Madhara ya kula ugali kwa wingi

Madhara ya kula ugali kwa wingi

stabilityman

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2024
Posts
807
Reaction score
1,750
Madhara ya kula ugali kupita kiasi:

  • Ongezeko la uzito – ugali una wanga mwingi (calories nyingi), hivyo kula kwa wingi bila mazoezi kunaweza kusababisha unene.
  • Sukari kwenye damu – ugali una glycemic index ya juu, hivyo unaweza kuongeza sukari haraka mwilini, hatari kwa wagonjwa wa kisukari.
  • Ukosefu wa virutubisho vingine – kama mlo unategemea ugali pekee bila mboga, protini, na matunda, mwili unaweza kukosa vitamini na madini muhimu.
  • Matatizo ya mmeng'enyo – ugali mgumu au kula kwa wingi bila maji ya kutosha kunaweza kusababisha choo kigumu (constipation).
  • Presha na moyo – ukizidisha na kuongeza mafuta/chumvi kwenye mchuzi unaoambatana na ugali, inaweza kuathiri afya ya moyo kwa muda mrefu.

Kwa upande mzuri, ugali ni chanzo kizuri cha nishati ukila kwa kiasi na kuambatanisha na mboga za majani, protini (samaki, nyama, maharage), na matunda ili mlo uwe kamili.
 
Tuwe wakweli; ugali/mahindi sio chakula hakuna lolote kwenye ugali kama virutubisho. Alieasisi utamaduni wa kula ugali, alileta utamaduni wa kipuuzi, bahati mbaya imekuwa ndio mtindo wetu wa maisha.
Nyanda za juu kusini; Rukwa, Katavi na Songwe, kuna utapiamlo, udumavu uliokithiri kwa watoto miaka 0-5, sababu ni mahindi kuwa chakula chao kikuu katika mzunguko wao wa vyakula.

Watoto wanadumaa, wanapata utapiamlo na hawakui kwa ulinganifu wa muda sababu ya vyakula vunavyotokana na mahindi.
Mtoto anaamka anapikiwa uji wa mahindi, mchana anapigwa ugali, maharage na tudagaa, usiku anapigw wali maharage na chai.
 
Ugali unakufanya uwe na nguvu ila akili kisoda
 
Katika hao uliowataja Songwe wanashikilia kombe, wale watu wanakula ugali bwana... kuanzia breakfast mpaka dinner ni ugali
 
Halafu vyakula vyetu nyie mwaviita urojo ilhal ndio hasaa vyenye nutrients
 
Ninaunga mkono hoja ila wataalamu wetu mnakosea mahali,

Ulipaswa kusema athari za kula vyakula vya wanga kwa wingi,
Ugali ni kundi la chakula sasa wewe umeongelea ugali tu kana kwamba hayo madhara yanapatikana katika ugali pekee.
Vipi kuhusu kula wali kwa wingi au nyama kwa wingi hakuna madhara.

Tunachofahamu "anything too much is harmful" na sio ugali pekee.
Tushauri juu ya kundi la chakula ugali unakuwa ni sehemu ya mfano wa kundi husika.
 
Tuwe wakweli; ugali/mahindi sio chakula hakuna lolote kwenye ugali kama virutubisho. Alieasisi utamaduni wa kula ugali, alileta utamaduni wa kipuuzi, bahati mbaya imekuwa ndio mtindo wetu wa maisha.
Nyanda za juu kusini; Rukwa, Katavi na Songwe, kuna utapiamlo, udumavu uliokithiri kwa watoto miaka 0-5, sababu ni mahindi kuwa chakula chao kikuu katika mzunguko wao wa vyakula.

Watoto wanadumaa, wanapata utapiamlo na hawakui kwa ulinganifu wa muda sababu ya vyakula vunavyotokana na mahindi.
Mtoto anaamka anapikiwa uji wa mahindi, mchana anapigwa ugali, maharage na tudagaa, usiku anapigw wali maharage na chai.
kuleni ugali wa mtama na samaki wa ziwa Rukwa
 
Katika hao uliowataja Songwe wanashikilia kombe, wale watu wanakula ugali bwana... kuanzia breakfast mpaka dinner ni ugali

Inasikitisha, udumavu na utapiamlo unatisha sana maeneo hayo. Nimeshuhudia kwa macho yangu; mtoto anapewa uji wa sembe asubuhi, mchana anapewa ugali mkubwa na maharage labda mboga mboga au dagaa. Usiku anarudia hivyo hivyo.
 
Ni tamaduni; samaki zipo, mtama, uwele, ulezi vyote vipo.
Kaya ikiwa na mahindi na maharage ya kutosha kula mwaka mzima, ndio inasema ina chakula cha kutosha.
ma afisa lishe wapite kutoa elimu. wamama wahudhuriapo clinic wapewe elimu, ... hapo huwa kuna ugumu wa mabadiliko ya haraka ila for the long run watabadilika tu.

binafsi huwa siipendi sembe
 
Sidhihaki yeyote ila ugali ndiyo chanzo cha uvivu wa akili na udumavu wa ubongo kwenye kupambanua mambo.

Tizama wanafunzi either wa bweni au wale wa siku, muda wa saa 4 asubuhi wakitoka kunywa uji wakirejea darasani ni kulala, vivyohivyo kwenye lunch wakirejea darasani ni kulala hakuna kipindi watachoelewa kwa muda huo zaidi waalimu huwa wanafosi tu kufundisha.

Kiukweli binafsi ningepiga marufuku matumizi ya hayo mahindi kwenye lishe iwe kunywa au kula, ili kuokoa kizazi cha Tanganyika.

#Hallelujah!!!
 
Kipindi nipo shule, mara baada ya kupiga pola aiseeeh nilikuwa nalala balaaaaa, uzuri tu baada ya kipindi cha pola kulikuwa na free period ya kama dakika 40 hivi, hivyo hadi ticha aje anakuta ule usingzi wa uji ushakata au umepungua makali ila tumelala sana.
 
Sidhihaki yeyote ila ugali ndiyo chanzo cha uvivu wa akili na udumavu wa ubongo kwenye kupambanua mambo.

Tizama wanafunzi either wa bweni au wale wa siku, muda wa saa 4 asubuhi wakitoka kunywa uji wakirejea darasani ni kulala, vivyohivyo kwenye lunch wakirejea darasani ni kulala hakuna kipindi watachoelewa kwa muda huo zaidi waalimu huwa wanafosi tu kufundisha.

Kiukweli binafsi ningepiga marufuku matumizi ya hayo mahindi kwenye lishe iwe kunywa au kula, ili kuokoa kizazi cha Tanganyika.

#Hallelujah!!!
m'badala wake uwe nini sasa
 
ma afisa lishe wapite kutoa elimu. wamama wahudhuriapo clinic wapewe elimu, ... hapo huwa kuna ugumu wa mabadiliko ya haraka ila for the long run watabadilika tu.

binafsi huwa siipendi sembe

Sio wewe tuu. Mtu yeyote mwenye kipato kizuri na akajua kula, hawezi ifanya sembe kama chakula cha kila siku kwenye nyumba yake. Katika kua kua yetu nakumbuka mara moja moja sana Bimkubwa alikuwa anapika kande. Na penyewe alikuwa anakula mwenyewe. 😊

Angalia watoto wa shule ishu ya macho. Macho yanawatesa sana wanafunzi mikoa hiyo nimetaja. Kutokuona mbali ni kawaida kabisa kwa mtoto wa form II.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom