Niliambukizwa HIV na mtu niliyemwamini!

Niliambukizwa HIV na mtu niliyemwamini!

Kaka pole sana, nashindwa hata nisemaje? But wewe ni strong Man,, I like your attitude..

Maisha haya yaache kama yalivyo, but muhimu kumuomba mungu tu akusimamie katika ku handle changamoto hii...

Mnaokataa kupima, siwaelewi,, be honest to yourself first ndio utaweza kuwa honest kwa mwenzako.. Kupima HIV ni muhimu sana kwa maisha ya sasa
 
Pole sana nafasi ya kuishi na kufikia malengo
unayo zaidi piga kazi jipe moyo ndg.
 
Be blessed kwa kukataa kuwaambukiza watu wengine. Since u still have life to live tafuta HIV positive partner na pia mtumie kinga kuepuka maambukizi mapya. Pia nenda kwenye vituo wanapokutana wenye HIV mbadilishane mawazo na namna ya kuishi positively. I have brother,friend, and co-worker who with HIV kwa miaka zaidi ya 15 sasa.
 
Pole kaka, unajua wengi hawapimi so ur not alone usiwaze sana utapata pressure bure sawa eehhh am so sorry, nakumbuka chuo watu walikuwa wanaanza mapenz na condom after sometims wanaacha yaani mhh, sasa mie nakushauri kitu kimoja, maana am sure damu yako bado inachemka yaani bado kijana, sasa kama hutajali ujiunge na chama cha kuishi na VVU mle huwa kuna kuwa na watu aina mbali mbali ambapo unaweza mpata mwenzi, kuna hadi wasichana wa miaka 18 wamo offcourse inasikitisha ila wapo watu rika mmbalimbali.
 
wdee imekula kwako.....sie twaendea kugegeda na rain coat zetu bwana...mnataka utamu halisia kazi kwenu

Hivi wewe unaakili kweli? Kuna maswala ya utani na ya msingi...angalia usimcheke mamba ndugu yangu


Sent using JamiiForums
 
Pole sana ndugu, najua ukimwi ulivyo coz nilimuuguza uncle wangu last year akanitoka... Inatakiwa ujikubali kama hivyo jitahidi kufuata ushauri wa madaktari unasaidia, yeye alikaa miaka kjaribu 20 na ukimwi, unachotakiwa usife moyo unauwezo wa kufanya ndoto zako achana na mawazo ya kwamba kifo kipo karibu maana hujui utakufa lini....

Ninachokushauri usikate tamaa unaweza kuoa na kupata watoto vile vile kama utapata ushauri mzuri wa daktari coz maisha hayajaishia hapo!! Hiyo ni changamoto ndugu yangu!

Muombe sana Mungu na atakusaidia kwa kila kitu, Mungu akubariki kwa moyo wako wa upendo kwa watu wengine.

Sent using JamiiForums
 
Bro hongera sana kwa kuwa wazi na kukubali hali. Ila nataka nikuhakikishie kuwa una maisha marefu sana kwa kukubali tu. Pia hata kama una VVU mtafute mwenzako wa hali yako na mnaweza kupata ushauri wa kitaalam mkazaa motto hana maambukizi na mkamlea hadi mkubwa kabisa. Hivi mnafahamu kuwa wakati ule VVU imeingia Tanzania miaka ya 80s na 90s inashika kasi kuna familia moja walipata na mama akawa mjamzito na wakazaa bila usalama na mtoto akapata VVU. Yule baba alifariki maana enzi za kemron haikusaidia sana. Yule mama alibaki akapambana na kemroni na masharti mengine hadi ARV zilipotua. Ninavyoongea yule mama bado yu hai na mwanaye ni mwal Muhimbili, tena nasikia ameshapata PHD? He is living with the HIV. Nina hakika kama kuna member hapa ana VVU kwa muda na anahudhuria clinic atakuwa ameshapata ushuhuda au habari za huyu mama na mtoto. Acha mawazo, kula vizuri, fuata masharti mengine ya afya na ninakuambia utaishi miaka nenda rudi hadi Mungu aamue fate yako. Ndugu yangu over 20s years ni HIV positive, rafiki yangu ni 14 years na hata ARV hajaanza. Keep up strong. We love you.
 
Pole kaka yangu hii dunia tunapita hakuna aliyefika.Mungu akulinde sana stay strong.na atakulipia kwa mema uyatendayo.
 
nashukuru dada yangu. Inaumiza sana unapofikiria mipango yako na ukafikiria mambo yaliyokutokea.[/QUOTE

Usijali kaka yangu.....haupo peke yako ni wengi wanapitia hayo.Jipe moyo na utashinda.
Usihuzunike kaka yangu sawa eeeeh?
 
Sure, upo sahihi hamna atayeishi milele bila kuonja umauti kwanza.
 
Mimi kwenda kupima labda niwe naharisha kama ngisi dhofle hali. Niwe nimishajikubali ila naenda kupima kupata uthibitisho tu. Labda pia nipigwe sindano ya usingizi nikizinduka nipo angaza.
Maisha yenyewe presha tupu, halafu nikijitambua marehemu mtarajiwa hapo chacha!!
angaza hakuzoeleki...pia utaambukizwa na unaemuamini
 
kwa kweli ni neema ya mungu mtu kupima ukajikuta mzima..honestly mimi ninamshukuru mungu saana kwa hilo sio kwamba nilikuwa kicheche saana ila bwana kama ulishawai kuvua chupi chance ya kuupata ni 100 kwa mia so kunusurika ni bahati.
hata hao wenye hiv walifanya hivo hivo kama mimi...utamu utamu...so mleta mada wala usiogope..usijione tofauti maisha ni haya haya enjoy
we love u so much
 
Pole sana na hongera kwa kushinda vita dhidi ya ukimwi (kwa kujikubali na kunuia kuwalinda wengine). Unaweza kuhusiana na wengine lakini kwa kutumia kinga kila wakati. Usisahau kuhudhuria clinic kwa ajili ya kumonitor hali ya afya yako.

Kunyanyapaa mwenye virusi ni ushamba. Kisukari na hypertension ni hatari zaidi ya hiv!
 
Mungu ni mwaminifu, elekeza maisha kwake wakati huu pia usiyape manunguniko nafasi bali kumshukuru Mungu na kumwomba akupe busara za kuishi kwa Aman na kuwasidia wengine kujiepusha na uzinzi kabla ya ndoa pia kuwa waaminifu.
Siku zote naamini kondom ndo zinatumaliza ila Bwana anaweza kutuokoa.
Bwana akutie nguvu na akutendee muujiza Wa maisha yote
 
Pole sana br, zidi kudumu ktkt sala na maombi huku ukizidi kulipa mema kwa maovu unayotendewa. Mungu atakulipa kila unalostahili.
 
Heshima kwenu wakuu.

Poleni na majukumu ya kila siku. Hili suala ni gumu kuliko linavyofikirika na jamii na watu ambao hawajapatwa na mikasa migumu. Ndio maana unyanyapaa unaendelea kutawala sana humu nchini na tatizo linazidi kushamiri. Nilikuwa na mchumba ambaye nilimpenda sana na ndiye niliyemuweka kuwa chaguo langu la maisha.

Mwanzoni mwa uhusiano wetu tulikuwa tukifanya mapenzi kwa kutumia condom na baadaye tulikuja kuacha kutumia baada ya kupima several times na kuona tupo vizuri na tulikuwa tumeshakubaliana kuja kuishi pamoja. nilimtambulisha kwa ndugu zangu kama ndiye ndugu yao atakayeongezeka na yeye alinitambulisha kwa baadhi ya ndugu zake.

Miaka ilivyozidi kwenda niliona mabadiliko kwa mwenzangu kitabia kwani kuna wakati alikuwa akinidanganya kwamba amesafiri kumbe yupo na hajaondoka. Kumbe mwenzangu alishaanzisha uhusiano na wazee wa mujini wenye pesa zao hivyo akawa ananipotezea kwani kwa wakati huo ndo nilikuwa namalizia mwaka wangu wa mwisho chuoni.

Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi kwani ilifika kipindi akanambia ile mipango tuisitishe. nilipomuuliza kwa nini, hakuwa na jibu la wazi. Ilinichanganya sana lakini nilipata faraja kutoka kwa rafiki zangu na ndugu nikatulia. Baada ya miezi kama sita kupita niliamua kwenda kupima na nikagundulika kwamba niko na maambukizi ya VVU, nilichanganyikiwa sana na niliona kama hakuna haja ya kuishi tena.

Sikumwambia mtu mwingine zaidi ya doctor mmoja na mimi mwenyewe kuugulia maumivu yangu peke yangu ila kuna wakati ndugu na jamaa walikuwa wakiniona nimebadirika ila nawaambia hakuna shida yoyote na nipo kawaida. Nilijitahidi kutokukaa peke yangu kwani mawazo ndo yangenizidia.

Mpaka sasa hivi nipo vizuri na nna afya njema ila napata wakati mgumu sana kwani wasichana wengi wanaonesha dalili za kutaka kuwa na uhusiano na mimi lakini nawaonea huruma sana kwani inaniuma sana nikifikiria kumwambukiza mtu mwingine. Wengi wao nimekuwa nikiwakwepa mpaka wengine wananitangazia kwamba jogoo wangu hawiki, huwa inaniuma sana kwani sitaki wajue na sipendi kuwafanya wawe kama mimi.

Nisiwasumbue sana, naomba nihitimishe kwa kusema; hili tatizo ni gumu sana hasa unapokuwa wewe ndiwe 100%. Tupigeni vita unyanyapaa ili watu wasiwe na mawazo ya kwamba TUFE WENGI. Pia unayemnyanyapaa hujui aliupata vipi kwani si kila mwenye VVU alikuwa kuruka njia. Kuna wengine wameupata kutoka kwa watu wanaowaamini sana! Na wengine miaka ya leo wamezaliwa nao hivyo sio kosa lao kwa hapo walipo.

SAY NO TO STIGMA BUT PROTECT YOURSELF FOR THE BEST OF YOU ALL.
Pole sana tena sana mdogo wangu. bilashaka utakua na umri mdogo lakini haina maana kwamba maisha yako yameishia hapo, bado una mambo wengi ya kufanya, endelea kujitafutia maisha kama ambae huna tatizo lolote. Ufike wakati utafute mwenza wako ambae mtapata maelekezo ya jinsi gani ya kuishi na hata kupata watoto. Nakupongeza kwa ujasiri wako na hatua yako ya kuwakinga wasio na hatia ni maamuzi ya kiungwana sana. Muelekee Mungu nae ndie atakae kufanyia wepesi wa maisha yako hapa duniani, pole sana...
 
Pole broo wala usihofu utaishi sana maadam mungu anakujalia kuwa na moyo wa kujali wengine .kula vinzur zingatia hasa kutibu magonjwa nyemelezi mapema nadhani mungu atakusaidia
 
Back
Top Bottom