Wana JF, MMU, naona hii imewagusa sana. Mnamuonea huruma, mnamshauri, ili mradi kila mmoja kasema lake. Basi hebu basi na sisi tuungane kila mmoja akapime ajue afya yake ili tujue namna ya kuishi hasa kwa kuwakinga wenzetu.
Glivec, kua na VVU sio mwisho wa maisha yako. Ishi vizuri, usiwaze sana, kula vizuri na muda unaotakiwa. Nikisema kula vizuri, sio chips kuku, no, proper diet. Usiweke kichwani. Fanya kama hauna VVU vile, ishi maisha yako, sahau kichwani mwako. Utaishi hata miaka 25. Malaria inaua kupita ukimwi. Ukimwi sio ugonjwa ni kwamba kinga yako imepungua.
kula vyakula vya kuongeza kinga yako ili uepuke kuanza dawa mapema maana zina side effect nyingi.
Unaweza kua na relationship ila kumbuka kinga wakati wote maana umepata fundisho.
Nina wifi yangu mume wake alikufa tangu mwaka 90 kwa ukimwi. yeye mwenyewe ni muathirika. alibahatika akaolewa tena na mwanaume muathirika mwenzie walikutana kwenye clinic zao. Nikikuonyesha hutaaamini kama wana VVU, kwa sababu wameamua kutokuiweka kichwani na afya zao zinaonekana kua 100% nzuri. wanaendelea na maisha yao, wamejenga majumba, wanabadilisha magari, life goes on. Tangu mwaka 90 alipokufa mume wake wa kwanza, jiulize wameshakufa wangapi ambao hawakua na VVU? Tafakari, chukua hatua