Nilichokigundua Kutoka Simba Mpya - Simba 0 - 1 TP Mazembe

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Leo nilipata wasaa wa kushuhudia Tamasha la Vichekesho kutoka kwa watani zangu pale Taifa.

Maana ilikuwa sio Tamasha bali ni vibweko tosha, hata ilikuwa bado kidogo nisahau kuwa ninapaswa kutazama Mwanajangwani aliyepoteza uelekeo kule Port Harcout - Nigeria. Kiufupi kichekesho kimojawapo kilikuwa ni kuwaona Mascots 4 kiwanjani. Hahaha.

Anyways tuachane na hilo.

Matarajio ya walio wengi leo pale Taifa ni kuona kama Usajili Mpya umefanikiwa kuziba mapengo au lah. Mwisho wa mechi imefahamika kuwa licha ya kuwa TP Mazembe haiko kwenye ubora wake bado usajili mpya haukuweza kufaa vya kutosha hata kuleta ushindi kwenye siku ya tukio kubwa kama ile. (Kuna mtu alininong'oneza kuwa pengine ni ujio wa Mgeni rasmi ndio ulisababisha ushindi kwa TP Mazembe), lakini haikuwan kweli.

Usajili wa Simba ulifanywa kwa lengo la kubahatisha ili kuona kama inawezekana kuziba mapengo ya Chama & Miqquie.

1. Benard Morrison

Huyu dogo ameacha kucheza mpira uwanjani na sasa amekuwa anaucheza mpira mwingi sana nje ya uwanja kuliko ndani ya uwanja. Ila kwa umachachari wake bado atawaweka benchi wakina Migomba.

2. Kanoute
Kijana ana kiwango cha kawaida na wala sio cha kutisha. Hajamfikia Chama hata nusu. Uwezo wake unafanana na mdogo wangu wa Baraka Majogoro wa Polisi Tanzania. Hapa pengo la chama halijazibwa.

3. Kibu
Kijana alihitaji muda zaidi wa kufanya vyema kwingine. Ni aina ile ile ya washambuliaji wa kibongo (Kama Ditram Nchimbi) ambao wana nguuuvu nyingi ila akili hazijai kisoda mara walisogeleapo lango la mpinzani.

4. P.O Sakho
Ana uwezo mguuuni ila ata struggle sana kufikia uweko wa Miqqiesone kwa sababu mpira wake hauna tofauti na Benard Morrison/Konde boy aliyekuja Yanga kufanya majaribio. Huyu naye ni machachari na sio hatari.

5. Banda
Atasumbua kibongo bongo tu na sio kimataifa, na mara wakina nyoso wakianza kumtomasa tomasa miguuni ataanza kushinda muhimbili kama yule dogo wa Azam yaani Prince Dube. Huyu naye ni machachari na sio hatari.

6. Beki - Ibaka
Bonge moja la beki, hana makosa makosa ya kishamba kama wakina wana & onyango. Hata hivyo hatopata sana nafasi kutokana na chemistry iliyoko kati ya wawa & onyango.

Bado ninadiliki kusema kuwa mtani alikuwa na kikosi kizuri zaidi msimu uliopita kuliko msimu huu. Kama msimu uliopita na ubora wake wote aliambulia alama 1 just imagine this time around.

Ikumbukeni tarehe 25.
 
Leo nilipata wasaa wa kushuhudia Tamasha la Vichekesho kutoka kwa watani zangu pale Taifa.

Maana ilikuwa sio Tamasha bali ni vibweko tosha, hata ilikuwa bado kidogo nisahau kuwa ninapaswa kutazama Mwanajangwani aliyepoteza uelekeo kule Port Harcout - Nigeria. Kiufupi kichekesho kimojawapo kilikuwa ni kuwaona Mascots 4 kiwanjani. Hahaha...
Simba wameupiga mwingi mpaka ukamwagika
 
Leo nilipata wasaa wa kushuhudia Tamasha la Vichekesho kutoka kwa watani zangu pale Taifa.

Maana ilikuwa sio Tamasha bali ni vibweko tosha, hata ilikuwa bado kidogo nisahau kuwa ninapaswa kutazama Mwanajangwani aliyepoteza uelekeo kule Port Harcout - Nigeria. Kiufupi kichekesho kimojawapo kilikuwa ni kuwaona Mascots 4 kiwanjani. Hahaha...
Pengo la chama na Luis bado kubwa sn
 
Uchambuzi wako haujaangalia uhalisia.Ngoja mechi zamashindano zianze ndo tutapata tathmini vizuri ya ulichokizungumza.Kwa mawazo yangu bado naona simba ilicheza vizuri ila ubora wao hauwezi kuonekana sana kwasababu ya kiwango walichokua nacho Mazembe.Tusubiri tarehe 25 tuone nani kasajili na nani alikua anazurura.
 
Mmejificha kwenye kichaka cha mazembe ila ukweli mmepigwa nyuma na mbele na watoto wa 2016
 
Uchambuzi wako haujaangalia uhalisia.Ngoja mechi zamashindano zianze ndo tutapata tathmini vizuri ya ulichokizungumza.Kwa mawazo yangu bado naona simba ilicheza vizuri ila ubora wao hauwezi kuonekana sana kwasababu ya kiwango walichokua nacho Mazembe.Tusubiri tarehe 25 tuone nani kasajili na nani alikua anazurura.
Kucheza vizuri ndio nini wakati overall possession ilienda kwa TP Mazembe?
 
Yanga imekuwaje tena mkuu kapigwa nyuma na mbele,,,namaanisha ugenini na nyumbani
Mabingwa wa Kihistoria wa Tanzania bado hawako kwenye ubora wa kushindana, let alone tittle contender.
 
Back
Top Bottom