Nile nini ili kuongeza wingi wa damu

Nile nini ili kuongeza wingi wa damu

wadau naomba mnisaidie nile nini ili niweze kuongeza wingi wa damu mwilini?

chukua fungu moja la matembele, tango moja, carrot 2 bila kumenya tango wala carrot saga kwa kutumia blender au juicer then ongeza ladha na asali kunywa juice yote; fanya hivi kwa week moja halafu baaday waweza punguza na ikawa sehemu ya utaratibu wako.
 
Beet roots zilinisaidia sana kuongeza damu kwa haraka, nenda kariakoo shimoni uulize wapi wanapouza hizo beet roots, mimi nilinunua kilo moja tsh 7000.

Osha vizuri kwa maji safi kata kata vipisi vidogo vidogo tengeneza juisi ya hilo tunda chanyanga na asali unywe, ni nzuri sana.
 
Wakati ukitafuta sababu ya kitabibu ya tatizo lako la wingi wa damu endelea kula betiruti chemsha kunywa juice yake na chakula chake cha ndani ukishaondoa juice. Rozela juice, ribena, mboga za majani hasa tembele na kisamvi iron inaongezeka. Pole sana ila sema sababu ya upungufu huo ili upate ushauri sahihi.
 
Du kumbe alifariki. Tena baon hakujibu posts pengine alizidiwa akafa. Masikitiko.
 
nadhani ungeanza kujibu swali la mdau hapo juu pengine ungepata ushauri mwingi. Ila kama ni mjamzito jaribu kula mboga za majani kwa wingi au kunywa aloevera

Mjamzito na aloevera? utaua! Labda ulimaanisha rosella.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom