Nilichogundua kuhusu Arusha

Leo nimeamka na facts tu sitaki malumbano ya kipopoma leo natembeza bakora ya kwenye makarabrasha kisomi zaidi na sitaki back fire ya kimbulula ya maneno ya vijiweni nmake sure unapingana na facts kwa facts................ Nadhani nimeeleweka.


Mikoa mitano maskini zaidi Tanzania hii hapa - millardayo.com

Stori kubwa kwenye magazeti ya leo June 09 2016 ni kuhusu Bajeti ya mwaka 2016/2017, moja ya stori iliyochomoza ni hii kwenye gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Mikoa mitano maskini zaidi Tanzania hii hapa”

Serikali imesema kuwa Kigoma, Geita, Kagera, Singida na Mwanza ndiyo mikoa mitano maskini zaidi nchini, aidha mikoa ya Dar es salaam, Kilimajaro, Arusha, Pwani na Manyara ndiyo mikoa mitano yenye ahueni ya umaskini nchini

Waziri wa fedha na mipango Dk Phillip Mpango alisema hayo jana wakati akiwasilisha bungeni taarifa ya hali ya uchumi ya mwaka 2015 na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Kumbe hapa tunalinganishwa na Kigoma au Kagera ambao hata Pwani na Manyara wanawachapa bakora.................kwa kweli inasikitisha sana.
 
Me nadhani ingekua vizuri kama hii thread ingeishia hapa sababu hili ndio jibu zuri tena limetolewa kwenye chombo tukufu cha Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Ni vyema tukaheshimu vyombo vyenye mamlaka na viongozi wenye dhamana waliosema Mwanza ni mkoa masikini uliopindukia na Arusha ni mkoa Tajiri
 
Mkuu ungefanya uungwana upande pale Ngarasero Lodge ukamate photo 2, 3 uwaekee hawa raia wajue kwanini Arusha iliitwa Geneva of Africa..
ucjal mkuu sahiv npo Mbuguni huku karb na Mererani, nikipanda juu kule ntarushia madude huku
 
Hahahahaha...
 
Hizo takwimu zipo wrong, hiyo link uliyoweka soma vizur content...ni 4star not five
 
Tunaongelea city....sijui umeelewa? Hatupo kimkoa...af takwimu zinasema arusha ni maskini pia ila kuna ahueni na sio tajiri kama unavyoropoka.....haya Kilimanjaro ni moja ya mkoa wenye ahueni kiumaskini kuliko mbeya, kwa kauli hii Ina maana mji wa moshi unalizidi jiji la mbeya? Mkuu usiwe nonsense sana
 
labda arusha ni pabaya sana ila hata paikiwa puzuri kuna maghorofa na kila kitu wewe itakusaidia nn? Hiyo mikoa mizuri mizuri inakusaidia nn kwenye maisha yako? Maghorofa na hoteli na kila kitu vina wenyewe tafuta vyako ufanye kwako pawe pazuri.
Hii ndo point kubwa kwenye hii mada
 
Mwanza ni Commercial City?? Vitu vingine ebu kuweni wapole na mtumie akili.. Mfano wa Commercial City Tanzania ni Dar Es Salaam.. Kodi wanakusanya almost 75% ya kodi yote nchini. Hiyo ndiye Commercial City, biashara inafanyika hapo. Mwanza ina population ya 2.7 Million kwa sensa ya 2012, yawezekana sasa imefika 3 Million, mikoa inayozunguka Mwanza na imbayo ingeitegemea Mwanza kama hiyo Mwanza yako ingekuwa kweli ni Commercial City ni Mara yenye population ya 1.7 Million, Shinyanga yenye 1.5 Million, Tabora yenye 2.2 Million na Kagera yenye 2.4 Million.. Yaani kwa kifupi Mwanza imezungukwa na Mikoa yenye population ya 7.8 Million na ukijumlisha na yake ya 2.7 million ni almost 10 Million.

Sasa Mwanza kama kweli ingekuwa ni Commercial City inayolisha hiyo mikoa inayoizunguka lazima mzunguko wa pesa ungekuwa ni mkubwa na pia kodi TRA wangekusanya nyingi tu hata kufikia nusu au theluthi ya Dar Es Salaam. Ila cha ajabu hiyo Commercial City unayosifia inapitwa mpaka na wilaya dhoofu ya Temeke kwa makusanyo ya kodi kwa almost mara mbili zaidi wakati population ya Temeke ni watu laki saba pekee.. Mwanza ni mji dhoofu lakini upo strategically tu, Ukiwachukua watu waliooza meno wao kwao ndio kukawa Mwanza na wa Mwanza wakaletwa Arusha ungekuta leo hii Mwanza inachukuana na Dar kwa makusanyo. Huwezi kuzungukwa na watu Million 10 alafu kodi unakusanya Billion 100 pekee kwa mwaka wakati Arusha yenye watu 1.6 Million inakusanya mara tatu yako...

Angalia makusanyo wa Arusha na Mwanza hapo chini. Mwanza imezidiwa mpaka na Kilimanjaro... Tukisema Mwanza imelala mkubali tu, hatubishani ili mradi uvutie kwako. Mwanza ni strategic City ambayo angalau ilitakiwa ikusanye hata Billion 800 mpaka 900 kwa mwaka. Mwanza kumedorora wala hatusemi kwa ubaya. Soon Mtwara itawaovertake kwa makusanyo..

 
Ajabu ni katika mikoa mitano tajiri, mitatu inatoka kule wasikokupenda. Mi nimewaambiwa kama Arusha ndiyo ingekuwa Mwanza alafu Kilimanjaro ikawa Shinyanga au Mara leo hii si ajabu kwa maisha bora na makusanyo ya kodi Dar ingekuwa inaisubiri hiyo mikoa. Mwanza imezungukwa na wakazi Million 10 ambao strategically wanautegemea huo mkoa. Mtu wa Mara, Bukoba, Kahama, Geita, Tabora wasingetakiwa waende Kariakoo kufunga mzigo. Hao wote wangetakiwa washuke Mwanza wafunge mzigo. Huku Arusha na Kilimanjaro wengi huwa hawaendi Dar kufunga mzigo, wanaenda Nairobi. Hivyo hivyo Mwanza ingetakiwa ihudumie 10 Million population lakini cha ajabu mtu anatoka Geita na Tabora kwenda Dar kuchukua mzigo. Alafu wako hapa wanasema mji wao ni wa kibiashara... Mji wa Kibiashara mnashindwa hata kukusanya kodi kuwazidi Kilimanjaro?? Mji wa biashara Dar inakusanya 75% ya kodi yote Tanzania ila Mwanza hata 1% haifiki alafu wamezungukwa na watu million 10 na bila aibu wanajiita mji wa kibiashara..

Mwanza imezungukwa na miji yenye utitiri wa madini, iko strategic kuunganisha nchi za Maziwa makuu ila wako dhoofu sana. Ukiangalia HDI ya Mwanza ulinganishe na zile za Arusha, Dar na Kilimanjaro unaweza kulia. Ukiangalia GDP Per Capita ya Mwanza ulinganishe na Arusha, Dar na Kilimanjaro utashangaa..
 
Kwahiyo hata Dar nao ni masikini???

Tunaongelea kwa uchumi wa Tanzania within the country report iliyosomwa bungeni ilifanywa na UNDP na huwa ni comparison na mataifa mengine.

Sasa tukija kwa regional development index unapata picha kamili Dar Kilimanjaro Arusha Manyara na Pwani ni mikoa tajiri na Mwanza na marafiki zake ni mikoa masikini iliyopindikia.

Pia jiulize inakuaje mikoa tajiri ipo karibu karibu???

Kilimanjaro
Arusha
Manyara.

Dar
Pwani

Kagera
Geita
Mwanza

Ni kwamba hiyo mikoa ukiachilia mbali interrelationships economically hata watu wake pia ni tofauti na hayo maeneo mengine.

Dar na Pwani wapo developed sanasana ni makao makuu ya nchi ndio yaliyowabeba shughuli zote za kiuchumi zipo Dar kutokana na mipango ya serikali lakini mikoa ya kaskazini ni kutokana na juhudi zao binafsi hakuna any major government influential ukilinganisha na Dar.
 
Na ndio maana nikamwambia kama watu wa Arusha na Kilimanjaro ndio wangekuwa wakazi wa Mwanza na Shinyanga leo hii Shinyanga na Mwanza ingekuwa habari nyingine.. Hata kwenye makusanyo ya kodi na uwekezaji wa viwanda mbalimbali na biashara mbalimbali za uchuhuzi. Watu wa kanda ya ziwa wote plus Kigoma, Rwanda, Burundi wangekuwa wanakuja kufunga mizigo yao Mwanza na si kwenda Dar/Kariakoo ambako ni umbali mrefu zaidi. Ule uwanja wa ndege ungeshapanuliwa siku nyingi kwasababu lazima kungekuwa na direct flights kutoka huko Duniani kuja pale kwa either wafanyabiashara kusafiri kwenda kununua mizigo au wawekezaji mbalimbali kuja kutafuta fursa. Uwezi ukazungukwa na watu million 10 ukabaki unafanya biashara ya samaki tu..
 
Hii ni kweli tupu Mwanza wapo strategically potential lakini bado sana kwenye resources exploitation hawajautilize ipasavyo ukilinganisha na kaskazini empire ambao wapo mbele sana in every sector on top of that pia ni runners wa uchumi wa Mwanza yenyewe.
 
Hyo dispensary yako haitakuwa lolote kwa hii ya wasabato

View attachment 406037

Kwa sasa imefikia hapa

View attachment 406039View attachment 406041


Leo me nimeshakuambia ni facts tu huko kwenye picture nimeshakupiga buku - 17.



Soma graph data Mkuu aliyoileta hapo jaribu kuangalia tofauti ya Arusha na Mwanza kwa ukusanyaji wa mapato kwa 2014/2015 na 2015/2016 utaona Arusha imepanda zaidi ya 60% ya mwaka jana huku Mwanza ikipanda kwa 24% ukilinganisha na mwaka jana tafadhali zingatia population baina ya mikoa hiyo miwili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…