TULIPOISHIA
Siku ya kwanza alituma meseji kadhaa usiku sana nikiwa nimelala, nilipoamka nikaifungua moja katikameseji hizo ilikuwa inasema 'vipi kwani mbona unatuma sms nyingi hewa hadi simu yangu inaganda?'
Mimi nikamjibu 'block namba yangu'
Kisha nikaanza kuzitiririsha tena sms hewa zisizo na idadi. Ilikuwa betri moja naweka kwenye kobe lingine kwenye simu kazi yangu ni moja tu, tangu nikiamka hadi ninapolala, yaani hata kama niko kitaa napiga miradi kazi yangu ni kubonyeza tu ile batani.
Hii vita ilikuwa ngumu upande wangu kwani pamoja na yote hayo Laima hakublock namba yangu, lakini nikasema atachoka tu na mwisho atanibloku mwenyewe.
Siku moja asubuhi nikiwa home nikapokea simu kwa mdada ambae alijitambulisha ni Aisha rafiki yake Laima.
ENDELEA..
YEYE 'shemeji ni muda mrefu sasa vipi bado unanikumbuka?'
MIMI 'Nakukumbuka Aisha habari za wapi sasa hivi'
YEYE 'Mimi bado niko nyumbani Newala, kwanza Shemeji nikupe pole kwa yote unayo yapitia, najuwa unampenda mno Laima na uliwekeza akili yako yote kwake lakini kitu cha kusikitisha ni kwamba Laima anakuona wewe ni rafiki yake tu kama walivyo marafiki wengine, na hii haijatokea kwa bahati mbaya bali toka ambapo mlianza mawasiliano.
Kipindi kile Laima alikuwa na mpenzi tayari ambae ni mwalimu mkuu wa shule hapa nyumbani, huyo mwalimu anamfanyia Laima kila kitu unachokijuwa, na Laima huna la kumwambia kuhusu huyo mwalimu.
Walikwisha panga kuoana zamani sana lakini kilichokuwa kikiwakwamisha ilikuwa ni mke wa huyo mwalimu kwani mwalimu alihofia angemchumbia Laima pengine wazazi wa Laima wasingekubali kumuozesha mtoto wao kuwa mke mdogo, lakini pia hata wazazi wangekubali bado angekutana na vumbi kubwa kutoka kwa mkewe ambae alikuwa anamwogopa mno kwa mambo ya kishirikina maana huyo mwanamke ni mtu wa tanga.
Kwahiyo alichokifanya mwalimu ni kutengeneza mazingira ya kumuacha mkewe kwa sababu nyingine tu na amefanikiwa muda tu, hapa tunapoongea sasa hivi mwalimu ameshapeleka Posa kwa kina Laima na yanasubiriwa tu majibu ya wazee.
Najua kwa sasa hii haitakuumiza kwasababu najua A to Z ya kinachoendelea kati yenu sasa hivi, na tangu mlikotokea lakini nakwambia tu ili uwe makini kwababu Laima anakwenda kuingia kwenye ndoa muda wowote kuanzia sasa na sijajuwa ni lini ataamua Kukuweka wazi juu ya hili hivyo isije kutokea dharura yoyote mawasiliano yako yakanaswa na huyo mwanaume wake mambo yakawa mengine'
MIMI 'Kwahiyo zoezi lote la mimi kujaribu kujitoa kwa laima unalifahamu? Kwanini hukuniambia haya yote tangu zamani na Kwanini Laima aliniaminisha ananipenda wakati hakuwa ananipenda hata kidogo?'
YEYE. 'Ndiyo ninafahamu kila unachokifanya ili kumtoa Laima akilini mwako, sikukwambia haya tangu mwanzo kwasababu najua tu Laima angejuwa maana ulikuwa kwenye kiza kinene cha mapenzi hivyo ungemwambia tu, lakini kwa sasa najua sio rahisi wewe kumwambia haya na hata ukimwambia haitaathiri urafiki wetu maana sasa kama wewe ungekuwa ni bidhaa basi muda wako wa matumizi unaenda kwisha. hivyo hata akikupoteza sasa na akajua sababu ni mimi haiwezi kuleta shida.
Kuhusu kukuigizia mapenzi alifanya baada ya kuona hawezi kuwa na wewe kama marafiki, kama unakumbuka mwanzo kabisa uliwahi kumtongoza akakukataa, alipokukataa wewe ukaamua uendelee na maisha yako kwa kumkalia kimya, wakati huo mlikuwa mna mawasiliano kama ya miezi mitatu au minne hivi, sasa yale mawasiliano ndiyo yalimfanya Laima asitamani kuwa mbali na wewe kimaongezi, Kumbuka kama nilivokwambia mwanzo Laima hakuwahi kucheza sana baada ya kuvunja ungo kama sisi wengine, hivyo kuna yale mapenzi ya kushiriki na wanaume vijana hakuwahi kuyapitia, hivyo alikuwa anajiponesha ile hali yake ya kutamani hicho kitu kupitia wewe.
na kingine ni kwamba, wewe ulikuwa kama faraja yake muda ambae anakwaruzana na huyo mwalimu wake, ndiyo maana unaona kuna kipindi alikuwa anakuganda sanaa.. na mkiwa kwenye maongezi anaongea vitu kutoka moyoni kabisa, basi hichi ndiyo kipindi huku kwa mzee mambo yameingiliana.
Lakini kingine ni kwamba wewe ni mchekeshaji mno Shemeji na dadaangu Laima kwa kupenda kucheka ni afrika mashariki na kati, hivyo hangetamani akupoteze hata kidogo kwa maana unamfurahisha vibaya sana anapoongea na wewe, kuna siku hadi Mama yake aliwahi kuniuliza kwamba huyu anaefanya Laima anacheka kijinga anapoongea na simu ni nani!
Nikamsimulia vizuri tu kuhusu wewe hivyo anakujua na habari zako anazo (baadae sana mamaake Laima aliwahi kuchukua namba zangu kwa Aisha kuna ishu ilikuwa anataka kuifatilia huku town, mimi nilikuwa mtu mrahisi kwake nina uzoefu na hiyo ishu na ananiamini)"
Tuliongea mengi sana na Aisha na akaniambia japo Laima aliigiza mapenzi kwangu lakini yeye anaamini mtu huwezi kuigiza mapenzi kwa muda mrefu na mtu ambae humpendi kabisa hivyo anaamini kama tutakuwa na maisha marefu kuna siku tutakuja kukutana kimwili tena ni Laima ndiyo ataanza kuaprochi.
Kumbuka hii sasa ilikuwa ni 2017.
iliutafuna sana moyo wangu kuona Laima amechagua kuihalalisha nyapu yake kwa kibabu nyapu ambayo amegoma kunipa mimi hata kwa dakika 5 tu. Niliumia sana lakini ile ilikuwa ndiyo tiba sahihi kwangu.
Nilimchukia mno Laima na tangu ile siku sikuwahi tena kumpigia wala kumtumia meseji.
2018 ndiyo ndoa yao ilifungwa na wakahama mtwara kwenda huko mikoa ya mbali. Ilipita kama miaka miwili hivi, bila kuisikia sauti ya Laima mwanamke aliyefanya niionje kwa vitendo ile kauli ya 'Mapenzi ni uchizi'
Mwanamke aliyefanya nisimwamini mwanamke mwingine yoyote hadi leo hii.
Laima ni mwanamke aliyeupitisha moyo wangu katika moto na kuunguza hadi ukaungua kabisa. Niwe mkweli tu kuanzia pale sijawahi kumpenda mwanamke hata kwa kiwango cha asilimia 10.
Ni kama moyo wangu hauumii tena katika mapenzi, hauumii kwasababu siupi nafasi ya kumpenda mwanamke.
Tangu pale nilijiapiza sita mpenda/sitazama kwenye mapenzi na mwanamke labda kumjali tu, kwa sababu naijua gharama ya kujitoa kwenye dimbwi la mapenzi.
Nashukuru hadi leo sijatoka katika misingi ya kiapo changu.
Niliwahi kuingia kwenye ndoa mara moja lakini niliingia na mwanamke ambae alinipendeza machoni tu sio moyoni, nilimwonesha dalili zote za kumpenda niliishi nae kwa kadili nilivyoona mimi kwamba nipo sahihi katika maisha ya ndoa tulipata na mtoto lakini mwisho Alitombesha akiwa na mtoto mchanga kabisa. (Siku nikilewa nitasimulia hiki kisa mwanzo mwisho ila leo niwaambie tu vijana wenzangu ambao hatujajipata kwenye maisha tusiingie kwenye ndoa, kuna muda utashindwa kujua wife anafanya visa kisa ni dhiki ama hakupendi, utapata msongo mwanangu)
Siku niliponusa harufu ya usaliti sikuumia sikupagawa wala kuwa na wasi wasi juu ya usaliti wa Mama watoto.
Kikubwa nilitafuta ushahidi tu ushahidi ulipokamilika nikamwita kumuuliza juu ya hilo jambo alipojaribu kukataa nikamuwekea mezani ushahidi usio na makando kando, kwakuwa Tangu mwanzo nilishamweleza kosa ambalo sitaweza kusamehe ni usaliti hakushangaa nilipompa talaka.
Hivyo japo sijamaliza kuishi lakini ninayojeuri ya kusema kwa sasa mapenzi hayaniumizi tena.
2020 Baada ya kupita miaka miwili nikwa sina mawasiliano na Laima, siku moja akanipigia nilipoiona tu namba yake sikushangaa huyu ni nani nikapokea na kumsikiliza, Kumbuka hapa ilikuwa ni miaka mitano tangu kufahamiana kwetu, hapa sikuwa tena hata na mawasiliano na Aisha.
Kwa sasa tulikuwa wakubwa tayari kila mmoja amekomaa kwa upande wake.
Tuliongea sana ile siku akanielekeza kuhusu ndoa yake na maisha yake kwa ujumla.
Nilicheka sana aliponiuliza kuhusu yule ndege wetu kwamba bado yupo au alishakufa.
Mimi pia nilimwambia kwamba sikuwa nimelong namba bali ni Deo ndiyo alinipa namba zake, alicheka sana na kunisifia kwa mbinu niliyokaingia nayo maana hakuwahi kustuka hadi hiyo siku namsanua.
Nilipomwambia kwamba movement zote za kule Newala ni Deo ndiyo alikuwa nyuma ya pazia anazisimamia alicheka karibu kufa.
Maneno aliyoyasema Aisha siku ananitoa katika kaburi la wafu wa mapenzi yalikuwa na usahihi wa karibia asilimia 999.9 maana yote aliyoyasema yalitimia (kasoro la kukutana kimwili tu) hadi kesho Laima akiwa katika hali mbaya ya mahusiano yao huwa ananitafuta, japo haniambii wala hani hadithii chochote kuhusu ndoa yao lakini kisaikolojia tu najua kwamba hayupo sawa.
MWIIIIIIIIiiiiiiiiiiiiiSHOOOoooooooooo.
Kama una swali juu ya hiki kisa kabla hakijatokea na hata baada ya kutokea uliza nitakujibu.
Lakini pia maoni ushauri na kila kitu na karibisha.
Pia unaweza kumtag mtu akapita kusoma hapa ili kunipa nguvu ya kusimulia visa vingine.
------------------------------------------
Jamani nipeni pongezi kidogo kuandika ni kazi ngumu mno, tena kuandika bila malipo yoyote ukizingatia Tajiri napoteza muda wa kuingiza mamilioni ya Dola 😂😂😂
Pia kama hujasoma kisa cha Hanifa kipitie hapa👇
Miaka michache nyuma tulianzisha kikundi cha sanaa ya uigizaji mtaani kwetu. Mimi ndio nilitoa hilo wazo na kuwashirikisha vijana wenzangu ambao niliona wanaweza kufanya sanaa ya maigizo. Nilitoa hilo wazo baada ya kuwa nimeacha kufanya mazoezi na kikundi cha MTWARA SUPER FILM, kikundi maarufu...
www.jamiiforums.com
kama nina baya semeni...