Tatizo la wingi wa damu

Tatizo la wingi wa damu

Naxria abdalla

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2025
Posts
200
Reaction score
374
Natumai hamjambo, nina tatizo la damu nyingi mwilini. Pia damu ni chafu, naomba maelekezo nini cha kufanya niweze kupunguza damu mwenyewe kabla sijaenda kuchangia.

Ahsanteni.

=====

UFUATILIAJI WA JAMIICHECK

Kuwa na damu nyingi kupita kiasi kitaalamu ni tatizo la kiafya na linahitaji uangalizi wa karibu wa madaktari bingwa ili kuzuia madhara makubwa ya kiafya.

Judith Chale, Msimamizi wa Huduma za Wachangiaji Damu, Mpango wa Taifa wa Damu Salama anatoa ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu jambo hili.


Kuhusu damu chafu

Kitaalamu, neno "damu chafu" mara nyingi hurejelea uwepo wa maambukizi ya vijidudu kwenye mfumo wa damu ambapo kunakuwa na vipimo vilivyofanyika na kupitia hapo unaweza kuambiwa labda una bakteria au changamoto nyingine ya kiafya, lakini kusema damu ni chafu inabaki kuwa dhana tu.

Nini Husababisha Mtu Kuwa na Damu Nyingi?

Kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuufanya mwili uzalishe damu nyingi kupita kiwango cha kawaida kinachohitajika, baadhi ni;

1. Matatizo ya Damu (Hematological Disorders)

Mwili unaweza kuwa na hitilafu ya kisaikolojia ambapo uboho wa mifupa (bone marrow) unazalisha seli nyekundu za damu kwa wingi bila udhibiti. Tatizo hili kitaalamu linajulikana kama Polycythemia Vera.

2. Mazingira na Mfumo wa Maisha

Kuishi Maeneo ya Milimani: Maeneo yenye miinuko mirefu yana kiasi kidogo cha hewa ya oksijeni, ili kufidia upungufu huo, mwili hulazimika kuzalisha seli nyekundu nyingi zaidi ili kusafirisha oksijeni.

Uvutaji wa Sigara: Huathiri kiwango cha oksijeni mwilini na kuchochea uzalishaji mkubwa wa seli za damu.



3. Matatizo ya Kiafya na Matumizi ya Dawa

Magonjwa ya Moyo: Huuathiri uwezo wa mwili kusambaza oksijeni na hivyo kusababisha mwili kuzalisha damu zaidi.

Matumizi ya Dawa za Homoni: Matumizi ya baadhi ya dawa kama vile Testosterone yanaweza kuchochea ongezeko la damu.

Uvimbe mwilini: Baadhi ya aina za uvimbe zinaweza kusababisha tatizo hili.


DALILI ZA KUWA NA DAMU NYINGI

Mtu mwenye tatizo la damu nyingi anaweza kuanza kupata dalili mbalimbali zinazoashiria hitilafu mwilini. Dalili zinazotajwa mara nyingi ni pamoja na:

Maumivu ya kichwa ya mara kwa mara.

Kizunguzungu au kuhisi kichwa kuwa kizito.

Kama unahisi dalili hizi, ni muhimu kuwahi hospitali kupata vipimo rasmi badala ya kujitibia.


TIBA NA USHAURI WA KITAALAM

Kama ilivyo kwa magonjwa mengine, huwezi kujua una damu nyingi bila kufanyiwa vipimo vya maabara. Ukifika hospitalini, unapaswa kuwaona madaktari bingwa wa magonjwa ya damu wanaoitwa Hematologists.

Madaktari hawa wataandika vipimo na vikithibitisha uwepo wa tatizo hilo, hatua za matibabu zitaanza.


KUHUSU TIBA

Moja ya njia kuu za kutibu tatizo hili ni kupunguza damu iliyozidi mwilini ambapo unakuwa mchangiaji wa damu kwa kutoa kila baada ya miezi mitatu au utaratibu mwingine kama utakavyoelekezwa na daktari.


Je, Damu Hiyo Inaweza Kuongezewa Wagonjwa Wengine? (Mtu mwenye changamoto ya damu nyingi)

HAPANA.

Damu inayotolewa kwa mtu mwenye tatizo la damu nyingi haitumiwi kusaidia wagonjwa wengine hospitalini. Hii ni kwa sababu mtu huyo tayari anachukuliwa kama mgonjwa, na kuna vigezo vikali sana vinaruhusu mtu kuwa mchangiaji wa damu salama.

Vigezo vya Kuwa Mchangiaji wa Damu Salama

Ili mtu aruhusiwe kuchangia damu itakayomsaidia mgonjwa mwingine, anapaswa kupitia mchakato mkali wa uchujaji unaoongozwa na vigezo vifuatavyo:

Afya Njema: Mchangiaji lazima awe mzima wa afya na asiwe na ugonjwa wowote sugu au unaoambukiza.

Umri: Awe na umri wa kati ya miaka 18 hadi 65.

Vipimo vya Awali: Kabla ya kutoa damu, mchangiaji anapimwa uzito, mapigo ya moyo, na wingi wa damu yake ili kuhakikisha zoezi hilo halitamfanya yeye mwenyewe aumwe.

Kuchangia damu kwa mtu mwenye afya njema ni kitendo salama, na mara baada ya kutoa damu, anaweza kuendelea na majukumu yake ya kila siku bila shida.


Upotoshaji Kuhusu limao na ndimu Kupunguza Damu

Hiyo ni dhana potofu mitaani inayodai kuwa matumizi ya ndimu, limao, au vitu vyenye asidi kali yanaweza kusaidia kupunguza kiasi cha damu mwilini.

Ukweli wa Kitaalamu: Matumizi ya limao au ndimu hayasaidii kabisa kupunguza damu mwilini. Huu ni upotoshaji na unaweza kuchelewesha matibabu sahihi ya hospitali.
 
epuka kufata ushauri wa mchongo wa wadau, humu karib kila mtu atajidai ni daktari sabb anajua kutumia internet.

Word of advice, it's better ufike hospitali for a clinical consultation, kuna vitu vingi itabidi uulizwe ili kupata data zitazosaidia kuformulate individualized plan ya kukabiliana na hali yako, sabb kila mgonjwa ni tofauti.
 
Mkuu damu yako ni nyingi kiasi gani yaani umepima ukakuta iko ngapi?
Pili unadai ni chafu imechafukaje, imechafuliwa na nini?
Tatu kwa hali ya kiafya unayoelezea wewe hata ukienda kutoa damu hawatokubali,mtu anayejiskia kuumwa kamwe haruhusiwi kuchangia damu.
 
. Hakuna neno damu chafu, na hakuna kitu kinaitwa damu chafu ndani ya mwili wa binadam na "katika taaluma ya Afya" . Jaribu kuelewa hivyo 🤝
So, ulitaka daktari atumie medical jargons kuwasiliana na mteja wake? 🤔

Pia kuna lugha (maneno) hutumika ili kupunguza mzunguko mrefu wa kuexplain medical jargons kwa mteja (client).
zinaweza zisiwe na maana hiyo medically ila zinasaidia huu mzigo wa kuelezea.


Au hujui hilo mkuu?
 
So, ulitaka daktari atumie medical jargons kuwasiliana na mteja wake? 🤔

Umedhihirisha wazi kwamba haujui kuna lugha (maneno) hutumika ili kupunguza mzunguko mrefu wa kuexplain medical jargons kwa mteja (client).

Ungelijua hili perhaps usingetumia miguvu mingi kupinga tu.
Ndo ujinga wa watu wa kiafrika, nimesha kuambia kuwa hakuna kitu kama hicho lakini wewe umekomaa na "medical terms" 😀😀.

Ndo nyinyi huwa mnawaambia wagonjwa mara wana U. T. I sugu, mara wana malaria 1, 2, 3, 4. 🚮 🚮 🚮.
 
So, ulitaka daktari atumie medical jargons kuwasiliana na mteja wake? 🤔

Umedhihirisha wazi kwamba haujui kuna lugha (maneno) hutumika ili kupunguza mzunguko mrefu wa kuexplain medical jargons kwa mteja (client).

Ungelijua hili perhaps usingetumia miguvu mingi kupinga tu.
Ngoja niendelee kusoma nitapata kitu
 
Ndo ujinga wa watu wa kiafrika, nimesha kuambia kuwa hakuna kitu kama hicho lakini wewe umekomaa na "medical terms" 😀😀.

Ndo nyinyi huwa mnawaambia wagonjwa mara wana U. T. I sugu, mara wana malaria 1, 2, 3, 4. 🚮 🚮 🚮.
😀 nimekosa, nimekosa mimi!

nilichomaanisha ni kwamba pengine daktari wake kaona atafute namna kuelezea kwa lugha rahisi tu, maana vipimo vya damu daktari wake ndo avijua., mie nawe hatujui. Ni mbinu ya communication, hufundishwa kwa madaktari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom