja Yanga kufanya majaribio. Huyu naye ni machachari na sio hatari.

5. Banda
Atasumbua kibongo bongo tu na sio kimataifa, na mara wakina nyoso wakianza kumtomasa tomasa miguuni ataanza kushinda muhimbili kama yule dogo wa Azam yaani Prince Dube. Huyu naye ni machachari na sio hatari.

6. Beki - Ibaka
Bonge moja la beki, hana makosa makosa ya kishamba kama wakina wana & onyango. Hata hivyo hatopata sana nafasi kutokana na chemistry iliyoko kati ya wawa & onyango.

Bado ninadiliki kusema kuwa mtani alikuwa na kikosi kizuri zaidi msimu uliopita kuliko msimu huu. Kama msimu uliopita na ubora wake wote aliambulia alama 1 just imagine this time around.

Ikumbukeni tarehe 25.
Fanya analysis ya kikosi chenu cha Yanga huko Nigeria ya Simba yaache

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Ni mapema sana kusema kikosi i kibovu au kizuri, hebu tuwape muda kidogo wajenge muunganiko!
Vijana wanahitaji mambo madogo watafanya kweli!
 
Kwa hiyo pamoja na preseason mbili Morocco na Tz Arusha na mechi kadhaa za kujaribia bado hamjaunganika na nyie? Mimi nilifikiri hili tatizo liko upande mmoja kumbe kotekote?
Ruti zoote hizo lakini hola D:D:D,,ndio ivyo madhee,sahivi ukifungwa chaka zuri la kijificha ni muunganiko.
Yanga washatufunza sababu na sisi Simba.
 
Back
Top Bottom